Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Sawa kabisa, hakuna mtu ambaye yuko juu ya Serikali. Lowassa akileta mchezo atupwa ndani.
 
Ninawalaumu watoto wake kuendelea kumruhu kusimama na kushiriki siasa katika umri ule. Kaichafua historia yake nzuri aliyoijenga kwa umri wake wote kwa kushabikia wapuuzi katika nchi

Unakosea kusema watoto wake sema mtoto wake Kinjeketile au KINJE
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

Julai 11, 2015:

1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

2. UPDATE 01:20

Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

1) Bernard Membe 2) John Magufuli 3) Asha Rose Migiro 4) January Makamba 5) Amina S. Ali

View attachment 267181


3: Update 12:00

Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.

4: Update 12:15
Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.

5: Update 12:51
NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)

-------


Naisubiria kwa hamu xna hyo tatu bora ili tujue nani ataingoza tanzanini kwa awamu ya tano
 
lazima tukukate tuuu we iweje upate wadhamini milion 48 wakati tanzania nzima tupo milion 45 tu?? tungekuacha vipi kwa mfano yani??
 
Updates kutoka dodoma!

Mwenyekiti alipo wasili kwenye ukumbi ukumbi uli lipuka na kuanza kuimba tunaima na lowasa! Ndipo jk alipo cheka na kusema haijawai kutokea...na kuwbia wasiwe na jaziba mkutano utaisha salama!

Askari wa kutuliza ghasia wamejaa wa kutosha ukumbini na wajumbe wote waliambiwa waache simu mlangoni pamoja na waandishi!


napata wasiwasi...Hivi inawezekana kweli Lowasa akahonga watu wote hao?
 
Ni wakati Wa Watanzania kuwapa wapinzani kura, sioni ulazima wa waliokatwa kung'ang'ania CCM. kuhama chama sio dhambi wahamie UKAWA.
 
Kwa mtazamo huu Rais wetu ni Mhe. Pombe Magufuli.
Sababu kuu ni hizi zifuatavyo:-
1. Anao msuli wa kupambana na UKAWA
2. Hana makundi CCM (ataunganisha wana CCM hata walioumizwa)
3. Anakubalika hata upinzani
4. Anakubalika kwa wasio na vyama
5. Ana rekodi nzuri ktk utumishi wake
6. Hana tuhuma za rushwa kwenye huu mchakato
7. Hajatukana wala kumdhalilisha mgombea mwenzie
9. Hakuwa mpenda vyombo vya habari na machapisho ili kujinadi
10. Kutegemea ilani ya chama badala ya kujinasifu na maono binafsi
11. Amekuwa na low profile through out the mchakato.
12. N.k
huyu jamaa alikua anajinadi kwa utumishi bora wakati wenzake wanahangaika na media. sijui kama ni mtu ya maamuzi ngumu..mimi naweka karata yangu kwa hii mtu.
 
Karamagi anasema Halmashauri kuu ndio wateuzi ....

Kwahiyo hakuna cha majina matano wala nini..??

Kificho anasema "Kazi nzuri na ameridhika sana?"

Ngeleja anasema...

Anaheshimu maamuzi ya chama na hapa walipofika ni pazuri...
 
Back
Top Bottom