Wanabodi leo nguvu ya Lowasa ndani ya CCM imejidhihirisha wazi na hii ni kutokana na wajumbe wanaomsapoti kuamua kupiga kura za bora tukose wote na hili likifanyika watamchagua mgombea mwanamke tena wa kutoka Zanzibar na hilo likifanikiwa tu Lowasa njia nyeupe Magogoni kwani kwa gharama alizotumia na ambazo anaendelea kutumia mpaka sasa na kama kweli ACT ni chama chake na kwa jinsi alivyotumia nafasi ya kutafuta wadhamini kujitangaza nchi nzima na kuona jinsi anavyokubalika je akigombea kupitia ACT au chama chochote huyo Mama ataweza kupambana na Mamvi? Kwa mnaoanglia mkutano wa CCM unaoendelea sasa hivi imedhihirisha wazi EL ni chaguo la wajumbe karibu wote wa mkutano huo kwani kila linapotajwa jina lake ukumbi wote unalipuka kwa kushangilia je hamuoni kama hao wajumbe wanaweza mpigia mgombea mwanamke ambae kwa hali halisi Nchi yetu bado haijawa tayari kuongozwa na Mwanamke? Pia Mamvi ana sapoti kubwa sana ya wabunge wa CCM akiondoka nao si atakua amekimaliza nguvu Chama Cha Mapinduzi na kujisafishia njia kuingia Ikulu?