Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Sasa naanza kuamini kuna watu mabwege zaidi duniani nyuma ya Lowassa! Mnasherekea kushindwa? Urafiki wa EL na Magufuli umeanza lini? Kikwete ndo mshindi hapo, hebu rudisheni japo hela za EL jamani! Mtamuua kwa presha!
 
Tatizo la Magufuri ni mkurupukaji anatoa maamuzi bila kuangalia negative effects mfano kuvunja shell kule Mwanza na Meli ya wachina na kuna wakandarasi kibao alivunja mikataba bila kufuata mwisho wa siku serikali inaliwalipa fidia.
 

magufuri ni mbunge Wa chato siyo Biharamulo na Chato Siku hizi iko Geita siyo Kagera tena
 
Kuna waandika hotuba kibao Ikulu watamsaidia hahitaji kurudi darasani
 
kwanza maghufuli siyo engneer mesoma chemisttry

aje magufuli ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??

ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta

1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba

2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu

3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija

5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula

6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation

7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi

8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu

9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe

10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina

11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara

13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi

14 mengine mtaongeze

kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,

kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,

kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko

ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai
 

Team mende mnakazi nani msafi katika Tanzania hii nitajie mmoja tu
 

Acheni kuendelea kumtesa lowasa nyie muwe na huruma bana,team lowasa na magufuli wapi na wapi? HIV hamshibi nyie watu?
 
ule mradi wa mabasi yakuenda mbio sasa kukamilika disember
 
Mgileadi like this
 
Magufuli sio presidential material, ni mkurupukaji. Wale wa kigamboni wajiandae kupiga mbizi

Haina tatizo, tutapiga tu mbizi ila rais hatakiwi kuremba remba, TUNATAKA mtu kama huyu sio kurembua rembua tu!! Tulipofikia inatakiwa watu warudishwe kwenye mstari, hata watendaji watakaokuwa chini yake itakuwa tumbo joto, nakumbuka amewahi msimamisha mtu kazi "laivu" kwenye Tv sababu ya utendaji kazi mbovu!
 
WildCard,

Naona umeishampitisha kabisa Dr.Magufuli, vipi UKAWA hawawezi kuchukuwa dola na kuunda cabinet.
Ni kweli usiopingika UKAWA watakuwa hali ngumu lakini ACT ndio kwishney!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…