Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kwani magufuli lilikuwa ni Chaguo lenu kweli team Lowasa? Au nyie ndo mmeshindwa kupata mnachokitaka, Magufuli ni one of the loyal people to Kikwete, hamuwezi kusema Kikwete hajampata mtu wake, you must be Joking. Mngetoka na Amina Salum au Migiro tungejua kweli mmemnyima Kikwete Chaguo lake. Unachosema sasa ni kujitafutia faraja.

Jamaa ndo mana hawajashinda akili zao kama Team Wema sepetu
 
aje magufuli aje migiro ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??

ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta

1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba

2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu

3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija

5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula

6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation

7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi

8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu

9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe

10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina

11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara

13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi

14 mengine mtaongeze

kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,

kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,

kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko

ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai

15.Kuwawajibisha wale waliokwapua mali za umma na kuzirudisha pamoja na kuzitaifisha mali zao.....
 
Kwani magufuli lilikuwa ni Chaguo lenu kweli team Lowasa? Au nyie ndo mmeshindwa kupata mnachokitaka, Magufuli ni one of the loyal people to Kikwete, hamuwezi kusema Kikwete hajampata mtu wake, you must be Joking. Mngetoka na Amina Salum au Migiro tungejua kweli mmemnyima Kikwete Chaguo lake. Unachosema sasa ni kujitafutia faraja.

Kwa mfumo wetu una waforce mawaziri kuwa loyal kwa rais! Ni waziri yupi hakuwa loyal kwa Kikwete zaidi Sitta ambaye alikuwa na machungu ya kutopewa u-PM?
 
Mamvia anaendeleaje leo na marejesho yake yatapatikana vipi aka mnarudisha chenji?
 
Kwa magufuli hata mimi ccm wamepata kura yangu....

kitu kibaya kabisa kwa ccm ni system.utamuona mtu mzuri kabisa wakati wa kugombea but akishaingia madarakani "system"iliyomuweka madarakani ndiyo inamuendesha.yaani utashangaa ule moto aliokuwa nao wote unapotea anabaki mtizamaji tu.yaani utabaki unashangaa hata huyu?.hapo kuna system inambeba,akishaingia lazima aitumikie
 
Yeah, ndivyo imekuwa!

Katika tano bora alikuja na watu wake watatu. Kaja na Membe (mtu wake), akaja na Asha Migiro (mtu wake) akaja na January Makamba (mtu wake). Amina Salum Ali (uzanzibari) na John Magufuli aliwekwe kiboya kiboya tu!

TeamLowassa tukafanya yetu pale Halmashauri kuu!

Tukala kichwa cha membe teh teh ............. kura 120
Tukala kichwa cha january teh teh ............ kura 124

Tukampaisha John Magufuli ........kura 290

Tukaenda pale Mkutano mkuu, nako tukafanya yetu!

Tumempaisha John Joseph Pombe Magufuli!

Hii si timu ya kupimia kwa kijiko.....utaumia!


kWA Taarifa yako Magufuli ameongezewa ulinzi na IKULU toka mwezi mmoja uliopita, na alikatazwa kutoa tamko au kuongea kuhusu kampeni. Na alizungukwa na watu wa kariub wa JK muda wote Dodoma. Poleni sana TeamLowassa. JK kawachezea shere si kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Haya taja bei
 

Attachments

  • 1436683255344.jpg
    1436683255344.jpg
    8.6 KB · Views: 169
magufuli haongeki na hana mchezo mtaishia jela kwa ufisadi
 
Speech? Hata bubu ana speech! We need action jamani. Hata shemeji alikuwa na sweet speech matokeo yake watanzania tumeachwa in hell!
 
Ni dhahiri sasa Magufuli ndie Mgombea uraisi kwa ticket ya CCM na UKAWA ni Dr.Slaa(ukimya wao ni mkakati tu wa kisiasa).

Je,kati ya hao wawili, ni nani anafaa kuwa raisi wa awamu ya tano?
 
Kwa wakati huu, mgombea yeyote anatakiwa ajikite kwenye masuala ya kiuchumi kwanza, awe na mipango ya kuunganisha mazao ya kilimo na viwanda kwa kujenga viwanda vya kusindika mazao. Aimarishe taasisi za serikali kama vile Benki Kuu, mifuko ya hifadh, TRA, TANESCO, TRL, TAZARA , Mamlaka ya bandari na nyinginezo, apunguze uwezo wa wanasiasa au viongozi wa wizara kuziingilia, zipewe nafasi zifanye kazi kwa weledi, ziwekewe malengo na zipimwe, sehemu ya faida za taasisi igawiwe serikalini. Tuangalia uwekezaji kwenye madini, mafuta, gesi, utalii, na chuma, uwekezaji uwe wa manufaa kwa nchi , ushirikishe kampuni za umma, watanzania binafsi na wageni. Kwa kukuza haya uchumi utakua sana ndipo tutakua na uwezo wa kuboresha huduma za jamii. Bila kusahau kuongeza walipa kodi na kupunguza matumizi ya fedha taslim, hii itabana mianya ya ukwepaji kodi.
 
Back
Top Bottom