aje magufuli aje migiro ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??
ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta
1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba
2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu
3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija
5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula
6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation
7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi
8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu
9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe
10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina
11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara
13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi
14 mengine mtaongeze
kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,
kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,
kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko
ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai