Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Mwalimu tena anategemewa kuwa Rais wa JMT. Mwl JK Nyerere alifanya kazi nzuri,akafuata Mwl Alli H. Mwinyi,naye alifanya yake. Lakini marais waliofuata wakiwa na taaluma tofauti na ualimu walifilisi/walinajisi hii nchi kwa kila aina ya ufisadi. Mwalimu John Pombe Magufuli Rais mtarajiwa kwa tiketi ya CCM
 
Usilolijua. Magufuli na Kikwete damdam. Amewakalisha kwa kweli. Tano bora yote ni watu wake kwa taarifa zenu. Pale angepita yoyote JK yuko shwari. Alipofanikiwa kumfyekelea mbali mtu wenu baaaasi alikuwa kamaliza kazi. Huyu ndo Kikwete! Haahaaahaaa
 
Ni dhahiri sasa Magufuli ndie Mgombea uraisi kwa ticket ya CCM na UKAWA ni Dr.Slaa(ukimya wao ni mkakati tu wa kisiasa).

Je,kati ya hao wawili, ni nani anafaa kuwa raisi wa awamu ya tano?


Magufuli
aje magufuli ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??

ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta

1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba

2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu

3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija

5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula

6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation

7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi

8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu

9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe

10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina

11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara

13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi

14 kurejesha nyumba za serikali

kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,

kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,

kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko

ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai


Magufuli Hafai Kuwa Rais: Siyo Msafi na Hajawahi kuwa Msafi
1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Hii hatua ya Magufuli halina tofauti na kile alichokiita CAG Professor Assad "Political Entrepreneurship". Professor Assad mara baada ya kuingia madarakani alisema wazi kwamba mradi wa Magufuli wa kuuza nyumba za serikali ni ufisadi mkubwa sana. Professor Assad alizidi kusema ya kwamba alichokifanya Magufuli yalikuwa kwa manufaa yake binafsi na ilikuwa ni "personal political entrepreneurship".

Katika uamuzi huo, Magufuli alienda mbali zaidi mpaka kugawa bure baadhi ya nyumba kwa ndugu zake na mahawara zake. Kwa mfano Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby's
Hotel iliyopo Mwenge/Bamaga jijini Dar es Salaam. Dada Kabula ambaye hajawai kuwa mtumishi wa umma tokea awamu ya kwanza mpaka leo hii Ocampo ninaposhusha huu uzi alifanikiwa kuhongwa nyumba mbili zenye Plot No. MSM/201 na Plot No. MK/521 (Mikocheni na Msasani).

Kwa hatua hiyo Magufuli aliliingiza serikali hasara kubwa sana, na hayo machungu mpaka leo hayajaisha na serikali bado linaendelea kubeba mzigo. Katika kipindi hiki tumeshuhudia watumishi wengi (Majaji, na watendaji wakuu, makatibu wakuu) wamekuwa wakiishi hotelini, huku gharama za vyumba zikiwa za hali ya juu sana almost dola 1200-1500 kwa mwezi ambayo ni sawa na Millioni 27 kwa mwezi; kwa mwaka ni Millioni 324 kwa mtumishi moja.



2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Kiutaratibu na sheria barabara utakiwa kuwa na upana (width) wa 6.5m ila imegundulika barabara nyingi kipindi hichi cha Magufuli zimekuwa zikijengwa kwa 5.7m to 6m na siyo 6.5m, je fedha za hizo baki 0.5m to 0.8m zinakwenda wapi, ni wazi fedha hizo uingia mifukoni mwa Magufuli na washirika wake wa Tanroads. Vile vile ni kipindi kirefu sasa Highway Economic
Assessment ya miradi ya barabara imekuwa hazifanyiki kitu ambacho kinapelekea barabara zetu nyingi kuwa chini ya viwango. Utafiti wa Ocampo unaonyesha kwamba barabara kuwa chini ya viwango ni swala la makusudi ambapo waziri na wasimamizi wa miradi husika wanakula na kugawana fedha za miradi….


3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu. Ubomoaji wa nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara umekuwa hauzingatii "UTU". Ni jambo la wazi wanaanchi wengi waliobomolewa nyumba zao mpaka sasa wako katika hali ngumu ya
maishana hawana uelekeo baada ya kufanyiwa unyama usiyothimilika na Magufuli.

Either wataalamu wengi pale wizarani katika mahojiano wanasema Magufuli hana tabia ya kufata sheria na utaratibu, wakitolea mfano swala la kuvunjwa kwa jengo la TANESCO (Ubungo) na jengo la Millenium Towers. Kwa hakika ni jambo jema sana kuwa na Rias kama JK aliyediriki kumpiga stop Magufuli, hivyo basi ni wazi anapaswa apate mtu wa juu yake katika kufanya maamuzi, ila yeye ndiyo akiwa mtoa maamuzi walai nchi tutaipoteza (Tafakari kwa kina).


4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

6. Umiliki wa Kebby's Hotel
Kebby's Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby's ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby's Hotel, awali alikuwa mke wa Januarius Maganga ambaye ni mtumishi mwandamizi katika makampuni ya IPP Media. Swali la kujiuliza kama Magufuli kadiriki kuvunja ndoa ya mtu angali ni waziri wa kawaida tu, je akiwa Rias itakuwaje? Jibu nafkiri unalo…. Na sitaki unipe jibu.

Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kutolea mfano sakata la waziri mdogo wa Uingereza aliye onekana na kimada barabarani. Kwa tamaduni za hao wenzetu huo ulikuwa ukosefu mkubwa wa maadili mpaka ikapelekea kufukuzwa kazi na waziri mkuu wa wakati huo.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..



10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, busara na kauli nzuri kwa binadamu wenzako; cha kushangaza Magufuli alidiriki kutumia lugha iliyotafsiriwa kama tusi kubwa sana na wananchi wa Dar es Salaam, pale alipoowambia wapige mbizi wakitaka kwenda Kigamboni. Ni jambo jema kwa kiongozi kuwa na msimamo ila msimamo wake uendane na lugha nzuri, ya uungwana na ya ubinadamu. Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............

Asanteni
Ocampo four
 
We muangalie kikwete akiongea jana hana raha kabisa anaongea kiunyonge.anachapia chapia kila saa.mpk akasahau kuwa yeye ni mwenyekiti. Pombe hakuwa chaguo lake bali aliwekwa km povu coz walikuwa na uwezo wa kumkata kirahisi.....hawakutegemea mori za kimasai zingepindua kila kitu. Alikuwa anataka kuongoza akiwa msoga kupitia kwa membe!! Yameenda kombo.kwa magufuli lazima aogope coz ni mtu ambaye haeleweki...dakika mbili mbele na ukumbuke 2005 wakina kikwete walimzimisha kabisa huyu jamaa coz alkuwa nae anataka urais..........je nae atarudi kwa kisasi? Kumbuka pia pombe kaibuliwa na mr.ben.....na ben hakupenda kikwete kabisa...na yaliyotokea jana nasikia kafurahi sana.........
 
Sidhani kama kuna tatizo kwake yeye kujiwekeza.Tuhuma kwamba Kebbys hoteli n yake,ina tatizo gani.Nyie mnataka asijiwekeze?Akipoteza kazi au akistaafu ataishije?Nyie ndo mnafanya kazi na kujisahau kuwa kuna maisha baada ya kazi.Hoteli yenyewe ni ya kawaida tu km 2star, kwa mtu anayejua kutumia masoko ya fedha vizuri na real estate, unaweza jenga ukiwa kapuku.Hakuwahi kuwa kıongozi wa chama,Oboma hakuwahi kuongoza kile chama cha Democrats na jamii za watu makini duniani kote, wanawaanda watu kuwa viongozi si kwa kupitia uongozi wa vyama hivyo.
 
Ukawa washachukua nchi... hii naapa.. iko wazi, Magufuli hana nyota ya kupendwa sana..

Yaani Dr. Slaa au Lowassa akiamua kugombea kupitia chama chochote, URAIS KWAO NI LAZIMA...!!!!

Lowassa akigombea CCM kwisha kazi yake, sbb wamemuonea sana... na najua ata react tu... CCM inakufa kabla ya Oct 25

Dua la kuku
 
Baadhi ya wajumbe jana ambao walikua timu lowasa walikua wanaonyesha dhahiri kuumia na uwepo wa mh bernad membe kwenye tano bora. ndio maana kwenye kura walikua wanasema bora tumpe sapport yetu magufuri. Ndicho kinachoonekana sasahivi ile timu ya lowasa imehamia kwa magufuri
 
Amchague Tundu lissu mwanasheria mkuu wa serikali, na ampe Makongoro kanyadhifa fulani ka kusafisha uchafu!
Kitanuka!!
 
Kama mnavyofahamu kwa mara ya kwanza Tanzania tunaenda kupata RAISI engeneer. Iko wazi watu hawa hawana public speaking skills achilia mbali wao wenyewe kuandaa speech. hawana mbinu za kusoma audience wanayoihutubia kwa kuzielewa nyuso zao., na mengine mengi. Hivyo ni wakati muafaka kwa wahusika kumrejesha raisi huyu class akapige course ya COMMUNICATION SKILLS ili asije sababisha matatizo huko mbele. Natoa hoja.

Stadi za kuongea katika hadhira anazo ni kubadili tu kidogo zikae kisiasa na si za kiufundi ujenzi. Pia atanolewa ikulu humo humo na wenye majukumu hayo katika mambo mengi tu zaidi ya hilo. Kifupi atatengenezwa kuwa Rais wa JMT. Tumwombee!
 
magufuli haongeki na hana mchezo mtaishia jela kwa ufisadi

CCM hawawezi kutoa rais wenye uthubutu wa hivyo. Magufuli ni zao la ufisadi na atabaki hivyo, amewekwa kulinda maslahi ya JK.
 
Magufuli si mtu wa JK wala Lowasa, subiri aapishwe muone pale ni kazi kwa kuzingatia taratibu, si ni huyu huyu JK na Pinda walikuwa wanamuingilia kwenye majukumu yake kwa sababu tu ya siasa wananchi wasichukie
 
Huyu magufuli tunayemsifia mbona wakat yupo kule kwenye samaki hajadeliver chochote cha maana? Ujenz kumemfanya asikike sana kwasabab bajet kubwa ya maendeleo ilikua inapelekwa kule kila mwaka but pia angalia ubora wa izo barabara zenyew sasa n majanga..
 
Magufuli ni mkerewe ndugu yangu sio mhaya wala msukuma........ni kakabila kadogo sana. But nadhani umeona kilichotokea.
 
kWA Taarifa yako Magufuli ameongezewa ulinzi na IKULU toka mwezi mmoja uliopita, na alikatazwa kutoa tamko au kuongea kuhusu kampeni. Na alizungukwa na watu wa kariub wa JK muda wote Dodoma. Poleni sana TeamLowassa. JK kawachezea shere si kidogo.

Unaanza kutulisha matango pori baada ya kuona Magufuli kapeta,wewe huko kwenye system umeyajuaje haya.Story za vijiweni unaleta hapa.Magufuli kafaidika kwa kutokuwa na makundi na vita ya Team Membe na Lowassa ndio imemsaidia,given na historia ya utendaji wake.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom