Habari zilizonifikia hivi punde kutoka mkutanoni Dodoma ni kwamba, tayari yale majina 5 yameshapatikana na sasa mazingira yanatengenezwa ili kuyataja rasmi na kwa mlio Dodoma hapo chungulieni nje mnaona ugeni gani mkubwa wa ghafla wana ulinzi na usalama hapo?
Mnajua ni kwanini ulinzi huo umeimarishwa ghafla mchana huu? Muda wowote kuanzia sasa, hayo majina yatatajwa na mchana huu baada ya mapumziko kidogo wajumbe wanarudi upesi ukumbini kufanya mchujo na kuwabakisha watia nia 3 tu ambao kesho ndiyo watashindanishwa ukumbini na hatimaye kupatikana mmoja.
Ninaloweza kusema na ambalo ni fumbo kwenu sisi wazalendo tunamshukuru sana na mzee Philip Mangula, wazee wa CCM na wenye heshima kubwa na mdahalo ule wa juzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, kwani kilichopitishwa kimetokana na matamshi, matakwa na wosia wao na nasema kuwa chama sasa kimerudi katika misingi ya Baba wa Taifa na Watanzania wenzangu haswa wazalendo na wenye uchungu na nchi hii popote mlipo tafadhalini anzeni kufurahi kwani Mwenyezi Mungu amesikia kilio chetu. Nimefurahi na akhsante Mungu. Sasa nitalala usingizi.
Kazi imekwisha, hakuna cha kaskazini wala kusini na maslahi na ustawi wa chama ndiyo umezingatiwa ili kuua makundi ambayo yangekidhoofisha chama.
Mchana mwema nyote ila msikae mbali na radio zenu kwani muda wowote patakuwa na breaking news ya utangazwaji wa majina hayo yaliyoingia 5 bora. Mimi sasa kwa furaha iliyoje nakwenda zangu kufurahi. Nchi imerudi rasmi kwa wazalendo.