Nchi inaendelea kutafunwa na maadui 3 tangu uhuru umasikini, ujinga na maradhi huku watawalawa wetu wakiendelea kutunisha mifuko yao binafsi na familia zao huku wakiwaacha wananchi wakifa kwa kiu, maradhi na njaa. Hakuna ajira wala masoko ya mazao yao yaliyolimwa kwa jembe la mkono. Mshahara wa mwalimu ni kichekesho ni dola 150 tu huku watawala wakishindana kujilimbikizia mali.
Mimi nadhani hata Makongoro anamcheka sana baba yake kwa kuisababishia familia umaskini, bila shaka anataka kugombea kiti cha urais uli arekebishe uchuro wa umaskini walioachiwa na baba yao. Mbaya zaidi wananchi tumetaitiwa na CCM mwanzo mwisho tusiweze hata kupepesa kope zetu kuikataa hali hii kwa kupitia visanduku vya kura.
ILa sasa wacheni mungu aitwe Mungu, huenda kuenguliwa kwa Lowassa kwa mizengwe ikawa kete muhimu sana kwa taifa katika ukombozi dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi nchini, ni nani ajuae?
Namuuomba Lowassa ajione kama sehemu ya ukombozi mpya kwa taifa hili, usisononeke wala kujizulu kama watalikata jina lako kwa namna yoyote ile, bali tumia kipaji, karama, umaarufu, haiba, utajiri, marafiki zako na ucha mungu wako katika kuuvunja mnyororo unaotaka kujengeka nchini wa kurithishana utawala wa dola kwa maslahi binafsi ya watu.
Hamishia nguvu zako UKAWA ili historia ikukumbuke japo kwa hilo pale utawala wa kimla utakapokuwa umejeruhiwa na kwenda kutafakari na kujipanga upya kuhusu namna bora ya kuboresha maisha ya wananchi na kero zao mbalimbali. CCM kulikata jina la lowassa ni saawa na kulewa madaraka