Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Mtu atapata stroke mwaka huu, yule daktari wa Ujerumani kashindwa kazi. Mmmmmmm tamaa ya kuingia Ikulu Nomaaaaaa!!! Chadema jasho lawatoka kwani walimshangila Lowasa zaidi kuliko Slaa. Mmmmmm ukanda ulikuwa unanukia.
 
Unaufahamu mshahara wa Magufuli? Kama huufahamu, utafute halafu linganisha huo mshahara na nyumba 60. Then, rudia kupost tena kwamba "nyumba 60 si ufisadi bali kuweka mali wazi", "Nyumba 60 ni kawaida kwake". Na nyumba 60 ni za nini? Kwani yeye tembo? Ukiangalia kwa makini utagundua hahitaji nyumba 60. Ni ushamba tu.
Kazi ya mshahara sio kujenga nyumba mkuu ukikaa na mawazo hayo mkuu kila jirani yako anaefanya maendeleo utamwona fisadi, nimetoa comment sio kwamba nakataa Magufuri hawezi kuwa fisadi bali nimeangalia hali halisi ya kile kinachotokea ndio maana nika site na mfano wa maisha yetu huku uraiani kuna watu wa kawaida tu wana nyumba 5 au 6 na ukiwaangalia walipopitia unaona wana derve though sio wote, unajua nilivyosema kwa Magufuri nilimaanisha kwa position yake anakopesheka mkuu wala hayo mambo yenu ya team nani sijui team nani kutoka moyoni kabisa mie simo kabisa, mie nilikuwa naongelea uwezekano wa yeye kujenga hasa ukizingatia nchi yetu ilivyo na miposho kibao isiyo na vichwa wala miguu ndo maana nikasema hivyo mkuu.

Tafakari ukiwa free bila kuweka chembe ya kishabiki huku unaangalia kinachotokea huku uraiani otherwise nyie endeleeni kutupa madhaifu ya Magufuri
 
kiukweli magufuli silitaki liwe rais ,misukuma ni mishamba sana itatusumbua sie watanzania.slaa chukua nchi

Wasukuma wanakwambia ninafasi yao kuongoza nchi,watampa kura bila kujali chama,kina ngosha wamedata aisee,jamaa anaweza pata shida mjini ambako raia wamejitambua na kuuelewa mfumo mzima wa ccm ulivyo kwamba hatakwenda kinyume na wao,lakini vijijini jamaa hata asipopiga kampeni atazoa kura zote,vile vizee vikifika vituoni vinauliza tu ....'ali hei u Magufuli...'maana yakee Yupo wapi Magufuli...kakionyeshwa kanatia na tiki,labda kuvidanganya napo ni ngumu maana vilisha kalili lile lile lijikofia la duara analovaaga sasa maga.mba wakitumia picha Magufuli akiwa na hilo kofia UKAWA twafwa,wasipo tumia basi UKAWA tuchangamukie fursa,mgombea wetu atinge lile kofia tuviingize mjini hivi vibabu uhuuuuuuuu,kama utani vile noma sana huyu mtu
 
Nakupa tano mkuu. Kwani ni wapi imeandikwa kuwa mtumishi wa umma ni lazima awe maskini. Unakuta mko ofisi moja but mna financial approach tofauti. Wewe unaejishughulisha kwa kutumia muda wako vizuri pamoja na kuanzisha shughuli ndogo ndogo nje ya ajira na nje ya muda wa kazi ikiwemo kuwa na nidhamu na matumizi ya fedha unayoipata, ukijenga tu, inakuwa nongwa.

Watanzania tunaweza mkuu tatizo tuna mawazo ya kijamaa sana kiasi kwamba mtu kuonyesha mafanikio yake anaogopa, nakupa mfano huwa tunanunua vitu kibao vya thamani tunaweka ndani kama simu, friji, majiko na kukaa nyumba nzuri za kupanga lakini mwingine akaiwekeza ela yake sehemu akapata mshiko wa nguvu wa kufanya mambo tunaanza kuchukua calculator ya kuanza kumpigia hesabu mshahara wake.
 
mbona kama wanatangaza Mwanamke ndo mgombea Urais sisiemu japo za umbea umbea zinasema ni Magufuli
...... Ni kama lkn....
 
Magufuri anaweza kuwa na nia nzuri ya kuwavusha watanzania,lakini wasiwasi wangu ni mfumo atakao kutana nao akishapewa ikulu...kikwete nae alipokelewa kwa mbwebwe kama hizi..inanipa shida sana

Ni kweli kabisaaaa, mtu anaweza akawa sahihi ila sasa mfumo ukamvuruga kabisaaaa
 
.
Magufuli Hafai Kuwa Rais: Siyo Msafi na Hajawahi kuwa Msafi
1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Suala hili Waziri mkuu mstaafu Mh.Sumaye alisha lifafanua kwa undani, uuzaji wa nyumba za Serikali ulikuwa kwa nia njema tu - we sema labda waliokosa fulsa hiyo ndio wanataka kumzulia Mh.Magufuli - nyumba zenyewe wamewauzia waswahili wenzetu, je wangekuwa wameuziwa wageni mgesema nini? Niliwahi kumsikia Magufuli akisema kwamba fedha ambazo zingepatikana zingetumika kujenga nyumba nyingine ili wawauzie wananchi, lakini wanahibuka watu humu na kutaka kumzulia mambo tu.

2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Msitake kudanganya watu na takwimu zenu za kubuni tu, kama mna chuki binafsi na Magufuli semeni wazi wazi! Kwani Watanzania hawana macho,nani ambaye hajui umahili wa Mh.John katika utendaji wake kazi - mpeleke Wizara yoyote 2 prove a point, jamaa huyu si mtu wa kawaida lazima tukubaliane na hilo. Haya tuje suala la barabara - yaani unataka kusema wewe binafsi huoni tofauti ya ufanisi wa kazi na uwajibikaji tangu Magufuli akabidhiwe Wizara ya ujenzi!!


3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu.

Mkuu jaribu kusoma Historia ya URUSI wakati wa utawala wa Stalin specifically kuhusu hatua za maendeleo ya Taifa hilo under his watch - walipiga hatua kubwa sana, na hii wakati mwingine walipaswa kufanya mahamuzi magumu ili wafikie malengo yao - Taifa haliwezi kukwamishwa na watu wachache wakorofi ambao hawataki kuhama na kupisha maendeleo ya watu walio wengi eti kwa kisingio cha human rights - na vyama vya upinzani vina-capitilize kwenye mantra za human rights kama mtaji wa kisiasa hawajali maendeleo, hivyo wanachochoea watu kuwa wakorofi kwa visingizo visivyo na mantiki, kwani nini hawataki kupisha ujenzi wakadai fidia baadae.

4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

Mkuu umetaja neno chuki mara ngapi hapa? Kisaikolojia hilo linathibitisha nini about your 'PERSONA' ni spitting image of your goodself - saying of the wise usema hivi: Kama huna jambo jema la kuzungumza kuhusu binadamu mwenzako the best U can do ni kukaa kimya.

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

Reading between the lines naweza ku-guess sababu, you keep repeating yourself over and over again kwa theme zile zile unachofanya ni kubadirisha maneno, lakini all in all unaonekana una chuki binafsi na Mh.John, come clean u-confess kama aliwahi kukutimua TANROADS au kwenye mizani.

6. Umiliki wa Kebby's Hotel
Kebby's Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.
Please revisit my comments kwenye item No.5 unajirudia rudia tu kwa kuwa huna point za kumu-nail Mh.Magu, unasema lolote like a drunken COMET, ndio baadhi ya Watanzania tulivyo kuwaharibia sifa na kujaribu kupaka matope binadamu wenzetu tukiwa na imani kwamba matope hayo yata-stick.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby's ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

Mtu akisoma comments zako hapo anaweza kufikili unazitoa kwenye script za movies huko Hollywood California, ni usanii tu wa kufurahisha baraza, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukuchukulia/kuwachukulia seriously.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Kesho ukija hapa na kudai kwamba Mh.Magufuli amedai kwamba yeye ni mkatoliki kuliko PAPA sitakushangaa!!!


8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

Hii kali!!! Unaweza kueleza member Mh.Mkapa alikuwa na wadhifa gani kwenye chama wakati alipopendekezwa kupeperusha bendera ya CCM? Jibu huna!

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..


10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, b Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

Naona hapa kidogo umekuwa sober na kutumia lugha ya staha, kinacho shangaza hapa ni pale Mh.Magufuli anapoleta utani nyinyi mnajaribu kujenga hoja kimakusudi ili aonekane hafai, Watanzania wana akili ya kung'amua mbinu zenu hizo zenye lengo za kumchafua, kama Wananchi wanampenda na kuona atatuvusha the Rubicon, nyinyi hamna uwezo kuzuhia Tsunami ya Mh.Magufuli.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

Mkuu soma majibu yangu No.4, hujabalika chochote bado unaendeleza your deep and emotional extreme dislike of Mh.Magufuli! Nikwambie kitu UMECHELEWA.

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............

Ni huyu huyu IVAN the terrible, the guy U love to hate!!!!
Asanteni
Ocampo four


Mmmmmh, you are done - finally.

 
Back
Top Bottom