11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….