Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Pole na majukumu kaka yangu Nape!!

Mimi niko uku kijijin karibu na Kenya kunaitwa Horohoro. Nashindwa kula wala kulala kusubiri hiyo tano bora yako ata usingizi ukija ndoto zote ninazoota nikuhusu dodoma na ccm yetu.

Nakuomba kaka yangu uwaambie na wenzio mnatutesa kwa kweli mana haya mateso ni makubwa sana kwetu kwann mnatufanyia hivo lakini.

Leo mlisema mtamaliza kila kitu lakini imeshindikana kwani tatizo ni nini kaka yang?

JK si anaikumbuka ile mihadi waliyoweka na Mzee kwanini sasa vikao vinakua virefu hivo?
Kama hawataki ni bora waseme mapema kuliko kupoteza mda.

Ikifika kesho mtaghairi tena iwe keshokutwa mana tunaujua ugumu uko wapi.Fanyajeni kwa umakini na kwa speed watanzania tunaumia kusubiri naww si unajua subir subiri yaumiza matumbo kaka!!

Kazi njema kaka
 
LOWASSA anatosha...Yeye Pekee ndiye anayeweza kupambana na hawa wahuni wa UKAWA.
Hili ndio tatizo la magamba…badala ya kumchagua raisi ambae atapambana na mafisadi, maradhi,ujinga ,rushwa nk wewe unamtaka Lowasa aje apambane na UKAWA…Tatizo hilo ndio maana tuko nyuma kwa kila kitu ktk Afrika Mashariki…Kenya wanaendelea kutupiga bao, Rwanda nayo pamoja na janga la Kimbali wamekwenda hatua kibao zaidi yetu…nasema tena CCM ni janga jamani la Taifa
 
Mliochangia humu you made my day maana nacheka tu hapa nilipo peke yangu..AMEKATWA.. nadhani akikatwa kweli hii itakuwa caller ring tone
 
1.Kuna tishio la watu kufanya fuja iwapo mtia nia X akikatwa
2.Wasio na ulazima wa kufika Dodoma kipindi hiki wanashauriwa kutofika Dodoma-RPC Dodoma
3.Ulinzi mkali kuzunguka viunga vya mji wa Dodoma.
4.Vikao kufanywa usiku wa manane-wanahofia ni nini!
5.Taarifa za vikao zimekuwa siri
6.TAKUKURU,TISS na Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusishwa katika vikao vya maamuzi
7.Kikao cha Maadili na Ulinzi kinaweza kuomba kupatiwa ushahidi wa tuhuma zinazohusiana na maadili-hii ni kwa mujibu wa katika ya CCM
5.Mgombea atajwa kuwa na tuhuma nyingi ikiwa ni pamoja na kuanza campaign kabla ya wakati.

Mpaka hapo bado tu hujapata jibu nini kinaendelea?
 
msomali bana wakati wengine wanaimba ikiwa ni pamoja mna mwenyekiti wake yeye wala anafikiria Al shabab na operesheni zao.Naona kamanda wake FaizaFoxy kimya kidogo nadhani yuko frontline kwa kisingizio cha mfungo

Imetoka WAP mada hio
 
Kama Zanzibar ni Nchi Uhalali wa Kugombea Bara Unatoka Wapi??

hill seal I usiulize kwenye urais turn uliza kwnye ubunge,uwaziri,makmu warais timu ya taifa na shilingi pia manager mijitu mingine inalaana ya ubaguzi eti watusjui million ndgo kuongza millionI kubwa hv wanzanzibari nawakwere wengi niwapi?
 
Kingunge, Kone na Msindai wanaratibu mpango wa kumng'oa Mwenyekiti wa CCM,KIKWETE
Wadau amani iwe kwenu.


Taarifa nilizopata hivi punde kutoka Dodoma zinasema kuwa baada ya Team Lowasa, Friends of Lowasa na 4U MOVEMENT kubaini kuwa jitihada za mafisadi za kufanikisha Lowasa anaenda Magogoni zinagonga mwanba, mawakala wa mafisadi hao chini ya uratibu wa Kingunge Ngombale Mwiru na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone wanaratibu mpango wa kumuondoa Madarakani Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete. Taarifa zinasema kuwa mawakala hao wa mafisadi wameshindwa kutekeleza mpango wao huo ndani ya kikao cha Kamati Kuu na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ambao utafanyika hivi punde.


Taarifa zinasema pia kuwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai naye amejiunga kwenye harakati hizo ili kuhakikisha kuwa kubwa la mafisadi nchini, Edward Lowasa linaenda Ikulu iwe kwa amani au kwa shari. Katika kuhakikisha kuwa lengo hilo linafanikiwa, muda mfupi uliopita Kingunge, Kone na Msindai wameonekana maeneo ya Chuo Kikuu cha St Gasper wakigawa fedha ambapo taarifa mjumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu aliyejiunga kwenye timu ya mafisadi amepewa shilingi milioni 5. Aidha, wajumbe hao wameahidiwa shilingi milioni tano nyingine ambazo wameahidiwa kupewa ikiwa watafanikiwa lengo lao hilo.


Baadhi ya wajumbe ambao wamepenyeza taarifa hizi wamedai kuwa wanachofanya akina Kingunge ni cha kipuuzi hasa baada ya Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa kuziba mianya yote ya mafisadi kumpitisha mtu wao. Kwamba Rais Kikwete anasimamia haki na wamempongeza kwa kusimamia misingi ya chama.


Wadau, hawa ndio mafisadi. Wameamua liwalo na liwe kuhakikisha kuwa fisadi lao linaenda Ikulu. Nawaomba Watanzania kusimama imara kupinga mkakati huu ovu ili chama chetu na nchi yetu isingie kwenye machafuko. Bahati nzuri wanaofanya vitendo hivi wanafahamika. Watambue kuwa kumchezea Mwenyekiti wa CCM ni kumchezea Mkuu wa nchi kwa vile Kikwete ana kofia mbili.
 
Kweli bana.mi mwenyewe huku watu wanapigiana simu 'amekatwa' 'amekatwa'.watu watapatwa na presha kesho!,,,,,,only time will tell!

Hajakatwa bado yupo pale juu jinsi ya kumtoa wanashindwa amini hivyo vichwa vyawauma kwa sasa
 
lala hujalazimishwa kusubiri unahangaika nini au umapiga debe ili baadae upate kitengo au ukuu wa wilaya
 
Na mm nalala maana nimesbil vya kutosha.ila bwan mamvi akikatwa nitapata ucngz safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…