Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

MAKAMBA AWAGARAGAZA MWIGULU NA KIGWANGALAH KAMATI KUU .....


kikao cha kamati kuu ndani ya chama cha mapinduzi. kikiwa kimemalizika na mihemmko ya wengi,Ikiwa juu zaidi ya kifuniko cha soda.

Wengi wakimsubiria kwa hamu Katibu wa chama cha Mapinduzi Ndg. Kanali Abdulrahman Kinana.
Kutaja walioingia nafasi Tano bora baada ya kuchujwa na Kamati Kuu.
Kikao kilichoanza saa nne asubuhi.
Kukiwa na mvutano mkali huku wajumbe wa Mkutano mkuu kutoka upande wa Zanzibar wakisimamia hoja ya muungano zaidi kumpata mwakilishi au mrithi atoke upande wa Tanzania visiwani.

Ni mtanange huu uliopolewa na busara za Mjumbe kutoka visiwani, Balozi Salim Ahmed salim ambaye alitanabaisha kuwa mchakato huu utaamuliwa na kura za Wajumbe wa NEC hata kama patakuwapo na muwakilishi hivyo kazi hii itaachiwa wajumbe.

Mnyetishaji wetu ambaye pia Aliweza kutupenyezea taarifa zaidi kwa upande wa Makundi ya Vijana.

Mpambano ulikuwa ni mkali sana na baadhi ya wajumbe wakigawanyika kuamua ni nani aingie kati ya walio katika kundi hilo.

Kura nyingi zilimwangukia January Makamba, Naibu waziri sayansi mawasiliano na Teknolojia alipata.
Nafasi nyingi zaidi kulinganisha na Wagombea wenzake.

Huku Mtia nia wenzake mh Mwigulu L. Nchemba akimfuatia. Pamoja na Hamisi kigangwala akishika nafasi ya Tatu.

kura Nyingi katika nafasi hii zimemwangukia Mbunge huyu wa Bumbuli.

Mtanange umekuwa mkali zaidi huku wajumbe wakiyumbishana zaidi kuhusu baadhi ya watia nia ambao wana uwezo na nguvu zaidi nani awemo au as iwepo,
Huku wagombea walio na umri mkubwa zaidi wakipumzishwa kwa maoni ya wajumbe wa kamati kuu ndani ya Chama.

kikao bado kinaendelea na wajumbe wanavutana lakini kimebakisha muda mfupi tu kumalizika.

Labda niseme tu kazi hii ilikuwa ngumu lakini Tumeafikiana kwa maamuzi ya wengi kwa kuwa chama ni cha Demokrasia na Demokrasia ndio imeamua zaidi.


Mara kwa mara Rais Kikwete amekuwa akisimama kuwaonya baadhi ya wajumbe ambao wanaenda kinyume na Kikao huku wakiomba miongozo ambayo inaonekana kama inataka kuvunja utaratibu uliopo.

Vilevile Nje ya Ukumbi Ulinzi umeimarishwa vyakutosha.
Askari wafarasi pamoja na makachero wengine waliovalia kiraia.
Wakirandaranda huku na huko kuhakikisha usalama upo na wa kutosha.

Wengi wanasubiria kwa shauku na mapigo ya moyo kwa wagombea yakipanda na kushuka kwa baadhi ya wapambe wa wagombea.

Chama kimeamua kusimama maslahi ya wengi kwa ujumla hivyo wagombea Tuliwateua leo hii mmoja wapo anaweza kuwa Rais nadhani chama hakitakuwa na wakati mgumu kumnadi kwa yeyote atakayeteuliwa. Kwa kupigiwa kura na wajumbe wa NEC katika kikao cha baadaye.

mmoja wa viongozi wa juu ndani ya chama akiongea na mwanahabari wetu hivi punde baada ya kikao cha kamati kuu kumalizika.

Katibu Mkuu muda si Mrefu kwanzia sasa Ataitangaza Top five ambayo pia imesheheni majina mapya ambayo yatashangaza wengi kutokana na kusheni majina ya watu wenye sifa ya kumrithi Rais Kikwete.

Imeandikwa na,

KIOGO MPINA,
DODOMA.
 
Kamati kuu hawapigi kura, hapo unaondoa credibility ya habari yako
 

 
Ndo hivyo aiseee
Sijui wametumia vigezo gani hapa. Naona Raisi akiwa mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…