Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Hii ndiyo top five list ya wagombea wa urais kwa tiketi ya ccm baada ya mchujo wa muda mrefu:bernald membe,john magufuli,asha rose migiro,january makamba na amina salumu aly.baadhi ya makada wa ccm naona hawaamini kinachoendelea hapa kana kwamba watu wao hawaonekani kwenye list.source:star TV,mwananchi news paper.
 
ONE, TWO, THREE, mr Eddo twende zetu kule kwa Wazalendo tukauchukue uraisi kama kumsukuma mlevii
 
ImageUploadedByJamiiForums1436570438.677544.jpg
 
CCM could have an easier campaign, they chose the hardway, UKAWA wanatakiwa washangilie kwa kweli. CC couldn't have botched the mission worse than they have!

Huku namuona "raisi wa kipekee duniani", huku namuona bidada UN iliyomshinda, huku namuona Amina-mwerevu, ila sio mwenye kufahamika.

wamejitahidi kwenye sehemu ya uadilifu, ila sehemu ya Mvuto overall top 5 yao iko around 40%. wajiandae kuchapisha noti za kutosha kuiuza hii timu.

Kama mamvi ataamua kumwaga mboga na kuhamia UKAWA, hawa top 5 yao yote ana uwezo wa kutunishiana nao misuli, kwani wengi wana vijikashfa vya kuwapakazia kwenye media. Ukichanganya na pesa zake.., Lowassa has a very goo chance to make 2015 a memorable election.

CCM had the driving seat, but as usual they gave the steering wheel away.

Dr.Slaa,Lipumba and team must be on Lowassa speed dial by now.

Uliyoongea yote ni kweli Mkuu,Kikwete kaamua kucheza karata hatari kabisa kuliko zote katika maisha yake sababu kwa hali ya mambo ilivyokuwa hauwezi kumkata Lowasa then ukamwacha Membe asonge. Na hauwezi ukamkata Mtu kama Jaji Ramadhani then ukampa nafasi Makamba Jr. Haya mambo ni kama yale ya KANU ya Moi na Uhuru wake vs wakina Kibaki.
 
Dk Magufuli anapeta hapa.
Watu wa Lowassa hawawezi kumchagua Membe.

Hao wengine watatu wamewekwa tu kama wasindikizaji, mmoja wao ndio ataenda Mkutano Mkuu.

Wapigwe tu vipi kaangukia pua?

Vipi Six mzee wa kuchakachua Katiba ya Wananchi?
 
Usim'under rate' Asha.Kumbuka alivyotoka UN kazi yake ya kwanza ilikuwa CCM, na alizunguka nchi nzima na akina Nape & Kinana. Hii ilikuwa ni mbinu ya kuwekeza.

Na Mwambie Tu Kuwa Kuna Kila Dalili Asha Rose Migiro Akapata Political Advantage Hapa Na Kuibuka Mgombea Rasmi Wa CCM Na Kuna Kila Uwezekano Tukaongozwa Na Mwanamke This Time. WHY? TEAM LOWASSA Hawawezi Kukubali Kumpa Nchi Magufuli Kwani Wanajua Akichukua Nchi Atawatesa Hivyo Hawamwamini Totally Na Hawamtaki Kabisa ISIPOKUWA System, Wazee Wote Wa CCM Kuanzia Mwinyi, Mkapa, JK ( Japo Kidogo ), Mangula, Msekwa Na Mawaziri Wakuu Wastaafu Karibia Wote Wanamtaka Dr. John Pombe Magufuli Na TEAM LOWASSA Hawawezi Kukubali Kumpa Nchi Mbaya Wao Bernard Membe ( Ambaye Kwa Kiasi Kikubwa Sana Anasapotiwa Na JK Pamoja Na Familia Yake Nzima ILI Aje Kulinda Maslahi Ya JK Binafsi Na Wanafamilia Wake ) Kwani Wanajua Kuwa ATAWAMALIZA Kwa Visasi Hivyo Watatumia USHAWISHI Wao Wote Ili Wampigie Kura Mama Dr. Asha Rose Migiro Na Watasaidiwa Mno Na Katibu Mkuu Wa CCM Abdularhman Kinana. Hivyo Basi Kwa Mazingira Hayo Na Labda Nguvu Ya Ziada Itumike Tu Ili Magufuli Awe Rais ILA Naiona Njia Ni Nyeupe Kwa Mama Asha Rose Migiro Kuwa Mgombea Rasmi Wa CCM ISIPOKUWA Huyu Mama Nje Ya CCM Hauziki Vilivyo Na Mapungufu Haya Ndiyo Yatafanya UPEPO Baadae Ubadilike Na Magufuli Apitishwe Kwani Kiuhalisia Ndiye Mtu Pekee Si Tu Anakubalika Bali Anaogopwa Na Anaheshimiwa Sana Hata Na Wapinzani Japo Wawili Hao Kama Binadamu Hawakosi Mapungufu Yao Na Kwa Uzuri Ni Kwamba Yanarekebishika. 60% Dr. Magufuli Na 40% Dr. Migiro. Huo Ndiyo Mtazamo Wangu Mdogo Na Alamsiki Nyote.
 
asante ccm kwa kutuwekea watu laini kama uji wa nazi tunaenda shinda kumi bila awamu hii
 
Mwigulu, Muhongo, Mwakyembe, Lowasa wote hawa wameachwa sababu hawakuwa au hawakutaka kuwa karibu na Mheshimiwa.
Kama ni Kamati ya maadili basi Membe, January wote hawakitakiwa kwani walifungiwa, walianza kampeni pamoja......
Membe na Lowasa walipaswa kuingia wote au kutoingia wote
 
Yaani wewe siku nikutia mkononi. ..endelea na ujinga wako tu

Wewe unanini cha kunifanya mimi? Nnakwambia kama ni mwanamme kweli sema wapi unataka nikukute na nione utakachokifanya, nnakuasa tu uje kuhadithia kitakachokukuta.
 
Sasa naelewa kwanin Membe alikuwa anawafagilia wenzake na kuahidi kuwaunga mkono kama akikatwa, nao sasa wana wajibu wa kiutu wa kumuunga mkono.

Bila shaka Pinda, Mwandosya, Makongoro kwa uchache sasa ni timu Membe
 
Duh,
Ama kweli usichokifahamu ni kama usiku wa giza!

Naona Membe anatafutiwa dirisha la kutokea lakini ninaamini Timu Lowassa ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu hawawezi kutoa kura zao kwa Membe.

CCM wakijigonga na kumchagua Membe watakuwa wanajipa kibarua kigumu kwa sababu Timu Lowassa itahakikisha inamwangusha ili wakose wote!

Nafasi ya CCM kushinda kwa sasa iko kwa Magufuli kwa sababu hana makundi ndani ya chama!
 
Back
Top Bottom