Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Ni shangwe na nderemo kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma yalipo makao makuu na Tanzania kwa ujumla baada ya Kufanyika mchujo wa Tano bora.

Ulikuwa ni mmpambano uliovuta wengi ni nani na nani watakaoingia kwenye ngwe hii ya Lala salama.

Hatimaye majina matano yametitokeza ya watia nia

1 . JANUARY MAKAMBA
2. JOHN POMBE MAGUFULI
3.BALOZI AMINA SALIM ALLY
4.ASHA ROSE MIGIRO
5.BENARD MEMBE

Kutokea kwa Jina la JANUARY MAKAMBA kumepokelewa kwa Furaha na Shangwe.

Umakini wake katika kujenga hoja na uwezo wake katika utendaji wa kazi unafahamika kwa watu wote.

Kwakuwa;
Rais ndiye kiongozi mkuu wa Nchi, na ndiye mwenye maamuzi yote muhimu ya juu ya Taifa, kwa Nafasi hii ya hadhi dhahiri ni kwa kiongozi huyu kijana na Mwadilifu mwenye mikono safi.

Kamati kuu ya Chama cha cha Mapinduzi iliyoketi jana kuanzia saa kumi alasiri ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho.

Ilionyesha juu ya Uasisi wa jambo jema hutoka kwa Mungu.

Japokuwa kulikuwa na Tabiri nyingi za majina yalikuwa yamepenya ndani ya chama , kamati hii ilifanya kazi kwa usiri mkubwa sana.

Kazi ya kupiga kura kwa wajumbe wa Mkutano mkuu haitokuwa Ngumu kutokana na sifa zilizo wazi kwa majina matano yaliyo teuliwa.

Kijana huyu muadilifu mwenye sera zenye kitu kipya ndani ya Tanzania na uwezo anuai wa kusimamia mawazo ya jumla na ufanisi wa kuandaa mipango.

Amewashangaza watu waliokuwa wakifikiria wakati wake sio sasa ni Bado hivyo Asubirie.

Kuwaachia wenye jana nyingi na kesho chache, hakuna Daktari asiyekuwa na uwezo wa kutibu Tatizo bila kulijua lazima Daktari afahamu chanzo cha Tatizo ndipo ajue dawa yake ni nini.

Kwa Tanzania tunaweza kupata Daktari mzuri kama wajumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi watafanya uchaguzi kwa umakini, na kutimiza mpango huu wa Mungu.

Imeandikwa na,
KIOGO MPINA,
DODOMA LEO.

Watanzania tuna shida sana. Ni hoja gani Makamba aliwa kujenga? Ni hekima sana kuwa mkweli hata kwako mwenyewe.
 
lowasa kwa sasa ametia headphone masikioni mwake anasikiliza wimbo unaitwa ..im i wrong?''...
 
tuweni wakweli jamani! Mbona kama siamini hivi kwa kile kilichotokea!
Kama kweli kigezo ilikua ni usafi wa mtu utaamini vipi kwamba waliopitishwa na kamati kuu ni bora kuliko waliachwa? Kama kigezo ilikua ni kukubalika kwa mtu utakubaliana vipi kwamba walipitishwa na kamati kuu ni bora kuliko walioachwa? Duh hatari.
hivi kuna udugu kati ya kikwete na membe
 
Hijawahi kutokea, mbwembwe zoote, pesa zoote na nguvu zoote alizotumia mh Edward lowasa na sasa ametolewa nje!

Janja ya lowasa ilionekana toka zamani alijifanya kuwa na upendo kwa makundi mengi ya kijamii ilhali akijulikana dhahiri kuwa hafai ktk urais.

Nimefurahi sana anguko la ufalme huu wa Giza CCM!
Mimi nimefurahi zaidi na zaidi, CCM kwa namna fulani wameonyesha ukomavu wa kisiasa. Lowassa ametumia gharama kubwa sana katika mchakato huu wa kutangaza nia na sasa chama chake kimemtosa live! Najiuliza swali moja hapa, haya mabilioni ya shilingi aliyoyatumia yatarudi vipi???? Hakika he is the biggest looser ever! Lakini Rais Kikwete alisema alipokuwa Tanga wiki iliyopita kuwa wagombea wanaotafuta madaraka kwa gharama kubwa, wananchi wawakatae kwa macho makavu. Kikwete ameonyesha kwa mfano.
 
Mkuu,
Kwani wewe umekuwa msemaji wa jukwaa hili?

Kama wewe huna muda hata wa kusoma comment zangu unaweza kuzipita kama vile huzioni!

Maandiko yangu hayawezi kubadili hali ya kisiasa!

Mimi siwezi kulaumiwa kwa maamuzi yaliyofanywa na wazee wa CCM!

Mimi ni msomaji na mchangiaji tu!

Ninafahamu ukisikia kelele...

nazisoma sana mkuu tatizo ni hivyo viambata
 
mzee wetu mwandosya tunamjua na heshima yake iko palepale, nafasi ya kuongoza mawaziri ni yake,
 
Hayo ya ccm mnayajua wenyewe UKAWA ndio watatupa serekali 2015-2025 hatuwezi rudia makosa
 
Wadau fungueni Luninga zenu kufatilia mchakato mzima sasa hivi.
 
Back
Top Bottom