Ni shangwe na nderemo kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma yalipo makao makuu na Tanzania kwa ujumla baada ya Kufanyika mchujo wa Tano bora.
Ulikuwa ni mmpambano uliovuta wengi ni nani na nani watakaoingia kwenye ngwe hii ya Lala salama.
Hatimaye majina matano yametitokeza ya watia nia
1 . JANUARY MAKAMBA
2. JOHN POMBE MAGUFULI
3.BALOZI AMINA SALIM ALLY
4.ASHA ROSE MIGIRO
5.BENARD MEMBE
Kutokea kwa Jina la JANUARY MAKAMBA kumepokelewa kwa Furaha na Shangwe.
Umakini wake katika kujenga hoja na uwezo wake katika utendaji wa kazi unafahamika kwa watu wote.
Kwakuwa;
Rais ndiye kiongozi mkuu wa Nchi, na ndiye mwenye maamuzi yote muhimu ya juu ya Taifa, kwa Nafasi hii ya hadhi dhahiri ni kwa kiongozi huyu kijana na Mwadilifu mwenye mikono safi.
Kamati kuu ya Chama cha cha Mapinduzi iliyoketi jana kuanzia saa kumi alasiri ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho.
Ilionyesha juu ya Uasisi wa jambo jema hutoka kwa Mungu.
Japokuwa kulikuwa na Tabiri nyingi za majina yalikuwa yamepenya ndani ya chama , kamati hii ilifanya kazi kwa usiri mkubwa sana.
Kazi ya kupiga kura kwa wajumbe wa Mkutano mkuu haitokuwa Ngumu kutokana na sifa zilizo wazi kwa majina matano yaliyo teuliwa.
Kijana huyu muadilifu mwenye sera zenye kitu kipya ndani ya Tanzania na uwezo anuai wa kusimamia mawazo ya jumla na ufanisi wa kuandaa mipango.
Amewashangaza watu waliokuwa wakifikiria wakati wake sio sasa ni Bado hivyo Asubirie.
Kuwaachia wenye jana nyingi na kesho chache, hakuna Daktari asiyekuwa na uwezo wa kutibu Tatizo bila kulijua lazima Daktari afahamu chanzo cha Tatizo ndipo ajue dawa yake ni nini.
Kwa Tanzania tunaweza kupata Daktari mzuri kama wajumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi watafanya uchaguzi kwa umakini, na kutimiza mpango huu wa Mungu.
Imeandikwa na,
KIOGO MPINA,
DODOMA LEO.
Watanzania tuna shida sana. Ni hoja gani Makamba aliwa kujenga? Ni hekima sana kuwa mkweli hata kwako mwenyewe.