Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kwa mtazamo huu Rais wetu ni Mhe. Pombe Magufuli.
Sababu kuu ni hizi zifuatavyo:-
1. Anao msuli wa kupambana na UKAWA
2. Hana makundi CCM (ataunganisha wana CCM hata walioumizwa)
3. Anakubalika hata upinzani
4. Anakubalika kwa wasio na vyama
5. Ana rekodi nzuri ktk utumishi wake
6. Hana tuhuma za rushwa kwenye huu mchakato
7. Hajatukana wala kumdhalilisha mgombea mwenzie
9. Hakuwa mpenda vyombo vya habari na machapisho ili kujinadi
10. Kutegemea ilani ya chama badala ya kujinasifu na maono binafsi
11. Amekuwa na low profile through out the mchakato.
12. N.k
 
Sijakuelewa naona umekurupuka tu ukisikia neno Muislam.

Unamuelezea nani Padre Slaa au Askofu Ramadhani?

Mbona mnapaniki mapema hivi mkuu?? Slaa ndo Rais wa awamu ya tano. UKAWA ni amani na mshikamano. Tushirikiane kwa pamoja kutokomeza mafisadi CCM.
 
nadhani nothing new japo kuna taarifa zinasambaa kuwa kwenye hotels na ukumbi wa mkutano kuna tifu. mlioko dodoma, tujulisheni kinachojiri
ni Membe kabebwa sijui hata km patakalika
bora wamuachie na Magufuli aende Mkutano Mkuu
maana hata NEC haijakaa eti Membe apitishwe Rose Migiro na Amina salum
Kura za kutokuwa na imani ndio mpango unaofuata na EL amesema yeye hahami
 
yaaani kwa akili zao wanadhani kikwete is Playing a blind game

Bingwa wa siasa Za Fitna CCM ni kikwete hakuna anayemfikia

Alafu ana organ na taasisi zote za state....eti ashindwe kum contain lowasa?

Cha msingi hawa jamaa wangeondoka tu warudi Monduli...Kikwete atawafanya kitu mbaya
Yaani wewe kama ulikuwa kwenye kikao changu cha mtaani, hiki ndio nilikuwa nawaambia! Au mimi na wewe tulikuwa pamoja mkuu? Ukweli ndio huo, hata Nchimbi anamuundermine JK Lakini nina hakika Hamjui vizuri kama anavyodai kuwa anamjua!!!!
 
nilitamani niende upinzani ila naona bado hawajajua thamani yao kwa nchi hii. kila siku ni mvurugano tu. bora nibaki kwenye chama cha baba. with time CCM itabadilika tu. ile mizee iliyokaa mule utadhani yenyewe ndio inamiliki chama itaondoka mmoja mmoja
Mrembo, wewe changua pakwenda. Sisi wazee hatutoki kwa chama hiki, ndo wenye chama
 
Wajumbe Zaidi Ya 1200 Wameazimia Wakiingia Tu Mkutanoni Wapige Kura Ya Kutokuwa Na Imani Na Mwenyekiti Wa Taifa Wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete Kisha Mkutano Uvurugike Na Kuwe Na Timbwilitimbwili Na Jambo Hilo Limeratibiwa Sana Na Mtia Nia ALIYEDANGANYWA NA UTITIRI WA UMATI WA WATU Kupitia Kwa Wapambe Wake Waliopo Mkoani Dodoma. Na Duru Zinaendelea Kusema Kwamba Kuna Uwezekano Mkubwa Mno Pakatokea Na Fujo Na Itakayopelekea MACHAFUKO Makubwa UKUMBINI Kwani Watu Wamegadhabika Sana Na Maamuzi Ya Jana.

Kama Mtakumbuka Vyombo Vyote Vya Habari Hasa TBC1, STAR Tv Na Clouds Tv Walitakiwa Waanze Kurusha Matangazo Yao Ya Moja Kwa Moja Tokea Saa 3 Asubuhi Leo Lakini Mazingira Hayajaruhusu Bado Kutokana Na Kwamba Kuna MTAFARUKU Unaendelea Na JK Sasa Anahaha Kumtuliza Na Kumweka Sawa Lowassa Lakini Bado Mmasai AMEKATAA KATA KATA Hivyo Kupelekea Kuchelewa Kuanza Kwa MCHAKATO Kamili Wa Mkutano Mkuu Na Mpaka Hivi Ninavyandika Uzi Huu Huko Dodoma Hali Si Nzuri Na Ulinzi Umeimarishwa Vilivyo Mithili Rais Obama Anakuja Tanzania Leo.

NINI KINAFANYIKA SASA?

Marais Wastaafu Wote, Wa Sasa Na Mawaziri Wakuu Wastaafu Sasa Wanafanya Mazungumzo Na Mheshimiwa Lowassa Ili Kumshawishi Na Kumpoza Kwa Ahadi Kuwa Baadhi Ya Watu Wake Watapewa Nafasi Katika Serikali Ya Awamu Ijayo Ila Bado Lowassa AMEDINDA ( Amekataa ).

KOSA GANI LA KIUFUNDI AMELIFANYA JK?

Hakika Katika Hili Hata Mimi Naungana Na Wachambuzi Wenzangu Wengine Wa Kisiasa Kwa Kumlaumu Moja Kwa Moja Mwenyekiti Wa Taifa JK Kwa Makusudi Na Kwa Kutumia Ushawishi Wake Na Turufu Yake Kama Rais Kumpendelea Kwa Wazi Wazi Mtia Nia Bernard Membe Wakati Kiutaalam Ilitakiwa Kama Akimkata Lowassa Basi Membe Nae Pia Akatwe Na Kama Aliamua Kumbakisha Membe Basi Hata Lowassa Angebakishwa ILI Kutengeneza Uwiano Wao Kwani Hakuna Ambaye Hajui Kuwa CCM Ina Makundi Mawili Tu Ambayo Ni Kundi Kubwa La Lowassa Na Kundi Kubwa La Membe. Rais JK Hii Dhambi Itakutesa Milele Kwa Ulichokifanya Kwani Katika Hili Hakika Karata Zako Ulizicheza Vibaya.

ATHARI GANI INAELEKEA KUTOKEA KWA CCM NA KWA NCHI?

Hakika Katika Hili Hakuna Jinsi Na Wala Tusipepese Macho Wala Kutikisa Masikio Kwamba Ni Dhahiri CCM Wasipojipanga Na Kulimaliza Hili Chama Kinaweza Kupoteza Umaarufu, Wabunge Na Kikaathirika Na Kuna Hatari Pia Ya Kutokea MPASUKO Mkubwa Ambao Pia Utahatarisha Hali Ya AMANI Ya Nchi Na Kuelekea Hata Katika Machafuko Na Kuna Kila Dalili Kama Hali Hii Haitotatuliwa Serikali ITATIKISIKA Na Kuwapa Mwanya Jeshi Kuchukua USUKANI Kwa Muda.

NINI KIFANYIKE ILI KUOKOA HALI HII?

Kwakuwa CCM Sasa Kuna MPASUKO Mkubwa Baada Ya Lowassa Kukatwa Na Membe Kubakishwa Katika Kinyang'anyiro Kitu Ambacho Sasa Wanatakiwa Wakifanye Ni Ama Kumuengua Membe au Kumurudisha Lowassa Ili KUKINUSURU Chama Kisha CCM Kwa Nguvu Moja Impitishe Dr. John Pombe Magufuli Apeperushe Bendera Kwa MASHARTI Kwamba Akiwa Madarakani Basi Ahakikishe Vigogo Wawili Hao Anawapa Majukumu Kwa Maslahi Ya Chama.

Hayo Ndiyo Machache Niliyonayo, Niliyoyapata Kwa Muda Huu Na Mtazamo Wangu Pia ILA Dodoma Sasa KIMENUKA Na Kuna HALI Ya Wasiwasi Mno IMETAWALA Huku Watu Wakiogopa Nini KITATOKEA.
 
embe ww sio mtendaji na wala vigezo hauna..ni basi tu una mvuto na hendisamu..sasa basi tunakuomba uache porojoo nyingii uache usaniii ufanye kazi km ukipita ukichaguliwa...Tunakuomba sana maana taifa linaangamia..umebebwa ndio hiyo inaoenekana kabisa wazi ila basi tunaomba ubebeke na uwe mtendaji ufanye kazi utupe maendeleo..in short prove thrm wrong.mambo ya kupenda kusafirisafiri kwa sasa achana nayo hatutaki muendelezo wa jk maana na ww unapenda sana goodtime ilo linaeleweka! Cha msingi bebeka basii tupo nyuma yako.

Ndugu tangu NCH ipate Uhuru nizaidi ya 50yrs nw Bado unaamini huko CCM kuna mtu anaweza kurekebisha hii NCH ccm ni sawa na MBWA Mzee hana michezo mipya nikukariri tu so hata haya Maombi yako hayanakazi nw wekeza Nguvu UKAWA cz Hatuwapa Serikali tunahitaji kuona Uwezo wao nawao wakizingua tunawatupa Lkn kufanya jambo lile lile miaka nenda rudi then kutegemea Matokeo tofauti nikujilisha uPEPO
 
Kwa mtazamo huu Rais wetu ni Mhe. Pombe Magufuli.
Sababu kuu ni hizi zifuatavyo:-
1. Anao msuli wa kupambana na UKAWA
2. Hana makundi CCM (ataunganisha wana CCM hata walioumizwa)
3. Anakubalika hata upinzani
4. Anakubalika kwa wasio na vyama
5. Ana rekodi nzuri ktk utumishi wake
6. Hana tuhuma za rushwa kwenye huu mchakato
7. Hajatukana wala kumdhalilisha mgombea mwenzie
9. Hakuwa mpenda vyombo vya habari na machapisho ili kujinadi
10. Kutegemea ilani ya chama badala ya kujinasifu na maono binafsi
11. Amekuwa na low profile through out the mchakato.
12. N.k

Una msafisha wenzie wapo Na rufaa
 
Yaani wewe kama ulikuwa kwenye kikao changu cha mtaani, hiki ndio nilikuwa nawaambia! Au mimi na wewe tulikuwa pamoja mkuu? Ukweli ndio huo, hata Nchimbi anamuundermine JK Lakini nina hakika Hamjui vizuri kama anavyodai kuwa anamjua!!!!

hawamfahamu Kikwete Vizuri

Ila Lowasa anafahamu what Kikwete Is Capable Of
 
Back
Top Bottom