Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

2005 kilikuwa na mshikamano mkubwa sana na kwa vile hawakuelewa wakatenda dhambi ya ubaguzi na sasa 2015 mbegu zilizopandwa zimetoa matunda machungu. Siajui kama wataweza kuvunja kambi safari hii na tweets zinazoonekana hadi sasa zinazidisha mpasuko wa makundi!
Sina uhakika kama UKAWA ndio imewachanganya zaidi au walipo ndipo walistahili wafike. Mungu ni mkubwa!
R.I.P Mwalimu, R.I.P Horace Kolimba ...viva UKAWA
 
Kwa janga hili wanalochuma CCM tunaweza kula wote tukiliangalia hili in long run, wanaweza kufanikiwa kumtuliza Lowasa kwa sasa akatulia ila October atakaposhinda Membe ndio mziki part two utakapoanza kwa sababu upinzani hawatakubali na kataa yao yaeza kua na mashiko kwa sababu Membe hana uwezo wa kuwachallenge upinzani watakaokua wamepewa nguvu na team Lowassa, na wakati huo huo CCM washazoea usultani kuachia madaraka hawatakubali ndio tutaona ya kwa jirani walipomtosa Odinga, itakapotokea hali kama hiyo hawa wenzetu wanapanda ndege na familia zao habari tutaipata wananchi wa kawaida.. naunga mkono mkuu getamycine alichosema either wamkate na Membe au wamrudishe Lowassa ili kuua hizi team na kurudisha umoja wa chama.

Hiv huyo lowassa ndo nan mpaka wanamsujudu kama Mungu anakubalika na wanachama au wananchi kwa sabab gan kubwa ni kwa sabab ya media kumpa airtime sana ila what goes around comes around ubabe waliowafanyia upinzan for years sasa dhamb inawatafuna am keep watching the game
 
Last edited by a moderator:
Nipo dodoma hakuna shida yeyote. Kwa mtazamo wa kitafiti wengi wa wananchi wa kawaida wanapongeza sana uamuzi wa CC kumg'oa Mh Lowasa. Hizo ni propaganda ili kushinikiza jina la Lowasa kurudishwa NEC ni Vitisho tu. Dodoma watu walishatangaziwa nchi nzima kama hawana shughuli maalum Dodoma wasije na wakija kwa lengo baya ninawaonelea huruma yatakayowapata ulinzi ni mkali sana. Na hakutakuwa na nafasi ya kujadiliana na Mtu au watu au kikundi cha watu.

Unajua kilichomponza Lowasa si yeye bali watu walionyuma yake.

Kwa mfano makanisa mengi katika wiki mbili zilizopita walikuwa wakihubiri Lowasa Lowasa lakini wiki ya mwisho ya lowasa kuksanya wadhamini ndiyo wale watu waliokuwa nyuma yake walipoanza kujitokeza. Mtazamo wa makanisa hasa ya kiroho umebadilika sana na sasa wako UKAWA.

NB: Kama Lowasa ataamua kuhama chama na kuhamia chama kingine cha siasa aachane na mafisadi walio nyuma yake atapata Urais kwa kupitia mlango wa Nyuma. lakini aking'ang'ania na kundi lake na vurugu zake Amekwisha kabisa!

"Unajua hatutaki kumsikia Kalamaji, Rostam,Chenge wala Tibaijuka" alisikika Kiongozi mmoja wa dini ya kikristo.

Bado ana nafasi ya kuwa Rais wa jamuhuri ya Tanzania bado anawapiga kura wengi sana.
 
Waliokuwa wakisema kikwete hana ubavu wa kumkata jina lowassa wako wapi?hivi mnamchukuliaje kikwete?
 
Back
Top Bottom