Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 16, Nov 2021

Bwashee kuna mada nyingine sio kufungulia uzi, zipotezee
 
Kuna jamaa waliiba kwa mzungu,wanapopelekwa mahakamani pingu mikononi na miguuni,Mzungu akawa anaridhika nakuwapa posho walinzi.
Mwisho ushahidi wakuwatia hatiani haukuwepo,
Mzungu akaanza kudai posho sake kwa wale maaskali.

Usimtese mtu kwa mgongo wa nafasi yako
 
Hajawahi kusoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2005. Ibara ya 13(6)(b) inasema hivi: 'no person charged with a criminal offence shall be treated as guilty
of the offence until proved guilty of that offence'. Mtuhumiwa akitiwa hatiani na mahakama kwa ugaidi kuanzia muda huo anaitwa 'gaidi' na si kabla. Labda yeye anaishi Kenya, lakini hata Kenya ni hivyo. Kukiuka sheria au kutumia nguvu kupita kiasi siyo tafsiri halisi au sahihi ya sheria.
 
Kule Nigeria Magaidi wameua mageneral watatu wa jeshi tit for tat.

Wiki hii hii Kule Msumbiji Magaidi wameua Wanajeshi 17 na Raia mmoja.

Ushahidi wa Ugaidi unaojulikana na Polisi pekee ni wa ajabu sana.

Kwamba Mbowe ni Gaidi na Matukio ya kigaidi aliyofanya/ aliyotaka kufanya mashahidi ni polisi tu hakuna hata Raia mmoja aliwahi kushuhudia? Huu ni ugaidi wa aina yake.
 
Raia ni wauza mbege na yule mpiga picha na mkulima wa mbogamboga, mtumishi wa Tigo
Tuna ushahidi wa kutosha. Siyo malaika
 
Hivi makaratasi tu waliotumia tayari majaji kuandikia hizi kesi ndogo sizinatosha kugharamia ujenzi wa vyoo mashuleni
 
Utumike kuwa mfano kwenye vitabu vyote vya elimu ya uraia Tanzania.
 
Kuna watu wanamdanganya huyo mama kuwa magu alikuwa anapendwa sana, hivyo na yeye ameamua kuiga kila kitu ili na yeye eti apate mvuto! Ndio maana naye kaingia kwenye ulimbukeni ule ule wa kutaka media covarage kwenye kila kitu.
Hivi mama mwenyewe hana mawazo binafsi?
 
Jamani huyo MBOWE si mumfunge fasta fasta mioyo yenu ifurahi?
Tumechoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…