Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na wenzake - Desemba 1, 2021. Shahidi asimulia alivyowekwa chumba cha mateso gerezani. Uamuzi kusomwa Desemba 14, 2021

Kuna muda nilikuwa nasoma mpaka natetemeka najiuliza vipi kama ingekua ni mimi? Aisee jamaa makatili sana
Acha kujidanganya wewe. Hiyo ni kesi ipo mahakamani, hapo kila wakili anatengeneza namna ya kuweza kushinda kesi. Sasa ukikaa ukaamini upande mmoja wa utetezi kwamba watu fulani ni makatili bila ya kuwa na uhakika unajipotosha.
 
Hiyo hapo ni trailer tu ya mashahidi wa utetezi katika kesi ndogo. Subito wenyewe kwenye kesi yenyewe. Mtasimama Dede!
 
Leo wakati anatoa Ushahidi wake anasema kwamba September 2020 akina Kingai na Mahita walienda Tabora mjini wakamvamia na kumteka, kisha wakamsafirisha hadi Nzega ambako alikataa siku kadhaa badae akasafirishwa hadi Dar es salaam huku akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni, alipofikishwa Dar akapelekwa kituo cha Polisi Tazara

Anasema akina Kingai na Mahita na Goodluck walimtesa sana kwa kipigo, walikuwa wanampiga na chupa za soda kwenye magoti na mikononi akilazimishwa aseme walipo akina Adamoo (Wakati wanamwamia aseme walipo akina Adamoo, akina Kingai walikuwa tayari washawakamata na kuwapa kesi ya Ugaidi so walikuwa Magereza) lakini pia walikuwa wanamlazikisha akubali kusema kwamba Mbowe alitaka kumtumia kutekeleza matukio ya Kigaidi lakini Komandoo Mhina alikataa akina Kingai wakaanza kummpiga shot ya umeme mpaka ilifika point akawa hawezi kutembea, kusimama wala kuketi.
 
Nchi hii mwanajeshi wa kikosi cha special forces anafanyiwa haya sisi wengine akina kajamba nani tutafanyiwa nini??

Yaani swala la haki za binadamu ni zero. Tunaishi kama mahayawani.

Mtu akiwa mwanajeshi akaachishwa kazi au kufukuzwa kazi kwa mujibu wa kanuni zao za kisheria hazuiliwi kufanta shughuli zake za kawaida za kujipatia kipato. Lakini hapo inaonekana ukiwa na uhusiano na chama cha upinzani tu unakuwa adui moja kwa moja. Hii sio sawa hata kidogo
 
Wes a de
 
Nimesoma kipigo alichopata shahidi nimekosa amani.Ni kipigo cha kunitisha.Ngumi za taya na chupa za soda za magoti
 
Mbaya zaidi kinachoniuma ni kuona wengi wa hao watesi ni waislamu,sasa sijui uislamu wao hauzungumzia muislamu kuwa na huruma na viumbe vya Mwenyezi Mungu
Unashangaa nini mnafiki wewe, ndio legacy ya mwendazake hio.
 
Daah huyu shahidi wa leo kama mpaka sasa hajalipwa stahiki zake basi tutakuwa na Jeshi la ovyo sana
Mkuu ni kweli kbsa japo kuna mambo mengi ila ukianza kufuatilia kwa undani kuna shida ndani ya hili jeshi linalojisifu kuwa na weledi, hata kama wana utaratibu wao ila lazima kila kitu kiwe clear ili kutokuacha maswali juu ya hili jeshi mpaka leo wahusika bado wana madai na hawana taarifa za kuachishwa kazi official kuna shida mahala siyo bure
 
Uwezekano wa kubambikiziwa ugonjwa wa akili Kisha ukanyanyapaliwa na kufukuzwa kazi na haki zako zinaliwa, maana Hawa jamaa wote wamefukuzwa kazi kwa trend inayofanana na kipindi kisichotofautiana Sana hapa Kuna tatizo!?
Hata mimi nimewaza sana kwamba hata kama wana makosa mbona hawa jamaa haki zao nyingi ni kama zimekiukwa sana huko jeshini kuachishwa kwao tu kazi kuna walakin mkubwa, siku zote jeshi huwa halihojiwi ila wana michezo michafu sana sema tu ni vile mengi hayasemwi wazi wazi
 
Wakati wa awamu ya 5 kuna kikundi kilikuwa juu ya sheria, sawa na miungu watu. Ndio maana mambo ambayo ktk makuzi yako uliamini hayawezi kutokea Tanzania yalikuwa yanafanywa na kikundi hicho.
 
Acha kujidanganya wewe. Hiyo ni kesi ipo mahakamani, hapo kila wakili anatengeneza namna ya kuweza kushinda kesi. Sasa ukikaa ukaamini upande mmoja wa utetezi kwamba watu fulani ni makatili bila ya kuwa na uhakika unajipotosha.
Sawa
 
Acha kujidanganya wewe. Hiyo ni kesi ipo mahakamani, hapo kila wakili anatengeneza namna ya kuweza kushinda kesi. Sasa ukikaa ukaamini upande mmoja wa utetezi kwamba watu fulani ni makatili bila ya kuwa na uhakika unajipotosha.
Walioteswa ndio wanaeleza mateso waliyopitia, kwa wenye kumbukumbu ya Magoti wa benki kuu jinsi alivyoteswa kwa chupa kupitia njia ya haja kubwa wataelewa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…