Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Ni hivi maneno hayo ya kiingereza ameyatumia Kwenye ripoti yake iliyowasilishwa hapo mahakamani Kama ushahidi.
Sasa anaulizwa aeleze maana yake kiswahili ndio kajichanganya
Hivyo basi kwa Maelezo take akina mbowe walikuwa wanamiliki silaha ili iwawezeshe kufanyia utalii.
Hoi ndio maana ya ripoti yake
Hii kesi tuliwaambia waifute,wakasema tunakomaa nayo,Sasa kinachoenda kutokea Kama Ni haki inafuatwa mwenyekiti ataachiwa huru,lakini Kama jaji anafanyakazi kwa maelekezo lazima matokeo yatakuwa yaleyale ya jaji aliejitoa
 
Ndio maana Watanzania wote tunataka Sheria zetu zote zitafsiriwe kwa lugha yetu ya Kiswahili, Pia Mwenendo wa kesi pamoja na Hukumu ziwe zinaandikwa kwa Lugha ya Kiswahili.
karibu 99%ya watanzania wote tunazungumza na kuandika lugha ya kiswahili lkn cha kushungaza Mahakama zetu bado zimekumbatia mfumo wa kikoloni wa matumizi ya kizungu!!
kwani kulikuwa na haja gani kumuuliza swali kwa kizungu?
angemuuliza kwa Lugha yetu ya Taifa hata mkulima wa kijijini angemjibu.

Huyo jamaa alikuwa anafanyiwa cross examination ya ripoti yake ambayo katumia maneno hayo ya kiingereza sasa wakili wa utetezi akamtaka ayaeleze kwa kiswahili ndio akatoa tafsiri hiyo.
Ushahidi wa jamaa ushaingia doa kwani kwa mujibu wa tafsiri yake hiyo ni kwamba akina mbowe walikuwa wanamiliki silaha ili waweze kufanya shughuli ya utalii
 
Ujinga tu. Sidhani eti kushindwa kutofautisha terrorist na terrorism ni issue yenye mashiko
Ushahidi unatakiwa utolewe bila kuacha shaka yeyote sasa inapotokea unaulizwa jambo ambalo umeliandika wewe ukashindwa kujibu maanake ni kwamba ushahidi wako hauna mashiko ni kuwatunga tu au umekaririshwa na ripoti hiyo hujaandika mwenyewe na hujafanya uchunguzi wowote.
 
Sio kweli kukosea kutamka neno hakufanyi ushahidi kutokuwa na mashiko sio kwa sababu ameghafilika kutoa tafsiri sahihi ya ilo neno na ushahidi wake utakuwa na dosari huko ni kujidanganya
 
Ushaidi wa Leo ni wakupoteza muda. Kama hawakuchukua finger print, watathibitishiaje mahakama kama hiyo bastola ilikuwa ya Adamoo??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee.. Hata kina Lema walikuwepo wako wapi?
Msigwa yuko wapi?
Sugu yuko wapi?

Na kama yameisha mnacholialia nini wakati mbaya wenu kafa?
HIVI zinakutosha kweli? Kila unachoandika ni ugoro tu.
 
Ushaidi wa Leo ni wakupoteza muda. Kama hawakuchukua finger print, watathibitishiaje mahakama kama hiyo bastola ilikuwa ya Adamoo??
Kwani iliokotwa barabarani si alipatikana nayo yeye baada ya kukamatwa?
 
Maswali ya mahakamani bwana, be like

Wakili: Ulikula nini?

Shahidi: Nilikula ugali na dagaa.

Wakili: Unaweza kuelezea mahakama ulivyokula?

Shahidi: ndio, nilimega tonge.

Wakili: enhee ulimega kubwa dogo?

Shahidi: kubwa.

Wakili: enhee kilichofuata

Shahidi: nikaweka mdomoni.

Wakili: ndio, nini kikafuatia?

Shahidi: nikaanza kutafuna.

Wakili: baada ya kutafuna?

Shahidi: nikameza.

Wakili: lakini hukuelezea kama ulinawa.

Shahidi: ni kweli sikuelezea, lakini nilinawa.

Wakili: hukuelezea pia kama ulitoezea kwenye mboga.

Shahidi: ni kweli nilitoezea lakini nilisahau kusema.

Wakili: dagaa walikuwa wa mchuzi au wakavu?

Shahidi: wakavu, waliokaangwa.

Wakili: sasa mbona unatuchanganya? Unawezaje kutooezea tonge tena kubwa kwenye dagaa waliokaangwa?

Shahidi: sifahamu.

Jaji: usiseme hufahamu, sasa hufahamu una maanisha nini?

Shahidi: sikumbuki kama walikuwa wa mchuzi au wakavu.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Mahakamani kama unatoa ushahidi wa uongo, lazima wakutafute uingie kwenye 18 tu, la sivyo uwe very smart na mwenye kumbu kumbu sana, halafu kila unalojibu watarejea jibu lako baadae..
Lakini hata kumuangamiza mwenzio kisa uongo, malipo ni humu humu duniani tu.

Ndugu zangu tujifunze kwa hiki kinachoendelea, tusiwe waongo..

Lakini shahidi mkweli ni ngumu mno akatoa ushahidi wenye kuitia mahakama shaka, mkweli huiondoa mahakama shaka..

Ndugu zangu uongo ni mbaya sana, unaweza kukufunga na kukuteketeza kabisa, vitabu vyetu vya dini vinapinga na kulaani watu waongo..

Methali 19:9- Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa;asemaye uongo ataangamia
Cross examination isikie kwa mwenzio lakini siku umetinga mahakamani kwa kosa ambalo kila upande una wakili/mawakili utaomba ardhi ipasuke uzame uko,kumbe hapo Mhe.Jaji alikuwa anafuatilia kwa makini maswali na majibu ya wakili na shahidi,hadi pale shahidi aliposema SIFAHAMU Jaji akaingilia kati usiseme hufahamu sasa unamaanisha nini???Mataga na sukuma gang mpo maana hamkawii kusema wanauliza maswali ya kijinga ha,ha,ha,haaaaaaa
 
Kwani iliokotwa barabarani si alipatikana nayo yeye baada ya kukamatwa?
Polisi wanasema wamemkuta nayo, yeye anasema wamemuwekea. Sasa hapo Nani anasema ukweri?? Na kwanini polisi hawakuchukua finger print ili wapati kidhibiti kisichokua na Shaka?
 
Republic kwisha habari yake wanatuchosha ,daaa mungu wambinguni

Ninachoamini mbowe nimtu wakusameheee
 
Hapa nimekaa nikijiuliza kwa nini yule dhalimu mwendazake hakupiga marufuku matumizi ya lugha ya malkia, tazameni sasa legacy alioiacha baada ya kusalimu amri kwa COVID-19! Orodha ya matopolo aliyoiacha kwa kweli inachefua.

Akitoka magu2016, anaingia Crimea, akitoka Crimea, anaingia zandrano, akitoka zandrano anaingia Omulasil, akitoka Omulasil anaingia wa ukae, akitoka wa ukae anaingia Dong Jin...yaani orodha ya takataka tupu, wamezolewa wapi hawa?

Hebu tujikumbushe aliyonena Baba wa Taifa Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, nanukuu, "Sisi Watanganyika, tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau

Halafu wapo wanaosingizia lugha wakidai Kiswahili kumbe hata Kiswahili chenyewe nacho tabu tupu. Ndugu zangu Watanzania, hii laana tunaimalizaje? Tumefikaje hapa tulipo? Taifa letu linachekwa hadi na viinchi tulivyosaidia kuvikomboa?
 
Mkuu Mag3 kwanza habari ya siku nyingi?

Mkuu umetaja yale majina ya member kwa hasira kisha ukamnukuu Mwalimu na ukahitimisha post kwa masikitiko. Itoshe tu kusema kwamba inasikitisha na kushangaza!
 
Hii nchi hakika viongozi wala wasimamizi wa mahakama huwa hawapati akili, kama hawa ma Judge wa hii kesi (Aliejitoa na Huyu Alikuwepo Sasa).

1) Wanasahau kwamba maisha hubadilika. Leo unaemkandamiza pengine kesho mungu anaweza akampa mamlaka juu yako.

2) Kuna maisha baada ya vyeo.

3) Kuna kudharaulika na kuharibu sifa zao za kazi waliozifanyia juhudi kwa miaka mingi, pengine maisha yao yote.

4) Mungu yupo, anaona na anajua kila kinachofanyika.
Ndo maana wanajitoa... Huyu Jaji wa sa hivi naye atajitoa very soon!
Mtu timamu hawezi kusikiliza na kusimamia maagizo toka juu ya kipuuzi kiasi kile!
Ushiriki wa jina la Sabaya na uwepo wa mashahidi waongo kwenye hii kesi ni uthibitisho kuwa:
✓Tuhuma zote ni haramu!
✓Mbowe na wenzake si magaidi!
✓Shahidi namba 2 ni mhujumu uchumi aende aliko Sabaya!
✓Mashahidi toka PT ni zero brainers!
 
Ndio maana Watanzania wote tunataka Sheria zetu zote zitafsiriwe kwa lugha yetu ya Kiswahili, Pia Mwenendo wa kesi pamoja na Hukumu ziwe zinaandikwa kwa Lugha ya Kiswahili.
karibu 99%ya watanzania wote tunazungumza na kuandika lugha ya kiswahili lkn cha kushungaza Mahakama zetu bado zimekumbatia mfumo wa kikoloni wa matumizi ya kizungu!!
kwani kulikuwa na haja gani kumuuliza swali kwa kizungu?
angemuuliza kwa Lugha yetu ya Taifa hata mkulima wa kijijini angemjibu.
Wapo wakulima vijijini wanajitambua vizuri sana!
Ishu ni polisi wamejazana ma zero brainers!
 
Huyu Njagu kasoma mpaka Botswana huko lakini bado ni koplo wengine form four harafu duala ila wana nyota inakuaje..
 
Yaani Waafrika ni shida tupu. Yaani Mwaafrika akishindwa kuelezea maana ya kiingereza inakuwa ni kicheko na inaanzishiwa thread hapa JF!! Ujinga mtupu!
Tatizo katumia muda mwingi kusema kasoma mpaka Botswana kwenye mambo ya vilipuzi ni mtaalamu mbobezi ina maana huko Gaborone alikua anaongea kizigua chetu asijue hata maana ya utalii kwa kimalkia..
 
Back
Top Bottom