Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Hivi jamani mbona kama mimi sijaelewa au nyie mmelewa vipi shahidi namba 3 anasema kaanza kazi 2013 na uko elfu 2004,2006 sijui kasoma kozi za mambo ya bunduki zanzibar na mambo mengine mara sijui 2010 kasomaje hayo mambo wakati kazi kaanza 2013?
Sasa hapo huelewi nn, kwani kozi na kazi inaanza nini
 
Barua iliyoambatanishwa na vithibitisho hailandani na report ya afande....

Barua inasema ufanyie uchunguzi hivyo vitu, yeye report yake inasema conspiracy to commit terrorism.
IGP alisema kuna ushahidi wa kutisha katika kesi hii. Nadhani tunaanza kuamini sasa.
 
Hii kesi ni ya kimkakati, ya kumvua nguo "mtu fulani', ambaye hayupo kwa sasa, wa kuelewa na aelewe
 
Tatizo katumia muda mwingi kusema kasoma mpaka Botswana kwenye mambo ya vilipuzi ni mtaalamu mbobezi ina maana huko Gaborone alikua anaongea kizigua chetu asijue hata maana ya utalii kwa kimalkia..
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
 
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
Kama hujui kitu kwanini ukitumie, angeandika tu kwa kiswahili, lakini kuandika kitu ambacho hujui maanake huo ni uzuzu.
 
Mawakili wa utetezi mbona maswali yenu butu
 
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
kumbuka yuko mahakaman akitoa ushahidi wa kile alichokiandika, sasa kama hujui ulichokiandika unaenda kutoa ushahidi wa kitu gan? mahakaman sio bar ujue
 
Polisi wanasema wamemkuta nayo, yeye anasema wamemuwekea. Sasa hapo Nani anasema ukweri?? Na kwanini polisi hawakuchukua finger print ili wapati kidhibiti kisichokua na Shaka?
Wanapima sijui kitako,mara mm...sijui Bore nini nini huko..Inakera.. Kesi ya Kipuuzi kama Polisi wenyewe walivyo wapuuzi..
 
Refa kuibeba timu yenye uwezo duni ni kazi kubwa Sana, aidha ajitoe au akubali kupopolewa.
 
Mashahidi wanapigwa na vitu vizito kichwani hadi wanajuta
 
Askari polisi anaejiita mtaalamu wa sikaha hajui kutofautisha kati ya tourist na terrorist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ