Yaliyojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi - Sept 17, 2021

Yaliyojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi - Sept 17, 2021

View attachment 1941718
Leo Mahakamani

Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini Mabalozi na wawakilishi wengine wa Mashirika makubwa ya dunia , wanaacha shughuli muhimu maofisini mwao na wakati mwingine wanatelekeza usingizi vitandani mwao ili wawahi Mahakamani kusikiliza kesi ya Mbowe ?

Kumbuka kwamba orodha yote ya Magaidi wa zamani na wapya wadau hawa wanayo , lakini jina la Gaidi Mbowe halimo , sasa wanashangaa kuona kumbe nchi hii inao Polisi makini kiasi hiki hadi kumvumbua gaidi ambaye dunia haikumuona !

View attachment 1941719

Ugaidi ni jambo la kuogopesha mno , unaweza kumsingizia mbaya wako jambo hili kwa vile amekushinda kila kitu , kakushinda kwa hoja , kakushinda kwa ushawishi , kakushinda kisiasa na kiuchumi ili umkomoe , lakini waweza kuharibu taswira ya nchi vibaya mno ! Hawa wazungu wanafahamu kwamba MBOWE SIYO GAIDI bali wanataka kujionea umakini wa Serikali ya Tanzania ili wajiridhishe na kuchukua hatua

View attachment 1941721
wanafuatilia pesa walizo mpatia mbowe ili wachafue hali yahewa ya nchi hii imekuwaje ameshindwa? na lazima azitapike mbowe hela za mabeberu na hawatakubali mahakama ikimuachia huru
 
Hakuna kazi ngumu kama kutetea uongo. Baada ya uhuru Mwl Nyerere alipoona ni vigumu sana kutetea uongo kwenye mahakama zenye majaji wenye kujitambua na waliokuwa wakiamini katika haki ndipo alipoamua kuanzisha ile sheria kandamizi ya kuweka watu kizuizini bila ya kuwafikisha mahakamani.

Watawala wa sasa kwa kujua kabisa aina ya majaji waliowateua pamoja na sifa zao, wanakuwa na ujasiri wa kutunga kesi ya uongo tu na kumburuza mtu mahakamani kwa kujua kwamba wataitumia mahakama kupindisha sheria ili kukidhi matakwa yao ya kisiasa.

Ila ukweli utajulikana kwani hii "kesi" inafuatiliwa sana ndani na nje ya nchi.
Let us be patient.
 
habari ndio kama unavyoona
TUKIWA_MAPUMZIKONI.%0A%0AAdv._Peter_Kibatala_akiteta_kidogo_kwa_lugha_ya_Buckingham_na_moja_ka...jpg
 
One wonders, why take too long for the trial to commence? Or maybe there is a "Liaison" going on between the court and the prosecution side to have the former throw in the towel so as to save the regime from further ignominy. It's just my supposition.
 
Hakuna kazi ngumu kama kutetea uongo. Baada ya uhuru Mwl Nyerere alipoona ni vigumu sana kutetea uongo kwenye mahakama zenye majaji wenye kujitambua na waliokuwa wakiamini katika haki ndipo alipoamua kuanzisha ile sheria kandamizi ya kuweka watu kizuizini bila ya kuwafikisha mahakaman...
Umetupa background nzuri ya historia ya Mahakama zetu.
 
Duuh, hebu fikiri kwa sauti kubwa kidogo, kwamba;

1. Mawakili upande wa mashitaka waliomba kesi ianze mapema saa 4abh, Jaji/mahakama na mawakili wa utetezi wakasema, SAWA NA IWE HIVYO....
Walikuwa kwenye kikao na jaji cha namna ya kupindua matokeo
 
Mliopo Mahakamani, Vipi leo mmeruhusiwa kuingia na Simu zenu? Au Laptop?
 
One wonders, why take too long for the trial to commence? Or maybe there is a "Liaison" going on between the court and the prosecution side to have the former throw in the towel so as to save the regime from further ignominy. It's just my supposition.
I am in a remote area, how is it going? has the trial commenced since you last posted?
 
Hali ya ndani ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa ni shwari

Leo tumepita getini bila bugudha na hakuna polisi wa nje zaidi ya hawa maalum wa mahakama

Hakika Jambo la jana kupigania haki ya mahakama na kutaka isimame kama mhimili huru ni nzuri sana

Jopo la mawakili wetu wa utetezi (mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake) kama kawaida yao, limefika on-time, Mapema sana ikiwa sifa yake kuu nidhamu, Ushirikiano, upendo na kwenda na muda, pia kusikiliza na kujali hisia na sauti za ndugu, jamaa, marafiki wa wateja wao (watuhumiwa)

Ndugu zangu mnaouliza kuhusu shahidi wa leo ni nani, hakika wasikilizaji hatuwezi kufahamu. Hiyo ni kazi ya Jamhuri kuwasilisha jina la shahidi wao mbele ya mahakama kati ya wale mashahidi 24 waliotajwa kwenye preliminary hearing...

Hivi sasa ni saa 4 asubuhi na dakika zake 19 kwa saa za Afrika ya mashariki, bado mheshimiwa Jaji na mawakili wa upande wa Jamhuri (serikali) hawajaingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa. Mahakama sasa imejaa TOP!

Pia, tunawashukuru jeshi la polisi kutoka moyoni kabisa, mmepungua ndani ya chumba cha mahakama, mbarikiwe.. Eeh! Mmeona watu wameingia wenyewe mahakamani, wamejipanga wenyewe na sasa wanasubiri mahakama ianze. SISI ni wastaarabu na tunahubiri ustaarabu kila siku #MboweSioGaidi

Hivi sasa ni saa 4 na dakika 25 saa za Afrika ya mashariki bado mawakili wa serikali na mheshimiwa Jaji hawajaingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa..

Pamoja na kwamba polisi leo sio wengi kama siku zote, lakini kuna mzozo umeibuka hapa Mahakamani. Wananchi wanasema wamekosa nafasi za kuketi, hivyo wanaomba askari polisi wapungue mahakamani, wakaimarishe ulinzi wa raia na mali zao, ili nafasi zipatikane nyingi. Bado wapo!

Askari mmoja hapa anahamaki na kusema polisi na usalama nao wanayo haki ya kusikiliza mwenendo wa kesi maana ni open court na wanahoji kwamba tunapata wapi haki ya kuipangia mahakama nani wa kuingia na kukaa ndani? Swali hilo ukiwauliza wao kwanini walituzia jana, hawana jibu?

Raia bado wanasisitiza askari wasimame na kupungua mahakamani ndani, walinde watu na mali zao, ili wananchi wapate nafasi ya kuketi. Wananchi wanawakazia macho na kuwatambua. Lakini tunawaeleza wananchi watulie, waache askari hao wafuatilie kesi. Wasipate sababu kwamba VURUGU..

Hivi sasa ni saa 4 na dakika 53 kwa saa za Afrika ya mashariki, bado kesi inayowahusu Freeman Mbowe na wenzake watatu haijaanza, tunamsubiria mheshimiwa Jaji na mawakili wa serikali waingie ndani ya chumba cha mahakama.
Hivi sasa ni saa 5 na dakika zake 6 saa za Afrika ya mashariki.

Hali ya eneo la mahakama ni shwari kabisa, ni kata ya Sinza, wilaya ya Ubungo, Mkoani Dar es Salaam

Hali ya hewa ni mawingu kiasi na nyuzi Joto 27.7 inayoruhusu kabisa shahidi kuendelea na kesi, bila visingizio!

Pamoja na mheshimiwa Jaji kusisitiza Jana kuwa kesi ianze leo saa 4 kamili Kufuatia ombi la mawakili wa serikali, Lakini mpaka sasa, ni 5 na dakika 15 kesi bado haijaanza, lakini hatuelewi, labda sababu zilizo nje ya uwezo wao. Tuendelee kuwa na subira, maana yavuta kheri..

Mstari wa pili kutoka mwisho, wameketi waandishi wa habari (leo tupo nao live), Wameingia Kwa wingi sana kuliko Siku zote (inspiration), Leo na wao wamenufaika na msimamo wa Jana. Wabarikiwe.

Mstari wa mwisho (Backbench) wameketi watu mchanganyanyiko wakiwepo Polisi na TISS.

Sema kwa sauti mbowe sio gaidi

Unpopular opinion: wewe unadhani kwa kuchelewa huku mawakili wa serikali kuingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Je, wanamshauri DPP aachane na hii kesi dhidi ya Freeman Mbowe na wenzake maana wanajua #MboweSioGaidi, namna gani?

Jopo la mawakili wa utetezi

1.Peter Kibatala
2.Jeremiah Mtobesya
3.Jonathan Mndeme
4.John Malya
5.Evaresta Kisanga
6.Hadija Aron
7.Maria Mushi
8.Gaston Garubindi
9.Seleman Matauka
10.Ferdinand Makore
11.Dickson Matata
12.Rita Ntagazwa
13.Alex Masaba
14.Michael Mwangasa

Habari njema sana, ule mtiti mdogo wa wananchi umesaidia benchi lilikuwa reserved kwa makarao, wameanza kukaa familia na ndugu wa watuhumiwa..

Ubishi na makavu yanasaidia sana.. Tusiache kuongea na kupiga kelele kuhusu haki zetu wakati wote ndugu zangu. Msiache kuongea.


Jopo la mawakili wa utetezi (wanaitwa mawakili wasomi, utake usitake), yaani mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake wakijadiliana jambo la kitaalam.. Unaweza kuwapa jina, hebu pendekeza jina, hii timu yao inapaswa kupewa jina gani?

Pamoja na kwamba watuhumiwa wamefikishwa mapema (tangu saa 3 asubuhi) na mawakili wa utetezi kufika mapema ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi, bado mawakili wa serikali hawajafika. Hivi sasa ni saa 5 na dakika 29 saa za Afrika ya mashariki

Shukrani za pekee leo zimuendee Wakili Gabriel Fikirini ambaye kafika mahakamani kwa mara ya kwanza akisafiri kutokea Jijini Mwanza kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kesi ya Freeman Mbowe na na wenzake..

Wakili Deogratius Mahinyila (@AdvMahinyila) aliyetoka Jijini Dodoma hadi Dar es Salaam kuongeza nguvu tangu wiki iliyopita.. Niliwapa simulizi yake kwa ufupi, niwape tena? Umri wake ni mdogo mara 3 ya umri wa Humphrey Polepole na mara 5 ya umri wa Mzee Kabudi.

Wakili Deogratius Mahinyila (@AdvMahinyila) atakumbukwa akiwa mgombea wa udiwani kupitia Chadema Dodoma, kata ya Berega, alishitakiwa kwa makosa uhujumu uchumi, akiwa gerezani, Isanga (gereza katili) akafanya mitihani ya uwakili na kufaulu kuwa wakili wa mahakama kuu.
Tuwaite human rights elites
 
wanafuatilia pesa walizo mpatia mbowe ili wachafue hali yahewa ya nchi hii imekuwaje ameshindwa? na lazima azitapike mbowe hela za mabeberu na hawatakubali mahakama ikimuachia huru
Damu ya Yesu Ikusaidia !Una shida Kwenye Maisha yako.
 
Back
Top Bottom