Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Unaumia na nini kwani mpaka unasema yooote hayo? njaa mbaya sana wewe utakuwa ni wale wabunge wa chadema waliokosa ubunge 2020
Point of correction hakukuwa na uchaguzi mwaka 2020 bali ilikuwa uchafuzi ila Mungu fundi kabisa kabisa jina lake lihimidiwe
 
Kibatala: Uliwakamata na Kifaa gani kinachohusisha Kukata Miti

Shahidi: Sikuwakamata na Kifaa chochote
ha ha ha ha, Kingai hapa ulitakuwa umkamate Adamoo na shoka kubwa ile ya kukatia miti ya Mninga, mahakama haifanyi kazi kwa kuhisi, haipigi ramli mzee wangu, inataka kitu live live - lete shoka babaaa ama misumeno
 
Hili ni tatizo la kisiasa zaidi kuliko sheria, utatuzi wake utaegemea siasa zaidi kuliko ushahidi wowote ule wa kisheria.
 
ha ha ha ha, Kingai hapa ulitakuwa umkamate Adamoo na shoka kubwa ile ya kukatia miti ya Mninga, mahakama haifanyi kazi kwa kuhisi, haipigi ramli mzee wangu, inataka kitu live live - lete shoka babaaa ama misumeno
Hii kesi ukiisikiliza tu hata kama huna idea ya sheria unaielewa na maamuzi unayatoa hapohapo
 
tuendelee kuiamini serikali yetu kama ilitenda haki kwa Sabaya hata hapa naamini haitatuangusha...
 
Hii kesi ipo very technical kwenye baadhi ya maeneo shahidi aliposema alifukuzwa kazi kwa sababu za ugonjwa wa kichaa upande wa utetezi wajitahidi wapate hicho kielelezo waje wakitumie kwenye utetezi
Utimamu wa akili kwa shahidi hauna Mana kwa maelezo aliyotoa sababu aliachishwa kazi baada ya kuonekana ana matatizo ya akili pia alipokuwa sawa ndo akapata Hilo deal la mbowe hvyo hata cheti Cha uthibitisho kipatikane au kikosekane kwenye hayo mazingira ya kesi hcho cheti hakina maana.
 
duh, aisee kazi ipo - Kingai umeyatafuata haya !! Mwambie Jaji huna kifaa cha kupimia DNA ya vitu vyenye ncha kali - ha ha ha ha
 
Mawakili wa utetezi kesi ya mbowe wanatafuta credit kwa MAJORITY'S badala ya kutafuta credit kwa JAJI ambae ndio mwamuzi wa kesi yenyewe.

Hivyo hvyo wafuasi wa upande wa utetezi wanashupalia ushabiki ambao hauna mantiki kwenye kesi wanaacha maswala ya msingi kwenye kesi.

Nimeona mengi mno kwenye kesi ya sabaya na hii ya mbowe watu wanajikitika kwenye maswali na maelezo ambayo sio msingi wa kesi hvyo hayana maana.

Nipo hapa nafatilia taratibu.
 
Ulikuwepo mahakamani kinuji au nikunifariji kwa kazi yenu ya ubambikiaji tu.
 
Uelekeo wa kesi haupimwi kwa namna hiyo, kuwepo kwa Mwenyekiti sio kila mara kunatoa tafsiri kuwa utaratibu ulifuatwa, nakumbuka mwaka 2015, nikiwa mahakama ya wilaya ya Bukombe. Polisi waliwaleta watuhumiwa wa ujangili wakiwa na nyara za serikali, silaha pamoja na magunia kadhaa ya bangi kama ushahidi.

Polisi waliokuja mahakamani kama mashahidi walieleza kuwa utaratibu wote ulifuatwa, zoezi la upekuzi lilifanyika kwa kumshirikisha mwenyekiti wa kijiji, ila wakati wa "cross examination" kuna askari mmoja aliulizwa ni namna gani waliingia kwenye nyumba ya watuhumiwa, ila kumbuka mashahidi wote waliotangulia walisema walifuata utaratibu na walifunguliwa, lakini askari wa mwisho alisema kuwa waliwaomba watuhumiwa wafungue mlango wakagoma, ndipo yeye alipovunja mlango na kuingia.

Sasa ukiangalia mtiririko wa ushahidi japo walijipanga kwa kuwaleta mashahidi kibao, ila waliteleza sehemu ndogo iliyoharibu kesi kwa upande wa serikali, kesi za jinai unaweza kuwa una kila aina ya ushahidi lakini upande mwingine ukiweza kuonyesha shaka dogo ushahidi wote unakuwa hauna maana kabisa. safari bado ni ndefu ni mapema mno kutabiri mwelekeo wa kesi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…