Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

asante ITV na wana JF wote...weekend hii .tangu jana usiku burudani saaafiii kabisa..... naongeza sekunde za maisha ....kuna watu na binadamu
 
naona unalima majaluba baada ya kupata ulabu teh teh teh, ulabu ukikutoka na kurudia ufahamu wako kwamba haujalima wala wewe si mkulima, urejee post 446.

You are a wasted talent, hukuwepo kwenye mjadala ukaishia kuhama toka kwa jirani mmoja hadi mwingine kufuata TV, bwa ha ha ha haaaaaaa.
let me break down mabishano yetu:-
A) mimi ni mkulima ambae kuona umuhimu wa hili kongamano na kutaka kujua suala la katiba linalomuhusu kila mtu nikaamua leo niangalie kwenye TV.... ambapo Tanesco kwa kutokuwajibika wakakata umeme... sikufa moyo nikahamia kwa majirani nikaangalia kidogo mpaka ITV walipokata.....
B) Nikaona kwamba kama wanahabari wetu wangekuwa Sharp hii kitu wangeirekodi na kuirusha youtube haraka haraka hata ndugu zetu wa nchi za nje na wasio na TV karibu wangeweze kuona (lakini si hivyo na wewe ukawatetea kwamba sio kazi yao nifanye mwenyewe)
C)Katavi akasema kina dada hawakuchangia wametuangusha.... Wewe ukasema kuna kina dada wakali... na mimi nikajibu ukali wa vitabuni haumsaidii mtu... leo ndio kulikuwa kuna vita kwahiyo wenyewe wanangoja tukipata katiba ndio wachangie?

In short ndugu yangu SPECIALIZATION kila mtu anabidi awajibike ili tuweze kukuza UCHUMI wetu mimi talima Tanesco watupe umeme... ITV, TBC na Wanahabari watupe HABARI...., sijui wewe mwenzetu unachangiaje huu Uchumi wetu
 
That is a psychology of public speaking,its called establishing rapport. Ili usikiliwe si lazima kama alivyofanya yule Dada Nkya kuwa shhhhhhh (shutup) watu. Issa Shivji ana uzoefu and he knows how to establish rapport. That's why he repeated that word twice in few seconds, it was simply to attract attention.

Usiwachanganye ambao hawakuuona live mdahalo, Mama Nkya alipopewa mic alianza kuongea na alikuwa hasikiki ukumbini, sisi tulio kuwa kwenye luninga sauti ilisikika vizuri, hivyo alikuwa ana test microphone kwa kutamka ...halo..halo... shhhh... alipojisikia kwenye speaker za ukumbini akaendelea.
 
Kwa ujumla wazungumzaji wamechambua katiba kwa ufasaha ingawa kuna wachangiaji ka wawili waliboa washiriki mpaka wakazomewa! Nampongeza sana Dr Lwaitama kwa mchango wake wa kina.
 
Kwa ujumla wazungumzaji wamechambua katiba kwa ufasaha ingawa kuna wachangiaji ka wawili waliboa washiriki mpaka wakazomewa! Nampongeza sana Dr Lwaitama kwa mchango wake wa kina.



Nami nawapongeza wote ila kwa muda mwingine sidhani kama viongozi ambao tunahitaji wajirekebishe au mtu ambae kwa namna yoyote anazungumziwa asiwepo kama leo aliposhiriki waziri wa katiba na sheria hadi kafadheheshwa kwa kuzomewa
 
Kitila Mkumbo,

Kazi nzuri sana, mmeonesha mwamko wa hali ya juu katika hili swala la katiba. Mjadala kama huu urudiwe na wachangiaji wachujwe ili kuwe na uelekeo unaoeleweka. Pia mtoke na roadmap ili katiba ibadilishwe. Hivi yule waziri wa katiba nk nk alikuwepo?

Alikuwepo - Celina Kombani, tena wamemchapa live alichokitamka kuwa ...hakuna pesa za kuandika katiba... na ..alikuwa anatikisa kiberiti...! Wakamwambia ameona kimejaa. Ila alionekana anaona aibu kwa matamshi yake ya awali, hatarudia kuropoka upuuzi siku nyingine kabla ya kuwasiliana na bosi wake!
 
Nachukua muda huu kumshukuru Dr Kitila kwa kutuanzishia post hii ambapo kutokana na mimi kuwa mbali nimeweza kupata habari kupitia wana JF wenzangu. Pia nawashukuru UDASA kwa kuandaa Kongamano hili. Nawashukuru Prof Issa na Jenerali kwa uchambuzi na hotuba zao kali na za kutufikirisha hadi leo tumeondoka na "kitu kizima" kuhusu Katiba. Kwa ufupi nimeweza kuona mawazo ya watu kuhusu katiba mpya, mambo muhimu yanayohitajika na ni namna gani tuyafikie. Mjadala kwangu umeibua hoja nzito na imani potofu kwa bunge letu tukufu kwamba pengine haliwezi kutoa haki kwa watanzania wote hasa kwa mfumo wa sasa ambao ni sawa na chama kimoja CCM tu ndani ya Bunge. Basi hili linadhihirisha na Prof Shivji amesema, Bunge haliwezi kuleta katiba, Rais na tume yake haviwezi, maana Tume inaripoti wapi? Sasa mapendekezo ya Dr Slaa ni mwafaka wa Katiba ya Wananchi.

Jenerali naye kaja na jipya, jina la nchi yetu ni tata!! Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na SIYO Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, Prof Shivji, Ujamaa na kujitegemea, neno limechakachuliwa ndani ya katiba. Thanks alot and good day!
 
huo mstari umesimama!

naunga mkono huo mstari,kwa UD bila migomo na maandamano,aaah hakuna kitakachojiri,huyo DR Kitila alivokua mwanafunz alikua kiongoz wa daruso+alianzsha migomo na maandamano,hvo ni vpande vya koz za udsm
 
Oh! Katavi na wenzako nawashukuru sana kwa kutumia fursa hii ya technohama katika kutufikishia ujumbe kutoka Nkrumah. Mie nilikuwa kitandani nimepozi lakini nimefuatilia hasa kulingana n apost zenu. Nawashukuru pia wazazi/walezi waliowapeni elimu hiyo. Thanks alot and keep it up!
 
Uko too general, unamaanisha kusoma na kuandika kiswahili tu au lugha zote.

Hata kiswahili wapo wengi wasiojua kusoma wala kuandika. Kwani dhana ya kisomo cha watu wazima ilifishwa na nani? Mbona mie nilikuwa nashiriki hata kutunga nyimbo za kuimba siku ya Kisomo tarehe 8/9;kila mwaka?
Hayo sio maneno yangu ni Prof. Shivji, na alikuwa anaelezea mfano ambao alikutana na mtu mmoja kwenye daladala na akamuuliza juu ya ufahamu wake wa masuala ya katiba, akamjibu kuwa hajui masuala ya katiba kwa sababu hajui kusoma wala kuandika. Ndipo prof Shivji akatoa kauli hiyo hapo!
 
Kuna jamaa kanifurahisha sana. Anadai tuepuke njia rahsi na nyepesi kuda katiba. Nchi yoyote ile yenye maendeleo imepita kwenye misuko suko na umwagaji damu. Awali Mabere Marando alisema katiba ilishaanza kuandikwa kwa umwagaji damu Arusha.

Hakuna kubembelezana hapa suala ni katiba mpya yenye kushirikisha wananchi.

Katiba nzuri inaandikwa pale nchi inapokuwa imepitia kwenye amani na BUMPS,... in short kama nchi haitaingia kwenye bumpy-stage katiba haitakuwa NZURI sana, MAANA ITAKUWA ni ya state ya amani tu..sasa in case nchi ikapata rabsharabsha za mvurugano kidogo katiba inakuwa bubu, na matokeo yake watu wanaanza kujitamkia vitu vya kufanya hovyohovyo kwa kukosa mwongozo mama!...
Nimesema toka mwanzo kuwa katiba ya South Africa ndiyo katiba bora kabisa kwa karne hizi KWA Africa,ni kwa msingi wa hoja yangu ya hapo juu!
 
Jamani wana JF Prof Shivji ameongea kwenye kongamano leo kwamba kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni ni hatari kwani CCM watachukua advantage ya uwingi wao bungeni kuikwamisha,does it make sense,kweli bado tuna bunge la watu wa kujali maslahi ya chama,naomba michango kwa hili.
 
Akhsante sana Dr Mkumbo! kwa kweli kilichofanyika leo ni cha kihistoria!!!


tumejifunza sana! hata sisi wa huku dodoma!

tafakuri iliyobaki ni kwamba je UDASA wanaweza kushirijkiana na academic association zetu katika vyuo vyoooote vilivyobaki, viwe vya uma na sio vya umma ili kusambaza impact nchi nzima?

YOU HAVE BEEN A HERO!

God Bless you!
 
vipi wakuu kuna mwenye audio au video yeyote anayeweza kutusaidia sisi wazalendo.......?
 
Katiba inayomfanya mtu mmoja kuwa Mungu mtu haifai----Bw. Rugazia.
Mfano msamaha anaotoa rais kwa wafungwa........du!!
jamaa alikuwa na maana pale rais anapoingilia na kusamehe watu wengine hata kabla ya kufikishwa mahakamani, nadhani ni kama mafisadi waliporuhusiwa kurudisha fedha walizoiba kinyemela na kila kitu kikaishia hapo.
 
Ni kweli marekebisho au utungwaji upya wa katiba hauendani na kutaka kuiondoa CCM madaraka wanancho wote wanatambua kuwa CCM imetangazwa kuwa mshindi na tume ya Uchaguzi ,hivyo mabadiliko ya Katiba yataendana kuondoa kile kilichomuweka CCM na kutafuta njia mbadala ya kuweka mtangazaji asiependelea upande wowote yule na pia awe mwenye kutenda haki na kuweka wazi kila kitu.

Another up for mwiba thanx
 
Back
Top Bottom