Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

asante ITV na wana JF wote...weekend hii .tangu jana usiku burudani saaafiii kabisa..... naongeza sekunde za maisha ....kuna watu na binadamu
 
let me break down mabishano yetu:-
A) mimi ni mkulima ambae kuona umuhimu wa hili kongamano na kutaka kujua suala la katiba linalomuhusu kila mtu nikaamua leo niangalie kwenye TV.... ambapo Tanesco kwa kutokuwajibika wakakata umeme... sikufa moyo nikahamia kwa majirani nikaangalia kidogo mpaka ITV walipokata.....
B) Nikaona kwamba kama wanahabari wetu wangekuwa Sharp hii kitu wangeirekodi na kuirusha youtube haraka haraka hata ndugu zetu wa nchi za nje na wasio na TV karibu wangeweze kuona (lakini si hivyo na wewe ukawatetea kwamba sio kazi yao nifanye mwenyewe)
C)Katavi akasema kina dada hawakuchangia wametuangusha.... Wewe ukasema kuna kina dada wakali... na mimi nikajibu ukali wa vitabuni haumsaidii mtu... leo ndio kulikuwa kuna vita kwahiyo wenyewe wanangoja tukipata katiba ndio wachangie?

In short ndugu yangu SPECIALIZATION kila mtu anabidi awajibike ili tuweze kukuza UCHUMI wetu mimi talima Tanesco watupe umeme... ITV, TBC na Wanahabari watupe HABARI...., sijui wewe mwenzetu unachangiaje huu Uchumi wetu
 

Usiwachanganye ambao hawakuuona live mdahalo, Mama Nkya alipopewa mic alianza kuongea na alikuwa hasikiki ukumbini, sisi tulio kuwa kwenye luninga sauti ilisikika vizuri, hivyo alikuwa ana test microphone kwa kutamka ...halo..halo... shhhh... alipojisikia kwenye speaker za ukumbini akaendelea.
 
Kwa ujumla wazungumzaji wamechambua katiba kwa ufasaha ingawa kuna wachangiaji ka wawili waliboa washiriki mpaka wakazomewa! Nampongeza sana Dr Lwaitama kwa mchango wake wa kina.
 
Kwa ujumla wazungumzaji wamechambua katiba kwa ufasaha ingawa kuna wachangiaji ka wawili waliboa washiriki mpaka wakazomewa! Nampongeza sana Dr Lwaitama kwa mchango wake wa kina.



Nami nawapongeza wote ila kwa muda mwingine sidhani kama viongozi ambao tunahitaji wajirekebishe au mtu ambae kwa namna yoyote anazungumziwa asiwepo kama leo aliposhiriki waziri wa katiba na sheria hadi kafadheheshwa kwa kuzomewa
 

Alikuwepo - Celina Kombani, tena wamemchapa live alichokitamka kuwa ...hakuna pesa za kuandika katiba... na ..alikuwa anatikisa kiberiti...! Wakamwambia ameona kimejaa. Ila alionekana anaona aibu kwa matamshi yake ya awali, hatarudia kuropoka upuuzi siku nyingine kabla ya kuwasiliana na bosi wake!
 
Nachukua muda huu kumshukuru Dr Kitila kwa kutuanzishia post hii ambapo kutokana na mimi kuwa mbali nimeweza kupata habari kupitia wana JF wenzangu. Pia nawashukuru UDASA kwa kuandaa Kongamano hili. Nawashukuru Prof Issa na Jenerali kwa uchambuzi na hotuba zao kali na za kutufikirisha hadi leo tumeondoka na "kitu kizima" kuhusu Katiba. Kwa ufupi nimeweza kuona mawazo ya watu kuhusu katiba mpya, mambo muhimu yanayohitajika na ni namna gani tuyafikie. Mjadala kwangu umeibua hoja nzito na imani potofu kwa bunge letu tukufu kwamba pengine haliwezi kutoa haki kwa watanzania wote hasa kwa mfumo wa sasa ambao ni sawa na chama kimoja CCM tu ndani ya Bunge. Basi hili linadhihirisha na Prof Shivji amesema, Bunge haliwezi kuleta katiba, Rais na tume yake haviwezi, maana Tume inaripoti wapi? Sasa mapendekezo ya Dr Slaa ni mwafaka wa Katiba ya Wananchi.

Jenerali naye kaja na jipya, jina la nchi yetu ni tata!! Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na SIYO Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, Prof Shivji, Ujamaa na kujitegemea, neno limechakachuliwa ndani ya katiba. Thanks alot and good day!
 
huo mstari umesimama!

naunga mkono huo mstari,kwa UD bila migomo na maandamano,aaah hakuna kitakachojiri,huyo DR Kitila alivokua mwanafunz alikua kiongoz wa daruso+alianzsha migomo na maandamano,hvo ni vpande vya koz za udsm
 
Oh! Katavi na wenzako nawashukuru sana kwa kutumia fursa hii ya technohama katika kutufikishia ujumbe kutoka Nkrumah. Mie nilikuwa kitandani nimepozi lakini nimefuatilia hasa kulingana n apost zenu. Nawashukuru pia wazazi/walezi waliowapeni elimu hiyo. Thanks alot and keep it up!
 
Hayo sio maneno yangu ni Prof. Shivji, na alikuwa anaelezea mfano ambao alikutana na mtu mmoja kwenye daladala na akamuuliza juu ya ufahamu wake wa masuala ya katiba, akamjibu kuwa hajui masuala ya katiba kwa sababu hajui kusoma wala kuandika. Ndipo prof Shivji akatoa kauli hiyo hapo!
 

Katiba nzuri inaandikwa pale nchi inapokuwa imepitia kwenye amani na BUMPS,... in short kama nchi haitaingia kwenye bumpy-stage katiba haitakuwa NZURI sana, MAANA ITAKUWA ni ya state ya amani tu..sasa in case nchi ikapata rabsharabsha za mvurugano kidogo katiba inakuwa bubu, na matokeo yake watu wanaanza kujitamkia vitu vya kufanya hovyohovyo kwa kukosa mwongozo mama!...
Nimesema toka mwanzo kuwa katiba ya South Africa ndiyo katiba bora kabisa kwa karne hizi KWA Africa,ni kwa msingi wa hoja yangu ya hapo juu!
 
Jamani wana JF Prof Shivji ameongea kwenye kongamano leo kwamba kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni ni hatari kwani CCM watachukua advantage ya uwingi wao bungeni kuikwamisha,does it make sense,kweli bado tuna bunge la watu wa kujali maslahi ya chama,naomba michango kwa hili.
 
Akhsante sana Dr Mkumbo! kwa kweli kilichofanyika leo ni cha kihistoria!!!


tumejifunza sana! hata sisi wa huku dodoma!

tafakuri iliyobaki ni kwamba je UDASA wanaweza kushirijkiana na academic association zetu katika vyuo vyoooote vilivyobaki, viwe vya uma na sio vya umma ili kusambaza impact nchi nzima?

YOU HAVE BEEN A HERO!

God Bless you!
 
vipi wakuu kuna mwenye audio au video yeyote anayeweza kutusaidia sisi wazalendo.......?
 
Katiba inayomfanya mtu mmoja kuwa Mungu mtu haifai----Bw. Rugazia.
Mfano msamaha anaotoa rais kwa wafungwa........du!!
jamaa alikuwa na maana pale rais anapoingilia na kusamehe watu wengine hata kabla ya kufikishwa mahakamani, nadhani ni kama mafisadi waliporuhusiwa kurudisha fedha walizoiba kinyemela na kila kitu kikaishia hapo.
 

Another up for mwiba thanx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…