Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu Mikoa ya Rukwa na Katavi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakuu leo tena yule Mgombea Urais pekee wa Tanzania asiye na kashfa yoyote ile anaendelea kuchanja mbuga kwenye mikoa ya Rukwa na Katavi , ambapo itapigwa mikutano minne na mkutano wa Mwisho utapigwa jioni kabisa Mpanda Mjini .

Kwa Taarifa za uhakika kuhusu kampeni za Tundu Lissu endelea kubaki hapahapa JF


========
UPDATES
Jimbo la Kwela na Nkasi Kaskazini
Picha za Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, katika Uwanja wa Kashato, Mpanda Mjini, Mkoa wa Katavi, ukiwa mkutano wa 3 kwa siku ya leo, Ijumaa, Septemba 18, 2020, baada ya
Chala (Nkasi Kusini) na Kilando (Nkasi Kaskazini), mkoani Rukwa.
Your browser is not able to display this video.

 
Thanks, picha za nyomi ya Rukwa please! Nasikia Sumbawanga walimpokea kwa saprise ya ajabu! Asanteni wanaRukwa!

Wana Sumbawanga washaamua wewe je unasubiri nini mtanzania - hii ndiyo nafasi pekee uliyonayo kulikomboa Taifa lako. UHURU - HAKI na Maendeleo ya watu viko mikononi kwako... saa ya ukombozi ni sasa.
 
Wanamuita "Beberu" na mwaka huu beberu hili lazima liwape mimba mbuzijike wa kijani!
Litaanza na yule "mbuzimsemakwelimpenziwamungu"

#Niyeye2020
 
Magufuli anapiga mikutano mpaka kumi na tano kwa siku. Lissu minne tena hapo amejitahidi sana. Sioni sababu ya kulalamika Magufuli akipata ushindi wa kishindo.
Kuna majimbo Magufuli anapiga mikutano mpaka minne. Lissu yeye anafanya mkutano mmoja tu.

Jimbo la nyamagana, Magufuli alifanya mkutano Igoma, national, buzuruga, mkuyuni na Buhongwa. Tar 28 Magufuli akipata kura zaidi ya 90% kuna mtu wa kushangaa wazee?.
Kwa ufanyaji mikutano wa lissu, je akipata kura chini ya 20% kuna watu watalalamika kua ameibiwa?.

Mpaka hapo munaweza kuona nguvu ya pumzi aliyonayo Magufuli. Kwakifupi Magufuli amemuacha mbali sana lissu.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kukaripia na kufundisha , Magufuli anakaripia na kupiga mkwara wapiga kura , Lissu anafundisha na kuomba kura
 
Hata akipiga 10 000 haituhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mikutano na matamasha.
 
Kupita Igoma ndo kufanya mkutano?acha kupotosha,salam na mkutano n vitu viwil tofaut
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…