Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Nifah

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2014
Posts
34,020
Reaction score
79,098
Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wa muziki Tanzania pamoja na ukanda wote wa Afrika Mashariki imewadia.

Tuzo hizi kwa mwaka huu zimepata msisimko mkubwa na hamasa ya mashabiki kupiga kura imeongezeka kuliko miaka yote tokea kuanzishwa kwa tuzo hizi.

Tuzo za mwaka huu zimekua zikichukuliwa na wengi kama 'kukata mzizi wa fitna' kwa wale mahasimu wawili wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambao ni Ali Saleh Kiba almaarufu 'King Kiba' na Naseeb Abdul almaarufu 'Diamond Platinumz'.

Tofauti na utoaji tuzo kwa wasanii na wanamuziki mbalimbali pia tuzo hizi zimekua zikipambwa na burudani za Live Music bila kuwasahau wachekeshaji ambao wamekua wakikonga nyoyo za mashabiki/wapenzi wa muziki na burudani.

Binafsi natamani kumuona Mpoki leo kama MC wa shughuli hii ya ugawaji wa tuzo ambae amekua kivutio kikubwa kutokana na ukosoaji/usifiaji wake ambao kwa wengine (hasa wasanii na wageni waalikwa) aligeuka kuwa mwiba mchungu kwa madongo yake.

Pia natamani kumuona mchekeshaji Frank Daganda.

Kwa taarifa za awali nilizozisikia ni kua yule msanii mchanga (underground) wa kike Ruby anayetamba na kibao chake matata 'Na Yule' leo atatumbuiza live.


Orodha ya wasanii waliongia katika kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Music Awards 2015:

MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA- KIUME
1. Mzee Yusuf
2. Christian Bella
3. Diamond Platnumz
4. Ally Kiba

MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA- KIKE
1. Vanessa Mdee
2. Khadija Kopa
3. Isha Mashauzi
4. Shaa
5. Dayna Nyange

3.MWIMBAJI BORA WA KIUME-TAARAB
1. Mzee Yussuf
2. Prince Amigo
3. Hassan Vocha
4. Hassan Ally
5. Mussa Kijoti

MWIMBAJI BORA WA KIUME- BONGO FLEVA
1. Ali Kiba
2. Ben Pol
3. Jux
4. Diamond
5. Belle 9

MWIMBAJI BORA WA KIUME- BENDI
1. Jose Mara
2. Kalala Junior
3. Khalidi Chokoraa
4. Chaz Baba
5. Nyoshi El Sadat

MWIMBAJI BORA WA KIKE- TAARAB
1. Khadija Kopa
2. Isha Mashauzi
3. Hadija Yussuf
4. Leyla Rashid
5. Fatuma Nyoro

MWIMBAJI BORA WA KIKE- BONGO FLEVA
1. Lady Jaydee
2. Vanessa Mdee
3. Linnah
4. Grace Matata
5. Malaika

MWIMBAJI BORA WA KIKE- BENDI
(Hakukuwa na washindani)

WIMBO BORA WA TAARAB
1. Hasid Hana Sababu – Hadija Yussuf
2. Lady With Confidence – Khadija
Kopa

WIMBO BORA WA MWAKA
1. Mwana – Ali Kiba
2. Nani kama Mama – Christian Bella
3. Gere – Weusi
4. Nitasubiri – Jux
5. Bongo Hip Hop – Fid

WIMBO BORA WA KISWAHILI (BENDI)
1. Otilia – FM Academia
2. Kiu Ya Haki – Mashujaa Band
3. Sauti ya Marehemu – Mapacha Watatu
4. Ganda la Muwa – Twanga Pepeta
5. Wale Wale – Vijana Ngwasuma

WIMBO BORA WA R&B
1. Nitasubiri – Jux
2. Unanichora – Ben Pol
3. Vitamin Music – Belle 9
4. Sisikii – Jux
5. Ni Penzi – Damian Soul

WIMBO BORA WA HIP HOP
1. Bongo Hip Hop – Fid Q
2. Mfalme – Mwana FA
3. Kipi Sijasikia – Proffesor Jay
4. Gere – Weusi
5. I See Me – Joh Makini
6. XO – Joh Makini

WIMBO BORA WA REGGA/DANCE HALL
1. Let Them Know – Maua
2. Mama Afrika – Warriors From The East
3. Maisha Magumu – Warriors From The East
4. Greeting For You – Ras Six
5. Tujimwage – Deddy

RAPA BORA WA MWAKA (BENDI
1. Ferguson
2. Msafiri Diouf
3. Sauti ya Radi
4. J4
5. Kabatano

MTUNZI BORA WA MWAKA- TAARABU
1. Mzee Yusuf
2. Thabit Abdul
3. Isha Mashauzi
4. Abdallah Fereshi
5. Hassan Ally

MTUNZI BORA WA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Ally Kiba
2. Diamond
3. Ben Pol
4. Barnaba
5. Jux

MTUNZI BORA WA MWAKA- BENDI
1. Jose Mara
2. Nyoshi El Saadat
3. Rogart Hegga Katapila
4. Hussein Jumbe
5. Richard Mangustino

MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP
1. Fid Q
2. Mwana FA
3. Joh Makini
4. Nikki wa Pili
5. Kala Jeremiah

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Nahreel
2. Man Water
3. Mesen Selekta
4. Tudd Thomas
5. Marco Chali

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- TAARAB

1. Enrico
2. Marlon Linje

MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA- BENDI

1. Allan Mapigo
2. Enrico
3. Said Comorien
4. Amoroso
5. Ababuu Mwana Zanzibar

VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA

1. Mdogo Mdogo – Diamond
2. Nitampata Wapi – Diamond
3. Mwana – Ally Kiba
4. Olethemba – Linah
5. Asante – AY

WIMBO BORA WA AFRO POP
1. Mwana – Ali Kiba
2. Mdogo Mdogo – Diamond
3. Niseme – Yamoto Band
4. Nitakupwelepweta – Yamoto Band
5. Kanyaboya – Mesen Selekta
6. Hawajui – Vanessa Mdee

WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA

1. Nani Kama Mama – Christian Bella
2. Basi Nenda – Mo Music
3. Nitampata Wapi – Diamond
4. Nasimama – Lady Jaydee
5. Historia – Lady Jaydee

.WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA

1. Waite – Mrisho Mpoto
2. Vuma – Vitalis Maembe
3. Tumetoka Mbali – Jagguar Music
4. Mama Shabani – Ifa Band
5. Omwana – B.K Sande

MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKIA
1. Baraka Da Prince
2. Beka Tittle
3. Afromaniac
4. Alice
5. Billnas

.WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/ KUSHIRIKIANA
1. Forever – Lady Jaydee ft Dabo
2. Mfalme – Mwana FA fr G-Nako
3. Kipi Sijasikia – Prof Jay ft Diamond
4. Kiboko Yangu – Mwana FA ft Ali Kiba
5. Kerewa – Shetta ft Diamond

BENDI BORA YA MWAKA
1. FM Academia
2. The African Stars
3. Mapacha Watatu
4. Mashujaa Band
5. Msondo Ngoma

KIKUNDI BORA CHA MWAKA- TAARAB
1. Jahazi Modern Taarab
2. Mashauzi Classic
3. Dar Modern Taarab
4. Five Stars
5. Wakali Wao Modern Taradance

KIKUNDI BORA CHA MWAKA- BONGO FLEVA
1. Yamoto Band
2. Weusi
3. Navikenzo
4. Makomando
5. B.O.B


============================


Updates:

Hii ni orodha kamili ya washindi wa tuzo za muziki Tanzania Kilimanjaro Music Awards 2015 zilizofanyika 13 June 2015 Mlinani City jijini Dar es salaam.

1. KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND

2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB

3. BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA

4. MSANII BORA CHIPUKIZI
- BARAKA DA PRINCE

5. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA -(WAITE) -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO

6. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA - NITAMPATA WAPI - DIAMOND PLATINUMZ

7. WIMBO BORA WA AFRO POP - MWANA ALI KIBA

8. VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA - MDOGOMDOGO - DIAMOND PLATINUMZ

9. MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI
- ENRICO

10. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA
- NAHREEL

11. MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP - JOH MAKINI

12. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI
- JOSE MARA

13. MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA
- ALI KIBA

14. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB-
MZEE YUSSUF

15. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIUME - ALI KIBA

16. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE
- VENESSA MDEE

17. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB
- MZEE YUSSUF

18. MWIMBAJI BORA WA KIUME BONGO FLEVA - ALI KIBA

19. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - ISHA MASHAUZI

20. MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA - VANESSA MDEE

21. WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI

22. WIMBO BORA WA MWAKA (MWANA)- ALI KIBA

23. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI
(WALEWALE) -VIJANA WA NGWASUMA

24. WIMBO BORA WA R&B (SIKSIKII)
- JUX

25. RAPA BORA WA HIP HOP - KIPI SIJASIKIA ( PROF J FT. DIAMOND PLATINUMZ)

26. MSANII BORA WA HIP HOP - JOH MAKINI

27. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
(SURA YAKO) - SAUTI SOL
 
Yaah waiting..... itakuwa Live ITV kuanzia saa 3! Mpoki kweli ana hitajika pale!

Kwakuwa Bella ata perform mimi nimefurahi sana....
 
Nimeona IG page ya Alikiba akiwashukuru mashabiki kwa kumpigia kura (siku 4 kabla) , hii confidence inamaanisha nini? Anyway tungojee kuona maajabu leo
 
Yaah waiting..... itakuwa Live ITV kuanzia saa 3! Mpoki kweli ana hitajika pale!

Kwakuwa Bella ata perform mimi nimefurahi sana....

Pia clouds walishatangaza kuwa wataonesha live.
Mimi hua napenda kuangalia kupitia clouds zaidi kuliko ITV maana huwa wako clear zaidi.

Kuhusu Bella nilikua sijui, asante kwa kuongezea nyama.
 
Le Mutuz ameanza kutapika nyongo huko IG ! Anasema haiwezekani majaji wawe ni siri lazima hapo ni gadem.
 
Nimeona IG page ya Alikiba akiwashukuru mashabiki kwa kumpigia kura (siku 4 kabla) , hii confidence inamaanisha nini? Anyway tungojee kuona maajabu leo

Kwa hiyo mtu akishukuru kupigiwa kura ni ushahidi wa nini?
 
Le Mutuz ameanza kutapika nyongo huko IG ! Anasema haiwezekani majaji wawe ni siri lazima hapo ni gadem.

Hahahahaaa, huyu jamaa sasa kazidi kwa matamkoz...siku hizi anayaita LE MUTUZ EXTRA STRAIGHT LIVE TALK!
Nimemuona tokea jana, na tusubiri tuone....
 

Attachments

  • 1434210439111.jpg
    1434210439111.jpg
    105 KB · Views: 2,208
  • Thanks
Reactions: BAK
Pia clouds walishatangaza kuwa wataonesha live.
Mimi hua napenda kuangalia kupitia clouds zaidi kuliko ITV maana huwa wako clear zaidi.

Kuhusu Bella nilikua sijui, asante kwa kuongezea nyama.

Advantage ya ITV ni kuwa kupitia DSTV tunaona na hadi watu wa nje ya nchi......lakini mwaka jana ilikuwa ni Clouds na EATV....
 
Huyo ni mtoto tumesha mzoea..atwambie ni lini walishakuwa revealed? Kinacho wekwa wazi huwa ni kura na kama una doubt una kwenda AUDITAX wanakuonesha....

Lile zee linang'ang'ania BASATA ndio wanaohujumu tuzo ili wamkomoe Diamond. Yule anatumiwa na habari zake ninazo zote, kama anajiamini alete hayo matamkoz yake huku aone.
 
Back
Top Bottom