Yaliyojiri kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 13 June 2015

Tuzo za mwaka huu zimekua zikichukuliwa na wengi kama 'kukata mzizi wa fitna' kwa wale mahasimu wawili wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambao ni Ali Saleh Kiba almaarufu 'King Kiba' na Naseeb Abdul almaarufu 'Diamond Platinumz'.

Kama wote wangekuwa nominated kimataifa ningesema sawa KTMA itakata mzizi wa fitina, lakini kwa vile ni mmoja tu ndie anayetambulika Kimataifa basi mzizi wa fitina ulishakatika wenyewe bila kusubiri KTMA ambayo imeshaanza kupewa lawama kibao.
 
#TEAM Diamond tutakuwa pamoja kuhakikisha uchakachuaji wa kupendeleana au kubebana tunaukemea...Kama kuna haki Diamond atatoka na tuzo nyingi kuliko msanii mwingine yoyote

Hivi umewai kujiuliza baada ya Diamond kuandika vile kwanini hakuendelea kuandika maana aliahidi kuandika part 2?
Mashabiki wa aina yako ndio walimfanya Diamond kuandika vile na wenye busara walimwambia hakupaswa kufanya vile na ndio maana hakuandika tena!
Hivi kama ni kweli kwanini hawakuchakachua ya tuzo zile saba!
Kwanza naomba ufikiri kwanza kwanini hakuandika tena?
 
Nitafurahi sana nikiona Alikiba akimbiza watu ktk tuzo.

Huyu jamaa ni mwanamziki bora. Anajua kuimba na kutunga na ana sauti nzr. Bahati mbaya hana Nyota nzr ya kung'aa sana, kupata pesa sana na huenda japo sina uhakika hana management nzr (Promoters, managers, whistleblowers, wazee wa kujipendekeza, wazee wa madili mjini, nk).
 
* Yeye ni binadamu na anaweza kuwa na hisia fulani kuhusu jambo fulani na anaweza kukosea pia. Sijesema kuna uchakachuaji tayari ila ikitokea tuna macho tutaona na tutazungumzia....
 
Kama wote wangekuwa nominated kimataifa ningesema sawa KTMA itakata mzizi wa fitina, lakini kwa vile ni mmoja tu ndie anayetambulika Kimataifa basi mzizi wa fitina ulishakatika wenyewe bila kusubiri KTMA ambayo imeshaanza kupewa lawama kibao.

Naungana na wewe mkuu KTMA hazikati mzizi wa fitina kati ya mahasimu hawa wawili.
 
Le Mutuz ameanza kutapika nyongo huko IG ! Anasema haiwezekani majaji wawe ni siri lazima hapo ni gadem.

Lemutuz anajipa vidonda vya tumbo bure kwa kushindwa kujua point ndogo sana kuwa dunia nzima kuna tofauti kubwa kati ya kupata tuzo na kupata umaarufu.
Kwa wafatiliaji watakumbuka Kanye West ktk function ya MTV award aliwahi kupanda jukwaani na kumpokonya mic msanii new school aliyekua akishukuru wapiga kura kwa kumchagua na kumshinda beyonce ambaye alikua nominee dhidi yake matokeo yake huyo msanii new school akapasua maanga kimuziki kwakutumia kick hiyo ya kudhalilishwa na mihemko ya kanye west na baadae kanye aliomba msamaha.
 
Hivi umewai kujiuliza baada ya Diamond kuandika vile kwanini hakuendelea kuandika maana aliahidi kuandika part 2?
Mashabiki wa aina yako ndio walimfanya Diamond kuandika vile na wenye busara walimwambia hakupaswa kufanya vile na ndio maana hakuandika tena!
Hivi kama ni kweli kwanini hawakuchakachua ya tuzo zile saba!
Kwanza naomba ufikiri kwanza kwanini hakuandika tena?
Mwaka jana nadhani ilikuwa ni aibu tu maana kwenye video bora unaiweka My #1 then unategemea ishindane na video gani?!Anyways Diamond ana Category 10,ila ni balaa eti kina Jux wameingia wimbo bora wa mwaka Diamond hakuna....
 
Ndugu yangu kama unaona "Nyota nyota" hapa tu sidhani kama utaelewa majibu ya hayo maswali uliyouliza.

Naomba uweke majibu hapa ya maswali niliyo kuuliza labda kama huna hakika na uwezi kutetea unacho kisema!
 
Nitafurahi sana nikiona Alikiba akimbiza watu ktk tuzo.

Huyu jamaa ni mwanamziki bora. Anajua kuimba na kutunga na ana sauti nzr. Bahati mbaya hana Nyota nzr ya kung'aa sana, kupata pesa sana na huenda japo sina uhakika hana management nzr (Promoters, managers, whistleblowers, wazee wa kujipendekeza, wazee wa madili mjini, nk).

Mkuu umeanza vizuri ila ukakoroga hapo katikati...
Hata hivyo hayo ni mawazo yako, NAYAHESHIMU!
 
Kama wote wangekuwa nominated kimataifa ningesema sawa KTMA itakata mzizi wa fitina, lakini kwa vile ni mmoja tu ndie anayetambulika Kimataifa basi mzizi wa fitina ulishakatika wenyewe bila kusubiri KTMA ambayo imeshaanza kupewa lawama kibao.

Hahahahaaa, kwani mnakosaga la kusema nyie? Bora ungeongelea kuchukua tuzo na sio kuwa nominated maana hata Kiba amewahi kuwa nominated (usiniulize wapi nenda kagoogle au nenda Wikipedia).
Ila bado ni mahasimu. ...
 
Mwaka jana nadhani ilikuwa ni aibu tu maana kwenye video bora unaiweka My #1 then unategemea ishindane na video gani?!Anyways Diamond ana Category 10,ila ni balaa eti kina Jux wameingia wimbo bora wa mwaka Diamond hakuna....

Hayo ni madhaifu tuu ya kibinadamu maana wanao pendekeza na kuchuja ni binadamu...tusichukulie kila kitu lengo lake ni kumshusha Diamond..! Hivi haya madhaifu yameanza leo? ni mwaka gani kumekosekana malalamiko?
 
+Mtoa mada nimependa uandishi wako yaani leo Chibu umemtaja vizuri kabisa badala "ndomo" kama ilivyozoeleka.

+ok tupo pamoja tunasubiri live update!

Asante, ningekua mwendawazimu kuweka ushabiki wangu katika post kama hii.
Hata mimi niliwaza kuwa kuna watu hawatoamini kua nitamuandika huyo jamaa kama anavyostahili!
 
Back
Top Bottom