Yaliyojiri Leo mahakamani kwenye kesi ya mchongo ya TUNDU LISSU..soma hapa

Yaliyojiri Leo mahakamani kwenye kesi ya mchongo ya TUNDU LISSU..soma hapa

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
14,521
Reaction score
46,663
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Agosti 13, 2026

Jana tuliishia part 236 so leo tunaendelea na -;

Part 237

Hatimaye, mida hii ya saa. 11:07 Asubuhi, Mahakama inaanza.

Wanaingia Mawakili wa Serikali,

Anaingia Mhe. Lissu na kundi la askari magereza, leo akiwa na vibe la kutosha kama kawaida yake anasalmia ile salama yake (People’s power 💪) anazungusha mkono, anawasalimia waliopo kule juu kwenye kighorofa then anamalizia kwa waliokaa hapa chini.

Inapigwa High Cooooooourt ya kikakamavu watu wote tunasimama.

Wanaingia Majaji wapo watatu kama kawaida yao then wanaketi kwenye viti vyao.

Karani anasoma case No.—- Jamhuri vs Tundu Lissu

Anasimama Wakili wa serikali anatambulisha jopo la mawakili wa Serikali kisha kawambia Majaji mtuhumiwa yupo.

Wakili wa Serikali anaomba radhi kwa kuchelewa anasema sababu ni kwamba walikuwa wanatafuta Shahidi na kwamba shahidi alipata changamoto za usafiri, hivyo wako tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa yani Mhe. Lissu kama yupo tayari kuendelea na kesi.

Mhe Lissu anasema mimi niko tayari kuendelea lakini huu utaratibu wa kuchelewa naomba msiuruhusu, hii ni case ya Uhaini na ndo kosa kubwa lililotamkwa mpaka kwenye Katiba ya Nchi yetu, siyo kosa la wizi wa mbuzi.

Kesi inamshtakiwa mmoja lakini mpaka sasa ina mwaka mmoja na zaidi naomba Mahakama iwe inafuata amri zake.

Wakili wa Serikali leo tuna shahidi mmoja anaitwa P huyu ni Shahidi asiyejulikana (Shahidi wa kificho)

Shahidi wa kificho anaingizwa kwenye kizimbani lile banda kama la kuku niliwahi kupost hapa.

Jaji: Shahidi tutakuuliza na utatujibu unaumri gani, dini yako?

Shahidi wa Kificho (P) : Miaka 26, dini yangu ni Muislam

Shahidi wa kificho (P) anapewa msaafu na kuapa

Wakili wa Serikali Thawabu Issa anamuongoza shahidi wa kificho (P)

Wakili wa Serikali: P unajishughulisha na nini?

Shahidi wa Kificho (P) : Mwandishi wa habari Jambo Tv, nimekuwepo kuanzia 2023 mpaka sasa, majukumu yangu ni kuchukua matukio ya video na picha.

Wakili wa serikali: Ujuzi wako kwenye hiyo kazi?

Shahidi wa kificho P : Eeeeeeh Ujuzi wangu eeeeh

Shahidi wa kificho (P) anaweweseka, ni kama hajaelewa swali.

Wakili wa serikali: Shahidi elimu yako?

Shahidi wa kificho P : Elimu yangu ni Diploma ya uandishi wa habari, niliipata Chuo cha Habari DSJ mwaka 2023.

Wakili wa serikali: Kwa namna gani unafanya hizo shughuri??

Shahidi wa kificho P : Nafanya kwa kutumia vifaa ambavyo ni camera aina ya Sony NX

Wakili wa serikali: Umesema matukio ya picha na video., hiyo unatumia kwenye matukio gani?

Shahidi wa kificho P : Kwa video pekee, kwa matukio ya picha natumia Canon.

Wakili wa Serikali: Shahidi unakumbuka tarehe 3/4/2025 ulipata jukumu gani?

Shahidi wa kificho P : Siku hiyo nilipewa jukumu na boss wangu kwenda kucover Mkutano wa Chadema kule Mikocheni nikiwa na mwenzangu P1, Boss wangu ni John Marwa.

Wakili wa serikali: Mkutano ulikuwa wapi?

Shahidi wa kificho P : Makao makuu Chadema

Wakili wa serikali: Tuendelee hapo...

Shahidi wa kificho P : Tulipack vifaa na kujiandaa na tukio husika, ilikuwa mishale ya saa 4 asubuhi.

Wakili wa serikali: hali ilikuwaje mlipofika?

Shahidi wa kificho P : Tulikuta kuna wanachama wa Chadema lakini pia Waandishi wa habari wa channel zingine kabla ya viongozi wa Chadema kufika.

Wakili wa serikali: Kwa siku hiyo ulijiandaa kwa matukio ya aina gani?

Shahidi wa kificho P : Ilikuwa kwa ajili ya kuchukua matukio na kwenda mubashara.

Mawakili wa serikali wananong'onezana...., hapa ni kama shahidi hakuelewa swali.😂

Wakili wa serikali: Mlikuwa mnarusha kwa njia gani?

Shahidi wa kificho P : Tulikuwa tunarusha kutoka kwenye matukio ya picha na kuyarusha YouTube.

Wakili wa Serikali: Majina mnayotambulika nayo kurusha mubashara???

Shahidi wa kificho P : kimyaa kidogo.....kisha anajibu; Jambo TV.

Part 238 itaendelea kwenye post inayofuata,
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 238

Wakili wa serikali: Tukio lilianza majira gani?

Shahidi wa Kificho P: Lilianza saa4 asubuhi na lilichukua masaa ma3 kukamilika?

Wakili wa serikali: Siku hiyo mlirusha maudhui ya nini?

Shahidi wa Kificho P: Tulirusha maudhui ya Chadema yaliyowakutanisha watiania kuzungumza mambo ya kiuchaguzi na masuala ya No reforms, No Election.

Wakili wa serikali: Unawakumbuka wazungumzaji?

Shahidi wa Kificho P : Nakumbuka ni Mwenyekiti Tundulissu, Makam Mwenyekiti John Heche na Katibu mkuu Mnyika.

Wakili wa serikali: Kwa namna ulivyowataja wazungumzaji, unakumbuka kauli?

Shahidi wa Kificho P : Kwa ujumla nakumbuka walizungumzia No reforms no Election na ni kwa namna gani wataenda kuingia kwenye huo uchaguzi.

Wakili wa serikali: Walisema wataingia kwa namna gani kwenye uchaguzi?

Shahidi wa Kificho P : Kwamba bila mabadiliko hakuna Uchaguzi na Mwenyekiti alikuwa akizungumza namna atakavyozuia uchaguzi huo.

Wakili wa Serikali: Mwenyekiti nani?

Shahidi wa Kificho P : Tundu Lissu

Wakili wa serikali: Unaweza kukumbuka baadhi ya maneno aliyosema?

Shahidi wa Kificho P : Aaah naweza kukumbuka machache tu, alizungumza TUTAZUIA HUU UCHAGUZI LAKINI PIA TUTAKINUKISHA.

Wakili wa serikali: Unaweza kutuambia hali ya vifaa mlivyokuwa mnatumia siku hiyo?

Shahidi wa Kificho P : Hali ya vifaa ilikuwa ni nzuri siku hiyo.

Wakili wa serikali: Malengo yalikuwa ni nini bwana P?

Shahidi wa Kificho P : Lengo ilikuwa ni kuhabarisha umma

Wakili wa serikali: Chombo chenu cha habari ilikuwaje kikafika eneo la tukio.

Shahidi wa Kificho P : Tulipata agizo kutoka kwa kiongozi husika

Hapa swali limerudiwa hii mara ya pili, mawakili wa serikali wananong'onezana ni kama kuna jibu wanatamani wangelisikia.😂

Wakili wa serikali: zoezi lenu la kurusha lilichukua muda gani?

Shahidi wa Kificho P : masaa matatu

Wakili wa serikali: Baada ya hapo nini kiliendelea?

Shahidi wa Kificho P : Tulirusha tukio zima na baada ya hapo tukaambiwa waandishi wa habari wote tutoke nje ili wazungumze mambo yao ya ndani.

Wakili wa serikali: Nikurejeshe tena kwenye tarehe 7/4/2025 unakumbuka nini kilitokea kinachohusiana na shughuri zako?

Shahidi wa Kificho P : Siku hiyo nilikuwa Dodoma kikazi, nikapokea simu yangu kutoka kwa boss wangu John Maro (sahizi imesikika Maro siyo Marwa tena) nikareport Kituo cha Polisi.

Anasimama Mhe. Lissu anasema Wakili wa serikali anamuwekea shahidi maneno mdomoni.

Jaji Ndunguru anasema labda pengine hujamsikia vizuri, shahidi amemtaja boss wake John Maro

Mhe. Lissu anasema kama mmemsikia ni sawa, mimi sikumsikia.

Wakili wa serikali: Boss alikuambia nini?

Shahidi wa Kificho P : Aliniambia niende nikakabidhi vifaa vya kurekodia memory card yenye picha.

Wakili wa serikali: ilikuwaje mpaka record ikawa kwenye card?

Shahidi wa Kificho P : Tunaporecord, hayo matukio huwa yanaingia moja kwa moja kwenye kadi.

Wakili wa Serikali: baada ya maelekezo nini kilifuata?

Shahidi wa Kificho P : Nilienda kituo cha polisi Dodoma kwa polisi aliyekuwa ananichukua maelezo na kumkabidhi kifaa kisha kusaini.

Wakili wa serikali: Sasa bwana P waambie hiyo tarehe 3/4/2025 huyo mtu alikuwa yupo katika mavazi gani?

Jaji: badili swali hapo unataka ajibu unachosema

Wakili wa serikali: sasa shahidi, eleza alikuwa katika hali gani?

Shahidi wa Kificho P : Rangi sijui ila alivaa combat.

Wakili wa serikali: Turudi yale maongezi ya mkutano, walikuwa wanaongelea uchaguzi gani?

Shahidi wa Kificho P : Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Mawakili wa serikali wananong'onezana kwa dakika kadha.

Wakili wa serikali: Waheshimiwa Majaji kwa shahidi huyu ni hayo tu.

Part 239 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 239

Jaji Ndunguru anamuuliza Mhe. Lissu kama ana maswali ya Dodoso?

Mhe. Lissu anaanza kumshona Shahidi wa kificho bwana P bila ganzi.😀

Mhe. Lissu : Ni kweli ama siyo kweli nyie Jambo TV mmefanya kazi na mimi kwa muda mrefu sana?

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Mhe. Lissu: Na ni kweli au si kweli kuwa, mmekuwa mkitangaza Mikutano yangu karibu nchi nzima.?

Shahidi wa kificho P : Ni Kweli

Mhe Lissu: Na mmekuwa mkicover habari zangu nchi nzima?

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Mhe Lissu: Na waeleze hawa Majaji kuwa hata nilivyotoka Ubelgiji mlinisindikiza hadi nyumbani kwangu?

Shahidi wa kificho P: sikumbuki

Mhe Lissu: Nitakukumbusha, ilikuwa ni waandishi habari Oscar na Shadrack Simba?

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Mhe. Lissu: Hata siku nilipokamatwa nilikuwa na hao waandishi wa habari Oscar na Shadrack Simba.?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Waeleze majaji kuwa ziara zote hizo tumekuwa tukienda safari moja?

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Mhe Lissu: Tumekuwa tukifikia hoteli moja na kula pamoja, kweli si kweli?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Nitakosea nikisema kuwa nyie waandishi wa habari pamoja na boss wenu John Maro tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana?

Shahidi wa kificho P: hujakosea

Mhe Lissu: Nitakuwa nakosea nikisema mmekuwa marafiki zangu?

Shahidi wa kificho P: Hujakosea

Mhe. Lissu: Wakati vyombo vingine vikiogopa kucover habari yangu nyie hamkuoogopa kucover habari yangu.?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Ni kweli/ Si kweli kuwa mlifunguliwa kesi TCRA mara tu baada ya kurusha huo Mkutano wangu?

Shahidi wa kificho P : Sikumbuki juu ya hilo

Mhe Lissu: sasa baada ya hayo, elezea kama kuna mwanachadema yoyote amekutishia au kukudhuru kwa namna yeyote ile?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Waeleze wahe. Majaji kama toka uliporusha hayo matangazo kuna mtu yeyote/ afisa yeyote/ mamlaka yeyote ambako umewapa taarifa kuwa umetishiwa kwa namna yeyote ile?

Shahidi wa kificho P : Hapana.

Kwa msiofahamu Mawakili wa Serikali waliomba huyu Shahidi atoe ushahidi kwa Siri kwasababu walidai kwamba kuna Wanachama wa CHADEMA walimtishia maisha, leo anasema hajawahi kutishiwa kwa sisi Wanawake hii ni kama mtu kakupa umbea halafu badae anakukana anasema aku mie sijakwambia.😂😂😂😂

Anyways tuendeleee

Mhe Lissu: Waeleze wahe. majaji kama una hofu yoyote au uoga wowote wa kutoa ushahidi hadharani?

Shahidi wa kificho P: Nina hofu

Mhe Lissu: Ooh kwanini una hofu shahidi? Eleza ukweli wa Mungu wako.???

Shahidi wa kificho P : Nina hofu kwakuwa hili suala ni very sensitive, Viongozi mnaweza msiwe na shida ila watu wengine ikawa tatizo.

Mhe Lissu: kama nimekuelewa shahidi umesema hujawahi tishiwa na mwanachama yoyote wa Chadema na sasa umesema viongozi siyo tatizo, ni sawa sawa?

Shahidi wa kificho P : Ndiyo

Mhe Lissu: Eleza kama aliyekuandika maelezo ni Inspector Endrew

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Sasa shahidi nitakusomea maelezo yako na nitakuonyesha maeneo ambayo umejichanganya na kisha nitaomba uiombe Mahakama kuyatoa kama kielelezo

Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka kum- impitch shahidi, Naomba wakili apewe kielelezo

Mawakili wa Serikali wamekuwa busy kidogo na file la vielelezo.

Mhe Lissu: Naomba niseme off record, Mahakama ilitoa order kuwa taarifa za mashahidi zifutwe, lakini naona mawakili wa serikali ndiyo wanafuta muda huu.

Shahidi wa kificho P anapewa kielelezo na Mawakili wa serikali.

Mhe Lissu: Shahidi eleza mahakama hayo ni maelezo yako?

Naomba ueleze kama sehemu ya makazi, eneo, mtaa, no. ya simu kama imefichwa?

Shahidi wa kificho P : Ndiyo

Mhe Lissu: Eleza kama mwaka wako wa kuzaliwa na jina la mzee limefichwa?

Shahidi wa kificho P : Ndiyo limefichwa

Mhe Lissu: Shule ya msingi na Sekondary ulizosoma zimefichwa?

Shahidi wa kificho P :Ndiyo

Part 240 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 240

Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa Kificho bwana P.

Anasimama Wakili wa Serikali anasema.... Tunaomba muongozo, ana cross wakati hajatenda document.

Mhe Lissu anajibu anasema naweka mambo sawa, sijaanza kucross, nataka nionyeshe kama kilichofanyika ni uzembe.

Wakili wa Kificho na yeye anasema Waheshimiwa Majaji kuna mambo mengine ni makosa ya kiubinadamu tu ila hizi taarifa zangu hazipaswi kuonekana.

😂😂😂 Ni kama upande wa Jamhuri walisahau kuficha taarifa za huyu Shahidi wa kificho kwa maana ya jina, anwani n.k sasa amejihami maana huko juu kasem zimefichwa wakat hazijafichwa, anahisi huenda Mhe. Lissu atachana mkeka.

Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji mimi nataka kuwaonyesha uzembe wao, wamedharau amri ya Mahakama, waliambiwa wafiche hawakuficha.

Jaji: Tuendelee

Mhe. Lissu: Anaanza kusoma kielelezo…

Mhe Lissu: Anaainisha maelezo yake aliyoyatoa Mahakamani ambayo anatarajia kumkanusha ukilinganisha na maelezo ya kielelezo, na hapa Mhe. Lissu ameainisha maeneo 7 ambayo atamkanusha.

Shahidi wa Kificho P: Sawa (anakubali kukanushwa)

Mhe Lissu: Sasa ili nifanye hiyo kazi nahitaji haya maelezo yawe ushahidi, sasa nakuuliza kama unaridhia kuwa haya maelezo yatumike kama kielelezo cha ushahidi hapa Mahakamani.?

Shahidi wa Kificho P : Ndiyo

Majaji : Eeh? (huku wakiwatizama Mawakili wa Serikali )

Mawakili wa Serikali: Hatuna pingamizi Wahesh Majaji.

Jaji: Kielelezo kimepokelewa na kupewa alama ya D16

Mhe Lissu na Mawakili wa serikali: Asante Waheshimiwa Majaji.

Majaji : Tuendelee

Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe kielelezo D16

Anaendelea kusema sasa shahidi hayo maelezo ni ushahidi mbele ya mahakama, Sawa sawa?

Shahidi wa Kificho P :Sawa

Mhe Lissu: Sasa shahidi,
Kwenye ushahidi wako leo, umesema tarehe 3/42025 ulipewa maelekezo na boss wako John Maro ukiwa na wenzako watano na ukamtaja mmoja ambaye ni P1 kwenda Mkutano wa Chadema, Sawa Sawa.?

Shahidi wa Kificho P : sawa

Mhe Lissu: Sasa nataka usome maelezo yako hapo anzia hapo watu ulioongozana nao.

Shahidi wa Kificho P : Anasoma..... Niliongozana na P2

Mhe Lissu: sawa, nimesema leo tutaongea ukweli mtupu.

Mhe Lissu anaendelea....

Kwenye maelezo yako umesema wazungumzaji walikuwa Mwenyekiti, Makam mwenyekiti na Katibu mkuu, sasa onyesha hayo maelezo kwenye iko kielelezo???

Shahidi wa Kificho P : Hakuna, ni wewe peke yako

Mhe Lissu: Sawa Sawa

Anaendelea Mhe. Lissu kwenye shahidi wako ulisema kuwa mazungumzo yao ilikuwa ni namna gani wataenda kuingia kwenye uchaguzi, hapo kwenye kielelezo yapo au hayapo?

Shahidi wa Kificho P : Hayapo

Mhe Lissu: Tarehe 7/4/2025 ukiwa Dodoma kikazi ulipokea simu kutoka kwa boss wako John Maro sasa eleza kama kwenye maelezo yako polisi ulisema hayo hata kuitaja tu hiyo tarehe 7/4/2025?

Shahidi wa Kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Sasa sema kuna sehemu ulipigiwa simu na boss wako John Maro akikueleza uende kituo cha polisi Dodoma? Eleza kama hayo maneno yapo.

Shahidi wa Kificho P : Hapana hayapo

Mhe Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema uliambiwa ukakabidhi memory card yako ya video ya Chadema, uliyochukuwa tarehe 3/4/2025, sema kama maelezo hayo yapo?

Shahidi wa Kificho P: Hayapo

Mhe Lissu: Sasa shahidi, umesema baada ya kupigiwa simu ulienda Kituo cha Polisi na kukutana na polisi uliyemkabidhi memory card na akakuandika maelezo, sasa eleza kama yapo kwenye kielelezo D16?

Shahidi wa Kificho P : hayapo

Mhe Lissu: Kwenye ushahidi wako hapa Mahakamani ulisema nilikuwa nimevalia combat lakini rangi hukumbuki, sasa elezea kama hayo maneno ya yaliyokuwa yanaelezea nilivyovalia yapo?

Shahidi wa Kificho P : Hayapo

Mhe Lissu: Ulisema walizungumza maneno mengi lakini ulisikia hili la walilokuwa wanarejerea Uchaguzi mkuu, yapo.

Shahidi wa Kificho P : Hayapo

Part 241 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 241

Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa kificho wa Jamhuri.

Mhe Lissu: Ulisema mlikuwa na Camera ya Sony NX, Kweli si kweli ?

Shahidi wa kificho P: Kweli

Mhe Lissu: Kwenye kielelezo mlikuwa na camera tatu, sasa kuna mashahidi wamekuja hapa Mahakamani wakasema kuwa camera iliyochukuwa ni Sony HXR- NX100, sasa eleza hii ni ipi?

Shahidi wa kificho P : Ni camera hiyohiyo, Sony NX ni kifupi.

Mhe Lissu: Ni sahihi kuwa Mkurugenzi John Maro aliwaambia muende mkutanoni kwakuwa alizipata kutoka kwa afisa habari wa Chadema, kama ilivyo kwenye kielelezo.

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: sasa kwa ufahamu wako, eleza kama mimi Lissu ni Afisa habari wa Chadem?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Kwa ufahamu wako, kama unafahamu afisa wa habari anaitwa BRENDA RUPIA?

Shahidi wa kificho P : Nafahamu

Mhe Lissu: Umesema hivi, wewe na wenzako mlipofika Makao Makuu Chadema, mlikuta wanachama wamefika ila viongozi hawajafika, ni sahihi?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Nani alikuwa anafanya maandalizi?

Shahidi wa kificho P : Sikulizingatia hilo

Mhe Lissu: Basi eleza kama uliniona nikifanya kazi hiyo?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Eleza sasa kwahiyo maandalizi uliyoyakuta na hayo uliyosema afisa habari wa chama ndiye aliyetoa taarifa kwa boss wako, sasa endapo mtu akija akasema mtu aliyeandaa Mkutano na aliyealika, atakuwa sahihi?

Shahidi wa kificho P : Itakuwa siyo sahihi

Mhe Lissu: Kwenye kielelezo D16 kuna maneno yanasema "Mimi nakumbuka katika huo mkutano wa ndani tulikuwa tunarusha live stream kupitia Jambo TV" nataka useme kama hayo yalikuwa ni maneno yako?

Shahidi wa kificho P : Ndiyo ni ya kwangu

Mhe Lissu: Pia nakumbuka kuna baadhi ya video tulirusha kwenye mitandao ya kijamii Instagram, Twitter ambazo Jambo Tv ilirusha, eleza kama kweli hayo yalikuwa ni maelezo yako.??

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Asante, truth is never a sin.

Sasa shahidi nimewekwa gerezani kwasababu mimi ndiye ninayedaiwa kuwa nilirusha video live nikaweka kwenye mitandao ya Jambo Tv, hiyo tuhuma ni ya kweli siyo ya kweli?

Shahidi wa kificho P: Sisi tulirusha kupitia wewe.

Mhe Lissu: Kupitia mimi sawa, Je mimi ndiye niliyerusha.

Shahidi wa kificho P : Sisi tulirusha kupitia wewe

😂😂😂 haapa watu imebidi wacheke kidogo maana kwenye maelezo ya Polisi, Shahidi anasema yeye ndo alirusha.

Mhe Lissu: Eleza kama niligusa camera zenu hata kidogo?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Eleza kama siku hiyo mimi nilikuelekeza wewe au wenzako kwamba rusheni hayo matangazo mubashara?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Eleza kama sikuhiyo mimi niliwaeleza mkisha rusha live mpeleke kwenye mitandao ya kijamii ya YouTube, Instagram na X?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Kwenye kielelezo D16, kuna maneno yanasema hizo taarifa zipo na mtu anaweza akazikuta kwenye hiyo mitandao?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli yapo

Mhe Lissu: Sasa eleza kama hayo ya kuhifadhi kwenye mitandao niliwaagiza mimi muhifadhi?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Sasa shahidi kwa kutuhumiwa kwa video ambayo sikuirusha wala sikuwataka mrushe, si ninaonewa.

Shahidi wa kificho P : Ndiyo maana uko hapa kujitetea hizi tuhuma

Watu wanacheka 😂😂😂😂

Part 242 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Kúna kundi la vijana watakuja kutukana viongozi wa serikali hapa ili wapate nafas za kuolewa ulaya kwa kigezo cha usalama
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 242

Mhe Lissu: Eleza kama ni kweli au si kweli kuwa wewe ni shahidi uliyekuwepo mkutanoni, hukuambiwa wala kusikia popote, umeshuhudia mwenyewe

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Mhe Lissu: Shahidi, katika kielezo D16, kuna maneno yanasema, maelezo ambayo yalikuwa yakiongelewa ni kuhusu Mkuu wa kitaifa na sera yao ya No reforms,No Election haya ni maelezo yako, kweli si kweli?

Shahidi wa kificho P : Ni maelezo yangu

Mhe Lissu: Sasa eleza kama viongozi wa chama cha siasa kujadili masuala ya uchaguzi na changamoto zao, ni kosa?

Shahidi wa kificho P: si kosa

Mhe Lissu: Uliandika, mimi nakumbuka matukio yote ambayo mimi nimekukabidhi, hata maneno ulikuwa unamwambia Inspector Chullu, kweli si kweli?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Sasa hiyo memory uliyokuwa unamkabidhi Inspector Chullu, sisi hatujaiona, mashahidi waliopita hawajaileta, sasa eleza kama wewe umeileta hapa?

Shahidi wa kificho P: Mimi sijaileta

Mhe Lissu: Eleza kama kwenye ushahidi wako hapa mahakamani hakuna mahali popote uliposema kwamba maneno ya Mwenyekiti ni kosa, kweli si kweli?

Shahidi wa kificho P: Kweli

Mhe Lissu: Ni kweli kwa maneno yako kwamba kwenye mkutano huo kulikuwa waandishi wa habari wa mitandao mingine?

Shahidi wa kificho P : Ni kweli

Mhe Lissu: Eleza kama hayo mliyokuwa mnarecord yalikuwa ya kihaini?

Shahidi wa kificho P: Sina hakika

Mhe Lissu: Eleza kama wewe na hao wengine mliokuwa mnarecord mmeshtakiwa kwa kosa la uhaini kwa kutoreport viashiria vya kosa la uhaini?

Shahidi wa kificho P : Hapana

Mhe Lissu: Katika hao waliozungumza Mkutanon na waliorusha matangazo, kuna mtu tofauti na Lissu aliyeshtakiwa kwa uhaini?

Shahidi wa kificho P: Hakuna

Mhe Lissu: Katika kielelezo D16 umesema ulikuwa na P2, Sawa Sawa?

Shahidi wa kificho P : Ni sawa

Mhe Lissu: Sasa huyu P2 alitoa ushahidi kuwa ni mtu wa Songea na trh 7/4/2025 na hakuenda Dodoma, ila wewe unasema alikuwa Dodoma

Shahidi wa kificho P : Huyo P2 tulikuwa naye Dodoma

Mhe Lissu anatabasamu, na kumshukuru sana shahidi, kisha anasema asante sana Majaji, mimi maswali yangu ni hayo tu.

😂😂😂 hakika shahidi wa leo amezungumza kadri ya ukweli wake

Jaji Re-examination?

Mawakili wa Serikali: Waheshimiwa majaji tunaomba dakika 5.

Minong'ono kidogo.

Mhe Lissu: Waheshimiwa wakati Mawakili wa serikali wanadiscuss naomba short break kidogo.

Mawakili wa Serikali: Waheshimiwa Kabla mshtakiwa hajatoka tunaomba kusema kuwa, kwa upande wetu sisi hatutakuwa na maswali ya re- examination kwa shahidi.

Majaji wanarecord

Mhe Lissu: Waheshimiwa majaji mimi nilikuwa na ombi langu

Mahakama: Sawa unaweza kwenda tu.

Mhe lissu anatoka kidogo na kundi la askari magereza huku akiwaonyeshea ishara ya nimewachinjilia mbali.

Watu wanacheka 😂😂😂

Baada ya muda kidogo, Mhe. Lissu anarudi, na Mahakama inaendelea;

Majaji : Shahidi umemaliza kutoa ushahidi wako, kwahiyo mahakama inakuruhusu uondoke zako.

Upande wa mashtaka?

Mawakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji kwa leo tulikuwa na shahidi mmoja tu, hivyo tunaomba kuhairisha kwa ajili ya kuandaa shahidi mwingine.

Mahakama: Kama kunakuwa na sababu za ucheleweshaji lazima na mshtakiwa apewe taarifa, pia tulikubaliana muwalete mashahidi kadri muwezavyo.

Mhe: Lissu: Waheshimiwa Majaji Kumekuwa na utaratibu kuwa nikiletwa hapa nawekwa Mahabusu na siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu wala kushahuriana nao, pia kuna mashahidi wangu wa utetezi ambao niliwataja nao sipati fursa ya kuonana nao, this is not fair trial, naomba maelezo yenu Waheshimiwa Majaji, nipate kushahuriana na mawakili wangu nikiwa hapa. Yale ya magereza nilifungua kesi na tunasubiri uamuzi, sasa naomba maelekezo ya hapa.

Jaji: Tumekusikia tuseme tu kuwa, hizo ni issue za administration, tunawasilisha na baadae tutakubaliana hapa.

Mahakama inahairishwa mpaka kesho saa3 Asubuhi.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
Hatimaye, mida hii ya saa. 11:07 Asubuhi, Mahakama inaanza.
Mkuu, 'PureView zeiss'
Sijasoma hayo yaliyoandikwa huko chini; na kabla ya yote nikushukuru sana kwa kazi hii mnayoifanya kuleta taarifa za hii kesi humu JF.

Hili linalohusiana na mstari huo niliounyanyua siyo la muhimu, lakini mazoea maddogo ya aina hii ndiyo huzaa ubovu mkubwa; kama tunavyoona walipotufikisha CCM hadi sasa.
Hiyo saa kumi na moja na dakika saba (11:07), kwa tafsiri ya lugha yetu hiwezi kuwa asubuhi.
Naomba tu tuepukane na makosa madogo yasiyokuwa na lazima kama haya..
 
Mkuu, 'PureView zeiss'
Sijasoma hayo yaliyoandikwa huko chini; na kabla ya yote nikushukuru sana kwa kazi hii mnayoifanya kuleta taarifa za hii kesi humu JF.

Hili linalohusiana na mstari huo niliounyanyua siyo la muhimu, lakini mazoea maddogo ya aina hii ndiyo huzaa ubovu mkubwa; kama tunavyoona walipotufikisha CCM hadi sasa.
Hiyo saa kumi na moja na dakika saba (11:07), kwa tafsiri ya lugha yetu hiwezi kuwa asubuhi.
Naomba tu tuepukane na makosa madogo yasiyokuwa na lazima kama haya..
Shukran Sana mkuu
 
"...Shahidi wa Kificho P : Siku hiyo nilikuwa Dodoma kikazi, nikapokea simu yangu kutoka kwa boss wangu John Maro (sahizi imesikika Maro siyo Marwa tena) nikareport Kituo cha Polisi.

Anasimama Mhe. Lissu anasema Wakili wa serikali anamuwekea shahidi maneno mdomoni.

Jaji Ndunguru anasema labda pengine hujamsikia vizuri, shahidi amemtaja boss wake John Maro

Mhe. Lissu anasema kama mmemsikia ni sawa, mimi sikumsikia..."

Akili aliyotumia hapa Lissu kwa majaji ni akili kubwa sana.
Ameweka record sawa kuwa kumbe majaji nao wamemsikia shahidi akimtaja boss wake kama "John Maro" badala ya "John Marwa"..
 
Mhe Lissu: Na waeleze hawa Majaji kuwa hata nilivyotoka Ubelgiji mlinisindikiza hadi nyumbani kwangu?

Shahidi wa kificho P: sikumbuki

Mhe Lissu: Nitakukumbusha, ilikuwa ni waandishi habari Oscar na Shadrack Simba?

Shahidi wa kificho P: Ni kweli

Sasa hapo wamficha nini? Ila Lissu akili mingi sana huyu Mnyampaa
 
Jaji: Tumekusikia tuseme tu kuwa, hizo ni issue za administration, tunawasilisha na baadae tutakubaliana hapa.

Mahakama inahairishwa mpaka kesho saa3 Asubuhi.
Shukrani sana kwa kazi nzuri hii mnayolifanyia taifa hili , mkuu 'Pure View zeiss'

Hizi ni kumbukumbu zitakazodumu miaka na miaka.
Msidhani michango yenu kwa ukombozi wa taifa hili ni midogo.

Kila mtu atachangia kwa kiasi chake na nafasi aliyopo kulikomboa taifa hili.
 
Back
Top Bottom