Yaliyojiri Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake - 30 Nov 2021

Nimekuwa nikifuatilua hii kesi ya mbowe, mwenendo ya kesi yenyewe na namna ushahidi unavyotolewa mahakamani na jamhuri.

Jamhuri inaonyesha wamejipanga muda mrefu sana kwasababu za kiupelelezi nakadhalika.

Na kwanamna wanavyotoa ushahidi wao hakika umenyooka sana kuliko hata ule ushahidi wa Sabaya wa kuunga unga na gundi.

Siamini kama jamhuri inaweza kupoteza pesa nyingi kutengeneza kesi kubwa namna hii.

Kumbuka mashahidi wanaotoa ushahidi katika kesi hii ukiconnect doti kama unapata jibu chanya.

Jamhuri wametumia kodi ya wananchi katika upelelezi wa kesi hii na mchakato mzima unaohusu hii kesi.

Sasa kama mbowe atakuja kushinda kesi,ni heri jamhuri hata kama mtu amefanya uhaini wowote watumie njia nyingine kumkabili kuliko kumpeleka mahakamani.

Na sasa hivi wanachofanya mawakili wa mbowe ni kuweka mapingamizi mengi ili yakitupwa na mahakama waweze kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia

Tunaomba judge asisikilize pressure kutoka kwa wanasiasa au wanaharakati fulani fulani na vyomba vya habari wenye mrengo ule wa kisiasa, kwasababu atainajinsi mahakama. Hata Dunia ipige kelele mhalifu ni muhalifu tu
Wanasiasa ndio wana tiapresha sana.
 
Kesi yenyewe ya ugaidi haijaanza hi ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa, ila ina uhusiano mkubwa na kesi kubwa, hi kesi ndogo wakiiporeza ila kesi kubwa inakosa ushahidi, ndo maana nguvu zote zimetolewa katika hi trial.
Unaelewa unachoongea lakin?? Kwahiyo hii ni kesi ndogo kuhusiana na nini bwana mkubwa?
 
Nimekuwa nikifuatilua hii kesi ya mbowe, mwenendo ya kesi yenyewe na namna ushahidi unavyotolewa mahakamani na jamhuri.

Jamhuri inaonyesha wamejipanga muda mrefu sana kwasababu za kiupelelezi nakadhalika.

Na kwanamna wanavyotoa ushahidi wao hakika umenyooka sana kuliko hata ule ushahidi wa Sabaya wa kuunga unga na gundi.

Siamini kama jamhuri inaweza kupoteza pesa nyingi kutengeneza kesi kubwa namna hii.

Kumbuka mashahidi wanaotoa ushahidi katika kesi hii ukiconnect doti kama unapata jibu chanya.

Jamhuri wametumia kodi ya wananchi katika upelelezi wa kesi hii na mchakato mzima unaohusu hii kesi.

Sasa kama mbowe atakuja kushinda kesi,ni heri jamhuri hata kama mtu amefanya uhaini wowote watumie njia nyingine kumkabili kuliko kumpeleka mahakamani.

Na sasa hivi wanachofanya mawakili wa mbowe ni kuweka mapingamizi mengi ili yakitupwa na mahakama waweze kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia

Tunaomba judge asisikilize pressure kutoka kwa wanasiasa au wanaharakati fulani fulani na vyomba vya habari wenye mrengo ule wa kisiasa, kwasababu atainajinsi mahakama. Hata Dunia ipige kelele mhalifu ni muhalifu tu
Msingi wa hoja yako ni imani basi. Ukiondoa imani "Siamini kama jamhuri inaweza kupoteza pesa nyingi kutengeneza kesi kubwa namna hii" hoja yako inabaki uchi. Hivi ni nani alikuambia kuwa Jamhuri na watawala ni kitu kimoja au mara zote huwa na maslahi ya pamoja? Unachopaswa kujua ni kuwa watawala wanatumia rasilimali za Jamhuri kutengeneza kesi isiyokuwepo kwa maslahi yao ya kuendelea kuwa madarakani.
 
Ila Mawakili wa Serikali wamewakalia vibaya sana akina Mbowe na wenzake. Kila kielelezo kinacholetwa na upande wa utetezi kinapigwa chini. Hakika katika kesi hii WS wameonesha umahiri mkubwa sana.

Ukitaka kuelewa ukweli wa haya mambo angalia maswali ya mahojiano kinzani(Cross examination) Mawakili wa Serikali ya jana kwa mshitakiwa namba mbili yalivyo-weaken kesi ya upande wa utetezi. Mpaka mwisho wa siku shahidi akabaki kusema ni sahihi kwa kila swali.

Mark my words. Kwa mwenendo huu wa kesi naona kabisa Mbowe na wenzake watafungwa na mahakama.
 
Mawakili wa mbowe wanachelewesha tu kesi,mara diary mara GPO badala ya kujikita kwenye kupangua kesi
Yaani kuna siku alikua anapinga maelezo ya askari kwamba wakati wa tukio alikua Arusha kikazi na sasa yupo oysterbay,
Kibatala hajui kwamba askari anaweza kuwa yupo mbinga lakini anafanya upelelezi chake chake?
Hadi leo hii sijaona popote ushahidi kwamba Mbowe aliikuwa anapanga vitendo vya ugaidi zaidi ya blah blah ya mashahidi. Hebu nikumbushe ushahidi ambao japo kwa asilimia 20 tu unaonesha vitendo vya kigaidi vya Mbowe.
 
Kwako wewe haki ni kina Mbowe kushinda!!

Ushahidi wa upande wa mashitaka ni wa wazi sana. Mawakili wa utetezi wamepwaya sana. Hivyo tuiache mahakama itende haki.
Ni wapi hadi sasa ushahidi wa Jamhuri angalau umeonesha kwa asilimia 20 tu ya vitendo vya ugaidi vya Mbowe?
 
Kwako wewe haki ni kina Mbowe kushinda!!

Ushahidi wa upande wa mashitaka ni wa wazi sana. Mawakili wa utetezi wamepwaya sana. Hivyo tuiache mahakama itende haki.
Wewe utakuwa shabiki wa kisiasa tu huna taaluma ya legal issues.
 
Ila Mawakili wa Serikali wamewakalia vibaya sana akina Mbowe na wenzake. Kila kielelezo kinacholetwa na upande wa utetezi kinapigwa chini. Hakika katika kesi hii WS wameonesha umahiri mkubwa sana.

Ukitaka kuelewa ukweli wa haya mambo angalia maswali ya mahojiano kinzani(Cross examination) Mawakili wa Serikali ya jana kwa mshitakiwa namba mbili yalivyo-weaken kesi ya upande wa utetezi. Mpaka mwisho wa siku shahidi akabaki kusema ni sahihi kwa kila swali.

Mark my words. Kwa mwenendo huu wa kesi naona kabisa Mbowe na wenzake watafungwa na mah
Mbona hata utetezi wana cross examination nzuri kuliko hao wakili was serikali. Kinachowapa ujasiri wakili wa serikali ni kwamba wanauhakika wa kushinda kwa sababu Jaji yupo nao time moja.
 
Kwako wewe haki ni kina Mbowe kushinda!!

Ushahidi wa upande wa mashitaka ni wa wazi sana. Mawakili wa utetezi wamepwaya sana. Hivyo tuiache mahakama itende haki.
Ushaidi gani wa ugaidi walioutoa upande wa jamuhuri dhidi ya washitakiwa?? Toka mwanzo wanaeleze ukamataji tu na kuwasafirisha washitakiwa na umo ndani wameweka uhongo mwingi Sana. Labda na Ile komedi ya kwenda kuzikagua bunduki ambayo hawakuchukua hata finger print ya huyo wanayedai walimkuta nayo🤣🤣🤣
 
Mawakili wa mbowe wanachelewesha tu kesi,mara diary mara GPO badala ya kujikita kwenye kupangua kesi
Yaani kuna siku alikua anapinga maelezo ya askari kwamba wakati wa tukio alikua Arusha kikazi na sasa yupo oysterbay,
Kibatala hajui kwamba askari anaweza kuwa yupo mbinga lakini anafanya upelelezi chake chake?
"Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Warumi 2; 8-9
 
Matata: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Pingamizi walilileta Upande wa Serikali Kwamba Nyaraka hizi siyo Relevant, Tunaona ni Pingamizi ambalo halina Mashiko. Kwa Sababu Hakuna Namna D/C Msemwa angeweza kuwa Oysterbay na wakati huo huo akawa Polisi Central DSM Wakati ni Vituo tofauti
kimeumana !!
 
Ushaidi gani wa ugaidi walioutoa upande wa jamuhuri dhidi ya washitakiwa?? Toka mwanzo wanaeleze ukamataji tu na kuwasafirisha washitakiwa na umo ndani wameweka uhongo mwingi Sana. Labda na Ile komedi ya kwenda kuzikagua bunduki ambayo hawakuchukua hata finger print ya huyo wanayedai walimkuta nayo🤣🤣🤣
Mkuu, nami kila nikifikiria kwa ushahidi ambao mpaka sasa umeshatoka, sioni kabisa kesi inayofanana na huo UGAIDI. Labda kama kuna USHAHIDI utakaotolewa huko mbele, ambao utakuwa tofauti kabisa na hayo tuliyoyasikia!
 
Back
Top Bottom