Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwenye kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa hadi - Nov 10, 2021

Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwenye kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa hadi - Nov 10, 2021

hii kesi inaonekana inaweza kunguruma zaidi ya miaka 2 kabla ya hukumu.
maana hata nusu ya mashahidi upande wa mashitaka bado.
hayo mapingamizi nadhani yanaweza kufika hata 200.
itafika mahali watu ulimi wote utatoka nje!
 
Sawa, lakini ukijua laana ya vitendo inamaumivu makubwa kuliko ya maneno na kuandika, imagine mama anayemulaana mtoto kwa kuvua nguo zake na mama anayeongee tu nimekulaani ni laana ipi itakuwa na nguvu? Na ndicho nilichomaanisha.
Lana kamili ni guilty consciousness ya alietenda. Hayo yatamkwayo kama hayakuingii akilini mwako na hujutii, hata angevua zote hakuna kitu.
 
Watu wanapewa ujaji kwa kujuana tu lakini kiukweli hawana sifa yoyote ya kuwa jaji na lengo lao ni kuwatumia katika mazingira kama haya.
Kwani amekutwa na shoka la kukatia miti? Au chainsaw?
 
Kwani amekutwa na shoka la kukatia miti? Au chainsaw?
Wanajua wenyewe bwana lakini kumbuka Sugu na Nyagali walifungwa jela bila kosa na hata hawa akina Mbowe and Co walitiwa hatiani pale Kisutu kwa amri za Magufuli.

Ukweli unabaki pale pale kwamba sasa hivi Tanzania haina mahakama za haki ni kama vile tuna Kangaroo Courts tu.
 
mbowe ni shetani tu hata kama unampenda alitaka kuharibu nchiyetu gaidi
Aliyeharibu nchi ni Yule aliyeamuru uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 wapitishwe mboga mboga nchi nzima, na uchaguzi mkuu 2020 bunge liwe la mboga mboga la wapiga makofi, Cha ajabu hajaona matunda aliyoandaa, akatwaliwa na Mwenye enzi asiyetaka upuuzi.
 
POROJO za LING'WENYA eti anadai alitishiwa silaha [emoji1787][emoji1787]
 
Sawa, lakini ukijua laana ya vitendo inamaumivu makubwa kuliko ya maneno na kuandika, imagine mama anayemulaana mtoto kwa kuvua nguo zake na mama anayeongee tu nimekulaani ni laana ipi itakuwa na nguvu? Na ndicho nilichomaanisha.
Machafuko ya kumwondoa Al Bashir yalianzishwa na msichana tu, hii ilitokana na hasira ya muda mrefu kurundikana kwa watu. Usione hasira dhidicya CCM inarundikana, na ikaja kuwashwa na tukio dogo tu la mkate! Usifurahie hali hii na kuishabikia.
 
Hizi huruma za keyboard hazisaidii kitu, Mimi kwa kuwasaidia kama Mbowe wanasingizia tumieni nguvu za kiroho za kupata haki kutoka kwa Mungu chagueni siku tatu za maombolezo au mbili za kumulilia Mungu haki ipatikane wafungwa na wote mtakaojitolea siku hizo msilale vitandani mwenu mtandike mikeka mlale chini kama waombolezaji wa kweli na ikiwezekana chakula kisipite kwenye vinywa vyenu yaani iwe msiba kweli kweli wa kumulilia Mungu atende haki ikiwa kweli hajafanya majibu mtayapata hizo ndo njia watu wa Mungu wanatumia kudai haki na ukweli ukiwa upande wao majibu yatapatikana ila tu ifanyike kwa watu wa familia zaidi bila kelele za mitandao na siasa maana hapa tunaongelea kuleta haki katika Taifa na siyo haki ya Chama flani.
Wewe leo unaita " hasira za keyboard", hata Rais wa Sudan aliongea Kama wewe. Unazosema hasira za keyboard zilifumuliwa na msichana mdogo tu nchi nzima ikawaka moto. Uvumilivu una mwisho, CCM kwa Sasa wanachekelea udhalimu unaoendelea, inawezekana wakachekelea kwa muda, lakini hasira za keyboard Kuna siku zitafumuliwa na suala dogo na nchi itawaka na hawataamini. Cha msingi ni kutenda haki, Kama mfumo wetu ni wa vyama vingi, vyote vifanye siasa, siyo kimoja kifanye siasa, vingine hata vikifanya jogging, Polisi hawa hapa....hasha, huko mbeleni, tunaelekea shimoni.
 
Inge kuwa nchi zingine kwa tuhuma kama hizi za Ugaidi Mbowe angesota sana Rumande hata miaka 10 bila kesi kuanza.
angalia Taifa kubwa kama USA kuna watuhumiwa wa makosa ya ugaidi wameshikiliwa huko ktk gereza la Guantanamobay kwa zaidi ya miaka 20.
Mboe yeye kila siku anakuja kutalii mahakamani ashukuru sana Tanzania inafuata utawala wa sheria, ingekuwa nchi zingine angesweka kwanza.
 
Watanzania Japo tuliwahi kuanza kwenda Shule Lakini nafikiri kuna kitu tunakosa.

Sahizi akina Mbowe tunawaona kama Hamnazo hivi, lakini Nina amini Ipo siku tutakumbuka Mapambano Yao. Na mungu atuweke hai hichi kizazi kije kishuhudie.

Serikali Ya SISIEMU haiwezi kutuletea maendeleo kwasababu wanajua watanzania tukiendelea, tutawaondoa Madarakani. Kwahiyo wanatumia Mwanya wa Ugumu wa Maisha kutusahulisha na Mabaya yote wanayo yafanya. Siku tukija Kustuka Tutasema Tulichelewa Sanaa. Lakini Tujifunze nchi zingine Tanzania Sisi Sio kisiwa Tutafika iliko Libya, Ethiopia, Na Nchi Nyingine. Siku watanzania Wakija kuamua kuwa wamechoka, Hawata msikiliza Mchungaji wala Shehee

Naamini Ipo siku, kikubwa Tuombe Uzima, Maisha Yawe rahisi Wananchi wengi tumiliki SMARTPHONE

MBOWE MATESO YAKO HAYATAENDA BURE…
Fukuto la kumwondoa Al Bashir lilianzishwa na msichana mdogo tu nchi nzima ikawaka moto, hii ni kutokana na mrundikano wa hasira wa siku nyingi wa raia. Kwa Sasa CCM wanafurahia udhalimu unaoendelea, nchi ya vyama vingi, lakini siasa wanafanya wao tu, vyama vingine hata vikifanya jogging, Polisi hawa hapa.... sanduku la kura haliheshimiwi, kabla ya kupiga kura, CCM tayari wamepata wabunge 80 bila kupingwa! Mahakama wamejaa majaji wa TISS, haya yote CCM wanachekelea, hawajui wanatupeleka shimoni.
 
ni Bora hili Gaidi limedhibitiwa maana linge aachwa lingesababisha hatari kubwa.

mfano mbaya angalia wafuasi wake jinsi walivyo na tabia za kijambazi, wauza madawa, wavuta bangi, yaani ni wakorofi sana, yote hayo walifundishwa na huyo kiongozi wao, ambaye kila kukicha alikuwa naratibu uhalifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni Bora hili Gaidi limedhibitiwa maana linge aachwa lingesababisha hatari kubwa.

mfano mbaya angalia wafuasi wake jinsi walivyo na tabia za kijambazi, wauza madawa, wavuta bangi, yaani ni wakorofi sana, yote hayo walifundishwa na huyo kiongozi wao, ambaye kila kukicha alikuwa naratibu uhalifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unaharisha sana mkuu? Ni vyema ukamuona Dr usije zidiwa.
 
POROJO za LING'WENYA eti anadai alitishiwa silaha [emoji1787][emoji1787]
Huko mbeleni usije ukabadilisha ID. Usizidishe mahaba sana kwenye kesi hii ukidhani kuna mtu atafungwa. Hafungwi mtu hapa. Mahakama za Tanzania haipokei ushahidi wa mashoga na wauza mbege. Shoga Power Kaaya na muuza mbege Anita
 
ni Bora hili Gaidi limedhibitiwa maana linge aachwa lingesababisha hatari kubwa.

mfano mbaya angalia wafuasi wake jinsi walivyo na tabia za kijambazi, wauza madawa, wavuta bangi, yaani ni wakorofi sana, yote hayo walifundishwa na huyo kiongozi wao, ambaye kila kukicha alikuwa naratibu uhalifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakiwemo,Katambi,Mashinji,Jualikali,covid 19.....kweli jamaa ni li gaidi nguli kabisa.
 
Gaidi hana sura babu we subiri hadi mwisho wa picha
Ungana nasi kumwombea Mh Friman Mbowe siyo gaidi
LITANIA MAALUM YA KUOMBEA KESI YA MBOWE NA WENZAKE!

KIONGOZI : Mwenyezi Mungu mwenye rehema! Twakushukuru kwa zawadi ya afya na uhai. Tunakuomba utusamehe makosa yetu. Tunatubu kwa ajili yetu na wenzetu na hasa kwa ajili ya Mbowe, Bwire, Lingw'enya, Adamoo, Jaji Joachim Tiganga, Mawakili wa Utetezi, Mawakili wa Mashtaka, Mashahidi katika pande zote mbili, Waendesha Mashtaka na watu walio katika mamlaka.

WAUMINI: Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunamuinua mbele ya Kiti chako cha Enzi Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza Kesi hiyo! Tunaomba ukampe kiu ya kutenda haki pasipo kuogopa vitisho na mashinikizo ye yote. Ukamuepushe na rushwa ya kutamani madaraka kupitia Kesi hii. Ukampe ujasiri wa kuhukumu kwa haki pasipo kuogopa wanadamu. Ukampe uwoga wa kupendelea na kufinya haki ili kuwaridhisha watu. Akatambue kuwa akisimama katika haki utamuinua zaidi na kumpa heshima ya kimbingu, akipendelea na kufinya haki atafedheheshwa!

WAUMINI : Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunawaweka mikononi mwako Mawakili Wasomi wa Upande wa Mashtaka! Kwamba wanao wajibu wa kuwaongoza Mashahidi kushuhudia kweli tupu. Kwamba wakifanya hivyo watainuliwa na kupewa heshima ya kimbingu na wataheshimiwa na wanadamu pia. Wakaogope kuwaongoza Mashahidi kushuhudia uwongo mbele ya Mahakama ili kujipendekeza kwa walio na mamlaka ambao wana maslahi binafsi na Kesi hiyo. Watambue kuwa kwa kufanya hivyo kutawaingiza katika fedheha, aibu na laana itakayoshuhudiwa na wengi kwa kuwa wewe ni Mungu unayechukia wanaowashuhudia watu wengine uwongo!

WAUMINI: Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunawaombea Mashahidi wa pande zote mbili! Ukawape ujasiri wale waliojiandaa kushuhudia iliyo kweli. Ukawape ujasiri wa kukataa kupanda kizimbani wale watakaoshawishiwa kushuhudia uwongo. Ukawanyime ujasiri wa kushuhudia uwongo na wakipanda kizimbani kwa ajili ya kushuhudia uwongo, wakakose amani na muelekeo. Wote watambue kuwa wakishuhudia uwongo watafedheheshwa na wakishuhudia ukweli wataheshimiwa na wewe na wanadamu pia!

WAUMINI : Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunawaombea Mawakili Wasomi wa Upande wa Utetezi! Tunaomba ukawape ujasiri wa kukataa ushawishi kupitia rushwa na vitisho! Wakawaongoze Mashahidi kusema kweli tupu. Wakatambue kuwa kupokea rushwa na kuwaongoza Mashahidi kushuhudia uwongo ni fedheha kwao na laana kubwa, lakini kukataa rushwa na kuwaongoza Mashahidi kushuhudia kweli tupu ni heshima kubwa kutoka kwako na kwa wanadamu!

WAUMINI : Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI: Tunawaombea Washtakiwa Mbowe, Bwire, Lingw'enya na Adamoo! Uwape utulivu wakitambua kuwa wewe ni Mungu mwenye haki. Ukawalinde dhidi ya hila zo zote mahali po pote wawapo barabarani, Mahakamani na hata Gerezani. Ukazilinde familia zao na watu wanaowategemea. Ukawape muda mzuri wa kukutafakari wewe wawapo Gerezani na hata kukukaribia wewe zaidi! Pale walipokukosea wewe na wanadamu, wakautumie muda huo kuzijutia dhambi zao ili wapate toba ya kweli!

WAUMINI: Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI: Tunawaombea wenye mamlaka ambao hawahusiki moja kwa moja lakini wako nyuma ya Kesi hiyo! Kama kuna waliohusika kuasisisi, kutunga na kuratibu uwongo basi ukawape neema ya kutubu na kujutia uovu huo, vinginevyo watambue kuwa fedheha, aibu na anguko viko mbele yao! Ukawape ujasiri wa kujitenga na hila ye yote kuanzia leo. Wakijua kuwa wakifanya hivyo watapata rehema na heshima kutoka kwako na wanadamu pia!

WAUMINI : Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunawaweka mikononi mwako wanaoendelea kupanga, kuratibu na kutekeleza hila wakati huu. Wawe wa Polisi Magereza, Jeshi la Polisi, Mahakama na watumishi wake, Waendesha Mashtaka, Mawakili, Serikalini, na Taasisi nyingine iwayo ye yote ile. Wamiminie Roho wako ili watambue uovu wao na kuuacha. Ukafarakanishe mawasiliano yao; hila, uwongo na uovu wao. Mikakati, hila na uwongo wao vikadhihirike hadharani ili wakafedheheshwe. Kama hawatatubu na kuacha na wakiendelea na hayo wakashushwe kutoka katika nafasi zao na kusiwepo na kumbukumbu lao tena katika sehemu zao za kazi!

WAUMINI: Ee Mungu twakuomba utusikie!

KIONGOZI : Tunaomba haya yote kupitia Jina la Yesu Kristo, atawalaye na kumiliki pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu! Amina!

WAUMINI : Amina!

NB: Sala hii inaweza kutumiwa katika makundi ya watu kuanzia watu wawili na kuendelea. Inaweza kutumika pia katika familia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Back
Top Bottom