Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ndogo ya Mbowe, Superitendent Jumanne Malangahe atoa Ushahidi

Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ndogo ya Mbowe, Superitendent Jumanne Malangahe atoa Ushahidi

Dar es Salaam. Shahidi wa kwanza katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ametoa ushahidi leo Jumatano Novemba 10, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kesi hii ndogo inatokana na pingamizi la mawakili wa utetezi kupinga kupokewa maelezo ya onyo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi.

Shahidi huyo, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru (OC-CID), mkoani Arusha, Mrakibu wa Polisi (SP) Jumanne Malangahe aliieleza mahakaka hiyo kuwa ndiye aliyeandika maelezo ya Mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

Shahidi anaongozwa na Wakili wa Serikali Robert Kidando.

Shahidi: Namfahamu Mohamed Abdilkahi Ling'wenya tangu Agosti 5, 2020 baada ya kumkamata eneo la Rao Madukani Moshi mkoani Kilimanjaro siku hiyo.

Shahidi: Nilimkamata kutokana na kuwepo kwa taarifa za kujihusisha na kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi ambavyo ni mpango wa kulipua au kuchoma vituo vya mafuta maeneo ya mikusanyiko ya watu kama masoko, kukata miti ama magogo na kuyaweka barabarani pamoja na kuwadhuru viongozi wa Serikali akiwemo akiyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Ole Sabaya.
Shahidi: Vitendo hivyo vilikusudiwa kufanyika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar, Mbeya na Mwanza

Shahidi: Dhumuni la vitendo hivyo lilikuwa ni kuleta hofu kwa wananchi na kuonesha kwamba nchi haitawaliki

Shahidi: Wakati namkamata siku hiyo nilikuwa na askari wenzangu watano, tukiongzwa na ACP Ramadhani Kingai akiyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Insp Mahita, DC Francis Ditek Konstebo Goodluck ambao alikuja nao Afande Kingai kutokea Arusha mjini.
Shahidi: Ukamataji huo ulifanyika saa 7 Mchana eneo hilo la Rau Madukani tulikofika tukiwa sisi watano, tukagawanyika maeneo mawili, moja akiongoza ACP Kingai, Mimi na Goodluck na eneo lingine alikwenda Insp. Mahita na Koplo Francis.

Shahidi: Tulijigawa maeneo mawili kulia na kushoto mwa Kibanda ambacho alikuwemo Mohamed Ling'wenya na wenzake wawili walikuwa Adamu Kasekwa na Moses Lujenge maarufu kama Kakobe.

Shahidi: Ukamataji kwa namna tulivyojigawa kibandanikulikuwa na njia mbili....

Jaji Tiganga: Samahani wakili, naona Kama shahidi anatoa ushahidi si kwenye kesi ndogo naomba afocus ushahidi wa kesi ndogo.
Wakili Kidando: Sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili: Sasa baada ya kumkamata mlimpeleka wapi?

Shahidi: Tulimpeleke kituo kikuu cha Polisi Moshi lakini kufika alibaki ndani ya gari sababu tulikuwa tunataka kwenda kumtafuta Moses Lujenge na Mohamed Ling'wenya alilidhia kwenda kutusaidia kumkamata.

Shahidi: Kwenye gari alibaki na ACP Kingai na DC Goodluck, mimi nilikabidhi vielelezo vilivyodhaniwa dawa za kulevya

Shahidi: Tulipitia maeneo mbalimbali mjini Moshi kama KCMC, Rao Madukani, Pasua, Majengo, Aisho Hotel mpaka Boma ambako Mohamed Ling'wenya mwenyewe alikuwa akituonesha kuwa angeweza kupatikana huko.

Shahidi: Ilipofika usiku saa tatu kuelekea saa nne tulikula chakula eneo la Boma tukiwa na mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya akiwa na hali nzuri na baada ya hapo tuliamua kurudi kituo cha Polisi maana hatukumpata Moses Lujenge.

Shahidi: Wakati huo kwenye gari mtuhumiwa alikuwa amekaa katikati yangu na Insp Mahita na mtuhumiwa mwingine alikuwa amekaa siti za nyuma na DC Goodluck.

Shahidi: Baada ya juhudi zote kumpata Lujenge tulirudi Polisi Moshi ambako tuliwakabidhi watuhumiwa kwa Askari wa mashtaka Polisi Moshi, saa nne kuelekea saa tano usiku.

Shahidi: Pale kituoni kama zilivyo taratibu baada ya kufikishwa mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya alipokewa ambapo aliulizwa haki yake na akawekwa mahabusu mimi na kiongozi wetu na Askari wenzangu tuliondoka kwenda kuendelea na shughuli nyingine za upelelezi.

Alikaa pale mpaka asubuhi Agosti 6, 2020 ambapo saa 1 tulifika pale tukiongozwa na Afande Ramadhani Kingai na mimi nilimchukua mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na mwenzake kuendelea kumtafuta Moses Lujenge kadri Mohamed Ling'wenya alivyokuwa akituongoza na kutushauri.

Shahidi: Zoezi la kumtafuta Moses Lujenge likiendelea kuanzia asubuhi hiyo mpaka jioni saa 12 ambapo hapakuwa na mafanikio ya kumpata Moses Lujenge. Katika kumtafuta Moses Lujenge tulipita maeneo ya pale Moshi mjini, KCMC, Boma Aishi Hotel na tulikwenda mpaka Arusha Sakina ambako watuhumiwa walisema kuna dada yake Moses Lujenge.

Shahidi: Katika maeneo yote ambayo Mohamed Ling'wenya alikuwa akituongoza maeneo ambayo tungeweza kumpata Moses Lujenge.

Shahidi: Muda wa saa 12 jioni tukiwa kituoni Moshi ndipo Afande Ramadhani Kingai alituelekeza kuwa tunatakiwa kusafiri kuwaleta Dar watuhumiwa hao kwa ajili ya kuendelea na Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wengine ambao walikuwa hawajakamatwa.

Shahidi: Sababu za kuwaleta Dar ndiko shauri la tuhuma zilizokutwa zikiwakabili lilipofunguliwa pamoja na uzito wa tuhuma zao.

Shahidi: Tulianza safari ya kuja Dar ikiwa saa moja na kufika Himo gari yetu ilipata tatizo na Afande ACP Kingai alifanya mawasiliano na uongozi wa Polisi Kilimanjaro na kuomba msaada wa gari lingine.

Shahidi: Tukiwa hapo tuliagiza chakula tukala na mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya akiwa hali nzuri

Shahidi: Kwenye saa 3 gari ya RPC Kilimanjaro ilifika ikiwa na derva wa RPC, DC Uwembo, gari aina ya Fortune na tukaanza safari

Shahidi: ACP Kingai alikaa mbele na dereva, katikati kushoto nikikaa Mimi na mtuhumiwa Adamu Kasekwa akikaa katikati na kulia akikaa Insp.Mahita na nyuma alikaa mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na DC Goodluck.

Shahidi: Safari yetu hiyo ya takribani saa 8 ilitufikisha kituo cha Polisi Kati Dar na ilikuwa ni majira ya saa 11 kuelekea saa 12.
Shahidi: Baada ya kufika kituoni hapo mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya alipokewa katika chumba cha mashtaka na niliwakabidhi mimi nikiwa na Afande Ramadhani Kingai.

Shahidi: Kwa mafunzo yetu Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kumpokea mtuhumiwa na kumuweka lockup

Shahidi: Walipokewa na kuwekwa mahabusu na sisi tuliondoka

Shahidi: Madai ya mtuhumiwa Mohamed Abdillahi Ling'wenya kuteswa mikononi mwa Polisi, hakuwahi kuteswa hata kidogo tangu tunamkamata na tulikuwa tunazunguka naye maeneo ya shughuli za wazi na alipokelewa na askari wa chumba cha mashtaka vizuri kwani angekuwa na tatizo asingepokewa

Shahidi: Tangu kumfikisha Polisi Agosti 5, 2020 na kumkabidhi mtuhumiwa hatukuendelea na chochote kuhusiana na mtuhumiwa kwani sisi wote tulielekezwa na kiongozi wetu Afande Kingai kuondoka kuendelea na majukumu mengine ya kiupelelezi.

Shahidi: Baada ya kumkabidhi kituo cha Polisi Kati Dar, tuliondoka kwa muda sisi na kiongozi wetu Afande ACP Ramadhani Kingai na majira ya saa moja asubuhi Agosti 7, 2020 Afande ACP Ramadhani Kingai alinielekeza kumhoji mtuhumiwa.

Shahidi: Nilifuatilia chumba cha kufanyia mahojiano hayo.

Shahidi: Kwenye saa 2 asubuhi nilifanikiwa kupata chumba na saa 2:10 nilikwenda kumtoa mahabusu mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na kwenda kukaa naye kwenye chumba hicho cha mahojiano kilichokuwa jirani kabisa na chumba cha mashtaka.

Shahidi: Nilipokwenda kumchukua mahabusu mtuhumiwa nilisaini kwenye kitabu Detention Register kutoka chumba cha mashtaka kuonesha kwamba sasa yuko mikononi mwangu.

Shahidi: Nikiona hiyo document naweza kuitambua kwa kuwepo kwa saini yangu eneo ambalo linaonesha kutoa mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano ya upelelezi

Wakili Kidando: Anaomba kielelezo cha kwanza kwenye kesi ndogo ya kwanza ili kumuonesha shahidi

Wakili Jeremiah Mtobesy :Anasimama na kutoa hoja kwamba wakili hajaeleza hicho kielelezo ni nini kwa kuwa si sehemu ya kesi hi ndogo sasa anapaswa aseme kama ni kielelezo au anaitaka kwa ajili ya utambuzi.

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji ni kweli hicho kielelezo si sehemu ya trial within trial hi lakini shahidi ameshaweka msingi wake katika ushahidi wake.

Jaji Tiganga: Wakili ameomba kielelezo hicho Kama kwamba kiko masijala sasa hatujajua anataka kufanyia nini, kwa hiyo ngoja tuone Kama anachotaka kufanya ndipo utaweza kusema
Wakili Kidando: Anaendelea kumhoji shahidi jinsi anavyoweza kuitambua DR hiyo naye shahidi anaeleza kuwa ni sahihi yake na tarehe ya kumtoa mtuhumiwa na jina lake.

Kisha Wakili Kidando anampa aikague Kisha aoneshe hayo maeneo aliyoyataja Kama alama za kuitambua

Shahidi anapekuwa DR hiyo Kisha anataja kuwa ni uwepo wa majina ya mtuhumiwa, kumbukumbu ya shauri na saini yake.

Naiomba mahakama iipokee DR hii kwa utambuzi

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa tuna objection kupokewa kwa nyaraka hii sababu shahidi hajaweka foundation maana hajasema tangu aachane na nyaraka hii alikutana nayo lini na vipi?

Yule anayeomba kuitoa lazina awe competent witness na competence ya shahidi inaenda mpaka shahidi anapo- authenticate document for admission.

Na Mahakama ya Rufani ilishasema shahidi lazima authenticate hiyo document na la pili katika authentication ni chain of custody ambayo inakwenda kwenye ku-lay foundation.

Ni rai yetu kwamba shahidi haja-lay chain of custody wala authentication.

Kwa mfano angeweza kusema kwamba kitabu hiki ni unique na kinatumika Central Police tu Dar na kwamba entries hizi akizifanya akiwa Central Police. Entries zake hizi tu hazimfanyi kuweza kuitoa.

Lakini kama nilivyosema tangu aachane nacho kitabu hiki Agosti 7, 2020 ame-lay foundation.

Mawakili wengine nao wanaunga mkono pingamizi hilo kwa hoja za Mtobesya na Wakili Kibatala anaongeza kuwa zoezi la kutoa kielelezo kwa utambuzi ni la kisheria na lina masharti yake ya kisheria na ya kiushahidi na hawezi kuja mtu kutoka mahali popote tu na kutaka kukiwasilisha.

Wakili Kibatala: Kielelezo hiki kipo katika kesi ndogo nyingine ambayo ni tofauti kabisa na hii na Kama Jamhuri walitaka kuitumia walipaswa kuiomba kwanza irudi kwenye custody yao au kufanya hatua nyingie.

Wakili Kibatala: Bahati mbaya hata shahidi hajazungumza uhusiano wake na shahidi wa pili katika kesi ndogo ya Adamu Kasekwa ambaye ndiye aliyeiwasilisha.

Wakili Kibatala: Kwa hiyo bado kuna vigezo ambavyo havikuzingatiwa hata kama inatolewa kwa utambuzi kwa hiyo tunaipinga kabisa

Kidando: Mheshimiwa Jaji sisi tunaomba ahirisho fupi ili tuweze kupitia hiyo nyaraka ili tuje kujibu hoja za wenzetu.

Wakili Kibatala: Hatuna pingamizi ila tunaweka tu angalizo lisiwe la muda mrefu maana tumechelewa kuanza kwa sababu ya ombi lao.

Jaji Tiganga: Dakika 30 zitanatosha? basi tutarudi saa 8:00.

Kesi inaahirishwa
Utetezi kabeni penati tu...mawinga wote wao..sasa ninyi kabeni penati lango liwe dogo!!
 
Martin Maranja Masese.
search huyo jamaa Twitter, utaziona updates za leo mkuu.
 
View attachment 2005439

Baada ya Mawakili wa Utetezi kuweka pingamizi kuhusu ushahidi wa Afande Jumanne, ikakubaliwa kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ili kupata majibu halali ya kisheria kutokana utata uliopo.

Kesi hiyo inaendelea leo Mahakamani hapo
Leo mmenyang'anywa tablets au kalamu zenu za kuandikia au kuna nini? Maana uzi wako ume - stagnate, hakuna updates ya kinachoendelea huko...!!
 
KINACHOENDELEA MAHAKAMANI

MAWAKILI WOTE UPANDE WA JAMHULI WAMEFIKA MAHAKAMANI.

MAWAKILI UPANDE WA UTETEZI WAMEFIKA KASORO MMOJA AMBAE AMEOMBEWA UDHURU NA ATAFIKA BAADAE.

•WAKILI UPANDE WA JAMHULI ANAMUELEZA JAJI KUWA KATIKA SHAURI DOGO(TRIAL WITHIN TRAIL) MASHAHIDI WATAKUWA SITA(06) NA VIELELEZO VINNE(04), NA LEO KUNA SHAHIDI MMOJA.

•SHAHIDI WA KWANZA AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA SHAHIDI NAMBA NANE(08) KATIKA KESI KUU:-
SP JUMANNE MARAGAHE,MIAKA 46, AFISA WA POLISI,MUISLAMU.

•WAKILI UPANDE WA JAMHULI ANAMUONGOZA SHAHIDI KUTOA USHAHIDI WAKE.
KINACHOENDELEA MAHAKAMANI

WAKILI UPANDE WA JAMHULI ANAMUONGOZA SHAHIDI KUTOA USHAHIDI WAKE KAMA IFUATAVYO;

WAKILI:-KAZI YAKO YA AFISA WA POLISI UNAIFANYIA WAPI.
SHAHIDI:-ARUMERU MKOANI ARUSHA.

WAKILI:-NAFASI YAKO NI IPO KATIKA WALYA YA ARUMERU
SHAHIDI:-MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI KATIKA WILAYA YA ARUMERU.

WAKILI:-KUNA MTU ANAITWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA,EBU ELEZEA HAPA MAHAKAMANI.
SHAHIDI:-NAMFAHAMU BWANA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA.

WAKILI:-TANGIA LINI UNAMFAHAMU.
SHAHIDI:-NAMFAHAMU TANGU 05/08/2020.

WAKILI:- ULIMFAHAMI VIPI.
SHAHIDI:-NILIMFAHAMU BAADA YA KUMKAMATA RAU MADUKANI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

WAKILI:-NINI KILITOKEA HADI KUMKAMATA.
SHAHIDI:-NILIMKAMATA BAADA YA KUWEPO NA TAARIFA KWAMBA ANAJIHUSISJA NA KILA NJAMA YA VITENDO VYA KIGAIDI.

WAKILI:-VITENDO GANI VYA KIGAIDI.
SHAHIDI:-VITENDO VYA KIGAINI KAMA VILE MPANGO WA KULIPUA VITUO VYA KUUZIA MAFUTA, KUCHOMA MOTO NA KULIPUA MAENEO YENYE MKUSANYIKO WA WARU WENGI KAMA MASOKO,KUKATA MITI AU MAGOGO KUYAWEKA BARABARANI PAMOJA NA KUWADHURU VIONGOZI WA SERIKALI AKIWEMO ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA HAI OLE SABAYA.

WAKILI:- VITENDO HIVYO VYA KIGAIDI VILIPANGWA KUFANYIKA SEHEMU ZIPI.
SHAHIDI:-VITENDO HIVYO VILIKUSUDIWA KUFANYWA KATIKA MIKOA KADHAA HAPA NCHINI AMBAYO NI DAR ES SALAAM,MBEYA ,MWANZA,ARUSHA NA KILIMANJARO.

WAKILI:-DHUMUNI HASA LA VITENDO HIVYO ILIKUWA NI NINI.
SHAHIDI:-DHUMUNI LA VITENDO HIVYO ILIKIWA KULETA HOFU AU KUWAOGOFYA WANANCHI NA KUWAONYESHA KUWA NCHI HAITAWALIKI.

WAKILI:-ULIKWA NA NA NANI WAKATI WA UKAMATAJI.
SHAHIDI:-SIKU IYO WAKATI NKAMAYA ENEO LA RAU MADUKANI NILIKUWA NA ASKALI WENZANGU AMBAO JUMLA TULIKUWA WATANO, TUKIONGOZWA NA AFANDE RAMADHAN KINGAI AMBAYE ALIKUWA KIONGOZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA ARUSHA. WENGNE NI INSP MAHITA, DITECTIVE FRANCIS, DITECTIVE GOODLUCK.

WAKILI:-HAO KINA INSP MAHITA, DC FRANCIS, DC GOODLUCK WALITOKA WAPI.
SHAHIDI:-HAWA NI ASKALI ALIOKUJA NAO AFANDE RSO RAMADHAN KINGAI.

WAKILI:-ELEZEA ILIKUWAJE KATIKA UKAMATAJI.
SHAHIDI:-UKAMATAJI ULIFANYIKA SAA 7 MCHANA KATIKA ENEO LA RAU MADUKANI AMBAPO TULIFIKA SISI WOTE WATANO NA TULIGAWANYIKA KATIKA MANENENO MAWILI, AMBAPO ENEO MOJA ALIKUWA RAMADHAN KINGAI MIMI MWENYEWE NA AFANDE GOODLUCK NA UPANDE MWINGINE WALIKUWA INSP MAHITA NA AFANDE FRANCIS.

WAKILI:-BAADA YA KUJIGAWA KATIKA SEHEMU MBILI,ELEZEA SASA UKAMATAJI ULIKUWAJE.

JAJI:- NAONA KAMA ANATOA USHAHIDI KWA UJUMLA NA SIO KWENYE KESI NDOGO.

WAKILI:-BAADA YA KUWA MMEMKAMATA MLIMPEKLEA WAPI.
SHAHIDI:-BAADA YA KUMKAAMATA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA TULIMPELEKA KITUO CHA POLISI KATI MOSHI. ALIKUWA NA MTUHUMIWA MWENZAKE ADAM HASSAN KASEMA.

WAKILI:-MLIPOFIKA HAPO KITUO CHA POLISI KATI MOSHI,MLIMPELEKA WAPI MTUHUMIWA HUYO.
SHAHIDI:-BAADA YA KUFIKA KITO CHA POLISI MTUHUMIWA ALIBAKI KWENYE GARI KWANI TULITAKA KWENDA KUMKAMATA MTUHUMIWA MWINGINE MOSES LIJENJE NA MTUHUMIWA.

WAKILI:-KWENYE GARI ALIBAKI NA NANI.
SHAHIDI:-KWENYE GARI ALIBAKI NA ASP RAMADHAN KINGAI NA DC FRANCIS. MIMI NA AFANDE MAHITA TULIINGIA KUTUONI NA NIKAMUELEKEZA KUFUNGUA KESI YA MADAWA YA KULEVYA.

WAKILI:-NINI KILIENDELEA NA MTUHUMIWA PALE KITUONI.
SHAHIDI:-BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI ZOTE PALE KITUO CHA POLISI TULITOKA NA MTUHUMIWA KWENDA SEHEMU MBALIMBALI AMBAPO MTUHUMIWA ALITOA USHIRIKIANO SEHENU AMBAZO TUNGEMKAMATA MOSES LIJENJE. TULIENDA SEHEMU MBALIMBALI AMBAZO YEYE MTUHUMIWA ALIKUWA AKIZIONESHA.

WAKILI:-KATIKA MAENEO YOTE MLIYOPITA NINI HASA KILIENDELEA DHIDI YA MTUHUMIWA MOHAMEDI LING'WENYA.
SHAHIDI:-ALIKIWA ANATUONGOZA MAENEO MBALIMBALI AMBAYO YANGEWEZESHA KUMPATA HUYO MTUHUMIWA MWINGINE HADI MAJIRA YA USIKU NA TUKAPATA CHAKULA KISHA TUKARUDI KITUO CHA POLISI KATI MOSHI BAADA YA KUTOKUFANIKIWA KUMPATA MOSES LIJENJE.

WAKILI:-
KATIKA NAENEO YOTE HAYO MLIKUWA NA AKINA NANI.
SHAHIDI:-KATIKA MAENEO YOTE TULIKUWA NA INSP MAHITA, DC FRANCIS, DC GOODLUCK NA DEREBA CONSTABLE AZIZI.

WAKILI:-MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA ALIKUWA AMEKAA WAPI.
SHAHIDI:-MTUHUMIWA ALIKUWA KATIKA YANGU MIMI NA INSP MAHITA.

WAKILI:-MTUHUMIWA MWINGINE ALIKUWA WAPI.
SHAHIDI:-MTUHUMIWA MWINGINE ALIKUWA AMEKAA NYUMA NA DC GOODLUCK.

WAKILI:-BAADA YA MIZUNGUUKO YOTE WALE WATUHUMIWA MLIWAPELEKA WAPI.
SHAHIDI:-BAADA YA KURUDI KITUO CHA POLISI,TUKAWAKABIDHI WATUHUMIWA ILIKUWA NA MUDA WA SAA NNE KUELEKEA SAA TANO USIKU.

WAKILI:-BAADA YA KUWAKABIDHI WATUHUMIWA KUTUO CHA POLISI NINI KILIENDELEA DHIDI YA MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA.
SHAHIDI:-BAADA YA KUWAKABIDHISHA WATUHUMIWA KATIKA KITUO CHA POLISI, WATUHUMIWA WALIHIFADHIWA LOCKUP WAKIWA NA AFANYA NZURI.

SHAHIDI:-MIMI NA ASKALI WENZANGU TULIONDOKA KUENDELEA NA SHUGHULI ZA KIPELELEZI.

WAKILI:-MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA ALIKAA PALE KITUONI KWA SIKU NGAPI.
SHAHIDI:-BAADA YA MTUHUMIWA MOHAMED ABDULAHI LING'WENYA KUKABIDHIWA PALE KITUONI ALIKAA HADI ASUBUHI TAREHE 06/08/2020.

WAKILI:-NINI KILIENDELEA HIYO SIKU YA TAREHE 06/08/2020.
SHAHIDI:-ASUBUHI YA TAREHE 06/08/2020 TULIWACHUMUWA WATUHUMIWA NA KWENDA NAO KUSAIDA KUMTAFUTA MTUHUMIWA MWINGINE MOSES LIJENJE.

WAKILI:-ZOEZI LA KUMTAFUTA MOSES LIJENJE LILICHUKUA MUDA GANI.
SHAHIDI:-ZOEZI HILO LA KUMTAFUTA MOSES LING'WENYA LILIENDELEA KUANZIA ASUBUHI SAA 11 MPAKA JIONI SAA 12 JIONI,NA HAPAKUWA NA MAFANIKIO YA KUMPATA MOSES LIJENJE.

WAKILI:-WAKATI MNAENDELEA KUMTAFUTA KATIKA MAENEO YOTE NINI KILIENDELEA DHIDHI YA MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA.
SHAHIDI:-WAKATI TUNAENDELEA NA ZOEZI LA KUMTAFUTA MOSES LIJENJE HAKUNA CHOCHOTE KILICHOENDELEA DHIDI YA KUTOA USHIRIKIANO.

WAKILI:-NINI KILIENDELEA BAADA YA KURUDI KUTOANI.
SHAHIDI:-BAADA YA KURUDI KITUONI NDIPO AFANDE KINGAI ALITUELEZA KUWA WATUHUMIWA WANATAKIWA KUSAFIRISHWA KWENDA DAR ES SALAAM ILI KUENDELEA NA UPELELEZI MWINGINE NA WATUHUMIWA AMABAO HAWAJKAMATWA.

WAKILI:-KWANINI WATUHUMIWA WASAFIRISHWE KWENDA DAR ES SALAAM.
SHAHIDI:-SHAURI LENYEWE KUFUNGULIWA KITUO CHA KATI CHA DAR ES SALAAM NA UZITO WA SHAURI LENYEWE NA UHARIFU ULIOKUWA UMEKUSUDIWA KUFANYIKA.

WAKILI:-SAFARI YA KWENDA DAR ES SALAAM ILIANZA SAA NGAPI.
SHAHIDI:-MIDA YA SAA MOJA USIKU TUKIANZA SAFARI YA KWENDA DAR ES SALAAM, LAKINI NJIANI TULIPATA NA CHANGAMOTO YA GARI, NA AFANDE KINGAI ALIPIA SIKU ILI KUPATA GARI LINGINE. TUKIWA PALE TUNASUBUKI GARI TULIPATA CHAKULA NA MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA HAKUWA NA TATIZO LOLOTE.

WAKILI:-SAFARI YENU ILIKUWAJE HADI KUFIKA DAR ES SALAAM.
SHAHIDI:-SAFARI YETU ILOKUWA YA TAKLIBAN MAASA 8 NA TULIFUKA KITUO CHA KATI DAR ES SALAAM ALFAJIRI YA TAREHE 07/08/2020.

WAKILI:-NINI KILIENDELEA DHIDI YA MTUHUMIWA MOHAMEDI LING'WENYA.
SHAHIDI:-KWANZA TULIPOFIKA KITUONI HAPO MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA ALIPOKELEWA NA ASKALI WA KITUONI.

WAKILI:-NA NI NANI ALIYEWAKABIDHI HAPO KITUONI.
SHAHIDI:-ALIYEWAKABUDHI NI MIMI MWENYEWE NA AFANDE RAMADHAN KINGAI.

WAKILI:-WAKATI MNAMKABIDHI MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA NINI KILITOKEA.
SHAHIDI:-KILICHOTOKEA PALE KITUONI WATUHUMIWA WALIPOKELEWA NAKUPELEKWA MAHABUSU, NA SISI TULIONDOKA.

WAKILI:-KUNA MADAI KWAMBA MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA ALITESWA BAADA YA KUKAMATWA
SHAHIDI:-TANGU TUNAMKAMATA NA KUMUWEKA CHINI YA ULINZI HAKUWAHI KUTESWA HATA KIDOGO, NA HATA ALIPOPOKELEWA KITUO CHA POLISI MOSHI HAKUWA NA TATIZO LOLOTE KWANI ANGEKUWA NA TATIZO ASINGE POKELEWA.

WAKILI:-TANGU MNAMKABIDHI PALE KITUONI MOSHI NINI KILIENDELEA DHIDI YA MTUHUMIWA MOHAMEDI ABDULAHI LING'WENYA.
SHAHIDI:-TANGU TUMEMFIKISHA KITUO CHA POLISI MOSHI TAREHE 05/08/2020 NA HADI ALFAJIRI YA TAREHE 06/08/2020 HAKUNA CHOCHOTE KILICHOENDELEA DHIDI YA MTUHUMIWA.
 
Atleast umejitahidi, updates za twitter sometimes zinachanganya hazina mpangilio mzuri kama hapa jf, muhimu endelea kuzishusha mpaka mwisho kesi itakapoahirishwa.
 
Kwa mwandiko wake huu, mimi nimeshindwa hata kuamini kuwa haya ndiyo yanayotokea huko mahakamani...!

Amosmgonja andika kwa kutumia herufi ndogo kama tulivyofundishwa shuleni katika "uandishi wa insha"
 
Jf sometimes michosho sana, sasa updates ziko wapi mpaka muda huu?

Kesi mpaka imeahirishwa hakuna update yeyote iliyowekwa zaidi ya mabishano
 
Leo mmenyang'anywa tablets au kalamu zenu za kuandikia au kuna nini? Maana uzi wako ume - stagnate, hakuna updates ya kinachoendelea huko...!!
Wamekosa cha kuandika. Itakuwa wamegaragazwa huko mahakamani. Ndiyo shida ya waandishi biased. Ling'wenya atakuwa kakubaliana na upande wa mashitaka kwamba hakuteswa, maelezo hayo aliyatoa hapo central police ya DSM kwa hiari yake.
 
Dunia nzima inafahamu kwamba Mbowe siyo Gaidi na inafahamu pia kwamba hizi ni njama za kishamba za serikali ya Tanzania kuogopa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi
tatizo CCM wameweka pamba masikioni, hawajali nini kitafuatia baada ya kutimiza azma yao ya kumfunga Mbowe.
 
Back
Top Bottom