View attachment 2005439
Baada ya Mawakili wa Utetezi kuweka pingamizi kuhusu ushahidi wa Afande Jumanne , ikakubaliwa kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ili kupata majibu halali ya kisheria kutokana utata uliopo .
Kesi hiyo inaendelea leo Mahakamani hapo
Dar es Salaam. Shahidi wa kwanza katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ametoa ushahidi leo Jumatano Novemba 10, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Kesi hii ndogo inatokana na pingamizi la mawakili wa utetezi kupinga kupokewa maelezo ya onyo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi.
Shahidi huyo, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru (OC-CID), mkoani Arusha, Mrakibu wa Polisi (SP) Jumanne Malangahe aliieleza mahakaka hiyo kuwa ndiye aliyeandika maelezo ya Mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling’wenya.
Shahidi anaongozwa na Wakili wa Serikali Robert Kidando.
Shahidi: Namfahamu Mohamed Abdilkahi Ling'wenya tangu Agosti 5, 2020 baada ya kumkamata eneo la Rao Madukani Moshi mkoani Kilimanjaro siku hiyo.
Shahidi: Nilimkamata kutokana na kuwepo kwa taarifa za kujihusisha na kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi ambavyo ni mpango wa kulipua au kuchoma vituo vya mafuta maeneo ya mikusanyiko ya watu kama masoko, kukata miti ama magogo na kuyaweka barabarani pamoja na kuwadhuru viongozi wa Serikali akiwemo akiyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Ole Sabaya.
Shahidi: Vitendo hivyo vilikusudiwa kufanyika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar, Mbeya na Mwanza
Shahidi: Dhumuni la vitendo hivyo lilikuwa ni kuleta hofu kwa wananchi na kuonesha kwamba nchi haitawaliki
Shahidi: Wakati namkamata siku hiyo nilikuwa na askari wenzangu watano, tukiongzwa na ACP Ramadhani Kingai akiyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Insp Mahita, DC Francis Ditek Konstebo Goodluck ambao alikuja nao Afande Kingai kutokea Arusha mjini.
Shahidi: Ukamataji huo ulifanyika saa 7 Mchana eneo hilo la Rau Madukani tulikofika tukiwa sisi watano, tukagawanyika maeneo mawili, moja akiongoza ACP Kingai, Mimi na Goodluck na eneo lingine alikwenda Insp. Mahita na Koplo Francis.
Shahidi: Tulijigawa maeneo mawili kulia na kushoto mwa Kibanda ambacho alikuwemo Mohamed Ling'wenya na wenzake wawili walikuwa Adamu Kasekwa na Moses Lujenge maarufu kama Kakobe.
Shahidi: Ukamataji kwa namna tulivyojigawa kibandanikulikuwa na njia mbili....
Jaji Tiganga: Samahani wakili, naona Kama shahidi anatoa ushahidi si kwenye kesi ndogo naomba afocus ushahidi wa kesi ndogo.
Wakili Kidando: Sawa Mheshimiwa Jaji
Wakili: Sasa baada ya kumkamata mlimpeleka wapi?
Shahidi: Tulimpeleke kituo kikuu cha Polisi Moshi lakini kufika alibaki ndani ya gari sababu tulikuwa tunataka kwenda kumtafuta Moses Lujenge na Mohamed Ling'wenya alilidhia kwenda kutusaidia kumkamata.
Shahidi: Kwenye gari alibaki na ACP Kingai na DC Goodluck, mimi nilikabidhi vielelezo vilivyodhaniwa dawa za kulevya
Shahidi: Tulipitia maeneo mbalimbali mjini Moshi kama KCMC, Rao Madukani, Pasua, Majengo, Aisho Hotel mpaka Boma ambako Mohamed Ling'wenya mwenyewe alikuwa akituonesha kuwa angeweza kupatikana huko.
Shahidi: Ilipofika usiku saa tatu kuelekea saa nne tulikula chakula eneo la Boma tukiwa na mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya akiwa na hali nzuri na baada ya hapo tuliamua kurudi kituo cha Polisi maana hatukumpata Moses Lujenge.
Shahidi: Wakati huo kwenye gari mtuhumiwa alikuwa amekaa katikati yangu na Insp Mahita na mtuhumiwa mwingine alikuwa amekaa siti za nyuma na DC Goodluck.
Shahidi: Baada ya juhudi zote kumpata Lujenge tulirudi Polisi Moshi ambako tuliwakabidhi watuhumiwa kwa Askari wa mashtaka Polisi Moshi, saa nne kuelekea saa tano usiku.
Shahidi: Pale kituoni kama zilivyo taratibu baada ya kufikishwa mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya alipokewa ambapo aliulizwa haki yake na akawekwa mahabusu mimi na kiongozi wetu na Askari wenzangu tuliondoka kwenda kuendelea na shughuli nyingine za upelelezi.
Alikaa pale mpaka asubuhi Agosti 6, 2020 ambapo saa 1 tulifika pale tukiongozwa na Afande Ramadhani Kingai na mimi nilimchukua mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na mwenzake kuendelea kumtafuta Moses Lujenge kadri Mohamed Ling'wenya alivyokuwa akituongoza na kutushauri.
Shahidi: Zoezi la kumtafuta Moses Lujenge likiendelea kuanzia asubuhi hiyo mpaka jioni saa 12 ambapo hapakuwa na mafanikio ya kumpata Moses Lujenge. Katika kumtafuta Moses Lujenge tulipita maeneo ya pale Moshi mjini, KCMC, Boma Aishi Hotel na tulikwenda mpaka Arusha Sakina ambako watuhumiwa walisema kuna dada yake Moses Lujenge.
Shahidi: Katika maeneo yote ambayo Mohamed Ling'wenya alikuwa akituongoza maeneo ambayo tungeweza kumpata Moses Lujenge.
Shahidi: Muda wa saa 12 jioni tukiwa kituoni Moshi ndipo Afande Ramadhani Kingai alituelekeza kuwa tunatakiwa kusafiri kuwaleta Dar watuhumiwa hao kwa ajili ya kuendelea na Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wengine ambao walikuwa hawajakamatwa.
Shahidi: Sababu za kuwaleta Dar ndiko shauri la tuhuma zilizokutwa zikiwakabili lilipofunguliwa pamoja na uzito wa tuhuma zao.
Shahidi: Tulianza safari ya kuja Dar ikiwa saa moja na kufika Himo gari yetu ilipata tatizo na Afande ACP Kingai alifanya mawasiliano na uongozi wa Polisi Kilimanjaro na kuomba msaada wa gari lingine.
Shahidi: Tukiwa hapo tuliagiza chakula tukala na mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya akiwa hali nzuri
Shahidi: Kwenye saa 3 gari ya RPC Kilimanjaro ilifika ikiwa na derva wa RPC, DC Uwembo, gari aina ya Fortune na tukaanza safari
Shahidi: ACP Kingai alikaa mbele na dereva, katikati kushoto nikikaa Mimi na mtuhumiwa Adamu Kasekwa akikaa katikati na kulia akikaa Insp.Mahita na nyuma alikaa mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na DC Goodluck.
Shahidi: Safari yetu hiyo ya takribani saa 8 ilitufikisha kituo cha Polisi Kati Dar na ilikuwa ni majira ya saa 11 kuelekea saa 12.
Shahidi: Baada ya kufika kituoni hapo mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya alipokewa katika chumba cha mashtaka na niliwakabidhi mimi nikiwa na Afande Ramadhani Kingai.
Shahidi: Kwa mafunzo yetu Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kumpokea mtuhumiwa na kumuweka lockup
Shahidi: Walipokewa na kuwekwa mahabusu na sisi tuliondoka
Shahidi: Madai ya mtuhumiwa Mohamed Abdillahi Ling'wenya kuteswa mikononi mwa Polisi, hakuwahi kuteswa hata kidogo tangu tunamkamata na tulikuwa tunazunguka naye maeneo ya shughuli za wazi na alipokelewa na askari wa chumba cha mashtaka vizuri kwani angekuwa na tatizo asingepokewa
Shahidi: Tangu kumfikisha Polisi Agosti 5, 2020 na kumkabidhi mtuhumiwa hatukuendelea na chochote kuhusiana na mtuhumiwa kwani sisi wote tulielekezwa na kiongozi wetu Afande Kingai kuondoka kuendelea na majukumu mengine ya kiupelelezi.
Shahidi: Baada ya kumkabidhi kituo cha Polisi Kati Dar, tuliondoka kwa muda sisi na kiongozi wetu Afande ACP Ramadhani Kingai na majira ya saa moja asubuhi Agosti 7, 2020 Afande ACP Ramadhani Kingai alinielekeza kumhoji mtuhumiwa.
Shahidi: Nilifuatilia chumba cha kufanyia mahojiano hayo.
Shahidi: Kwenye saa 2 asubuhi nilifanikiwa kupata chumba na saa 2:10 nilikwenda kumtoa mahabusu mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya na kwenda kukaa naye kwenye chumba hicho cha mahojiano kilichokuwa jirani kabisa na chumba cha mashtaka.
Shahidi: Nilipokwenda kumchukua mahabusu mtuhumiwa nilisaini kwenye kitabu Detention Register kutoka chumba cha mashtaka kuonesha kwamba sasa yuko mikononi mwangu.
Shahidi: Nikiona hiyo document naweza kuitambua kwa kuwepo kwa saini yangu eneo ambalo linaonesha kutoa mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano ya upelelezi
Wakili Kidando: Anaomba kielelezo cha kwanza kwenye kesi ndogo ya kwanza ili kumuonesha shahidi
Wakili Jeremiah Mtobesy :Anasimama na kutoa hoja kwamba wakili hajaeleza hicho kielelezo ni nini kwa kuwa si sehemu ya kesi hi ndogo sasa anapaswa aseme kama ni kielelezo au anaitaka kwa ajili ya utambuzi.
Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji ni kweli hicho kielelezo si sehemu ya trial within trial hi lakini shahidi ameshaweka msingi wake katika ushahidi wake.
Jaji Tiganga: Wakili ameomba kielelezo hicho Kama kwamba kiko masijala sasa hatujajua anataka kufanyia nini, kwa hiyo ngoja tuone Kama anachotaka kufanya ndipo utaweza kusema
Wakili Kidando: Anaendelea kumhoji shahidi jinsi anavyoweza kuitambua DR hiyo naye shahidi anaeleza kuwa ni sahihi yake na tarehe ya kumtoa mtuhumiwa na jina lake.
Kisha Wakili Kidando anampa aikague Kisha aoneshe hayo maeneo aliyoyataja Kama alama za kuitambua
Shahidi anapekuwa DR hiyo Kisha anataja kuwa ni uwepo wa majina ya mtuhumiwa, kumbukumbu ya shauri na saini yake.
Naiomba mahakama iipokee DR hii kwa utambuzi
Wakili Mtobesya: Mheshimiwa tuna objection kupokewa kwa nyaraka hii sababu shahidi hajaweka foundation maana hajasema tangu aachane na nyaraka hii alikutana nayo lini na vipi?
Yule anayeomba kuitoa lazina awe competent witness na competence ya shahidi inaenda mpaka shahidi anapo- authenticate document for admission.
Na Mahakama ya Rufani ilishasema shahidi lazima authenticate hiyo document na la pili katika authentication ni chain of custody ambayo inakwenda kwenye ku-lay foundation.
Ni rai yetu kwamba shahidi haja-lay chain of custody wala authentication.
Kwa mfano angeweza kusema kwamba kitabu hiki ni unique na kinatumika Central Police tu Dar na kwamba entries hizi akizifanya akiwa Central Police. Entries zake hizi tu hazimfanyi kuweza kuitoa.
Lakini kama nilivyosema tangu aachane nacho kitabu hiki Agosti 7, 2020 ame-lay foundation.
Mawakili wengine nao wanaunga mkono pingamizi hilo kwa hoja za Mtobesya na Wakili Kibatala anaongeza kuwa zoezi la kutoa kielelezo kwa utambuzi ni la kisheria na lina masharti yake ya kisheria na ya kiushahidi na hawezi kuja mtu kutoka mahali popote tu na kutaka kukiwasilisha.
Wakili Kibatala: Kielelezo hiki kipo katika kesi ndogo nyingine ambayo ni tofauti kabisa na hii na Kama Jamhuri walitaka kuitumia walipaswa kuiomba kwanza irudi kwenye custody yao au kufanya hatua nyingie.
Wakili Kibatala: Bahati mbaya hata shahidi hajazungumza uhusiano wake na shahidi wa pili katika kesi ndogo ya Adamu Kasekwa ambaye ndiye aliyeiwasilisha.
Wakili Kibatala: Kwa hiyo bado kuna vigezo ambavyo havikuzingatiwa hata kama inatolewa kwa utambuzi kwa hiyo tunaipinga kabisa
Kidando: Mheshimiwa Jaji sisi tunaomba ahirisho fupi ili tuweze kupitia hiyo nyaraka ili tuje kujibu hoja za wenzetu.
Wakili Kibatala: Hatuna pingamizi ila tunaweka tu angalizo lisiwe la muda mrefu maana tumechelewa kuanza kwa sababu ya ombi lao.
Jaji Tiganga: Dakika 30 zitanatosha? basi tutarudi saa 8:00.
Kesi inaahirishwa