Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

MUNGU afunue yaliyopo uvunguni.
Hakuna siri tutaacha jua mwaka huu, wewe uliwahi jua kuwa simu zako, sms, picha zako kuna watu wapo pembezoni mwa bahari wanaangalia? wanasikiliza?
unafikir kwanini Mwendazake alisemaga Jojo anasarandiwa na mkurugenzi wake, DAS mpaka Das akatumbuliwa?
 
mwendazake ndo ilikuwa tabia yake ndo maana kina nape na mzee makamba ,kinana sauti zao zilivujishwa
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimekuelewa mkuu, hapo kabla nilidhani vyeo vinaendana na dhamira kuu ya mtandao huu!

Kwa hiyo dhamira ya mtandao huu ni kuwa na mawazo yaliyo sawa? Mnafail sana mnapotaka kujiona mtu aliye na mlengo tofauti na wako kuwa hafai,hapa tunatumia ID Fake,unawezaje mkejeli
mtu kisa tu amekuwa na mtazamo tofauti na wako? Unamjua huyo mtu in real life? Mitandao hii isitufanye tukakosea watu heshima kisa tu unatumia ID fake.
 

Inawezekana kabisa na wao MIC wana utaratibu wao,swala hapo pengine liwe kujiridhisha,Je Freddy alifanya hayo yote bila Top Mgt kufahamu? Na kama ni ndiyo Freddy alijua kabisa alichokifanya kitakuja kutumika Mahakamani na yeye atasimama kama shahidi,siamini katka muktadha huo kama anaweza kuwa na courage ya kufanya hili bila Top Managament kuwa na taarifa.Kumbuka Freddy Makahakamani anasimama kuiwakilisha MIC (Tigo) na siyo yeye kama Freddy.
 
Haki yako unastahili pongezi za kila aina
 
Hii Tanzania kuna mtu hamfahamu mbowe? Nimeshangaa sana huyo shahidi msomi hafahamu mbowe ni kiongozi wa upinzani .
 
Nilitegemea akina Kibatala waulize ili Swali ili kujiridhisha.
Na ikitokea ndivyo basi ni muda muafaka eidha kuzikwepa kampuni za simu au kuziburuza mahakamani!

Hii kesi hadi ifike mwisho kuna mengi tutakuwa tumejifunza kuboresha survival skills.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mahakamani Kuna mambo Hadi maswali unnessary hivo ya nini?
Hawa mawakili waliowaweka wako pale ili kucheza na trend za mitandaoni, kijipatia umaarufu na wateja.Hakuna cha maana wanacho-push.
 
Mjinga n mjinga tu period, iwe ID fake iwe nje ya mtandao kama n mjinga ww n mjinga tu
 
Nilitegemea akina Kibatala waulize ili Swali ili kujiridhisha.
Na ikitokea ndivyo basi ni muda muafaka eidha kuzikwepa kampuni za simu au kuziburuza mahakamani!

Hii kesi hadi ifike mwisho kuna mengi tutakuwa tumejifunza kuboresha survival skills.
Hujafuatilia, kaulizwa maswali yote
 
Tigo na mnisikie Tena Kwa makini! Kuanzia Leo naitupa line yenu na kuachana na huduma zenu! Utaratibu Gani huu wa kutoa Siri za wateja wenu? Mna maana mteja kwenu Hana haki ya kupata faragha na ulinzi kutoka kwenu?
Naanzisha Uzi wa kuwakataa ninyi na huduma zenu kwani mnatuuza polisi bila kufuata Sheria za mawasiliano!
 
Acha urongo,polisi ni sita tu wengine wote ni raia wema.
Hao Raia una uhakika kuwa kweli ni Raia wa kawaida.... Bongo anything is possible. Mama Mtalo wa Rau tayari anaonyesha kuwa siye yule mama original mpika mbege....!!
 
Ni mtu mjinga tu anaeweza kuona maswali haya ni mepesi na hayana maana!
mpaka shahidi anatoka mahakamani haijulikani laini ya mbowe ilisajiriwa na nani kosa kubwa waulizeni mawakala huko mtaani kila wakala ana ID inayomfanya aingie kwenye mtandao na kumsajiri mtu hivyo basi ni kweli mboe alijisajiri mwenyewe.


Wakili Mallya: Ulisema ujuzi umepata kutokana na uzoefu, mafunzo na changamoto za kazi ulimweleza Jaji ni changamoto gani ulikuwa unapata?

Shahidi: Hapana

Wakili Mallya: Huyu mtu unasema anaitwa Freeman Mbowe kwenye maelezo taarifa umetaja kilimanjaro umeielezea mahakama?

Shahidi: Hapana

Wakili Mallya: Kilimanjaro kuna jiji

Shahidi: Hapana

Wakili Mallya: Huyu Mbowe alisajili mwenyewe?

Shahidi: Wakili anashindwa kuelewa hizi taarifa tulizuchukua Nida

Wakili: Hii nyaraka imetoka kwenu au Nida

Shahidi: Nida

Wakili: Aliyemsajili Mbowe nani?

Shahidi: Simjui

Wakili Mallya: Kwa kuwa taarifa za aliyemsajili Mbowe hazipo, kwa hiyo Mbowe alijisajili mwenyewe, nipo sahihi?

Shahidi: Hauko sahihi

Wakili Mallya: Ukiombwa taarifa za mimi na rafiki yangu tunatumiana pesa utatoa au hutoi?

Shahidi: Sitatoa

Wakili: Ulipoombwa taarifa za Mbowe ulihoji ni za nini

Shahidi:Sikuhoji

Wakili: Ukiwa kama mwanasheria hukuona sababu ya kuhoji kosa?

Shahidi: Sio sehemu ya majukumu yangu.

wakati akihojiwa na Mallya alisema haya,

Wakili Mallya: Kwanini hukuuliza Mbowe ana kosa gani ukatoa taarifa

Shahidi: Kwanza wakati zinaombwa sikujua ni nani, niliona tu namba na kuifanyia kazi.

wakati akihojiwa na Kibatala alisema hivi,

Wakili Kibatala: Unajua kwenye ishu hii Freeman Mbowe ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha upinzani

Shahidi:Simfahamu

Wakili Kibatala: Hujui Freeman ni Kiongozi wa chadema

Shahidi: Simfahamu Freeman Mbowe.

Huku sio kujichanganya huku ni kusema uongo period.
 
Nilitegemea akina Kibatala waulize ili Swali ili kujiridhisha.
Na ikitokea ndivyo basi ni muda muafaka eidha kuzikwepa kampuni za simu au kuziburuza mahakamani!

Hii kesi hadi ifike mwisho kuna mengi tutakuwa tumejifunza kuboresha survival skills.

Na ndiyo faida ya kupeana hapa mawazo mbadala,mtu unajikuta unapata uelewa mkubwa sana wa mambo flan,mpaka sasa wewe na The Palm Tree, ninajifunza mengi kwenu kutokana na mnavyoweza kuzijenga hoja kinzani.
 
Mkuu mtu akiangalia ataona umeandika bonge la point, ila una mwanasheria anayetoa ushahidi wa kujidanganya kwa kiwango hiki. Eti mwanasheria anasema hamjui Mbowe, yaani anaona akisema anamjua basi ataonekana msaliti. Simaanishi Mbowe ni maarufu sana, ila kwa mtu kama yeye kusema hamjui Mbowe ni ujuha na utoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…