Ikiwa leo ni tarehe 2 November 2021 , kesi hii inayobeba sehemu kubwa ya habari za Tanzania inaendelea tena Mahakamani hapo .
Baada ya ushahidi wa Muuza Mbege wa Rau Kukamilika , Leo upande wa Jamhuri utaleta shahidi wa Tano miongoni mwa wale 24 waliopangwa kutoa ushahidi huo .
Kama kawaida JF itakuletea moja kwa moja kesi hii kutoka Mahakamani , usiondoke .
===========
Jaji ameingia Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe Imeshatajwa
Wakili wa Serikali Robert Kidando Anatambulisha
1.Pius Hilla
2.Nassoro Katuga
3,Abdallah Chavula
4.Ester Martin
5.Jenitreza Kitali
6.Tulimanywa Majige
Kibatala anatambulisha Jopo lake
1. Michael Mwangasa
2.Seleman Matauka
3.Nashon Nkungu
4.Alex Massaba
5.Michael Lugina
6.Maria Mushi
7.Hadija Aron
8.Dickson Matata
9.Jonathan Mndeme
10.Fredrick Kihwelo
11. John Malya
Jaji Mashtakiwa 1,2,3 na 4 Wananyanyuka kuashiria uwepo wao
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tunashahidi Mmoja Kwa Leo Lakini Kabla ya Kuendelea Leo tuna ombi, Na Maombi yetu yatamuhusu Shahidi Wa Leo Mheshimiwa
Jaji: Wakati wa Kufile Mashahidi tuliorodhesha Majina Kama Frank Kapala
Jaji: Ndiyo
Wakili wa Serikali: na Kule Kwenye Comito Proceedings Katika Ukusara wa 32 wa zile proceeding za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilitaja Kama Frank Kapala Lakin kama tulivyo leta information Barua ya 11 August 2021 Ndiyo alitaja kama Frank Kapala Mheshimiwa Jaji Kwa Usahihi ....Shahidi huyu anaitwa Frank kapara.
Wakili wa serikali: Kwa hiyo tunaomba Kumbukumbu sahihi za Mahakama zi-note kama Frank Kapara Kwa kifungu 264 Sura ya 20 cha CPA Rev Ya 2009 Na Kwa sababu Ushahidi wa Shahidi huyu ulisomwa wakati wa Comito Proceedings tunaomba turuhusiwe Kuendelea na Shahidi huyu.
Jaji: Kifungu gani?
Wakili wa Serikali: 264 Sura ya 20 kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Maombi yetu ni hayo tu
Mtobesya: Tumesikia Maombi ya Upande wa Mashitaka na Kwa sababu Wanasema Substance ndiyo Iliyo contain Ushahidi Wake tangu Maelezo yake Polisi. Kwa Upande wetu hatuoni Kama inaathiri Haki za Mteja wetu, Hatupingi hilo Ombi Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Kwanza, Asante.
Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili hatuna Pingamizi.
Wakili Fredrick Kihwelo: hatuna Pingamizi Kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu.
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi Kwakuwa wameleta Maombi Rasmi.
Jaji: Samahani Kidogo, Unachotaka Kirekebishwe Unaweza Ku-Spell
Wakili wa Serikali: FREDY KAPALA
Jaji: Basi maombi ambayo yameletwa Kurekebisha Kumbukumbu za Mahakama Kuwa Shahidi alikuwa Frank Kampala na Sasa atafahamika kuwa ni FREDY Kapala Na hiyo ndiyo Itakuwa kumbukumbu Mpya ya Mahakama, NATOA AMRI. Mawakili wote Wananyuka na Kukubaliana na Jaji.
JAJI: Shahidi aletwe sasa
Wakili wa Serikali: Ameenda Kuitwa
Jaji: Anakuwa Shahidi Wa Ngapi huyo
Wakili wa Serikali: Shahidi 05
Jaji: Utetezi Ndiyo..?
Kibatala: Ndiyo
Jaji: Majina yako
Shahidi: Naitwa Afredy Kapala
Jaji: Umri
Shahidi: 38yr
Jaji: kabila
Shahidi: Mpare
Jaji: Shughuli yako
Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya Tigo
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni Kweli, kweli tupu Eenheeeee Mwenyezi Mungu nisaidie.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wakili Nasorro Katuga atamuongoza
Wakili wa Serikali Nasorro: Nitakuuliza Maswali
Wakili wa Serikali: Umesema Unashughulika na nini?
Shahidi: Nimeajiriwa na kampuni ya kibiashara inaitwa TIGO
Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Kampuni ya kibiashara
Shahidi: Kwa sababu kampuni iliyosainiwa Brela ni MIC Tanzania
Wakili wa Serikali: Jina la Kibiashara ndiyo
Shahidi: Tigo
Wakili wa Serikali: Kampuni ya MIC Tanzania Ltd Inafanya Shughuli gani?
Shahidi: Mawasiliano ya Simu pamoja na Mihamala ya Kifedha
Wakili wa Serikali: Mwambie Mheshimiwa Jaji Umeajiriwa lini
Shahidi: March Mwaka 2012
Wakili wa Serikali: Umeajiriwa kama nani?
Shahidi: Kama Mwanasheria wa Tigo
Wakili wa Serikali: Katika Kitengo Kipi
Shahidi: Kitengo cha Sheria
Wakili wa Serikali: Umesema Kampuni yako inajishughulisha Kutoa Mawasiliano ya Simu na Mihamala ya kifedha Iambie Mahakama kwa nani?
Shahidi: Kwa Wateja Ambao wanamiliki line za Mitandao ya Simu
Wakili wa Serikali: Hawa wateja Wa Tigo Wanapatikana Vipi?
Shahidi: Wanapatikana Kwa Kununua line za Tigo na Wakaitumia basi Wanakuwa Wateja wetu. Na ili ifanye kazi lazima ifanyiwe Usajili.
Wakili wa Serikali: Kwenye Kusajili mnasajili Kitu gani?
Shahidi: Kwa mtu ambaye ana kitambukisho cha NIDA tunatumia NATIONAL IDENTIFICATION NUMBER. Mtu anaye sajili ataingiza Namba ya Kitambulisho Cha Taifa Itasoma Taarifa.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama process za Manunuzi ya Line kama zipo?
Shahidi: Mtu yoyote anaweza Kufika kwenye Duka au sehemu ambayo kuna Wakala anauza hizo line za Tigo akiwa na Kitambulisho Cha Taifa, Lakini pia Kuna Wageni ambao wanatakiwa kutumia passport....
Wakili wa Serikali: Mtu anaye jua atafanya nini?
Shahidi: Ataweke Kidole Kigumba, Zitasoma Taarifa zote ambazo zipo Kwenye NIDA, Kama Jina Na tarehe ya kuzaliwa Kwa hiyo Taarifa hiyo itachukuliwa Na kuhifadhiwa Kwenye Mfumo wa Tigo kama Taarifa za Owner au Mtumiaji wa hiyo line.
Wakili wa Serikali: Mtu asiyejua NIDA, unaposema Zinaenda Kutally na Taarifa za NIDA unamaanisha Nini?
Shahidi: NIDA nimfumo wa Usajili wa Vitambulisho Vya Taifa ambao unatunzwa na Authority
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama unaposema Taarifa zile zitachukukiwa na Kuhifadhiwa Tigo, Nani atazichukua
Shahidi: Tunasema Ki Electronic kuna Mfumo wetu ikizipata na Ikatally inatunza Kwetu, Kwa hiyo Mifumo inawasiliana
Wakili wa Serikali: Jinsi ya Kusajili line Taratibu ziko Vipi
Shahidi: Ukishanunua Laini na Kwamba wewe sasa Unawasiliana, Tuna kutumia Meseji Kuwa kama Unataka Kutumia huduma ya Mihamala ya Fedha, Ukisema Okey tunakupa Vigezo na Masharti.
Wakili wa Serikali: Hiko Kitendo Mnakiitaje?
Shahidi: Umejiregister Kwenye Huduma ya Tigopesa
Wakili wa Serikali: Nikurudiahe kwako sasa wewe Mwenyewe, Tigo Umeajiriwa kama Mwanasheria Je Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Kushauri Viongozi Maswala Yanayohusu Sheria, Kutengeneza Kusoma, kupitia na Kusaini Mikataba Kufuatilia, Kusimamia Kesi zote zinazohusiana na Tigo ...Kumsaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama Katika Kupata Taarifa Mbalimbali Kutoka kwa Wateja zinapohitajika.
Wakili wa Serikali: Jingine, Baada ya kutoa hizo Taarifa
Shahidi: Kama Kuna Jinsi Yoyote Kusaidia Chombo chochote Katika Kutafuta Taarifa, Naweza Kusaidia Siyo VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama tu Bali hata Mtu Binafsi anaweza kupata Msaada wangu.
Wakili wa Serikali: Ni Vipi Mtu Binafsi, Mtu X anaweza kupata Taarifa za Mtu Y
Shahidi: Mtu Mmoja Kupata Taarifa za mtu Mwingine HAIWEZEKANI
Wakili wa Serikali: Kwa mujukumu hayo uliyoyataja, Unamajukumu gani au Ujuzi gani inayo Kusaidia katika Kutekeleza Majukumu yako
Shahidi: Kama Mwanasheria wa kampuni Nina Digrii ya Sheria, Nimesomea India JSS law college. Under MYSORI University, Ambayo niliipata 2009 Nilisoma Pia Advanced Computer Course, MYSORI University India 2007. Nilisoma Pia Advanced Diploma in Practice Nilimaliza Mwaka 2012 Baada ya hapo Kuna Training mbalimbali ambazo Nimezipata Nikiwa kazini 2012 nilipoanza Kazi
Wakili wa Serikali: Zitaje Training gani
Shahidi: Nilipopata kazi ilikuwa ni Majukumu yangu Nilikuwa nimeingia Kampuni ya Telecom Nilipata Training Ya Mwezi na nusu
Wakili wa Serikali: Ulisomea nini ktk hiyo Training
Shahidi: Mifumo ya Kujifunza Kutumia, ilikupata Taarifa Wa kwanza ni oracle Wa Kusaidia Kupata Taarifa mbalimbali zilizopo Sehemu za Kazi.
Shahidi: Kuna system Nyingine ambayo CONVIVER iliyokuwa Inasaidia Kupata Mihamala Yote ni soft ware BILL QUERY Iilikuwq Inasaidia Kujua matumizi Mbalimbali ya Mteja Upande wa Vocha Na SMAP ni Mfumo Sawa QUERY Kwa hiyo nilikuwa nasaidia VYOMBO Vya Ulinzi Na Usalama Kupata ...Information
Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka Ulikuwa unafanyiwa na nani
Shahidi: Ofisini na Mtu anaitwa Mr.....
Wakili wa Serikali: Ofisi za Tigo ziko wapi
Shahidi: Ofisi za Tigo Zipo Makumbusho DERM COMPLEX
Wakili wa Serikali: Unakumbuka Training Nyingine
Shahidi: 2015 palikuwa na Training Nyingine Baada ya Mifumo Kubadilika Baada ya oracle ikaja SQL Server CONVIVER ikaja Kubadirishwa Ikaja TELVIVER IKAJA ENVIVER ambayo sasa Ikaja Information Mbayo Ukiingia Unaona Matumizi ...na Kila Kitu. Wanakufundisha Kule Unakoenda Kuchukua zile Information Siyo Kila amtu anaruhusiwa Kwenda Kuchukua Unafundishwa Jinsi gani ya Kuzilinda.
Wakili wa Serikali: Baada ya Mifumo Kubadilika sasa
Shahidi: Ikabidi tupate Training, Jinsi zinavyofanya kazi na Tabia zake
Wakili wa Serikali: Katika Training zako ulipata Lolote Kuhusiana na Information ambazo unaenda kufanyia Kazi
Shahidi: Wanakufundisha General Overview
Wakili wa Serikali: Umetaja Training za 2012 na 2015 Je una Training Nyingine
Shahidi: Zipo Nyingine hizo ni Major Kila Siku Dunia Ikileta System Mpya tutaambiwa tu Kuna Training za Kila Siku Katika Majukumu ya kazi
Wakili wa Serikali: Nikurudishe Nyuma Wakati Unataja Majukumu Yako Unasema Unasaidia VYOMBO Vya Ulinzi na Usalama. Je Ni VYOMBO gani
Shahidi: VYOMBO Vyote Vya Usalama Ukijumlisha Polisi, Jeshi, Kama ni Anga kama ni Ardhi na VYOMBO Vyote Vinavyofanya Uchunguzi wa Kisayansi. 2.Taarifa za Mihamala ya Fedha, Kutuma na Kupokea fedha 3. Kuna Recharge ya Vocha na Kutumia pamoja na Matumizi yake 4. Taarifa za Usajili 5. Taarifa Nyingine zote zinazoambatana Kama NIDA, LOCATIONS, BILL MBALIMBALI ANAZOLIPA
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama sasa Unawasaidia Kuwapa Taarifa, Je ni Taarifa zipi Mnawapa, ulikuwa unatumia Neno zinazoruhusiwa Kisheria
Shahidi: Zozote ambazo zitakuwa zinahitajika sisi tunazo 1.Kuna Kupiga na Kupokea Simu, Za wateja wetu zinaitwa Call Details ...
Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Hizo Taarifa wewe unazitoa wapi
Shahidi: (Tigo) Taarifa zote za kampuni pamoja na Wateja wake Zinakuwa Stored Kwenye Server
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Nani anaitoa Taarifa kwenye Server
Shahidi: (Tigo) Taarifa zote Zinakuwa Served Automatically Mtu anapo piga Simu Mnara Unasima na Taarifa zinashuka na Zina switch kwenda Automatically Kwenda Kwenye Server Kuwa stored. Lakini pia Kuna watu ambao ni Observers wa kungalia na Ku Audit kazi Nzima ya Server
Wakili wa Serikali: hizo Taarifa unazozitoa Unasema Zinakuwa self Generated, Je kiuadilifu kuwa hizi ni zile zilizojitengeneza, Uadilifu wake kwenye Server?
Shahidi: (Tigo) Kama kampuni ina Mifumo ya tofauti ilitengenezwa Mahususi Kulinda hizi Server na The Whole System