Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ya Mbowe na wenzake. Superitendent Jumanne Malangahe atoa ushahidi, Kesi imeahirishwa hadi Nov 9, 2021

Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ya Mbowe na wenzake. Superitendent Jumanne Malangahe atoa ushahidi, Kesi imeahirishwa hadi Nov 9, 2021

Tuombe Mungu sana hawa jamaa wanaotuhumiwa pamoja na Mbowe wasije wakawa watu wa system. Maana hawashindwi.

Hili swala nimelifikiria leo. Isije ikawa jamaa alipelekewa watu wa TISS kujifanya ni walinzi wake afu mwisho wa siku wakiri kuhusika na huo ugaidi unaotajwa then wale namba wote baadae wao watolewe kwenda kuendelea na mbinu chafu.

Dhuluma huwa na mbinu nyingi ila mwisho ukweli husimama.
 
Yawezekana Rais Samia kaamua iendelee ili awaumbue hawa watu, kumbuka hii kesi ilikuwa fomulated kipindi cha yule DPP aliyetumbuliwa. wacha tuone hadi mwisho.
Sasa tumbuka yeye, kama unavyosema ni kweli!
 
Umeona holes nyingi sana! Kibaya zaidi ni kuhusu hao washukiwa kuwa watatu mpaka hatua za mwisho. Huku timu za wakamataji zikiwa mbili na zote hazielezi mtu wa tatu alikuwa nani!! Binafsi nadhani huyu wa tatu alikuwa Urio na ndio informer so wasingeweza kumkamata!! Sasa ninadhani hata jaji hawezi kuwa na picha ya sehemu ya tukio. Mara grocery, kibanda umiza, mara wamekaa tu, mara walikuwa wakisajiri laini za simu! Mara watatu wamekaa na kutambulika, lakini kuanzia hapo ghafla ni watu wawili. Mara wameenda Arusha kumtafuta Lijenje lakini wakiwa hawajui jina la dadake wala anaishi wapi lakini walienda anyways!!

Mashahidi wengine wanasema ilikuwa ni madawa ya kulevya, namba 08 kawa smart - kasema inafikiriwa ni madawa ya kulevya. Na bado hizo kete haziko mahakamani kama madawa au si madawa. Risasi tatu dhidi ya moja iliyoletwa mahakamani.

Sitashangaa nikisikia jamaa walikuwa na silaha wanayoimiliki isiyo halali lakini hawakuwa wahalifu. Ikimbukwe walikuwa sio hata waajiriwa wa Mbowe bado so sijui silaha hiyo ingehusika vipi na magogo ya barabarani, maandamano yasiyo na kikomo. Jamhuri itashindwa kuunganisha silaha hii na ugaidi!! Ni
kwa sababu kumiliki silaha hakumfanyi aliyenayo kuwa mhalifu kimatendo. Kumiliki kihalali hakumfanyi mtu kudhaniwa hataitumia kuua mtu mwingine - actually wanapewa ili wauwe. Je bastola hii ilikusudiwa kumuua mtu specific, that is hard to prove mpk sasa.
Mi mpaka sasa sioni huo ugaidi uko wapi

Hakuna kituo kilicholipuliwa, hakuna magogo yaliyolatwa na kuwekwa barabarani,hakuna kiongozi alieshambuliwa

Watuhumiwa hawana rekodi za Mambo ya ugaidi

Ni kwamba Polisi wameamua tu kujitungia script zao na kuzipa title ugaidi wakati watuhumiwa hawana hata chembe za huo ugaidi.

Sasa sijui jaji atahukumu kwa kosa gani

Hata hayo madawa ya kulevya Polisi wanazo stock za kutosha huko kwenye maofisi yao ukikosana.nao tu wanakuwekea kwakua wanajua Sheria ni Kali basi huchomoki

Ila nashukuru MUNGU nilisoma kwa bidii shule na sikuwahi fikiria kuja kuwa Polisi
 
Nasubiri maswali atakayoulizwa J4 kesho panapo majaaliwa ni kucheka kwa kwenda mbele huyo kazi anayo kesho kwa wale wananchi hadi wao wanajiogopa...
Kesho patachimbika, lazima aulizwe suala la kumuwekea meno ya tembo yule profesa arusha,. Atarusha ngumi kesho J4
 
Tuombe Mungu sana hawa jamaa wanaotuhumiwa pamoja na Mbowe wasije wakawa watu wa system. Maana hawashindwi.

Hili swala nimelifikiria leo. Isije ikawa jamaa alipelekewa watu wa TISS kujifanya ni walinzi wake afu mwisho wa siku wakiri kuhusika na huo ugaidi unaotajwa then wale namba wote baadae wao watolewe kwenda kuendelea na mbinu chafu.

Dhuluma huwa na mbinu nyingi ila mwisho ukweli husimama.
Wangelikuwa watu wa system wangelisubiri kwanza wakusanye ushahidi wa kutosha ili kuweza kumtia hatiani na sio kama sasa na huu ushahidi wa kuunga unga.
 
Dalili zote kesho ni pingamizi la upande utetezi kutupwa na jaji kukataliwa.
 
Naomba mnielemishe juu ya neno "CITATION" ina maana gani?.
 
Huyu hakimu anapokea maelekezo kutoka kwa madam kabisa. Haiwezekan huu utumbo uwepo mahakamani mpaka leo na inaonesha mahakama sio muhimili unaojitegemea.

Kwanini wasichutame wakafuta kesi hii maana wanazidi kujidhalilisha na kutudhalilisha watanzania wote. Inakera sana
Haiwezi kuishia njiani kesi, kisa ushahidi mbaya,, kitendo tu cha kesi kusikizwa kila siku (haijapata kutokea) maana yake kuna mtu above, kachoshwa na hii kesi na anataka iishe chap,, vinginevyo hii kesi ingeenda miaka hata mitano,,
 
Huyu Shahid wa leo Jumanne ndo yule alienda kumdhulumu mstaafu Mzee Maeda kwa kumuwekea pembe za ndovu
 
Naona Mh Jaji anatupilia mbali pingamizi kwa mara ya tano au sita vile,halafu jopo la mawakili wa utetezi linajitowa na kina Mbowe wanakaa kimya mahakamani kusubiri hukumu yoyote ile.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwa elimu tu sio haba. Inanifundisha na mimi kuwa makini kwenye kazi yangu niliyosomea.

Akina Kibatala had been always a class to learn.

Angekuwepo yule Kichwa Tundu Lissu a learned civilized person naona Majaji kesi wangeitema.
Mzee wa Csqr =Bsqr +Asqr!! Umenena kweli
 
Back
Top Bottom