Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Huyo jamaa maswali mengi anajibu sijui na sifahamu.
 
Naona sasa kibatala anamtengenezea shahidi hali ya kujihisi msaliti asiyefaa kwa kuwasukumia wenzake kwenye moto.
Hii itamtesa kisaikolojia hata baada ya kumaliza ushahidi wake, na pengine mahusiano yake na wanajeshi walio ktk utendaji wake

Ana roho mbaya Sana huyo jamaa.
 
Wachaga hasa ukoo wa urio poleni.....au huyu siyo urio, ni jina tu la kutafutia kazi, aliiba cheti cha mtu?
 
Naona sasa kibatala anamtengenezea shahidi hali ya kujihisi msaliti asiyefaa kwa kuwasukumia wenzake kwenye moto.
Hii itamtesa kisaikolojia hata baada ya kumaliza ushahidi wake, na pengine mahusiano yake na wanajeshi walio ktk utendaji wake
Huyo hata akirudi jeshini ataishi kwa shida sana maana wanamuona kama snitch Fulani,hata maboss wake watakua makini nae maana haaminiki tena.
Wasipomfukuza watapekeka huko kwenye mavita akafie huko
 
Huyo hata akirudi jeshini ataishi kwa shida sana maana wanamuona kama snitch Fulani,hata maboss wake watakua makini nae maana haaminiki tena.
Wasipomfukuza watapekeka huko kwenye mavita akafie huko
akitoka hapo na cheo kinapanda katokomezagaidi lilitaka kupindua nchi mbowe ni GAIDI
 
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki:Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022


Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

  • Wakili Pius Hilla,
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

  • Wakili Michael Mwangasa
  • Sisty Aloyce
  • Gaston Garubindi
  • Idd Msawanga
  • Maria Mushi
  • Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tutaendelea na Shahidi, Tupo tayari Kuendelea

Shahidi anaingia kutoka Nje

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: nakukumbusha Kwamba Tarehe 28 ulikuwa upo chini ya kiapo na leo utaendelea kutoa ushahidi wako chini ya kiapo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba sababu ya kelele za Jenereta tufunge madirisha tafadhali.

Kibatala: Mr Urio how are you?

Shahidi: Am fine

Kibatala: Did you have a nice Weekend?

Shahidi: like speak again

Kibatala: Did you have a nice Weekend?

Shahidi: like That!

Kibatala: Shahidi Umesha wahi Kukutana na Mazingira ya Kuambi Maneno Mazito Unayosema ya Ugaidi

Shahidi: Sijawahi Kukutana nayo

Kibatala: Umesema hauna tatizo la Kumbukumbu

Shahidi: Sina tatizo la Kumbukumbu

Kibatala: Iweje usikumbuke Tarehe 2 Muhimu Wewe Kukutana na Mbowe na Kwenda Ofisini Kwa DCI Ukizingatia wewe ni Mwanajeshi, na Luteni wa Jeshi

Shahidi: Mhe Jaji Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni Ndugu yangu, Nilikuwa sijui kuwa ni kweli au si Kweli, Mpaka nikaona kuwa Kumbe ni Serious

Kibatala: Wewe Luteni unaona Umejibu swali Langu la inawezekana Vipi usikumbuke Tarehe

Shahidi: Sijawahi Kusikia Maneno Mazito, Ndiyo Maana Nikaenda kutoa Riport Polisi Wafanye Uchunguzi

Kibatala: Swali langu inawezekana Vipi Ushindwe Kukumbuka Tarehe ya Matukio Kama hayo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mimi naona Kama Nimejibiwa

Jaji: Swali lilikuwa linawezekanaje Kuwa asahau Tarehe za Mambo Muhimu

Shahidi: Ilikuwa ni Mara ya Kwanza, Kusikia Kutoka Kwa Mheshimiwa Mbowe, Sikuwa nategemea

Kibatala: Vipi Kuhusu Tarehe ya kwenda Kwa DCI na yenyewe Ulikuwa shocked

Shahidi: Siyo Duty yangu Mimi Kukumbuka, Kazi yangu Ilikuwa Kutoa Riport tu

Kibatala: Kwakuwa Unaomekana Kujivua Duty ya Record Ya Tarehe, Unaweza za Ku tuisaidia Kwanini na Yeye DCI hakumbuki Tarehe Uliyo Kwemda Ofisini Kwake

Shahidi: Sifahamu, Siwezi Kumjibia

Kibatala: Siku Unakwenda Kwa DCI Kingai alikuwa Summoned akaja, Unaweza Kutuisaidia Kwanini huyu Kingai Mtu wa Tatu na Yeye hakumbuki ni Tarehe ipo Mlimkutana

Shahidi: Siwezi Kujua ni Kwa nini

Kibatala: Ni kwanini hata Inspector Swila ambaye ndiyo Afisa wa Upelelezi Aliyefungua Faili Tarehe 18 July 2020, Hakumbuki Tarehe hiyo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Kwa wewe Kama Luten Wa Jeshi unaona ni sahihi Kwa Nyinyi Watu wote hakumbuki Tarehe

Shahidi: Siwezi Kujibia

Kibatala: Umewahi Kusikia Msemo "The Lights are on but nobody at home"

Shahidi: Hapana Sijawahi Kusikia

Kibatala: Kwanini Tarehe 11 August 2020 ndiyo Maelezo Yako yaandikwe Mtoa Taarifa Ambaye ndiyo Ulisababisha Faili Kufunguliwa Tarehe 18 July 2020?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Wewe ni Luteni wa TPDF uoni Kwamba Inategemewa Maelezo Ya Mtoa Taarifa Kuandikwa Mapema Kadriri inavyowezekana

Shahidi: Siwezi Kujibia Polisi, Sababu Wao Wana Utaratibu Wao wa Kazi na Mimi Nina Utaratibu Wangu Wa kazi

Kibatala: DCI alikifafanulia Kwamba Kwanini Maelezo Yako hayawezi Kuchukuliwa Siku ambayo wewe Umeenda ku report

Shahidi: Hawakufafamua chochote

Kibatala: Tarehe 11 August 2020 kwa Ushahidi Wako Ndiyo Ulikwenda Kutoa Maelezo Ushahidi Wako Kwa Inspector Swila.. Inspector Swila alikufafanulia Kwanini alisubiri Mpaka Mwezi Mmoja Baadae?

Shahidi: Hakufafanulia

Kibatala: Tukisema Kuwa Mlitunga Kesi Mapema Kisha Baadae Ndiyo Makaanza Kutafuta Watuhumiwa, Nitakuwa Nakosea Kwa Fact hizo

Shahidi: Utakuwa unakosea

Kibatala: Unafahamu Dhana ya Infiltration,.?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Maana yake

Shahidi: Kutoka sehemu Moja Kwenda sehemu Nyingine Kwa siri

Kibatala: Ni sahihi pia Maana yake Pana ni Kutuma Mtu Kwenda Kwenye Kambi ya Upinzani, Ili Kupata Taarifa Kamili

Shahidi: Hapana, Tactics inasema Kwamba ni Kitendo Cha Kutuma Mtu Kwa Siri

Kibatala: Nikumbushe tena Elimu yako

Shahidi: Form Four

Kibatala: Unafahamu Decoy

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Luteni wa Jeshi hufahamu Decoy

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mlijadili Kwa Pamoja Kumpeleka Mtu kwa Mbowe akiwa na Vifaa aweze Kupeleleza na Kurekodi Ushahidi

Shahidi: Hatujawahi Kujadili

Kibatala: Ni Kweli Katika Ushahidi Wako Kwamba Mheshimiwa Mbowe alikwambia atachukua Dola Kwa namna yoyote, Je Uchaguzi ulitajwa

Shahidi: Nafahamu Uchaguzi Ulitajwa

Kibatala: Bado Jeshi lilikuwa halina Role to Play Kwamba wewe ni Mwanajeshi uliye kazini na Mbowe anataka Ex Commandos, Bado Jeshi lilikuwa halina sababu ya Kupewa Taarifa?

Shahidi: Ni Taarifa ambazo hazina Ushahidi, Bado Jeshi litapeleka Kule Kule Kwa Polisi

Kibatala: Unamfahamu Aliyekuwa Chief of Staff Luteni Generali A. Shimbo

Shahidi: Namfahamu

Kibatala: akiwa katika Majukumu Yake ulikuwa Jeshini

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namnukuu Tarehe 13 10 2010 "Katika Uchunguzi huu, Jeshi limejipanga Kuhakikisha Uchaguzi Unakuwa wa Amani na utulivu".. Uliwahi Kusikia?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Bado Unasisitiza Kwamba Mambo Ya Kiuchaguzi Jeshi halihusiki

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: huoni Kwamba Kwa Kutoa Kwako Taarifa Jeshi lingefanikisha Kuweka Decoy, (Mamluki) wa Kwenda Kukusanya taarifa ambazo ni sahihi?

Shahidi: The issue ni kwamba Mtu anaitwa Freeman Mbowe hapokei Simu za Kawaida, anasema Nitumie picha na Profile yake ili ajiridhishe Kwamba bado Wapo Katika Service, Kwa hiyo Endapo tungetuma Mtu ambaye bado yupo katika Service angegundua

Kibatala: Kwa hiyo Tactical appreciation Yako ilikwambia Kwamba Mheshimiwa Mbowe ana uwezo wa Kujua profile zao?

Shahidi: Ndiyo, Unafikiri Kwanini alitaka Picture na Profile zao?

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Wote Kuna Mahala Popote Ulisema Kwamba Mbowe alikwambia Kwamba ana Access ya Mtu Mwingine Jeshini

Shahidi: Hapana

Kibatala: Tujadili Kuhusu Tactical Appreciation, Ni sahihi Kwamba Kamanda anakutana na Mazingira Fulani ambayo Kamanda anapanga Vikosi Vyake Kukabiliana na Mazingira hayo kwa Muda kwa Kupanga Mkakati

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Sasa Wewe Palikuwa na Several Unknown, Nimekuuliza Kama Mbowe alikuwa na Access Jeshini Ukasema hujui, Sasa huoni Kwamba Tactical appreciation Yako Ilikuwa si sahihi

Shahidi: Huyu Bwana ningemwambia kuwa Sitaki angemtumia nani, Ndiyo Maana nilifanya Tactical Appreciation na Kwenda Kuripoti Kwa DCI

Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwamba Katika hali hiyo Kuna mambo Kadhaa wa Kadhaa ulikuwa huyafahamu, Ndiyo Maana Ukasema Kwamba Ulikuwa hujui Kama alikuwa ameshaongea na Watu Wengine

Shahidi: Ndiyo nilikuwa sina Uhakika Kama Mbowe ana Option A, B na C

Kibatala: Sasa Jambo hilo Linaendana na Tactical Appreciation

Shahidi: Ndiyo linaendana

Kibatala: Kazi yangu ni Kuuliza Maswali

Kibatala: Umesema Ulikuwa huna Uhakika Mbowe alikuwa na Option A, B na C, Je ulijihakikishia Kwa Kumuhoji

Shahidi: Sikumuhoji

Kibatala: Unathibitisha alikuwa na Trust Yako yote

Shahidi: Sijui Kwa Yeye Sasa

Kibatala: Nakuuliza Wewe

Shahidi: Je ni Mimi peke yangu anaye niamini

Kibatala: Hakuna Mahala Uliposema Kwamba Mbowe alikutishia Wewe au Familia yako

Shahidi: Sijasema

Kibatala: Kwamba Mbowe alikuahidi Cheo Kama Incentive yako

Shahidi: Mbowe Hawezi Kunipa Cheo Jeshini

Kibatala: Kwa hiyo Mbowe alikuwa hawezi Kukuhaidi Cheo Sababu alikuwa Mbunge

Shahidi: Sahihi hawezi

Kibatala: Nashukuru Kwa jibu lako Zuri

Kibatala: Wakati Mbowe anakupa Maombi , Ulimkubalia au Moyoni Ulimkatalia

Shahidi: Ilikuwa Tactical Appreciation, Ile Kwamba nitachoma Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Masoko,

Kibatala: Na Kumdhuru Sabaya pia Ulikuwa Unachakata

Shahidi: Sijawahi Kumtaja Sabaya Mimi, Nilitaja Viongozi

Kibatala: Akili ya Kawaida ya Luteni haikuwa na zaidi ya Kumchimba Kwamba anataka Kulipua Vituo gani, Kukata Miti sehemu gani?

Shahidi: Hata Ingekuwa ni Mimi, Ukishaanza Kunidodosa nakosa trust na wewe.

Kibatala: Wakati Mnakutana Kupanga Matendo ya Ugaidi, Mahakama Itakapopima, Maneno yako Dhidi ya Maneno ya Mbowe sababu Hakuna Sauti Nyingine wala Decoy?

Shahidi: Ndiyo Maana nikatuma Vijana

Kibatala: Kwani Vijana hawa si Washtakiwa? Au Wapelelezi Wako?

Shahidi: Washtakiwa

Kibatala: Unakubaliana na Mimi sasa Mahakama itabidi ipime neno lako dhidi ya Mbowe kwa sababu Hapakuwa na Mtu Mwingine pale

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakumbuka Wakati wa Utejelezaji Wa Majukumu Yako, namna ulipompata Ling'wenya

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Unakumbuka Uliongea na Baba Yake Ling'wenya

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Unakumbuka Kwamba uliongea naye Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unakumbuka uliongea naye Majira gani

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unafahamu a kwamba Mzee Ling'wenya alikukatalia Kumtoa Mwanaye sababu ya Mambo yaliyomtokea Mwanaye Jeshini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwamba Yeye alishamtafutia Mwanaye Kazi ya kokoto

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba huyu Mzee (Baba yake Ling'wenya) ni Mwenyekiti wa Kijiji fulani huko Kusini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Baba Yake alipokutafuta baada ya Kusikia Mwanae kakamatwa Unakumbuka Ulimjibu nini

Shahidi: Sikumbuki, Ila Niliwambia kuwa amuulize Boss wao

Kibatala: Kwani Boss wao ndiye aliye Mpigia Kumuombea Ruhusa Kwamba Kuna kazi

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Ulimwambia Mzee Ling'wenya Kwamba Kuna kazi Kwa Mbowe lakini nataka akafanye Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Maana ya Intrapment

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Maana ya Kumtoa Mtu kafara

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unakumbuka Kwamba Nilikuuliza Unasali Wapi kwa sababu gani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: umeapa kwa Biblia Je Unafahamu Kuhusu Daniel

Shahidi: Nafahamu Kuwa walitupwa Kwenye Tundu la Simba

Kibatala: Wewe Kuna tofauti na Walichomfanyia Daniel na Ling'wenya Mkristo Mwenzangu.?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwamba Ling'wenya alikuwa na kazi yake ya Kubonda Kokoto wewe Kwa Kikao Chenu na DCI ukamtafuta Kumwimgiza kwenye Matatizo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wakati Baba Yake Ling'wenya anakutafuta Kukuuliza Kwamba Mwanaye yupo wapi Ukajibu Ongea na Boss wake, Ni kweli

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu kwamba Mzee Ling'wenya alistaafu Bila Doa Lolote Serikalini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kama Mzazi, anaumia Ka Ilivyokatwa kwa Mama Maria Kumuona Mwanaye anateseka Msalabani wakati hajafanya Kitu chochote

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je inawezekana kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari.?

Shahidi: Inategemea kwa Mazingira

Kibatala: Je ni Mazingira Gani kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari?

Shahidi: Kiongozi anaweza asiwe Sehemu Moja

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwanini Kwenye Platoon Kiongozi anakuwa Mbele, Hata katika Biblia

Shahidi: Sifahamu, Sijawahi Kuona

Kibatala: Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa alipatwa na Battle Traumatic Fatigue

Shahidi: Mimi sifahamu Sijawahi Kusikia ana historia hiyo

Shahidi: Je Shahidi alitoa cheti cha Daktari

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Ulisema Kwamba ulienda Kwenye Ofisi ya Admin officer ukasoma Mafaili yao

Shahidi: Siyo Mafaili ya Taarifa individual, Bali Taarifa za Matukio tangu Siku Natoka

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Ujui sababu ipi ambayo ilipelekea Adam Kasekwa Kufukuzwa Jeshini

Shahidi: Sijui zaidi ya Utovu wa Nidhamu

Kibatala: Unafahamu ni Maeneo gani Mahususi ambayo Walitembelea kwa ajili ya Kumdhuru Sabaya

Kibatala: Wewe Ukiwa katika kazi Maalum, Hukuona sababu kuuliza Kwa Bwire ni wapi Walipanga Kufanya Uhalifu

Shahidi: Mimi siyo Kazi Maalum

Kibatala: Kwani aliyetafuta Vijana ni Polisi au wewe?

Shahidi: Mimi

Kibatala: Mbowe aliomba Polisi wamtafutie Vijana?

Shahidi: Hapana

Shahidi: Bwire Hakuniambia

Kibatala: Katika Ushahidi Wako hujui wala hujazungumzia Kuhusu Milestone, Kokoriko na Triple B

Shahidi: Sijazungumzia

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Walikamatwa kwa tuhuma za Kupanga Kufanya Uhalifu wa Kumdhuru Sabaya

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ni kweli Uliwatafuta Vijana Kwa ajili ya Kufanya Ukamataji kabla ya Uhalifu haujatokea

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Bado Hukuona Sababu ya Kumuuliza Bwire

Shahidi: Polisi Walitakiwa Wafanye Uchunguzi Wao

Kibatala: Kwani nani aliyemtafuta Adamoo

Shahidi: Ni mimi

Kibatala: Kwani nani alikuwa anaaminiwa na Adamoo kati yako na Polisi

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: akuna Taarifa a kwamba siku za Adamoo na Ling'wenya Wanakamatwa walikuwa wanapokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wao, Je huyo Msiri ni wewe

Shahidi: Siyo Mimi

Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako palikuwa na amtu Mwingine aliyekuwa anatoa Taarifa kwa DCI na Kingai

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kwa Ufahamu Wako wewe Kuna mtu Mwingine ambaye alikuwa anawajua Adamoo na Ling'wenya

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Kwamba Adamoo na Ling'wenya Siku Wanakamatwa pale Rau Madukani walikuwa wanafanya nini.

Shahidi: Wala sijui Kama Walikamatwa Rau Madukani

Kibatala: Unafahamu a kwamba pale Rau Madukani Mohammed Ling'wenya alikuwa na Dada yake anaitwa Athima

Shahidi: Sifahamu, Hakuwahi kuniambia

Kibatala: Wewe Hukumu uliza Bwire

Shahidi: Sikumuuliza

Kibatala: Ulikuwa unafahamu Kwamba Moses Lijenje ana Dada yake anaishi Arusha

Shahidi: Hapana Sijui

Kibatala: Na wala Msiri wao unasema Siyo wewe

Shahidi; Siyo Mimi

Kibatala: Kuna sehemu katika maelezo yako Uliandika "Nilimpatia ACP kingai Namba za Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya aweze Kuwa fuatilia" ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Swala la Kwamba ACP kingai alikuwa namba za watu Watatu Mpaka Siku wanakamatwa, Je uliliongelea.?

Shahidi: Sikuongelea

Kibatala: Ni Suala la Kuwapa namba za Simu ni Swala la Muhimu au siyo la Muhimu

Shahidi: Ni suala la Muhimu

Kibatala: Unafahamu kwanini Kingai Wala Mtu Mwingine yoyote Hakuna anaye zungumzia Swala la Wewe Kuwapa namba za Simu kabla

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Swala la Kingai Kuwa na namba za Simu za Watu hawa Zina Implication gani Katika Uchunguzi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mashahidi ambao Wamekutangulia, Walikuwa Wanamtafuta Lijenje Manually wakati Wana namba zao za simu

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba hata baada ya Watu hawa kukamatwa Kingai hakufanya chochote Katika Kuwafahamisha Wapendwa Wao

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Wakati Wa Tarehe 12 August 2020 Ulisema Ulimkabidhi Inspector Swila na kuandikishwa ID02

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mwanzo Ukasema Kwamba Wakati Unamkabidhi Simu yako Ulitoa Line ya Vodacom ambayo ilikuwa na Mawasiliano yako na Watu Wengine

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwahiyo wewe Ulimkabidhi Inspector Swila Simu bila Sim card

Shahidi: Nilitoa ya vodacom ni kabakisha Moja

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Sim Card ya Vodacom,ulirudisha lini.?

Kibatala: Katika Nyaraka ipi Tukiangalia Tutaona Mlikabidhiana Sim Card ya Vodacom na Inspector Swila

Shahidi: Ipo

Kibatala: Ipo hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana, Hapa Mahakamani Haipo

Kibatala: Ipo wapi

Shahidi: Sikujua Kama Inahitajika Mahakamani

Kibatala: Ile Simu ya Tecno Uliyowasha hapa, Ina SimCard ndani

Shahidi: Sikukagua kama ina Sim Card ndani

Kibatala: aliye sema Kwamba Ile simu ina Sim Card ndani ni nani

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: nikuombee utuonyeshe sim Card

Shahidi: Vyovyote Vile itakayokuwa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P34

Kibatala: haya Fungua utuonyeshe humo ndani Kuna Sim Card ya Mtandao gani

Shahidi anafungua

Shahidi: HAKUNA LINE HATA MOJA (SimCard)

Kibatala: Unafahamu thamani ya Kiapo chako

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba unawajibu wa Kulinda hadhi ya Jeshi la Wananchi Tanzania

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Ukweli na Uongo wako Unapimwa Katika Vitu Vidogo Vidogo Kama hivyo

Shahidi: Nafahamu
Denis urio hoi sema ukweli ukuweke huru simcard iko wapi?
 
Mawili tu yangu:
Kibat: Uliambiwa anataka kuchukua dola. Nikiasi gani cha dola au na pound watachukua
Shahi: Kimyaaaaa

Kibat: Ulisema wanataka kuchoma masoko na sasa soko la Karume lilichomwa. Je inawezekana ni Mbowe alitoka gerezani kuja kuchoma?

Shahi: Hapana. Niseme ukweli nimelazimishwa kutoa ushahidi. Kibat utaniua nisamehe.

Mahak: Kichekooooo!!!!!! Mpaka ikulu wamesikia [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Leo ndio nimetambua Urio Ni mpumbavu Sana. Yani aliwatoa wenzake kama chambo. Yani kumbe lingwenya alikuwa amepata shughulika ya kokoto kaenda kumtoa huko ili amtumie kwenye mpango wake. Halafu anaulizwa anajibu kwa jeuri. Tanzania Ina watu wakatili Sana, unapoteza Maisha ya wenzako kwa manufaa binafsi na haujari.
Nitajie mchaga asiyekuwa katili.

Wachaga na Wakinga wanafanana sana!
 
KIMEUMANA... !!

Kibatala:
Katika Ushahidi Wako, Unasema Uliwapa Tsh 195,000 katika TSh 199,000 Uliyotumiwa, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba TSh 4,000 Ilienda wapi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwa hiyo TSh 4,000 ya Ugaidi hujasema Ipo wapi

Shahidi: SIYO YA UGAIDI, BALI YA KUWASAFIRISHA

Kibatala: kwa hiyo Wenzetu Wanasema Yote TSh 199,000 ilitumika Kwenye Ugaidi, Kumbe siyo Ugaidi

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
 
yaani hiyo ndiyo umeona ni point kubwa saaaana aliyoiongea kibatala? hopless kibatala hana jipya anamfungisha tu mbowe hana point y akumnasua na huo ugaidi wake
[emoji848]
Screenshot_20220131-120803.jpg
 
Back
Top Bottom