Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Sijawahi kuona utawala wa kijinga kama huu duniani, yaani unapambana kufunga watu badala ya kuwatengenezea mazingira safi ya kufanya kazi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KALICHOKOZE UONE KAMA UNAMASHAKA NALO KAMA HUJAITA MAJI MMAKama kweli jeshi letu lina watu wenye vyeo vya hadhi ya luteni wa jeshi mwenye akili kama ya urio naanza kupata mashaka na jeshi letu
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Acha wewe, unafikiri kubananishwa kizimbani mchezo? Hata Kibatara akisimama pale na ukali wote alionao lazima jasho limtoke. Pale sali sana usifike mzeeKama kweli jeshi letu lina watu wenye vyeo vya hadhi ya luteni wa jeshi mwenye akili kama ya urio naanza kupata mashaka na jeshi letu
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Acha wewe, unafikiri kubananishwa kizimbani mchezo? Hata Kibatara akisimama pale na ukali wote alionao lazima jasho limtoke. Pale sali sana usifike mzee
mchawi na shetani huwa hana anachofaidikaHv watungaji wa hii movie wanafaidika nn????
Kibatala noma sana, kamsogeza hatimaye kaingia mwenyewe akaishia kucheka tu [emoji23]kibatala anamuingiza kingi aliwe kichwa
Maskini Luten wa watu hata lunch haitapandaHabari Wakuu,
Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki:Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022
Fuatana nami kupata yatakayojiri
UPDATES:
Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na
- Wakili Pius Hilla,
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka
- Tulimanywa Majige
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
- Wakili Michael Mwangasa
- Sisty Aloyce
- Gaston Garubindi
- Idd Msawanga
- Maria Mushi
- Nashon Nkungu
- John Mallya
- Dickson Matata
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tutaendelea na Shahidi, Tupo tayari Kuendelea
Shahidi anaingia kutoka Nje
Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea
Jaji: nakukumbusha Kwamba Tarehe 28 ulikuwa upo chini ya kiapo na leo utaendelea kutoa ushahidi wako chini ya kiapo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba sababu ya kelele za Jenereta tufunge madirisha tafadhali.
Kibatala: Mr Urio how are you?
Shahidi: Am fine
Kibatala: Did you have a nice Weekend?
Shahidi: like speak again
Kibatala: Did you have a nice Weekend?
Shahidi: like That!
Kibatala: Shahidi Umesha wahi Kukutana na Mazingira ya Kuambi Maneno Mazito Unayosema ya Ugaidi
Shahidi: Sijawahi Kukutana nayo
Kibatala: Umesema hauna tatizo la Kumbukumbu
Shahidi: Sina tatizo la Kumbukumbu
Kibatala: Iweje usikumbuke Tarehe 2 Muhimu Wewe Kukutana na Mbowe na Kwenda Ofisini Kwa DCI Ukizingatia wewe ni Mwanajeshi, na Luteni wa Jeshi
Shahidi: Mhe Jaji Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni Ndugu yangu, Nilikuwa sijui kuwa ni kweli au si Kweli, Mpaka nikaona kuwa Kumbe ni Serious
Kibatala: Wewe Luteni unaona Umejibu swali Langu la inawezekana Vipi usikumbuke Tarehe
Shahidi: Sijawahi Kusikia Maneno Mazito, Ndiyo Maana Nikaenda kutoa Riport Polisi Wafanye Uchunguzi
Kibatala: Swali langu inawezekana Vipi Ushindwe Kukumbuka Tarehe ya Matukio Kama hayo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mimi naona Kama Nimejibiwa
Jaji: Swali lilikuwa linawezekanaje Kuwa asahau Tarehe za Mambo Muhimu
Shahidi: Ilikuwa ni Mara ya Kwanza, Kusikia Kutoka Kwa Mheshimiwa Mbowe, Sikuwa nategemea
Kibatala: Vipi Kuhusu Tarehe ya kwenda Kwa DCI na yenyewe Ulikuwa shocked
Shahidi: Siyo Duty yangu Mimi Kukumbuka, Kazi yangu Ilikuwa Kutoa Riport tu
Kibatala: Kwakuwa Unaomekana Kujivua Duty ya Record Ya Tarehe, Unaweza za Ku tuisaidia Kwanini na Yeye DCI hakumbuki Tarehe Uliyo Kwemda Ofisini Kwake
Shahidi: Sifahamu, Siwezi Kumjibia
Kibatala: Siku Unakwenda Kwa DCI Kingai alikuwa Summoned akaja, Unaweza Kutuisaidia Kwanini huyu Kingai Mtu wa Tatu na Yeye hakumbuki ni Tarehe ipo Mlimkutana
Shahidi: Siwezi Kujua ni Kwa nini
Kibatala: Ni kwanini hata Inspector Swila ambaye ndiyo Afisa wa Upelelezi Aliyefungua Faili Tarehe 18 July 2020, Hakumbuki Tarehe hiyo
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je Kwa wewe Kama Luten Wa Jeshi unaona ni sahihi Kwa Nyinyi Watu wote hakumbuki Tarehe
Shahidi: Siwezi Kujibia
Kibatala: Umewahi Kusikia Msemo "The Lights are on but nobody at home"
Shahidi: Hapana Sijawahi Kusikia
Kibatala: Kwanini Tarehe 11 August 2020 ndiyo Maelezo Yako yaandikwe Mtoa Taarifa Ambaye ndiyo Ulisababisha Faili Kufunguliwa Tarehe 18 July 2020?
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Wewe ni Luteni wa TPDF uoni Kwamba Inategemewa Maelezo Ya Mtoa Taarifa Kuandikwa Mapema Kadriri inavyowezekana
Shahidi: Siwezi Kujibia Polisi, Sababu Wao Wana Utaratibu Wao wa Kazi na Mimi Nina Utaratibu Wangu Wa kazi
Kibatala: DCI alikifafanulia Kwamba Kwanini Maelezo Yako hayawezi Kuchukuliwa Siku ambayo wewe Umeenda ku report
Shahidi: Hawakufafamua chochote
Kibatala: Tarehe 11 August 2020 kwa Ushahidi Wako Ndiyo Ulikwenda Kutoa Maelezo Ushahidi Wako Kwa Inspector Swila.. Inspector Swila alikufafanulia Kwanini alisubiri Mpaka Mwezi Mmoja Baadae?
Shahidi: Hakufafanulia
Kibatala: Tukisema Kuwa Mlitunga Kesi Mapema Kisha Baadae Ndiyo Makaanza Kutafuta Watuhumiwa, Nitakuwa Nakosea Kwa Fact hizo
Shahidi: Utakuwa unakosea
Kibatala: Unafahamu Dhana ya Infiltration,.?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Maana yake
Shahidi: Kutoka sehemu Moja Kwenda sehemu Nyingine Kwa siri
Kibatala: Ni sahihi pia Maana yake Pana ni Kutuma Mtu Kwenda Kwenye Kambi ya Upinzani, Ili Kupata Taarifa Kamili
Shahidi: Hapana, Tactics inasema Kwamba ni Kitendo Cha Kutuma Mtu Kwa Siri
Kibatala: Nikumbushe tena Elimu yako
Shahidi: Form Four
Kibatala: Unafahamu Decoy
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Luteni wa Jeshi hufahamu Decoy
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mlijadili Kwa Pamoja Kumpeleka Mtu kwa Mbowe akiwa na Vifaa aweze Kupeleleza na Kurekodi Ushahidi
Shahidi: Hatujawahi Kujadili
Kibatala: Ni Kweli Katika Ushahidi Wako Kwamba Mheshimiwa Mbowe alikwambia atachukua Dola Kwa namna yoyote, Je Uchaguzi ulitajwa
Shahidi: Nafahamu Uchaguzi Ulitajwa
Kibatala: Bado Jeshi lilikuwa halina Role to Play Kwamba wewe ni Mwanajeshi uliye kazini na Mbowe anataka Ex Commandos, Bado Jeshi lilikuwa halina sababu ya Kupewa Taarifa?
Shahidi: Ni Taarifa ambazo hazina Ushahidi, Bado Jeshi litapeleka Kule Kule Kwa Polisi
Kibatala: Unamfahamu Aliyekuwa Chief of Staff Luteni Generali A. Shimbo
Shahidi: Namfahamu
Kibatala: akiwa katika Majukumu Yake ulikuwa Jeshini
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Namnukuu Tarehe 13 10 2010 "Katika Uchunguzi huu, Jeshi limejipanga Kuhakikisha Uchaguzi Unakuwa wa Amani na utulivu".. Uliwahi Kusikia?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Bado Unasisitiza Kwamba Mambo Ya Kiuchaguzi Jeshi halihusiki
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: huoni Kwamba Kwa Kutoa Kwako Taarifa Jeshi lingefanikisha Kuweka Decoy, (Mamluki) wa Kwenda Kukusanya taarifa ambazo ni sahihi?
Shahidi: The issue ni kwamba Mtu anaitwa Freeman Mbowe hapokei Simu za Kawaida, anasema Nitumie picha na Profile yake ili ajiridhishe Kwamba bado Wapo Katika Service, Kwa hiyo Endapo tungetuma Mtu ambaye bado yupo katika Service angegundua
Kibatala: Kwa hiyo Tactical appreciation Yako ilikwambia Kwamba Mheshimiwa Mbowe ana uwezo wa Kujua profile zao?
Shahidi: Ndiyo, Unafikiri Kwanini alitaka Picture na Profile zao?
Kibatala: Katika Ushahidi Wako Wote Kuna Mahala Popote Ulisema Kwamba Mbowe alikwambia Kwamba ana Access ya Mtu Mwingine Jeshini
Shahidi: Hapana
Kibatala: Tujadili Kuhusu Tactical Appreciation, Ni sahihi Kwamba Kamanda anakutana na Mazingira Fulani ambayo Kamanda anapanga Vikosi Vyake Kukabiliana na Mazingira hayo kwa Muda kwa Kupanga Mkakati
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Sasa Wewe Palikuwa na Several Unknown, Nimekuuliza Kama Mbowe alikuwa na Access Jeshini Ukasema hujui, Sasa huoni Kwamba Tactical appreciation Yako Ilikuwa si sahihi
Shahidi: Huyu Bwana ningemwambia kuwa Sitaki angemtumia nani, Ndiyo Maana nilifanya Tactical Appreciation na Kwenda Kuripoti Kwa DCI
Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwamba Katika hali hiyo Kuna mambo Kadhaa wa Kadhaa ulikuwa huyafahamu, Ndiyo Maana Ukasema Kwamba Ulikuwa hujui Kama alikuwa ameshaongea na Watu Wengine
Shahidi: Ndiyo nilikuwa sina Uhakika Kama Mbowe ana Option A, B na C
Kibatala: Sasa Jambo hilo Linaendana na Tactical Appreciation
Shahidi: Ndiyo linaendana
Kibatala: Kazi yangu ni Kuuliza Maswali
Kibatala: Umesema Ulikuwa huna Uhakika Mbowe alikuwa na Option A, B na C, Je ulijihakikishia Kwa Kumuhoji
Shahidi: Sikumuhoji
Kibatala: Unathibitisha alikuwa na Trust Yako yote
Shahidi: Sijui Kwa Yeye Sasa
Kibatala: Nakuuliza Wewe
Shahidi: Je ni Mimi peke yangu anaye niamini
Kibatala: Hakuna Mahala Uliposema Kwamba Mbowe alikutishia Wewe au Familia yako
Shahidi: Sijasema
Kibatala: Kwamba Mbowe alikuahidi Cheo Kama Incentive yako
Shahidi: Mbowe Hawezi Kunipa Cheo Jeshini
Kibatala: Kwa hiyo Mbowe alikuwa hawezi Kukuhaidi Cheo Sababu alikuwa Mbunge
Shahidi: Sahihi hawezi
Kibatala: Nashukuru Kwa jibu lako Zuri
Kibatala: Wakati Mbowe anakupa Maombi , Ulimkubalia au Moyoni Ulimkatalia
Shahidi: Ilikuwa Tactical Appreciation, Ile Kwamba nitachoma Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Masoko,
Kibatala: Na Kumdhuru Sabaya pia Ulikuwa Unachakata
Shahidi: Sijawahi Kumtaja Sabaya Mimi, Nilitaja Viongozi
Kibatala: Akili ya Kawaida ya Luteni haikuwa na zaidi ya Kumchimba Kwamba anataka Kulipua Vituo gani, Kukata Miti sehemu gani?
Shahidi: Hata Ingekuwa ni Mimi, Ukishaanza Kunidodosa nakosa trust na wewe.
Kibatala: Wakati Mnakutana Kupanga Matendo ya Ugaidi, Mahakama Itakapopima, Maneno yako Dhidi ya Maneno ya Mbowe sababu Hakuna Sauti Nyingine wala Decoy?
Shahidi: Ndiyo Maana nikatuma Vijana
Kibatala: Kwani Vijana hawa si Washtakiwa? Au Wapelelezi Wako?
Shahidi: Washtakiwa
Kibatala: Unakubaliana na Mimi sasa Mahakama itabidi ipime neno lako dhidi ya Mbowe kwa sababu Hapakuwa na Mtu Mwingine pale
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakumbuka Wakati wa Utejelezaji Wa Majukumu Yako, namna ulipompata Ling'wenya
Shahidi: Nakumbuka
Kibatala: Unakumbuka Uliongea na Baba Yake Ling'wenya
Shahidi: Nakumbuka
Kibatala: Unakumbuka Kwamba uliongea naye Tarehe ngapi
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Unakumbuka uliongea naye Majira gani
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Unafahamu a kwamba Mzee Ling'wenya alikukatalia Kumtoa Mwanaye sababu ya Mambo yaliyomtokea Mwanaye Jeshini
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba Yeye alishamtafutia Mwanaye Kazi ya kokoto
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba huyu Mzee (Baba yake Ling'wenya) ni Mwenyekiti wa Kijiji fulani huko Kusini
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Baba Yake alipokutafuta baada ya Kusikia Mwanae kakamatwa Unakumbuka Ulimjibu nini
Shahidi: Sikumbuki, Ila Niliwambia kuwa amuulize Boss wao
Kibatala: Kwani Boss wao ndiye aliye Mpigia Kumuombea Ruhusa Kwamba Kuna kazi
Shahidi: Ni Mimi
Kibatala: Ulimwambia Mzee Ling'wenya Kwamba Kuna kazi Kwa Mbowe lakini nataka akafanye Mipango ya Ugaidi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Maana ya Intrapment
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Maana ya Kumtoa Mtu kafara
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Unakumbuka Kwamba Nilikuuliza Unasali Wapi kwa sababu gani
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: umeapa kwa Biblia Je Unafahamu Kuhusu Daniel
Shahidi: Nafahamu Kuwa walitupwa Kwenye Tundu la Simba
Kibatala: Wewe Kuna tofauti na Walichomfanyia Daniel na Ling'wenya Mkristo Mwenzangu.?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwamba Ling'wenya alikuwa na kazi yake ya Kubonda Kokoto wewe Kwa Kikao Chenu na DCI ukamtafuta Kumwimgiza kwenye Matatizo
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Wakati Baba Yake Ling'wenya anakutafuta Kukuuliza Kwamba Mwanaye yupo wapi Ukajibu Ongea na Boss wake, Ni kweli
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu kwamba Mzee Ling'wenya alistaafu Bila Doa Lolote Serikalini
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kama Mzazi, anaumia Ka Ilivyokatwa kwa Mama Maria Kumuona Mwanaye anateseka Msalabani wakati hajafanya Kitu chochote
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Je inawezekana kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari.?
Shahidi: Inategemea kwa Mazingira
Kibatala: Je ni Mazingira Gani kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari?
Shahidi: Kiongozi anaweza asiwe Sehemu Moja
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwanini Kwenye Platoon Kiongozi anakuwa Mbele, Hata katika Biblia
Shahidi: Sifahamu, Sijawahi Kuona
Kibatala: Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa alipatwa na Battle Traumatic Fatigue
Shahidi: Mimi sifahamu Sijawahi Kusikia ana historia hiyo
Shahidi: Je Shahidi alitoa cheti cha Daktari
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Ulisema Kwamba ulienda Kwenye Ofisi ya Admin officer ukasoma Mafaili yao
Shahidi: Siyo Mafaili ya Taarifa individual, Bali Taarifa za Matukio tangu Siku Natoka
Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Ujui sababu ipi ambayo ilipelekea Adam Kasekwa Kufukuzwa Jeshini
Shahidi: Sijui zaidi ya Utovu wa Nidhamu
Kibatala: Unafahamu ni Maeneo gani Mahususi ambayo Walitembelea kwa ajili ya Kumdhuru Sabaya
Kibatala: Wewe Ukiwa katika kazi Maalum, Hukuona sababu kuuliza Kwa Bwire ni wapi Walipanga Kufanya Uhalifu
Shahidi: Mimi siyo Kazi Maalum
Kibatala: Kwani aliyetafuta Vijana ni Polisi au wewe?
Shahidi: Mimi
Kibatala: Mbowe aliomba Polisi wamtafutie Vijana?
Shahidi: Hapana
Shahidi: Bwire Hakuniambia
Kibatala: Katika Ushahidi Wako hujui wala hujazungumzia Kuhusu Milestone, Kokoriko na Triple B
Shahidi: Sijazungumzia
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Walikamatwa kwa tuhuma za Kupanga Kufanya Uhalifu wa Kumdhuru Sabaya
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Ni kweli Uliwatafuta Vijana Kwa ajili ya Kufanya Ukamataji kabla ya Uhalifu haujatokea
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Bado Hukuona Sababu ya Kumuuliza Bwire
Shahidi: Polisi Walitakiwa Wafanye Uchunguzi Wao
Kibatala: Kwani nani aliyemtafuta Adamoo
Shahidi: Ni mimi
Kibatala: Kwani nani alikuwa anaaminiwa na Adamoo kati yako na Polisi
Shahidi: Ni Mimi
Kibatala: akuna Taarifa a kwamba siku za Adamoo na Ling'wenya Wanakamatwa walikuwa wanapokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wao, Je huyo Msiri ni wewe
Shahidi: Siyo Mimi
Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako palikuwa na amtu Mwingine aliyekuwa anatoa Taarifa kwa DCI na Kingai
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Kwa Ufahamu Wako wewe Kuna mtu Mwingine ambaye alikuwa anawajua Adamoo na Ling'wenya
Shahidi: Hapana
Kibatala: Unafahamu Kwamba Adamoo na Ling'wenya Siku Wanakamatwa pale Rau Madukani walikuwa wanafanya nini.
Shahidi: Wala sijui Kama Walikamatwa Rau Madukani
Kibatala: Unafahamu a kwamba pale Rau Madukani Mohammed Ling'wenya alikuwa na Dada yake anaitwa Athima
Shahidi: Sifahamu, Hakuwahi kuniambia
Kibatala: Wewe Hukumu uliza Bwire
Shahidi: Sikumuuliza
Kibatala: Ulikuwa unafahamu Kwamba Moses Lijenje ana Dada yake anaishi Arusha
Shahidi: Hapana Sijui
Kibatala: Na wala Msiri wao unasema Siyo wewe
Shahidi; Siyo Mimi
Kibatala: Kuna sehemu katika maelezo yako Uliandika "Nilimpatia ACP kingai Namba za Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya aweze Kuwa fuatilia" ni sahihi
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Swala la Kwamba ACP kingai alikuwa namba za watu Watatu Mpaka Siku wanakamatwa, Je uliliongelea.?
Shahidi: Sikuongelea
Kibatala: Ni Suala la Kuwapa namba za Simu ni Swala la Muhimu au siyo la Muhimu
Shahidi: Ni suala la Muhimu
Kibatala: Unafahamu kwanini Kingai Wala Mtu Mwingine yoyote Hakuna anaye zungumzia Swala la Wewe Kuwapa namba za Simu kabla
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Swala la Kingai Kuwa na namba za Simu za Watu hawa Zina Implication gani Katika Uchunguzi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Mashahidi ambao Wamekutangulia, Walikuwa Wanamtafuta Lijenje Manually wakati Wana namba zao za simu
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba hata baada ya Watu hawa kukamatwa Kingai hakufanya chochote Katika Kuwafahamisha Wapendwa Wao
Shahidi: Hapana Sifahamu
Kibatala: Wakati Wa Tarehe 12 August 2020 Ulisema Ulimkabidhi Inspector Swila na kuandikishwa ID02
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Mwanzo Ukasema Kwamba Wakati Unamkabidhi Simu yako Ulitoa Line ya Vodacom ambayo ilikuwa na Mawasiliano yako na Watu Wengine
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Kwahiyo wewe Ulimkabidhi Inspector Swila Simu bila Sim card
Shahidi: Nilitoa ya vodacom ni kabakisha Moja
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Sim Card ya Vodacom,ulirudisha lini.?
Kibatala: Katika Nyaraka ipi Tukiangalia Tutaona Mlikabidhiana Sim Card ya Vodacom na Inspector Swila
Shahidi: Ipo
Kibatala: Ipo hapa Mahakamani
Shahidi: Hapana, Hapa Mahakamani Haipo
Kibatala: Ipo wapi
Shahidi: Sikujua Kama Inahitajika Mahakamani
Kibatala: Ile Simu ya Tecno Uliyowasha hapa, Ina SimCard ndani
Shahidi: Sikukagua kama ina Sim Card ndani
Kibatala: aliye sema Kwamba Ile simu ina Sim Card ndani ni nani
Shahidi: Ni Mimi
Kibatala: nikuombee utuonyeshe sim Card
Shahidi: Vyovyote Vile itakayokuwa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P34
Kibatala: haya Fungua utuonyeshe humo ndani Kuna Sim Card ya Mtandao gani
Shahidi anafungua
Shahidi: HAKUNA LINE HATA MOJA (SimCard)
Kibatala: Unafahamu thamani ya Kiapo chako
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba unawajibu wa Kulinda hadhi ya Jeshi la Wananchi Tanzania
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Ukweli na Uongo wako Unapimwa Katika Vitu Vidogo Vidogo Kama hivyo
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Nakuuliza tena, Wakati Unakabidhi Inspector Swila Simu Ilikuwa na Sim Card au Haina Sim Card
Shahidi: Ilikuwa na Sim Card
Kibatala: Unafahamu kwamba SimCard imepelekwa Wapi
Shahidi: Ilikuwa na Line ya Airtel Iliyobakia, Sifahamu Ipo wapi
Kibatala: Ile Sim Card Ya Vodacom na Zile simu zingine 3, katika Maelezo Yako ya Tarehe 12 August 2020 Ulizungumzia Katika Maelezo yako?
Shahidi: Sikuandika katika Maelezo Yangu
Kibatala: sisi tuna thibitisha Wapi Kwamba Ulikabidhi hizo Simu 3 wakati hazipo katika Maelezo yako wala Hakuna Hati ya Makabidhiano
Shahidi: lakini zipo Hapa Mahakamani
Kibatala: Ungekuwa Polisi Nimgekuuliza Unafahamu Chain of Custody wewe, ila wewe Afisa wa Jeshi Nitakuonea
Kibatala: Unafahamu Kwamba Hizo Simu 3 Zina Mahusiano na Kesi Hapa Mahakamani
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Zile simu zingine Mbili Kule Morogoro ulimwachi nani na Zilikuwa Chini ya Uangalizi wa nani
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Wala Hukumwambia Jaji Kama huko Ulipoziacha Zina password au hazina
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je unafahamu Kwa nini yule aliyekwambia ulete Simu 3 Kesho yake, hajazungumzia chochote Kuhusu hizo Simu 3
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu au hufahamu Kwamba Freeman Mbowe alikuwa na Kaka wa Damu, Generali ambaye katika Kifo cha huyo Generali Rais Magufuli alienda kwa Mbowe Kumpa pole
Shahidi: Nilisikia
Kibatala: Na unataka tukubali sisi watu wazima Kuwa aliacha Ndugu yake wa damu aliyenyonya naye ziwe Moja akutafute wewe?
Shahidi: Yule si alishastaafu
Kibatala: alistaafu lini
Shahidi: Sijui
Kibatala: Kati ya Wewe Luteni uliye kazini na Generali ambaye amestaafu nani anawafahamu Watu wengi Jeshini Waliopo na Waliotangulia?
Shahidi: Jenerali
Kibatala: Unasema Siku ya Kwanza Mbowe alikutafuta Siku ya Kwanza, Ukashangaa
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa
Shahidi: Rudia Swali
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu Mtu Muhimu Kama wewe bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa
Shahidi: Kwanza Mimi siyo Mtu Muhimu
Kibatala: Wacha Jaji aandike Kuwa wewe siyo Mtu Muhimu
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa
Shahidi: Siyo Utamaduni Wetu
Kibatala: Je ulitoa Taarifa Jeshini Kwamba Kiongozi Wa Chama Cha Upinzani Chadema Kakutafuta
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Kwenye Maelezo Yako Ulisema Kuwa Mliendelea Kuwasiliana naye kwa sababu wewe na Yeye Wote ni Kabila Moja
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Kwa hiyo hili la Ukabila ndiyo Kilikufanya uendelee Kuwasiliana na Mbowe
Shahidi: Hapana ni Mawasiliano
Kibatala: si Ndiyo Mawasiliano na Mwenyekiti wa Chadema wakati wewe Umesema hamfungamani na Chama Chochote
Shahidi: Mbowe ni Mbowe na Chadema ni Chadema
Kibatala: Kwanini sasa Katika Maelezo yako unasema "Freeman Mbowe Mwenyekiti Wa Chadema"
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: hapo ulimtenganisha Mbowe na Chadema?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Shahidi Ushahidi Wako Unasema Kwamba TSh 500,000 ulitoa TSh 300,000 Ikabakia TSh 200,000, Ukawapa Adamoo Ling'wenya TSh 199,000
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: katika Maelezo yako Uliandika Kwamba Mhe Mbowe alikumbushia Kuhusu Vijana, ukamwambia Kuwa wamepatikana 2
Kibatala: kwa hiyo wewe Kwa Maelezo Yako Ulisema Tarehe 20 July 2020 alinitumia Laki TSh 500,000 nikatoa TSh 300,000 Laki 2 Ikabakia Kwenye simu
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Katika Maelezo Hakuna Mahala Ulisema Uki Alisha TSh 200,000 Kwenye simu
Shahidi: Hakuna nilipoandika
Kibatala: Alikwambia Inspector Swila Maana ya haya Maelezo
Shahidi: Hakuniambia
Kibatala: Baada ya Siku Chache wapatikama Vijana Wawili nikawapatia TSh 195,000
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Maelezo yako na unachosema Kwenye Kizimba Vinafanana au Vinatofautiana?
Shahidi: Vinatofautiana
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P 1 na P 13
Kibatala: Nimeshika hapa Maelezo ya Onyo ya Adam Kasekwa ambayo Wenzetu Wanasema alikiri
Kibatala: Katika Ushahidi Wako, Unasema Uliwapa Tsh 195,000 katika TSh 199,000 Uliyotumiwa, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba TSh 4,000 Ilienda wapi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Kwa hiyo TSh 4,000 ya Ugaidi hujasema Ipo wapi
Shahidi: SIYO YA UGAIDI, BALI YA KUWASAFIRISHA
Kibatala: kwa hiyo Wenzetu Wanasema Yote TSh 199,000 ilitumika Kwenye Ugaidi, Kumbe siyo Ugaidi
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Maelezo haya yanasema kuwa alipokea TSh 87,000 kila Mmoja, Je Ni kweli au si Kweli
Shahidi: Sikumpatia Mtu Mmoja Mmoja, Niliwapa Kwa Pamoja
Kibatala: Kama Adam Kasekwa kasema Walipewa TSh 87,000, Atakuwa Kasema Uongo
Shahidi: atakuwa kasema Uongo
Kibatala: Unakubaliana Kuwa 87,000 Mara Mbili ni TSh 174,000? Unakubali unakataa
Shahidi: amount hiyo Mimi sijui
Kibatala: Nakuuliza kimahesabu 87,000 Mara Mbili ni TSh 174,000
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Adam Kasekwa anasema Jumla Uliwapa Tsh 174,000, Wewe Unasema TSh 195,000, Je Inatofautiana
Shahidi: Inatofautiana
Kibatala: Na Adam Kasekwa anasema Kwamba Fedha hiyo Uliyotumiwa na Mbowe ilikuwa ni Kuwarejeshea (Refund) ni sahihi au Siyo Sahihi
Shahidi: Ni sahihi
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba na sisi tuwe tunaangalia Kama Maelezo yapo Sahihi
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Pia awe anasoma Kile ambacho Kimeandikwa Kwa Mfano Hakuna Sehemu imeandikwa TSh 174,000 lakini Kuna TSh 87,000
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Majibu Kuhusu Majibu ya Kielelezo P 1 yaondoke
Kibatala: Ni sawa tufute Mstari Mmoja halafu tuanze Upya
Kibatala: Sasa Nilikuwa nakuuliza awali shahidi Kuhusu Maelezo yako inasema hivi, Baada ya Siku Mbili Waliopatikana Vijana Wawili Adamoo na Ling'wenya Ambao Niliwapatia TSh 195,000, tulipo kutana Eneo la Msavu
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Kwa hiyo Ni sahihi Kwamba hiyo Tsh 195,000, Kwamba Uliwapatia Kama Gharama ya Nauli zao Kutoka Walipo toka Kuja Morogoro
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Walipo kuja Morogoro Kutoka Walipo toka Uliwapa Tsh 195,000 kwa Ujumla au Lah.
Shahidi: Niliwapa Kwa Ujumla
Kibatala: Adam Kasekwa anasema Walikuja na Ling'wenya, "kwa kutumia Simu ya Mke wangu, Alinipigia Kuna kazi ya VIP PROTECTION, Maelezo sahihi anayo Luteni Urio"
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: anasema "alitupatia Kila Mmoja TSh 87,000 Kwa Maelezo ya Ling'wenya"
Shahidi: sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha zote hizo ilikuwa kwa ajili ya Refund
Shahidi: Ilikuwa kwa ajili ya Kuwafidia
Kibatala: Safi sana
Kibatala: Unakumbuka Ulisema Kwamba Uliwapa Nauli ya kwenda Wapi Adamoo na Ling'wenya Kutoka Morogoro
Shahidi: Niliwapa Cash Tsh 195,000, ila Sikumbuki niliwapatena TSh ngapi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba ile 199,000 Iliyotuma Baadae ndiyo Uliwapa Nauli ili waende Kwa Mbowe
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu Katika Maelezo Yake Adam Kasekwa, Katika Ukurasa wa Nne Mstari ya Mwisho, ni kila Mtu Kufika Moshi.. Wewe Unasema Walikwenda Dar es Salaam Kukutana na Mbowe, Je Statement hii Inafanana au inatofautiana?
Shahidi: Inatofautiana
Kibatala: nimeshila Maelezo ya Mohammed Ling'wenya Kielelezo namba P13, anasema kuwa "Baada ya mazungumzo Luteni Urio Aliniuliza Kuwa Mshahara wa Mtwara TSh ngapi, Nika jibu ni posho ya Elfu 15 kwa Siku, Basi Luteni Urio akanishauri Mshahara uwe Kuanzia TSh 800,000"
Je, ni sahihi Kwamba Ulimshauri Kuhusu Mshahara
Shahidi: Hapana
Kibatala: anaendelea Kusema Kuwa "alitupatia TSh 190,000 nauli ya kwenda Moshi"... Je ni sawa au zinatofautiana na Maelezo yako
Shahidi: tofauti, Pia tofauti hata na Ile ya Adamoo
Kibatala: You're Very Smart
Kibatala: Ling'wenya anazungumzia TSh 190,000, wewe unazungumzia TSh 199,000, Kuna tofauti ya TSh 9000
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa Wapokeajo wa hizi pesa wanasema Kuwa Matumizi Yake yalikuwa siyo Ugaidi bali nauli
Shahidi: Sikubaliani na wewe
Kibatala: Kwani wewe Umesikia Wao wanasema Kwamba ile Fedha ilikuwa kwa ajili ya Nini, Adama Kasekwa Si kwa ajili ya Refund na Mohamed Ling'wenya ilikuwa kwa ajili ya Kwenda Moshi?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Hapa Walikuwa wamekutana na Mbowe?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Walikuwa bado hawajafanya Ugaidi
Shahidi: Walikuwa ndiyo hawajafanya Ugaidi
Kibatala: Unafahamu kwamba wenzio Wanasema Hizo TSh 199,000 Mbowe zilifadhili ugaidi?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: ooh! Kumbe hata wenzako wamekuficha?
Kibatala: Ling'wenya nasema pia alipewa pesa akanunue Mavazi, Ni kweli
Shahidi: Si Kweli
Kibatala: Kwamba wewe unasema Ling'wenya alipewa pesa ya Kwenda Dar es Salaam, Yeye anasema Kwenda Moshi, Mmetofautiana..?
Shahidi: Ni sahihi tumetofautiana
Kibatala: eneo lingine Mlilotofautiana Ling'wenya anasema alipewa pesa ya Kurejeshwe Nauli wewe Unasema Nauli ya kwenda Dar es Salaam
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe Kielelezo Namba P 26
Kibatala: Ni kweli Kwamba Mbowe alikwambia umtafutie Ex commandos bila Kikomo
Shahidi: Hakuniambia Idadi yeye alisema Wao Waje tu
Kibatala: Kwenye Kielelezo P26, Ni sahihi Kwamba Kwa Mujibu wa Tarehe 20 July 2020 Saa 1 na Dakika 39 yeye Mbowe anasemaje
Shahidi: "Kaka Wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu sana"
Shahidi: Lakini kabla ya hiyo Meseji Kuna Mawasiliano ya Simu
Kibatala: Yapo wapi
Shahidi: Hayapo hapo
Kibatala: Soma Kama Ilivyo, Kwa Mujibu Wa Meseji hiyo Mbowe anauliza Watu wangapi
Shahidi: Kaka Wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu
Kibatala: kwa hiyo Namba hapo ni 3 au 4
Shahidi: Ndiyo Waliopatikana
Kibatala: Nenda Kwenye Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 3 na sekumde 30, Nani katuma hiyo Meseji
Shahidi: Ni Mimi
Kibatala: Unafahamu hiyo namba hapo
Shahidi: naona Meseji Kwemda Kwa Mbowe tu
Kibatala: kwa ni Meseji hiyo Uliyotuma hiyo Meseji Kwenda Kwa Mbowe, Je ni Namba ipi ya simu
Shahidi: Nilitumia Mtandao Wa Telegram
Kibatala: Mtandao Wa Telegram Unapotumia unahitaji Mtandao
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Namba Uliyotumia Mtandao huo wa Telegram ni namba ipi
Shahidi anaangua kichekoo ghafla hapa.....
Kibatala: Shahidi Usiche, Ndiyo Maana nilikwambia The Truth Shall set you Free.. Mwambie Mheshimiwa Jaji namba yako ipo au haipo
Shahidi: Haipo
Kibatala: Soma Katika Extraction Report hapo Wanasema Namba gani hiyo
Shahidi: 1130138344 DENIS OWNER
Kibatala: Namba hiyo Unaifahamu au huifahamu
Shahidi Sifahamu
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Shahidi apewe nafasi ya Kutoa Ufafanuzi
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wakili anataka Kufanya Submission Muda huu, asubirie Kwenye Re: examination, Swali langu Je Shahidi anaifahamu namba au haifahamu?
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Kama anataka Kuuliza namba, Ni Vizuri Shahidi afafanue tu
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji mimi naona Kuna tatizo na Line
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wametoa OBJECTION Nime re-battle, Wao Wafanye rejoinder siyo Mr. Kidando atoe Hoja mpya..
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwenye Rekodi za Mahakama Aliyetoa Kielelezo hicho ni Inspector Ndowo, Hatuoni Haki Kwa shahidi Kuulizwa Kielelezo hicho, Si Sawa kuzuiwa Kutoa Maelezo
Jaji: Kama nimesikia Vizuri Mr. Kibatala alikuwa anauliza Kuwa Shahidi anaifahamu au haifahamu hiyo namba, Mimi sijasikia akijibu hilo swali, alipotaka Kufanya Kufafanua Ndiyo Mr Kibatala akakataa, sasa hayo atamueleza Wakili Wake
Jaji: Ni Sahihi Kwa Shahidi Kujibu Maswali anayo Ulizwa na Wakili tu..
Kibatala: Shahidi Hiyo namba Unaifahamu au haifahamu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Kuna Wakili yoyote alikwambia Fafanua
Shahidi: Hapana
Kibatala: Unafahamu Juu ya Application inaitwa Free Sms
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ni application ambayo unatuma Meseji halafu pia unaweka namba kwa namba yako na Kuweka ya mtu unaye mtumia
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kuna wakili yoyote aliyekuuliza Kuhusu Free Sms
Shahidi: Hakuna
Kibatala: na Hakuna Wakili yoyote amekuomgoza Kuitambua hiyo Free Sms ilikuondoa hiyo dhana
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Soma, Hapo, Kuna Maelezo Unasema su siyo Salama Sana, Niwezeshe ili tuweze Kukutana
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Kuna Sehemu Yoyote Katika Kielelezo namba P 34 ambayo Freeman Mbowe amekueleza wewe Kwamba Mtumie Njia ya Mawasiliano Mbadala Kwa Sababu Simu Siyo Salama
Shahidi: Meseji ya Mwisho
Kibatala: haya tusomee
Shahidi: "Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu Deshi Deshi"
Kibatala: kwa hiyo kwa Tafsiri yako Ndiyo Kasema kuwa Simu Siyo Salama
Shahidi: Ndiyo Nilivyo Tafsiri
Kibatala: Katika hiyo Meseji ya Mwisho Kuna Neno simu siyo Salama
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Taja namba ya Mbowe Katika hiyo Meseji ya Mwisho
Shahidi: 0713933386
Kibatala: Soma Sasa Katika Kielelezo Kama hizo Meseji zinafanana au Tofauti
Shahidi: Zinafanana
Kibatala: Sasa soma namba ambayo ipo katika Kielelezo namba P 26 Meseji hiyo hiyo
Shahidi: Inatoka namba 729414989
Kibatala: ambayo ni Namba ya nani
Shahidi: FREE
Kibatala: Je namba ULIYOSOMA Mwanzo na Sasa hivi zinafanana.?
Shahidi: Hapana hazifanani
Kibatala: Kuna tofauti eeeeh!?
Shahidi: Ndiyo Kuna tofauti
Kibatala: Kubwa au Ndogo
Shahidi: Kubwa
Kibatala: Uliongozwa Kufafanua hiyo Tofauti
Shahidi: Sikuongozwa
Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Saa 2 na Dakika 15 na Sekunde 54
Shahidi: "Naomba nitumie nauli ya Ku' mobilise nikutane nao Moro"
Kibatala: Nani alikuwa anaomba nauli
Shahidi: Mimi ndiye niliye kuwa naomba nauli
Kibatala: Kwa hiyo DENIS URIO ndiye aliye Omba nauli kwa ajili ya Kuwa Mobilise
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Baada ya wewe kuomba nauli ndiyo Mbowe sasa akatuma TSh 500,000
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nitafutie Meseji yoyote ambayo Mbowe anatoa wazo yeye la kutuma yeye TSh 500,000
Shahidi ametumia dakika 1 kutafuta hapa..
Shahidi: HAKUNA
Kibatala: Ni nani kwa mujibu wa Kielelezo namba P 34 (Simu) aliye propose kuwa pesa ya Ku'. obilise iwe TSh 500,000?
Shahidi: Mimi Denis Urio
Kibatala: Kwa Mujibu Wa Meseji ya Tarehe Ngapi na Mwezi wa Ngapi ambayo wewe ndiyo Mtoa wazo
Shahidi: Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 19 na Sekunde 53
Kibatala: ambayo Meseji hiyo wewe Ulituma Kutoka Kwenye namba gani ya Kwako
Shahidi: Haionekani namba
Kibatala: ONGEZA SAUTI
Shahidi: Haionekani namba
Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 24 na Sekunde 02
Shahidi: "Usiwe unatumia namba yako Kutuma Pesa, Tumia Wasaidizi Wako au Wakala Kutuma"
Kibatala: Ni nani aliyetuma Meseji hii
Shahidi: Mimi Denis Urio
Kibatala: Nikumbushe Kule Kwa DCI na Kingai Uliambiwa Jambo gani Vile
Shahidi: Kuwapeleka Watu
Kibatala: Ni sahihi Katika Maelezo Yako uliyo andika, Uliambiwa Uendelee na kazi ya kumtufutia Vijana na Kuku Sanya Ushahidi
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Hao Wasaidizi Wa Mbowe Washa wahi Kukutumia pesa
Shahidi: Hapana
Kibatala: Katika Mawasiliano yako na Mbowe Uliwahi kutajiwa au Kupatiwa Fedha Kufanya Muamala na Mtu anaitwa Willy Kijana wa Mbowe? Na Wily alikutumia TSh ngapi
Shahidi: 199,000
Kibatala: Ndiyo Fedha ambazo Uliwapa Adamoo na Ling'wenya
Shahidi: Ndiyo hiyo
Kibatala: Swali la Mwisho kabla ya Lunch
Kibatala: Hiyo namba ya Willy ambayo ilituma hiyo Fedha ya TSh 199,000, Uliwapa akina DCI na Kingai
Shahidi: Haikuja namba, Alinitumia namba baadae
Kibatala: Hiyo namba hata Ka Ulipewa baadae, Ulimpa DCI au Kingai
Shahidi: Sikumpa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Kama Wenzangu wataridhia tupate Health Break baadae tuendelee na Cross Examination, Naomba pia nirudishe Vielelezo
Jaji: nahairisha Kwa Dakika 45 Mpaka Saa 7 na Dakika 45 ambapo Shahidi ataendelea Kutoa Ushahidi
Jaji: anatoka Mahakamani
KALICHOKOZE UONE KAMA UNAMASHAKA NALO KAMA HUJAITA MAJI MMA
Kibatala wewe jaza kurasa tu kwa maneno na maswali ila Urio amakuzidi ujanjaLeo Urio atuammbie ana tokea hoteli ya mahabusu gani?
Pia atuambie Mbowe alitaka kuchukua dola ipi? Dola ya Marekani au dola ya Zombabwe?
Mbowe sio gaidi!!!
[emoji849]akitoka hapo na cheo kinapanda katokomezagaidi lilitaka kupindua nchi mbowe ni GAIDI
Kila akila anamuona KingaiMaskini Luten wa watu hata lunch haitapanda