Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Ngoja tuone baada ya nusu saa jaji atakuja na maamuzi gani, ila kwa record ambazo amekuwa nazo na kwa utata ulioibuka saizi tunaweza kubashiri maamuzi atakayokuja nayo
 
Nashon ale wa mbuzi hivyo hivyo ila asihisi uonevu au upendeleo kwa upande fulani
 
Nashon Nkungu: Kuna msemo mmoja unasema "Muosha huoshwa", Mahakama hii hii Wakili aliyesimama Abdallah Chavula ndiye aliyesimama kuhoji mashahidi Wakina Adamoo kwamba komandoo mmoja anapiga askari wangapi.. Hatuku' Object, tulimuacha aulize Maswali yake hapa..
Hapa wakili msomi nkungu angesema tu Nyani haoni kundule😃😃
 
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake Jan 27, 2022

Fuatana nami kupata yatakayojiri

========

Jaji
ameingia Mahakamani Muda huu Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na
  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na
  • Wakili Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Michael Mwangasa
  • Paul Kisabo
  • Seleman Matauka
  • Alex Massaba
  • Maria Mushi
  • Khadija Aaron
  • Evaresta Kisanga
  • Michael Lugina
  • Sisty Aloyce
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo na Shahidi Mmoja ambaye Jana Alianza Kutoa Ushahidi Wake, Tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea

Jaji nakukumbusha kuwa Jana Ulikuwa Kiapo, na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula ataendelea Kumuongoza Shahidi

Wakili wa Serikali: Jana tuliishia 12 August 2020, Je Iambie Mahakama Wewe Ulifanya nini

Shahidi: Nilipeleka Simu ambazo sikwenda nazo Kwa Inspector Swila

Wakili wa Serikali: Ulimpeleka Wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Simu hizo tatu ulizo Mpelekea Inspector Swila Zilikuwa ni Mali ya nani

Shahidi: Zilikuwa ni Mali yangu

Wakili wa Serikali: Simu hizo tatu zilikuwa za aina gani

Shahidi: Tecno C9, Itel na Samsung ndogo ya Tochi

Wakili wa Serikali: Hebu tueleze Sasa nini Kilitokea Ulipofika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

Shahidi: Baada ya Kufika Nilikutana na Inspector Swila Nikamkabidhi Simu zote, Kwa Kunikabidhi Nyaraka ambayo Niliandika Majina yangu, Ilikuwa ina IMEI namba Baada ya Hapo akaandika Majina yake, nikasaini na Yeye akasaini

Wakili wa Serikali: Kwa Hiyo Jumla Nyaraka Ngapi zilizokabidhiwa

Shahidi: Jumla ni Nyaraka Nne

Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo ya Tarehe 12 August 2020 ziliandaliwa Nyaraka Ngapi

Shahidi: Nyaraka 3

Wakili wa Serikali: Nani aliziandaa zile Nyaraka

Shahidi: Aliziandaa Inspector Swila, Alinipa nikasaini akazitoa kopi akanikabidhi

Wakili wa Serikali: Shahidi Nikurejeshe Kwenye Nyaraka Iliyoandaliwa Tarehe 11 August 2020, Iliyoandaliwa na Inspector Swila, Ukiona Utaitambuaje?

Shahidi: Nitaitambua Kwa Majina Yangu Matatu, Denis Leo Urio, Nitaitambua Kwa Tarehe Niliyokabidhi ambayo ni Tarehe 11 August 2020, Nitaitambua Kwa Sahihi Yangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Nyaraka aweze Kuitambua

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Karatasi kwa Makini, halafu Iambie Mahakama Kama Unaifahamu

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naitambua Nyaraka hii Kwamba Nilisaini Mimi, Kwamba ina Majina yangu Matatu, Ina IMEI namba ya Simu yangu ya Tecno,

Wakili wa Serikali: Majina yako Yapo

Shahidi: Ndiyo Yapo

Wakili wa Serikali: Je Tarehe ipo

Shahidi: Tarehe ipo

Wakili wa Serikali: Ulisema Utaitambua Kwa Sahihi yako, Je Ipo.?

Shahidi: Ndiyo ipo

Wakili wa Serikali: Sasa Ungependa Mahakama Ifanye nini Juu ya hiyo Nyaraka

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ningependa Mahakama itambue hiyo Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba itambue Kama Kielelezo

Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema Ipokelewe Kama Kielelezo, Bali amesema Anaomba Mahakama itambue Nyaraka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi ni Maafisa Wa Mahakamani tuna Wajibu wa kusaidia

Jaji: Wakili Kibatala

Kibatala: Mheshimiwa kama Anaomba Kwa ajili ya a Utambuzi Ibakie hivyo

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Nyaraka anaombwa kwa ajili ya Utambuzi Hatuna Pingamizi

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji na Mimi pia sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji na Mimi Sina Pingamizi Juu ya Utambuzi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na mimi pia Sina Pingamizi Kama Nyaraka Inapokelewa kwa ajili ya Utambuzi Nyaraka Inatoka Benchi la Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji Pale Juu

Jaji: Naipokea Nyaraka Kama ID namba 2

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Wakili wa Serikali: Shahidi Awali Ulieleza Mahakama Kwamba Siku ya Tarehe 11 August 2020 Ulimkabidhi Simu TECNO CAMMON Inspector Swila Shahidi Je Simu hii Ukiona Utaweza Kuitambuaje

Wakili wa Serikali: Kingine kitachokufanya Utambue

Shahidi: Kama Ukiwasha inatoka Picha ya Familia Yangu Kwenye Screen Saver

Wakili wa Serikali: Unaposema picha ya Familia Unamaanisha Nini

Shahidi: Nime save Kwenye Screen Saver Ina Display Picha Ya Mke wangu

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Nikienda Kwenye Program ya Telegram nitakuta Mawasiliano Baina yangu Mimi na Mbowe, Mawasiliano Ya Meseji

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama itupatie Kielelezo Cha Mashitaka Namba 34

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumkabidhi Shahidi Kielelezo hiki, Kwa ajili ya Utambuzi

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tazama hii Simu, Jaribu Kuangalia Yale uliyokuwa Unaeleza Mahakama Kama Yapo

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Mwonekano Wa Nje hii Ndiyo Simu Yangu yenyewe

Wakili wa Serikali: Mwonekano gani Wa Nje

Shahidi: Cover Jeusi Screen protector kupasuka Kwa Juu Simu yenyewe ni TECNO CAMMON

Wakili wa Serikali: Shahidi Vipi Kuhusiana na Yale Mengine

Shahidi: Mpaka niwashe Simu

Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hii ndiyo picha ya mke wangu

Wakili wa Serikali: ionyeshe mahakama, mahakama ione

Jaji: Wakili Mallya, ungependa uone picha ya mke wake

Wakili John Mallya: hapana mheshimiwa Jaji, tunateta Jambo jingine kabisa

Shahidi: Mawasiliano yangu ya Ujumbe Mfupi Kati yangu Mimi na Freeman Mbowe haya hapa

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano yapo Kwenye nini

Shahidi: Tulikuwa tuna wasiliana Kwa Mfumo wa Telegram

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanaomba Kujiridhisha

SIMU ya Shahidi Inapelekwa kwenye Benchi la Utetezi

Wakili Kibatala Anaenda Kwa Shahidi Kizimbani Kuangalia Mawasiliano Ya Telegram Kwenye Simu

Wakili John Malya na Yeye anaomba Kwenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Wakili Dickson Matata Mheshimiwa Jaji namimi naomba Kwenda Kujiridhisha Matata anafika na Kukagua Simu ya Shahidi Bado Wakili Matata Yupo Kizimbani Wakili Nashon Nkungu Na Yeye anaenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi

Mawakili Wa Serikali Wanateta Kwa Pamoja


Wakili wa Serikali: Shahidi hizo Meseji Ulizo Onyesha Mahakama Unaweza Kuzisoma.?

Shahidi anasoma Meseji July 2020,

Kaka Mtu tatu ni Muhimu sana,

Yes Bro Kuna Members Wawili Mpaka sasa, Mmoja Yupo Tunduma na Mmoja Yupo Dodoma

Security Ni Muhimu Sana, Wasije kutelekezwa, Siwezi Kuwatelekeza..

Naomba Unitumie Nauli ya Kuwa Mobilise Niende nao Moro

Kwa Namba Ipi

Laki 5 inatumwa

Nashukuru Nimepata Usiwe Unatumia Namba yako Binafsi Kutuma, Tumia Watu wengine au Wakala

Wapo Wapi Bro

Nipo nao Njiani

Mkuu Shikamoo Vipi Maendeleo ya mgonjwa wako

Wale Watu wawili nipo nao nasubiri Maelekezo yako

Kaka Nashukuru,

Je wanaweza Kuja Dar Naomba Unitumie Nauli na Dar Wapi watafikia Wanaweza Kuja Dar na Kesho Wakaenda Hai

Nitumie Nauli

Kwa namba ipi

Kwa namba yangu

Usitume Kwa namba yako

Nitatuma Gari ya kuwapokea Ubungo

Namba ninayo watumia ni Ya Dereva Wangu anaitwa Willy yeye Ndiye atakaye Wapokea

Nashukuru Nimepata

Asante Bro Hope Wameondoka

Wawili Wapo Ruvu Wawili bado Uwe unatuma Pesa ya Kutosha ya akuwa Mobilise

Kaka bado Nipo Kamati Kuu,

Tuma Meseji

Shikamoo Kaka Vipi Mgonjwa wako Wale Wapo Tayari Kuondoka

Nilishindwa Kupokea simu yako sababu ya Deshi Deshi Naamini umenielewa,

Shahidi: Mwisho wa Kunukuu

Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano Uliyokuwa Ukiyasoma Yalikuwa ni Baina ya nani na nani

Shahidi: Ni Baina yangu Mimi na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Rejea Meseji ya Kwanza Kusoma

Shahidi: Kaka wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu Sana, Siku zimekwisha

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Hao Mtu tatu au Nne Nini hasa a Kilikuwa kinazungumzwa

Shahidi: Nilikuwa Nimeongea naye hapo NYUMA kuhusu Kuwatafuta Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya na Moses Lijenje Kwamba hata hao waende Siku zinaenda

Wakili wa Serikali: Huo Ujumbe Ulikuwa Unatoka Kwa nani

Shahidi: Unatoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 14 na Sekunde 50

Shahidi: Ya Tarehe ngapi

Wakili wa Serikali: Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Mmoja Kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: Tarehe hiyo hiyo 30 Mwezi July 2020, Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 2

Shahidi: Bro Kuna Members Wawili Mpaka Saa hizi, Mmoja Yupo Tunduma anahusika na Magari ya kwenda nje na Mwingine yupo Dodoma SGR

Wakili wa Serikali: Huyo aliyepo Tunduma anafanya Kazi ya Kusafirisha Magari Kwenda Nje ni nani

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Na Mwingine anaye fanya kazi SGR Dodoma ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni nani alikuwa kazaliwa Mwaka 1980

Shahidi: Ni Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Ni nani kazaliwa Mwaka 1986

Shahidi: Ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Haya Inayofuata Baada ya hiyo, Isome

Shahidi: Simu Siyo Salama, Niwezeshe niweze Kukutana nao

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo kwenda kwa nani

Shahidi: Niliandika Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Ulimaanisha nini Kusema Simu Siyo salama

Shahidi: Simu Siyo Salama, Kum insure Kuwa Hakuna Mtu wa Kut' track

Wakili wa Serikali: Soma Inayofuata

Shahidi: Kikubwa ni Security ya Shughuli zao Wanazofanya Saa hizi, Wasije Kutelekezwa baadae

Wakili wa Serikali: Meseji hiyo ni ya nani

Shahidi: Inatoka Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Hao wawili Kwa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?

Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao

Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Enheeeee Meseji inayofuata

Shahidi: Sema Tu Kaka nifanyeje

Wakili wa Serikali: Hiyo Meseji Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata

Shahidi: Mmoja kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986

Wakili wa Serikali: akiyezaliwa Mwaka 1986 ni nani

Shahidi: Ni Moses Lijenje na Mwaka 1986 ni Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Soma inayofuata

Shahidi: Naomba Unitumie Nauli ni Mobilise nikutane nao Morogoro

Wakili wa Serikali: Nani hao Uwa Mobilise, na Meseji Imetoka Kwa na nani Kwenda Kwa nani

Shahidi: Meseji Imetoka. Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe, Wakukutanao Moro ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje

Wakili wa Serikali: Shahidi naKurudisha Nyuma, Kuna a Meseji hao wawili Kuanzia Siyo Mbaya walikuwa wakina nani na Siyo Mbaya ni nini hasa

Shahidi: Alikuwa ni Moses Lijenje na Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata

Shahidi: Kwani Kiasi gani na Kwa Simu ipi

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Mlikuwa Mnazungumzia Kiasi cha Nini

Shahidi: Kiasi cha pesa

Wakili wa Serikali: Kwa ajili ya Shughuli gani

Shahidi: Kwa ajili ya nauli ya Kuwachukua Khalfani Bwire na Moses Lijenje Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Meseji ilikuwa ni ya nani na inaenda kwa nani

Shahidi: Ya Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Soma hapo

Shahidi: Laki 5, 0787 555200

Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji

Shahidi: Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Sawa, Tayari kaka

Wakili wa Serikali: Meseji Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata

Shahidi: Nashukuru Nimepata

Wakili wa Serikali: hii nayo imeandikwa na nani Kwenda Kwa Nani

Shahidi: Kutoka Kwangu Kwenda Kwa mbowe

Wakili wa Serikali: Tusomee Meseji ya Mwisho Kabisa

Shahidi: Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu ya Deshi Deshi Deshi naamini Umenielewa

Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu

Wakili wa Serikali: Shahidi izime hiyo Simu alafu Irejeshe Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nirejeshe Kielelezo P34

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulimpeleka Simu Kwa Inspector Swila aina ya Techno C9 Je Simu hiyo Ukiona Kipi Kitaku fanya Utambue

Shahidi: Upande wa Kushoto Juu Housing Imepasuka, Ukiwasha haiwezi Kuwaka, Haiwezi Ku Display Kitu, Vilevile Ina rangi Nyeusi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P28

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako naomba ni Muonyeshe shahidi Kielelezo

Wakili wa Serikali: Shahidi habu itizame hii Simu

Shahidi: Hii ni Simu yangu aina ya Tecno C9, Sababu Nimeitambua Kwenye Housing yake Juu Kushoto imepasuka, halafu Ina Rangi Nyeusi, na Uki switch On haiwezi Kuonyesha

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Ruhusa ya Mahakama Shahidi aweze Kuiwasha Simu

Shahidi: Haiwaki

Wakili wa Serikali: Shahidi Siku hiyo Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila, simu aina ya Itel, Je Utaitambuaje

Shahidi: Mfuniko, Cover ina Rangi Ya Blue Nyuma, Screen Protector Yake Mbele Juu Imepasuka, Ukiwasha itakuwa Na Picha Kwenye Screen Saver Either Mke wangu au Watoto Wangu au Wote

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupatiwe Kielelezo namba 33

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Simu, Tuambie

Shahidi: Nimeitambua hii Simu aina ya Itel, Kama Nilivyosema Kuwa Ina Housing ya Blue na Juu Kwenye Screen Kioo Chake Kimebanduka

Wakili wa Serikali: Shahidi Vilevile Unasema Siku ile ya Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila Ulikabidhi Simu aina ya Samsung Je Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Ni simu Ndogo, Samsung ya torch lakini Pia Chini Kwenye eneo la Earphone Kulia Imekatika

Wakili wa Serikali: habu Shika Simu hii, utueleze

Shahidi: Naitambua ndiyo Simu yangu ndogo Samsung ya Torch, nyeupe na lakini Kwenye earphone Plug ni nyeupe

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie, awali wakati tunakuhoji Uliambia Mahakama Kwamba Ulifahamiana na FREEMAN MBOWE Kuanzia Mwaka 2012 Mpaka Mwaka 2020, Je ilikuwa Ina Maana Gani

Shahidi: Nilikuwa na Maana Kwamba, Baada ya Kuhitaji Vijana Wa kwenda Kuchukua Dola na Kuwapata alikata Mawasiliano na Mimi Kuanzia Tarehe 24 July 2020 alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Mahusiano yenu Baina yako wewe na Freeman Mbowe Kiujumla yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri, lakini alikata Mawasiliano na Mimi, Wala sijui kwanini alikata Mawasiliano na Mimi

Wakili wa Serikali: Jumla ya Kiasi gani Cha Fedha Ulicho pokea Kutokana Kwa Freeman Mbowe Uliyokuwa Unapokea Kwa ajili ya Kumpelekea wale Watu

Shahidi: Jumla ni Tsh 699,000

Wakili wa Serikali: Umekuwa Unamtaja Freeman Mbowe Mara Nyingi Sana, Je ukimuona unaweza kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakupekea kumtambua

Shahidi: Body Morphology, anapenda kuvaa miwani, mnene Kiasi na mweusi kiasi

Wakili wa Serikali: Sasa tuambie kama yupo hapa mahakamani

Shahidi: Yule pale kavaa T-shirt, kavaa miwani

Mahakama: Kicheko kwa maana Freeman Mbowe hajavaa miwani leo

Wakili wa Serikali: Shahidi eleza basi, unasema ulipopokea ujumbe kutoka kwa Freeman Mbowe, ujumbe ule wewe ulienda kutolea taarifa kwa Boazi DCI na Ramadhan Kingai, ukiacha hao wawili nani mwingine uliyewahi kumpelekea taarifa hiyo?

Shahidi: Sikuwahi kumpa mtu yoyote taarifa

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama ni Kwanini Hukwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa wako wa kazi Jeshini

Shahidi: Si kwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa zangu wa kazi Kwasababu ni Taarifa za Uhalifu, Ndiyo Maana Nilienda Moja kwa Moja Kwa DCI Kwenye Vyombo Vya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Ni wakati Gani Ulipeleka Taarifa Kwa Viongozi wako

Shahidi: Nilipeka Taarifa Kwa Viongozi...........

Wakili JOHN MALLYA... Mheshimiwa Jaji hiyo ni Leading Question, Hakuna Sehemu shahidi anasema Kuhusu Viongozi wale

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Labda alikuwa hanifuatilii, Mwanzo Niliuliza Kabla Wakili

JOHN MALYA: bado hajaJibu Hoja

Jaji: Rudia Swali

Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo Ulimwambia nani

Shahidi: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo nilimwambia Kiongozi wangu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kiongozi Wako Una maanisha nini

Shahidi: Ni Mkuu wa Kikosi ninacho fanyia Kazi cha 92KJ

Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu ni hayo tu Anaketi..

************************************************

Wakili Nashon Nkungu: Nimesikia Mwanzo Unasema Wewe ni Mkristo

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Dhehebu gani

Shahidi: Roman Catholic

Nashon: Unasali Wapi

Shahidi: Huko Ngerengere

Nashon: Unasali Jumuiya

Shahidi: sababu Ya Majukumu siudhurii Mara kwa Mara

Nashon: Unafahamu a kwamba Baada ya Kesi hii Unaweza Kutoka Kama shujaa au Mtu asiye na Thamani Duniani

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Msemo unaosema Kuwa ni Heri Kufa Jasiri Kuliko Kuishi Katika Utumwa, Unafahamu Kwamba Kesi hii Inafuatiliwa Nchini na Duniani Kote

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyuma ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Naomba Mheshimiwa Jaji arudie hapo

Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyima ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda

Shahidi: Hata sasa Nipo Pamoja na Jeshi

Nashon: Baada ya Kueleza hayo, Naamini Umetafakari Vizuri

Nashon: tuanze hapo Unaposema Jeshi lipo na wewe, Kivipi

Shahidi: Wanafahamu Kuwa nimekuja Kutoa Ushahidi

Nashon: Nikisema Kwamba Hujatoka kazini Kwako Utakataa

Shahidi: Ndiyo Nimetoka Kazini Kwangu

Nashon: Je Unaruhusa au Movement Order

Shahidi: Ndiyo ninayo

Nashon: Unayo hapo Mahakamani

Shahidi: Hapana Nimeiacha Hotelini

Nashon: anaitwa Nani

Shahidi: CO wangu

Nashon: Anaitwa nani

Shahidi: Siwezi Kumtaja hapa Mahakamani

Nashon: kwanini uwezi Kumtaja

Shahidi: Mpaka Nipate Maelekezo Ya Kutaja Viongozi Wa Ulinzi

Nashon: Maelekezo Kutoka kwa nani

Shahidi: Mahakama

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba apewe Ruhusa anitajie

Jaji: Shahidi Kwani Mahakama Imekukataza

Shahidi: Anaitwa Light Keno CJP

Nashon: Twende sehemu nyingine, Je kwa mwaka mnatoa makomandoo wangapi?

Shahidi: Siwezi kusema pia

Nashon: huwezi Kusema kwa sababu hutaki au Kiburi chako tu?

Nashon: Kwa sababu ni Siri

Nashon: Tutajie siri zingine ili tusikuulize

Shahidi: Siwezi kusema

Nashon: Nimesikia Unasema Kwamba Kikosi Chako Cha 92 KJ, Je Kuna kikosi +kingine

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Kitaje

Shahidi: Siwezi Kutaja Mambo ya Jeshi

Nashon: Kwanini

Shahidi: Kwa sababu Kesi Inafuatiliwa ndani na Nje ya Nchi na Nina Kiapo

Nashoni: Hapa Umekula Kiapo Kingine

Shahidi: Ndiyo siwezi Kutaja sasa

Nashon: Mheshimiwa Jaji Naomba atutajie

Jaji: Naona Kashasema Hawezi Kusema

Nashon: Haya na wewe kozi yako ya mwisho ya ukomandoo ulifanya lini

Shahidi: Mwaka 2010

Nashon: Kozi zipi ulifanya

Shahidi: SIWEZI KUSEMA

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Mahakama, Section 364 ya Sheria ya Ushahidi, Inahusu General Jurisdiction ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji ni 264 ya CPA ambayo inasema Mahakama Kuu Itakuwa na Mamlaka, Kuwa Shahidi anapofika Shahidi aweze Kutoa Ushahidi, Na Shahidi amefika

Hataki Kutoa Majibu, Tunaomba Mahakama Yako itoe Mwongozo na pia Imuonye..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Muda Kidogo tupitie Mahakama Ipo Kimyaaa

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: anasimama Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, Tumemsikiliza Wakili Msomi Mwenzetu Wakili Nashon Nkungu, Kwa Heshima Zote Siye hatukubaliani na Maombi yake anayoyataja kwa kuwa hayana Mashiko Kisheria

Mheshimiwa Jaji Wakili anaomba Mahakama Imlazimishe Shahidi Kujibu swali lake la Level gani ya Mafunzo aliyo yafanya, Shahidi amemueleza hilo Suala la Siri Hawezi Kutamka hadharani Yeye ni Wa level gani Katika fani yake

Na Wakili kabla ya hapo amekuwa aliuliza Maswali Kadhaa kuhusu Ikama ya Jeshi la Tanzania, Shahidi amemueleza Kwamba hawezi Kueleza Kutokana na Kiapo Chake

Ameeleza Pia Kuhusu Kifungu Cha 264 cha Criminal Procedure Act, Ambapo Wakili anasema Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Kupitia Kifungu hiki, Naomba Nikisome.......... Anakisoma...

Tafsiri ipo wazi Hapa, Kwamba Subject to the Provision of this Act...... Maana yake description Ya Mahakama Katika hili Inategemea na Sheria zingine. Masuala ya kiushahidi, Kupokelewa Kwa Ushahidi Mahakamani Kuna Sura yake Maalum ambayo ni Sura Ya 6 ya Sheria ya Ushahidi ya 2019

Na Sheria hiyo Ina vifungu Mahususi Kinacho Elekeza ni Mazingira Yepi Shahidi anaanza Kulazimishwa Na Mahakama Kujibu Swali.. Mhe Jaji Kifungu Cha 158 cha Sheria hiyo kimeeeleza Ni wakati gani Mahakama, na Mazingira Yepi hasa Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Ajibu Swali

Na si hicho tu, lakini hata Kifungu cha 156 Cha Sheria hiyo hiyo nacho Kinatoa Mazingira Yepi,, Mheshimiwa Jaji Mimi nitajielekeza Kifungu cha 155 Kifungu Kidogo Cha Kwanza....... Nanukuuu

Mheshimiwa Jaji Swali la level ya Mafunzo ya Shahidi Ni swali ambalo halina Mahusiano na Kinacho Jadiliwa Mbele ya Mahakama au Kilichopo Mbele ya Mahakama

Mheshimiwa Jaji Maswala ya namna hii, labda yawe yanapelekea Ku Injure character ya witness basi Shahidi anaweza Kulazimishwa Kuyajibu. Kinyume na hapo Shahidi hawezi Kulazimishwa

Mhe Jaji, Wakili hajaonyesha Mahakama Lengo la suala lake la Kufahamu Mafunzo ya Shahidi Ni Ku' Injure Character yake. Suala la Forces inatoa Makomandoo Wangapi, Force Ina vituo Vingapi Vya Makomandoo, Ni Maoni yetu Maswali ya Namna hiyo hayalengi Ku Distort Character Ya Shahidi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji siysi tunachokiona hapa Inawezekana msomi ameshindwa kumtingisha Shahidi, Anataka kumlazimisha shahidi azungumze masuala ya ikama ya jeshi..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani ukisoma Kifungu Cha 155 Sura ya 6, kinasema.. Anasoma..

Wakili wa Serikali: Hata Maswali Yenyewe haya follow under 155, Untest Velacity Ya Shahidi Kwa Kutaka Kufahamu Kuna Vituo Vingapi Vya Makomando, Unatest Velacity ya shahidi Kutaka Kujua Mafunzo yake ni ya level gani, Unatest Velacity Kwa Kutaka Kujua Makomando Wanazlishwa Kwa Mwaka Mara ngapi

Wakili wa Serikali: Shahidi amekuja Mahakamani Kwa Kusema Yeye ni Askari Wa Jeshi la Wananchi, Kutoka Kikosi cha 92 KJ, Cheo Chake ni Luteni na Jukumu lake anasimama Askari Walio Chini yake 30..

Shahidi amekuja Kutoa Ushahidi Kwa Kile Kilichopekea Kesi Hii Kuwapo Mahakamani, Katika Ushahidi Wake Hakuna Mahala ameeleza Kwamba Jeshi La Wananchi Tanzania lilihusika Kwa namna Yoyote Ile

Wakili wa Serikali: Sasa Mheshimiwa Jaji Katika Mazingira hayo, Utaona Maswali la Wakili hayana Relevance, Hata Ukiangalia Kwa Namna Yoyote Ile haya Affect Character Ya Shahidi..

Baada ya maelezo hayo marefu kutoka kwa Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, mawakili wa serikali wametana wote na wanajadiliana kwa dakika kadhaa...

Anaendelea

Wakili wa Serikali: Wakili wa Serikali Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Hoja ya Wenzetu haina Msingi, ajielekeze Katika Masuala ambayo anaweza Kutest Velacity ya Shahidi.. Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi Yupo sahihi..

Kwa namna ambayo Maswali yameulizwa Mahakama haina Mamlaka ya Kumlazimisha Shahidi ayajibu kamwe... Mheshimiwa Jaji naomba nimkaribishe Mwenzangu Pius Hilla aendelee

Wakili wa Serikali: Hata Kama angejielekeza Mahakama Katika Utaratibu Huu, haingefaa, Na Mahakama Haiwezi Kujiwekea Utaratibu Wake Pale ambapo Kuna Utaratibu Uliowekwa Kisheria..

Jaji: karibu, Bila Kurudia Kile ambacho amezungumza Mwenzako..

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nitajitahidi Kuwa Brief Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyepo Kizimbani aliulizwa swali Kuhusiana na level yake Ya Ukomando, haaieleza Mahakama Kwamba Kwa Kiapo Chake

Hawezi Kueleza level ya Mafunzo yake. Mheshimiwa Jaji tunakazia Maneno Kwa Kiapo chake Mheshimiwa Jaji ni kosa LA Jinai Ku' Communicate Information ambayo ni Confidential Mhe Jaji sect 4(1) ya CAP 47 ya National Security, Inasema Ni Kosa la Jinai Ku Communicate Information

Na hauruhusiwi Kufanya hivyo, Kwakuwa Shahidi amesha eleza Kwa Kiapo Chake Harusiwi Ku Communicate Kwa Kiapo Chake Kusema Level ya Mafunzo ambayo amefanya, Kuna Maswali ambayo Shahidi anaweza Kujibu na mengine hatakiwi Kujibu.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nimalizie Kwa Kusema Kwamba Taarifa Ya Kuhusiana na Level Ya Ukomando wa shahidi Kwa Mujibu wa Kiapo Chake hawezi Kusema.. Na Kwa kuwa Kuna Backup Ya Sheria, Remedy siyo Kulazimishwa, Bali wakili aelekezwe Wakili Kuuliza Maswali Sahihi

Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama Itupilie Mbali Maombi ya wakili (Nashon Nkungu)

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, it's Very Interesting, Leo nimeshuhudia OBJECTION Ya kupinga Identification ya Shahidi, Kama Nilikuwa namuuliza Shahidi ana Elimu gani........

Anakatishwa na Objection..

Wakili wa Serikali Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Samahani, Hakuna suala la Identification ya Shahidi, Kilichopo hapa Ni Kutaja Kumlazimisha Shahidi Kusema Mambo ambayo hawezi Kusema..

Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, Niendelee Kwenye Submission yangu, Naomba Mahakama Kwa Wivu Mkubwa Mahakama ilinde Mamlaka yake, Hapa shahidi amekula Kiapo Kimoja, la sivyo Mwanzoni Wakati wa Kiapo angesema anakula Kiapo Lakini anakiapo Kingine kinamkataza Kusema Yeye ni nani

Sisi tunaomba Kiapo alichokula hapa Mahakamani Kiwe Juu Ya Viapo Vingine Vyote, Hakuna Sheria ambayo Wametoa Kwamba Inakataza, Bali Tunaona Kwamba Ni Vifungu Vinavyoruhusu Kujua Shahidi Ni nani Na Elimu yake ni Ipi..

Mheshimiwa Jaji Nikienda Kwa Section Moja Moja Kama ambavyo imetajwa hapa, Naona Vyote ni Permissive, Vyote ni Relevant kwa Sababu Lengo lake Ni Kutaka Ku Establish Je ana ujuzi Wa Kile anachokiongea, anatoka Kweli Ngerengere?

Hatuoni kwa namna Gani suala Hilo lina kuwa Relevant, Mheshimiwa Jaji Kiusalama Hakuna Mambo ambayo yanakiuka, Hatuoni Shida Kusema Mtu fulani na Kusema Yeye ni nani, Wamekuja Hapa Watu Wakasema Wao Nia Inspector, Wao ni Ma RCO

Nashon: Mheshimiwa Jaji Hizo Section ambazo wame zitaja Zina refers Kwenye Kifungu cha 151.. Kwamba Hapatakuwa na Excuse Juu ya Kutoa Ushahidi.. Tunahitaji accuracy, Tunahitaji Conformity, Kwa sababu Watakuja Hata Washtakiwa Watasema wao Wana Kiapo..

Nashon Nkungu: Kuna msemo mmoja unasema "Muosha huoshwa", Mahakama hii hii Wakili aliyesimama Abdallah Chavula ndiye aliyesimama kuhoji mashahidi Wakina Adamoo kwamba komandoo mmoja anapiga askari wangapi.. Hatuku' Object, tulimuacha aulize Maswali yake hapa..

Tunaomba Haki iwe pande zote Mbili, Mheshimiwa Jaji Kwenye kutumia Kifungu Sahihi au siyo Sahihi, Ni Kifungu ambacho tunaona ni sahihi...

Nashon: Kuhusiana na Powers Kuhusu Ku' Compel Shahidi, Kwa Kuweka hii Hoja Vizuri Mahakama Kwa Kutumia hivi Vifungu Vya 141, 156, 155, 158 Vyote ni Vifungu Wezeshi ambavyo vinaipa Mahakama Mamlaka Wajibu wa Kutoa Ushahidi

Nashon: Kama Hakuna Kifungu Kinachokataza, Ni Msimamo Wetu Kwamba Shahidi Yupo Compellable Kuweza Kujibu.. Mheshimiwa Jaji Kwenye Hoja Nyingine Kwenye 158 cha Sheria ya Ushahidi Kifungu Kipo Subject kwenye Subsection Two ya 158 ya Sheria ya Ushahidi

Narudia Kumuomba Shahidi ajibu swali langu Kama alivyoulizwa

Wakili Nashon Nkungu: Anakaa Chini Mahakama Ipo Kimya Kidogo

Jaji: Mme' site sheria kadhaa na vifungu kadhaa, Ili niweze kutoa maamuzi ambayo ni sahihi naomba kupitia kidogo hivi, kwa dakika 30 kisha tutarejea..

Jaji anatoka..
Mimi naomba nijifunze jambo. Mkuu Nyendo,unawezaje kutype kwa kasi kiasi hiki updates za matukio haya moja kwa moja?
 
kaa kwa kutulia usubirie nondo za mawakili wasomi wa utetetezi.mutujuwa hamujuwi
Huyo anapoteza muda wa mahakama kwa kuchukua muda mrefu wa kuuliza mwaswali ambayo ni irrelevant hana lolote. Ukitaka kujua anauliza maugoro fuatilia issue ya P.G.O kwenye trial within trial rulling yake ilikujaje huko amepoteza muda mreefu kuuliza maugoro na wafuasi wake kwenye maudaku yao ya space ya maria waliamini kuwa wameshinda , uliona majibu yalitokaje?
 
Na hizo meseji na miamala ya simu?
Mahakamani hakuna mambo ya kufikirika kama hekaya za Abunuasi. Hapo ni ushahidi wa kitukio je kama walikutana halafu FM akamnyandua Urio unadhani kuna ushahidi.
 
Ngoja tuone baada ya nusu saa jaji atakuja na maamuzi gani, ila kwa record ambazo amekuwa nazo na kwa utata ulioibuka saizi tunaweza kubashiri maamuzi atakayokuja nayo
Absolutely, na hii itamuwezesha shahidi kitojibu maswali mengi kwamba ni siri za jeshi.
 
Huyo anapoteza muda wa mahakama kwa kuchukua muda mrefu wa kuuliza mwaswali ambayo ni irrelevant hana lolote. Ukitaka kujua anauliza maugoro fuatilia issue ya P.G.O kwenye trial within trial rulling yake ilikujaje huko amepoteza muda mreefu kuuliza maugoro na wafuasi wake kwenye maudaku yao ya space ya maria waliamini kuwa wameshinda , uliona majibu yalitokaje?
naona pia wanamkingia shahidi kifua,hawataki aulizwe maswali .kwa nini wamemleta mahakamani?
 
naona pia wanamkingia shahidi kifua,hawataki aulizwe maswali .kwa nini wamemleta mahakamani?
Kumbuka utetezi wana mashahidi wawili ambao siku wakija kutoa ushahidi wanatatoa ushahidi chamber- haktakuwa na viherehere wa CHADEMA wala mleta updates- na haya kaomba Mh. Kibatala
 
Kumbuka utetezi wana mashahidi wawili ambao siku wakija kutoa ushahidi wanatatoa ushahidi chamber- haktakuwa na viherehere wa CHADEMA wala mleta updates- na haya kaomba Mh. Kibatala
Kwahiyo?
 
Back
Top Bottom