Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwananchi online wapi nihamie uko?Wewe nawe ni kilaza kwel. Kwan hizo msg na text za telegram leo ndio unazisikia. Ushaidi wa mwanzo alieleza kila kitu sema mwandishi aliruka ilo eneo, na uzi ukaja huku ukilaumu kwanini aliruka. Pitia mwananchi online utaona
Sawa mkuu. Tusubiri ushahidi wake ufike mwisho halafu utuoneshe "maushahidi mazito"Wale waliokuwa wanadanganyana kwenye kitchen Party ya akina maria na fatuma kuwa urio ,urio hayupo sasa huyo hapo anafunguka na maushahidi mazito ta telegram, huyu shahidi ndio anawamaliza kabisa
Keshalala mbereJaji amerejea?
Baada ya kuona wakili wa utetezi ana chenga za maudhiMaswali mawili tu wameshaanza kuahirisha kesi 😂
Hakuna mahala popote toka kwa shahid yeyote message za telegram zikiandikwa au kuzungumzwa sasa ndio mwanzo urio kamezeshwa ushahidi anatema kama churaWewe nawe ni kilaza kwel. Kwan hizo msg na text za telegram leo ndio unazisikia. Ushaidi wa mwanzo alieleza kila kitu sema mwandishi aliruka ilo eneo, na uzi ukaja huku ukilaumu kwanini aliruka. Pitia mwananchi online utaona
hujui na hutakaa ujue msingi wa swali kama hili - kaa chini ndugu.Sasa idadi ya makomandoo Tanzania inahusiana nini na kesi ya ugaidi ya Mbowe
Kindumbwe ndumbwe muosha huoshwa wangoje devo toka kwa Tinganga urio hafundishiki yupo traumatisedBaada ya kuona wakili wa utetezi ana chenga za maudhi
Hujui kitu, nyamaza. Hakuna maswali ya hovyo, kuna majibu ya hovyo na ndio maana unaweza kusikia mtu anaulizwa "homeboy" maana yake nini na akasema "sijui". Ngoja nikupe kionjo kidogo. Urio hakuwepo Ngerengere wakati washitakiwa wanafukuzwa. Lakini anasema alifahamu kutoka Administration kuwa wamefukuzwa. Huyu huyu Urio alikuwa na namba za hawa watu, je walikuwa ni marafiki wa kawaida kwake au alipataje kujua namba zao?? Ataulizwa kabla ya kuwasiliana nao kwa jambo la Mbowe, ni lini tena aliwasiliana nao wakati wakiwa wamefukuzwa. Je aliwafundisha mbinu za jambo lolote? Kwanini yeye ndio achague hawa katika wote anaojua, je alifahamu hawa ndio wanaweza kukata miti, kulipua vituo vya mafuta na masoko? Shahidi ndiye aliyewatambua washitakiwa kabla hawajaja kwa Mbowe - je anafahamu uwezo wao katika kutenda hayo????Sheria ya ushahidi ina masharti yake na imetoa mwongozo ni swali gani linafaa kuulizwa na kujibiwa, ni wajibu wa mahakama kusimamia kuwa yale maswali yanayokubaliwa na sheria ndio yanaulizwa, sasa huyu wakili anajiulizia tuu maswali ya hovyo kama lileswali waliokuwa wa namuuliza shahihidi habari za baba yake aliyekuwa IGP
CCM bana, yaani kwa akili zenu hivi kuna Jaji duniani anaweza kumtia mtu hatiani miaka 30 kwa michongo kama hii, sana sana mnaidhalilisha nchi yetu pendwa kimataifa.Huyu Gaidi Mboe aliwarubuni hao jamaa, mipango yake ilikuwa kuvuruga amani ya nchi na sio kumlinda.
eti bila aibu linadai walikuwa walinzi!!!
jambazi mkubwa huyu.
Huyu Gaidi alikuwa na mtandao ndani kwa ndani yaani alikuwa na vibaraka wengi ambao walikuwa wanamsaidia jinsi ya kuihujumu serikali. huyu lazima achezee miaka ya kutosha.
Hakuna.Kuna record yoyote ya video au audio?
Shahidi alinusa harufu yanuhalifu. Hao polisi waliobeba ka.Huyu Shahidi mkuu atafungwa kwa kuisababishia serikali hasara kwa taarifa za uongo
Sent from my Lenovo TB-7305X using JamiiForums mobile app
Habari Wakuu,
Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake Jan 27, 2022
Fuatana nami kupata yatakayojiri
========
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na
- Wakili Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
- Wakili Nashon Nkungu
- John Mallya
- Dickson Matata
- Michael Mwangasa
- Paul Kisabo
- Seleman Matauka
- Alex Massaba
- Maria Mushi
- Khadija Aaron
- Evaresta Kisanga
- Michael Lugina
- Sisty Aloyce
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo na Shahidi Mmoja ambaye Jana Alianza Kutoa Ushahidi Wake, Tupo Tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea
Jaji nakukumbusha kuwa Jana Ulikuwa Kiapo, na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula ataendelea Kumuongoza Shahidi
Wakili wa Serikali: Jana tuliishia 12 August 2020, Je Iambie Mahakama Wewe Ulifanya nini
Shahidi: Nilipeleka Simu ambazo sikwenda nazo Kwa Inspector Swila
Wakili wa Serikali: Ulimpeleka Wapi
Shahidi: Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Simu hizo tatu ulizo Mpelekea Inspector Swila Zilikuwa ni Mali ya nani
Shahidi: Zilikuwa ni Mali yangu
Wakili wa Serikali: Simu hizo tatu zilikuwa za aina gani
Shahidi: Tecno C9, Itel na Samsung ndogo ya Tochi
Wakili wa Serikali: Hebu tueleze Sasa nini Kilitokea Ulipofika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Shahidi: Baada ya Kufika Nilikutana na Inspector Swila Nikamkabidhi Simu zote, Kwa Kunikabidhi Nyaraka ambayo Niliandika Majina yangu, Ilikuwa ina IMEI namba Baada ya Hapo akaandika Majina yake, nikasaini na Yeye akasaini
Wakili wa Serikali: Kwa Hiyo Jumla Nyaraka Ngapi zilizokabidhiwa
Shahidi: Jumla ni Nyaraka Nne
Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo ya Tarehe 12 August 2020 ziliandaliwa Nyaraka Ngapi
Shahidi: Nyaraka 3
Wakili wa Serikali: Nani aliziandaa zile Nyaraka
Shahidi: Aliziandaa Inspector Swila, Alinipa nikasaini akazitoa kopi akanikabidhi
Wakili wa Serikali: Shahidi Nikurejeshe Kwenye Nyaraka Iliyoandaliwa Tarehe 11 August 2020, Iliyoandaliwa na Inspector Swila, Ukiona Utaitambuaje?
Shahidi: Nitaitambua Kwa Majina Yangu Matatu, Denis Leo Urio, Nitaitambua Kwa Tarehe Niliyokabidhi ambayo ni Tarehe 11 August 2020, Nitaitambua Kwa Sahihi Yangu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Nyaraka aweze Kuitambua
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Karatasi kwa Makini, halafu Iambie Mahakama Kama Unaifahamu
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naitambua Nyaraka hii Kwamba Nilisaini Mimi, Kwamba ina Majina yangu Matatu, Ina IMEI namba ya Simu yangu ya Tecno,
Wakili wa Serikali: Majina yako Yapo
Shahidi: Ndiyo Yapo
Wakili wa Serikali: Je Tarehe ipo
Shahidi: Tarehe ipo
Wakili wa Serikali: Ulisema Utaitambua Kwa Sahihi yako, Je Ipo.?
Shahidi: Ndiyo ipo
Wakili wa Serikali: Sasa Ungependa Mahakama Ifanye nini Juu ya hiyo Nyaraka
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Ningependa Mahakama itambue hiyo Nyaraka
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba itambue Kama Kielelezo
Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema Ipokelewe Kama Kielelezo, Bali amesema Anaomba Mahakama itambue Nyaraka
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi ni Maafisa Wa Mahakamani tuna Wajibu wa kusaidia
Jaji: Wakili Kibatala
Kibatala: Mheshimiwa kama Anaomba Kwa ajili ya a Utambuzi Ibakie hivyo
Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Nyaraka anaombwa kwa ajili ya Utambuzi Hatuna Pingamizi
Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji na Mimi pia sina Pingamizi Juu ya Utambuzi
Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji na Mimi Sina Pingamizi Juu ya Utambuzi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na mimi pia Sina Pingamizi Kama Nyaraka Inapokelewa kwa ajili ya Utambuzi Nyaraka Inatoka Benchi la Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji Pale Juu
Jaji: Naipokea Nyaraka Kama ID namba 2
Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo
Wakili wa Serikali: Shahidi Awali Ulieleza Mahakama Kwamba Siku ya Tarehe 11 August 2020 Ulimkabidhi Simu TECNO CAMMON Inspector Swila Shahidi Je Simu hii Ukiona Utaweza Kuitambuaje
Wakili wa Serikali: Kingine kitachokufanya Utambue
Shahidi: Kama Ukiwasha inatoka Picha ya Familia Yangu Kwenye Screen Saver
Wakili wa Serikali: Unaposema picha ya Familia Unamaanisha Nini
Shahidi: Nime save Kwenye Screen Saver Ina Display Picha Ya Mke wangu
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Nikienda Kwenye Program ya Telegram nitakuta Mawasiliano Baina yangu Mimi na Mbowe, Mawasiliano Ya Meseji
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama itupatie Kielelezo Cha Mashitaka Namba 34
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumkabidhi Shahidi Kielelezo hiki, Kwa ajili ya Utambuzi
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tazama hii Simu, Jaribu Kuangalia Yale uliyokuwa Unaeleza Mahakama Kama Yapo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Kwa Mwonekano Wa Nje hii Ndiyo Simu Yangu yenyewe
Wakili wa Serikali: Mwonekano gani Wa Nje
Shahidi: Cover Jeusi Screen protector kupasuka Kwa Juu Simu yenyewe ni TECNO CAMMON
Wakili wa Serikali: Shahidi Vipi Kuhusiana na Yale Mengine
Shahidi: Mpaka niwashe Simu
Kibatala: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Hii ndiyo picha ya mke wangu
Wakili wa Serikali: ionyeshe mahakama, mahakama ione
Jaji: Wakili Mallya, ungependa uone picha ya mke wake
Wakili John Mallya: hapana mheshimiwa Jaji, tunateta Jambo jingine kabisa
Shahidi: Mawasiliano yangu ya Ujumbe Mfupi Kati yangu Mimi na Freeman Mbowe haya hapa
Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano yapo Kwenye nini
Shahidi: Tulikuwa tuna wasiliana Kwa Mfumo wa Telegram
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanaomba Kujiridhisha
SIMU ya Shahidi Inapelekwa kwenye Benchi la Utetezi
Wakili Kibatala Anaenda Kwa Shahidi Kizimbani Kuangalia Mawasiliano Ya Telegram Kwenye Simu
Wakili John Malya na Yeye anaomba Kwenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi
Wakili Dickson Matata Mheshimiwa Jaji namimi naomba Kwenda Kujiridhisha Matata anafika na Kukagua Simu ya Shahidi Bado Wakili Matata Yupo Kizimbani Wakili Nashon Nkungu Na Yeye anaenda Kizimbani Kwa Shahidi Kushuhudia Mawasiliano ya Telegram ya Simu ya Shahidi
Mawakili Wa Serikali Wanateta Kwa Pamoja
Wakili wa Serikali: Shahidi hizo Meseji Ulizo Onyesha Mahakama Unaweza Kuzisoma.?
Shahidi anasoma Meseji July 2020,
Kaka Mtu tatu ni Muhimu sana,
Yes Bro Kuna Members Wawili Mpaka sasa, Mmoja Yupo Tunduma na Mmoja Yupo Dodoma
Security Ni Muhimu Sana, Wasije kutelekezwa, Siwezi Kuwatelekeza..
Naomba Unitumie Nauli ya Kuwa Mobilise Niende nao Moro
Kwa Namba Ipi
Laki 5 inatumwa
Nashukuru Nimepata Usiwe Unatumia Namba yako Binafsi Kutuma, Tumia Watu wengine au Wakala
Wapo Wapi Bro
Nipo nao Njiani
Mkuu Shikamoo Vipi Maendeleo ya mgonjwa wako
Wale Watu wawili nipo nao nasubiri Maelekezo yako
Kaka Nashukuru,
Je wanaweza Kuja Dar Naomba Unitumie Nauli na Dar Wapi watafikia Wanaweza Kuja Dar na Kesho Wakaenda Hai
Nitumie Nauli
Kwa namba ipi
Kwa namba yangu
Usitume Kwa namba yako
Nitatuma Gari ya kuwapokea Ubungo
Namba ninayo watumia ni Ya Dereva Wangu anaitwa Willy yeye Ndiye atakaye Wapokea
Nashukuru Nimepata
Asante Bro Hope Wameondoka
Wawili Wapo Ruvu Wawili bado Uwe unatuma Pesa ya Kutosha ya akuwa Mobilise
Kaka bado Nipo Kamati Kuu,
Tuma Meseji
Shikamoo Kaka Vipi Mgonjwa wako Wale Wapo Tayari Kuondoka
Nilishindwa Kupokea simu yako sababu ya Deshi Deshi Naamini umenielewa,
Shahidi: Mwisho wa Kunukuu
Wakili wa Serikali: Hayo Mawasiliano Uliyokuwa Ukiyasoma Yalikuwa ni Baina ya nani na nani
Shahidi: Ni Baina yangu Mimi na Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Rejea Meseji ya Kwanza Kusoma
Shahidi: Kaka wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu Sana, Siku zimekwisha
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Hao Mtu tatu au Nne Nini hasa a Kilikuwa kinazungumzwa
Shahidi: Nilikuwa Nimeongea naye hapo NYUMA kuhusu Kuwatafuta Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya na Moses Lijenje Kwamba hata hao waende Siku zinaenda
Wakili wa Serikali: Huo Ujumbe Ulikuwa Unatoka Kwa nani
Shahidi: Unatoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu
Wakili wa Serikali: Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 14 na Sekunde 50
Shahidi: Ya Tarehe ngapi
Wakili wa Serikali: Tarehe 20 July 2020
Shahidi: Mmoja Kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986
Wakili wa Serikali: Tarehe hiyo hiyo 30 Mwezi July 2020, Nenda Kwenye Meseji ya Saa 2 na Dakika 2
Shahidi: Bro Kuna Members Wawili Mpaka Saa hizi, Mmoja Yupo Tunduma anahusika na Magari ya kwenda nje na Mwingine yupo Dodoma SGR
Wakili wa Serikali: Huyo aliyepo Tunduma anafanya Kazi ya Kusafirisha Magari Kwenda Nje ni nani
Shahidi: Ni Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: Na Mwingine anaye fanya kazi SGR Dodoma ni nani
Shahidi: Ni Moses Lijenje
Wakili wa Serikali: Ni nani alikuwa kazaliwa Mwaka 1980
Shahidi: Ni Moses Lijenje
Wakili wa Serikali: Ni nani kazaliwa Mwaka 1986
Shahidi: Ni Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: Haya Inayofuata Baada ya hiyo, Isome
Shahidi: Simu Siyo Salama, Niwezeshe niweze Kukutana nao
Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo kwenda kwa nani
Shahidi: Niliandika Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Ulimaanisha nini Kusema Simu Siyo salama
Shahidi: Simu Siyo Salama, Kum insure Kuwa Hakuna Mtu wa Kut' track
Wakili wa Serikali: Soma Inayofuata
Shahidi: Kikubwa ni Security ya Shughuli zao Wanazofanya Saa hizi, Wasije Kutelekezwa baadae
Wakili wa Serikali: Meseji hiyo ni ya nani
Shahidi: Inatoka Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Meseji inayofuata
Shahidi: Hao wawili Kwa kuanzia Siyo Mbaya, Hawawezi Kutekelezwa, Wanakuwa na Mimi Full time, Wamekwambia Wanataka nini.?
Wakili wa Serikali: Meseji hii ilikuwa Imetoka Kwa nani
Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Neno hawa Wawili Kuanzia Siyo Mbaya ni akina nani hao
Shahidi: Ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje
Wakili wa Serikali: Enheeeee Meseji inayofuata
Shahidi: Sema Tu Kaka nifanyeje
Wakili wa Serikali: Hiyo Meseji Imetoka Kwa nani
Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata
Shahidi: Mmoja kazaliwa Mwaka 1980 na Mwingine Kazaliwa mwaka 1986
Wakili wa Serikali: akiyezaliwa Mwaka 1986 ni nani
Shahidi: Ni Moses Lijenje na Mwaka 1986 ni Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: Soma inayofuata
Shahidi: Naomba Unitumie Nauli ni Mobilise nikutane nao Morogoro
Wakili wa Serikali: Nani hao Uwa Mobilise, na Meseji Imetoka Kwa na nani Kwenda Kwa nani
Shahidi: Meseji Imetoka. Kwangu Kwenda Kwa Freeman Mbowe, Wakukutanao Moro ni Khalfani Bwire na Moses Lijenje
Wakili wa Serikali: Shahidi naKurudisha Nyuma, Kuna a Meseji hao wawili Kuanzia Siyo Mbaya walikuwa wakina nani na Siyo Mbaya ni nini hasa
Shahidi: Alikuwa ni Moses Lijenje na Khalfani Hassan Bwire
Wakili wa Serikali: Meseji inayofuata
Shahidi: Kwani Kiasi gani na Kwa Simu ipi
Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji
Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Mlikuwa Mnazungumzia Kiasi cha Nini
Shahidi: Kiasi cha pesa
Wakili wa Serikali: Kwa ajili ya Shughuli gani
Shahidi: Kwa ajili ya nauli ya Kuwachukua Khalfani Bwire na Moses Lijenje Kwenda Kwa Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Meseji ilikuwa ni ya nani na inaenda kwa nani
Shahidi: Ya Mbowe Kuja Kwangu
Wakili wa Serikali: Soma hapo
Shahidi: Laki 5, 0787 555200
Wakili wa Serikali: Nani aliandika Hiyo Meseji
Shahidi: Mimi Kwenda Kwa Freeman Mbowe
Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata
Shahidi: Sawa, Tayari kaka
Wakili wa Serikali: Meseji Imetoka Kwa nani
Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Soma Meseji inayofuata
Shahidi: Nashukuru Nimepata
Wakili wa Serikali: hii nayo imeandikwa na nani Kwenda Kwa Nani
Shahidi: Kutoka Kwangu Kwenda Kwa mbowe
Wakili wa Serikali: Tusomee Meseji ya Mwisho Kabisa
Shahidi: Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu ya Deshi Deshi Deshi naamini Umenielewa
Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani
Shahidi: Imetoka Kwa Freeman Mbowe Kuja Kwangu
Wakili wa Serikali: Shahidi izime hiyo Simu alafu Irejeshe Mahakamani
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nirejeshe Kielelezo P34
Wakili wa Serikali: Shahidi Ulimpeleka Simu Kwa Inspector Swila aina ya Techno C9 Je Simu hiyo Ukiona Kipi Kitaku fanya Utambue
Shahidi: Upande wa Kushoto Juu Housing Imepasuka, Ukiwasha haiwezi Kuwaka, Haiwezi Ku Display Kitu, Vilevile Ina rangi Nyeusi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P28
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako naomba ni Muonyeshe shahidi Kielelezo
Wakili wa Serikali: Shahidi habu itizame hii Simu
Shahidi: Hii ni Simu yangu aina ya Tecno C9, Sababu Nimeitambua Kwenye Housing yake Juu Kushoto imepasuka, halafu Ina Rangi Nyeusi, na Uki switch On haiwezi Kuonyesha
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Ruhusa ya Mahakama Shahidi aweze Kuiwasha Simu
Shahidi: Haiwaki
Wakili wa Serikali: Shahidi Siku hiyo Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila, simu aina ya Itel, Je Utaitambuaje
Shahidi: Mfuniko, Cover ina Rangi Ya Blue Nyuma, Screen Protector Yake Mbele Juu Imepasuka, Ukiwasha itakuwa Na Picha Kwenye Screen Saver Either Mke wangu au Watoto Wangu au Wote
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupatiwe Kielelezo namba 33
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu Tizama hii Simu, Tuambie
Shahidi: Nimeitambua hii Simu aina ya Itel, Kama Nilivyosema Kuwa Ina Housing ya Blue na Juu Kwenye Screen Kioo Chake Kimebanduka
Wakili wa Serikali: Shahidi Vilevile Unasema Siku ile ya Tarehe 12 August 2020 kwa Inspector Swila Ulikabidhi Simu aina ya Samsung Je Ukiona Utaitambuaje
Shahidi: Ni simu Ndogo, Samsung ya torch lakini Pia Chini Kwenye eneo la Earphone Kulia Imekatika
Wakili wa Serikali: habu Shika Simu hii, utueleze
Shahidi: Naitambua ndiyo Simu yangu ndogo Samsung ya Torch, nyeupe na lakini Kwenye earphone Plug ni nyeupe
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie, awali wakati tunakuhoji Uliambia Mahakama Kwamba Ulifahamiana na FREEMAN MBOWE Kuanzia Mwaka 2012 Mpaka Mwaka 2020, Je ilikuwa Ina Maana Gani
Shahidi: Nilikuwa na Maana Kwamba, Baada ya Kuhitaji Vijana Wa kwenda Kuchukua Dola na Kuwapata alikata Mawasiliano na Mimi Kuanzia Tarehe 24 July 2020 alikata Mawasiliano na Mimi
Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Mahusiano yenu Baina yako wewe na Freeman Mbowe Kiujumla yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri, lakini alikata Mawasiliano na Mimi, Wala sijui kwanini alikata Mawasiliano na Mimi
Wakili wa Serikali: Jumla ya Kiasi gani Cha Fedha Ulicho pokea Kutokana Kwa Freeman Mbowe Uliyokuwa Unapokea Kwa ajili ya Kumpelekea wale Watu
Shahidi: Jumla ni Tsh 699,000
Wakili wa Serikali: Umekuwa Unamtaja Freeman Mbowe Mara Nyingi Sana, Je ukimuona unaweza kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakupekea kumtambua
Shahidi: Body Morphology, anapenda kuvaa miwani, mnene Kiasi na mweusi kiasi
Wakili wa Serikali: Sasa tuambie kama yupo hapa mahakamani
Shahidi: Yule pale kavaa T-shirt, kavaa miwani
Mahakama: Kicheko kwa maana Freeman Mbowe hajavaa miwani leo
Wakili wa Serikali: Shahidi eleza basi, unasema ulipopokea ujumbe kutoka kwa Freeman Mbowe, ujumbe ule wewe ulienda kutolea taarifa kwa Boazi DCI na Ramadhan Kingai, ukiacha hao wawili nani mwingine uliyewahi kumpelekea taarifa hiyo?
Shahidi: Sikuwahi kumpa mtu yoyote taarifa
Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama ni Kwanini Hukwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa wako wa kazi Jeshini
Shahidi: Si kwenda Kutoa Taarifa Kwa wakubwa zangu wa kazi Kwasababu ni Taarifa za Uhalifu, Ndiyo Maana Nilienda Moja kwa Moja Kwa DCI Kwenye Vyombo Vya Uchunguzi
Wakili wa Serikali: Shahidi Iambie Mahakama Ni wakati Gani Ulipeleka Taarifa Kwa Viongozi wako
Shahidi: Nilipeka Taarifa Kwa Viongozi...........
Wakili JOHN MALLYA... Mheshimiwa Jaji hiyo ni Leading Question, Hakuna Sehemu shahidi anasema Kuhusu Viongozi wale
Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Labda alikuwa hanifuatilii, Mwanzo Niliuliza Kabla Wakili
JOHN MALYA: bado hajaJibu Hoja
Jaji: Rudia Swali
Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo Ulimwambia nani
Shahidi: Baada ya Ukamataji Taarifa hizo nilimwambia Kiongozi wangu
Wakili wa Serikali: Unaposema Kiongozi Wako Una maanisha nini
Shahidi: Ni Mkuu wa Kikosi ninacho fanyia Kazi cha 92KJ
Wakili wa Serikali: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu ni hayo tu Anaketi..
************************************************
Wakili Nashon Nkungu: Nimesikia Mwanzo Unasema Wewe ni Mkristo
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Dhehebu gani
Shahidi: Roman Catholic
Nashon: Unasali Wapi
Shahidi: Huko Ngerengere
Nashon: Unasali Jumuiya
Shahidi: sababu Ya Majukumu siudhurii Mara kwa Mara
Nashon: Unafahamu a kwamba Baada ya Kesi hii Unaweza Kutoka Kama shujaa au Mtu asiye na Thamani Duniani
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Unafahamu Msemo unaosema Kuwa ni Heri Kufa Jasiri Kuliko Kuishi Katika Utumwa, Unafahamu Kwamba Kesi hii Inafuatiliwa Nchini na Duniani Kote
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyuma ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Naomba Mheshimiwa Jaji arudie hapo
Nashon: Unafahamu Kwamba Ukieleza Ukweli yaliyo Nyima ya Pazia, Hata Jeshi Litakulinda
Shahidi: Hata sasa Nipo Pamoja na Jeshi
Nashon: Baada ya Kueleza hayo, Naamini Umetafakari Vizuri
Nashon: tuanze hapo Unaposema Jeshi lipo na wewe, Kivipi
Shahidi: Wanafahamu Kuwa nimekuja Kutoa Ushahidi
Nashon: Nikisema Kwamba Hujatoka kazini Kwako Utakataa
Shahidi: Ndiyo Nimetoka Kazini Kwangu
Nashon: Je Unaruhusa au Movement Order
Shahidi: Ndiyo ninayo
Nashon: Unayo hapo Mahakamani
Shahidi: Hapana Nimeiacha Hotelini
Nashon: anaitwa Nani
Shahidi: CO wangu
Nashon: Anaitwa nani
Shahidi: Siwezi Kumtaja hapa Mahakamani
Nashon: kwanini uwezi Kumtaja
Shahidi: Mpaka Nipate Maelekezo Ya Kutaja Viongozi Wa Ulinzi
Nashon: Maelekezo Kutoka kwa nani
Shahidi: Mahakama
Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba apewe Ruhusa anitajie
Jaji: Shahidi Kwani Mahakama Imekukataza
Shahidi: Anaitwa Light Keno CJP
Nashon: Twende sehemu nyingine, Je kwa mwaka mnatoa makomandoo wangapi?
Shahidi: Siwezi kusema pia
Nashon: huwezi Kusema kwa sababu hutaki au Kiburi chako tu?
Nashon: Kwa sababu ni Siri
Nashon: Tutajie siri zingine ili tusikuulize
Shahidi: Siwezi kusema
Nashon: Nimesikia Unasema Kwamba Kikosi Chako Cha 92 KJ, Je Kuna kikosi +kingine
Shahidi: Ndiyo
Nashon: Kitaje
Shahidi: Siwezi Kutaja Mambo ya Jeshi
Nashon: Kwanini
Shahidi: Kwa sababu Kesi Inafuatiliwa ndani na Nje ya Nchi na Nina Kiapo
Nashoni: Hapa Umekula Kiapo Kingine
Shahidi: Ndiyo siwezi Kutaja sasa
Nashon: Mheshimiwa Jaji Naomba atutajie
Jaji: Naona Kashasema Hawezi Kusema
Nashon: Haya na wewe kozi yako ya mwisho ya ukomandoo ulifanya lini
Shahidi: Mwaka 2010
Nashon: Kozi zipi ulifanya
Shahidi: SIWEZI KUSEMA
Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Mahakama, Section 364 ya Sheria ya Ushahidi, Inahusu General Jurisdiction ya Mahakama
Mheshimiwa Jaji ni 264 ya CPA ambayo inasema Mahakama Kuu Itakuwa na Mamlaka, Kuwa Shahidi anapofika Shahidi aweze Kutoa Ushahidi, Na Shahidi amefika
Hataki Kutoa Majibu, Tunaomba Mahakama Yako itoe Mwongozo na pia Imuonye..
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Muda Kidogo tupitie Mahakama Ipo Kimyaaa
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: anasimama Ikupendeze Mheshimiwa Jaji, Tumemsikiliza Wakili Msomi Mwenzetu Wakili Nashon Nkungu, Kwa Heshima Zote Siye hatukubaliani na Maombi yake anayoyataja kwa kuwa hayana Mashiko Kisheria
Mheshimiwa Jaji Wakili anaomba Mahakama Imlazimishe Shahidi Kujibu swali lake la Level gani ya Mafunzo aliyo yafanya, Shahidi amemueleza hilo Suala la Siri Hawezi Kutamka hadharani Yeye ni Wa level gani Katika fani yake
Na Wakili kabla ya hapo amekuwa aliuliza Maswali Kadhaa kuhusu Ikama ya Jeshi la Tanzania, Shahidi amemueleza Kwamba hawezi Kueleza Kutokana na Kiapo Chake
Ameeleza Pia Kuhusu Kifungu Cha 264 cha Criminal Procedure Act, Ambapo Wakili anasema Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Kupitia Kifungu hiki, Naomba Nikisome.......... Anakisoma...
Tafsiri ipo wazi Hapa, Kwamba Subject to the Provision of this Act...... Maana yake description Ya Mahakama Katika hili Inategemea na Sheria zingine. Masuala ya kiushahidi, Kupokelewa Kwa Ushahidi Mahakamani Kuna Sura yake Maalum ambayo ni Sura Ya 6 ya Sheria ya Ushahidi ya 2019
Na Sheria hiyo Ina vifungu Mahususi Kinacho Elekeza ni Mazingira Yepi Shahidi anaanza Kulazimishwa Na Mahakama Kujibu Swali.. Mhe Jaji Kifungu Cha 158 cha Sheria hiyo kimeeeleza Ni wakati gani Mahakama, na Mazingira Yepi hasa Mahakama Inaweza Kumlazimisha Shahidi Ajibu Swali
Na si hicho tu, lakini hata Kifungu cha 156 Cha Sheria hiyo hiyo nacho Kinatoa Mazingira Yepi,, Mheshimiwa Jaji Mimi nitajielekeza Kifungu cha 155 Kifungu Kidogo Cha Kwanza....... Nanukuuu
Mheshimiwa Jaji Swali la level ya Mafunzo ya Shahidi Ni swali ambalo halina Mahusiano na Kinacho Jadiliwa Mbele ya Mahakama au Kilichopo Mbele ya Mahakama
Mheshimiwa Jaji Maswala ya namna hii, labda yawe yanapelekea Ku Injure character ya witness basi Shahidi anaweza Kulazimishwa Kuyajibu. Kinyume na hapo Shahidi hawezi Kulazimishwa
Mhe Jaji, Wakili hajaonyesha Mahakama Lengo la suala lake la Kufahamu Mafunzo ya Shahidi Ni Ku' Injure Character yake. Suala la Forces inatoa Makomandoo Wangapi, Force Ina vituo Vingapi Vya Makomandoo, Ni Maoni yetu Maswali ya Namna hiyo hayalengi Ku Distort Character Ya Shahidi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji siysi tunachokiona hapa Inawezekana msomi ameshindwa kumtingisha Shahidi, Anataka kumlazimisha shahidi azungumze masuala ya ikama ya jeshi..
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani ukisoma Kifungu Cha 155 Sura ya 6, kinasema.. Anasoma..
Wakili wa Serikali: Hata Maswali Yenyewe haya follow under 155, Untest Velacity Ya Shahidi Kwa Kutaka Kufahamu Kuna Vituo Vingapi Vya Makomando, Unatest Velacity ya shahidi Kutaka Kujua Mafunzo yake ni ya level gani, Unatest Velacity Kwa Kutaka Kujua Makomando Wanazlishwa Kwa Mwaka Mara ngapi
Wakili wa Serikali: Shahidi amekuja Mahakamani Kwa Kusema Yeye ni Askari Wa Jeshi la Wananchi, Kutoka Kikosi cha 92 KJ, Cheo Chake ni Luteni na Jukumu lake anasimama Askari Walio Chini yake 30..
Shahidi amekuja Kutoa Ushahidi Kwa Kile Kilichopekea Kesi Hii Kuwapo Mahakamani, Katika Ushahidi Wake Hakuna Mahala ameeleza Kwamba Jeshi La Wananchi Tanzania lilihusika Kwa namna Yoyote Ile
Wakili wa Serikali: Sasa Mheshimiwa Jaji Katika Mazingira hayo, Utaona Maswali la Wakili hayana Relevance, Hata Ukiangalia Kwa Namna Yoyote Ile haya Affect Character Ya Shahidi..
Baada ya maelezo hayo marefu kutoka kwa Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, mawakili wa serikali wametana wote na wanajadiliana kwa dakika kadhaa...
Anaendelea
Wakili wa Serikali: Wakili wa Serikali Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote Hoja ya Wenzetu haina Msingi, ajielekeze Katika Masuala ambayo anaweza Kutest Velacity ya Shahidi.. Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi Yupo sahihi..
Kwa namna ambayo Maswali yameulizwa Mahakama haina Mamlaka ya Kumlazimisha Shahidi ayajibu kamwe... Mheshimiwa Jaji naomba nimkaribishe Mwenzangu Pius Hilla aendelee
Wakili wa Serikali: Hata Kama angejielekeza Mahakama Katika Utaratibu Huu, haingefaa, Na Mahakama Haiwezi Kujiwekea Utaratibu Wake Pale ambapo Kuna Utaratibu Uliowekwa Kisheria..
Jaji: karibu, Bila Kurudia Kile ambacho amezungumza Mwenzako..
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nitajitahidi Kuwa Brief Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyepo Kizimbani aliulizwa swali Kuhusiana na level yake Ya Ukomando, haaieleza Mahakama Kwamba Kwa Kiapo Chake
Hawezi Kueleza level ya Mafunzo yake. Mheshimiwa Jaji tunakazia Maneno Kwa Kiapo chake Mheshimiwa Jaji ni kosa LA Jinai Ku' Communicate Information ambayo ni Confidential Mhe Jaji sect 4(1) ya CAP 47 ya National Security, Inasema Ni Kosa la Jinai Ku Communicate Information
Na hauruhusiwi Kufanya hivyo, Kwakuwa Shahidi amesha eleza Kwa Kiapo Chake Harusiwi Ku Communicate Kwa Kiapo Chake Kusema Level ya Mafunzo ambayo amefanya, Kuna Maswali ambayo Shahidi anaweza Kujibu na mengine hatakiwi Kujibu.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nimalizie Kwa Kusema Kwamba Taarifa Ya Kuhusiana na Level Ya Ukomando wa shahidi Kwa Mujibu wa Kiapo Chake hawezi Kusema.. Na Kwa kuwa Kuna Backup Ya Sheria, Remedy siyo Kulazimishwa, Bali wakili aelekezwe Wakili Kuuliza Maswali Sahihi
Mheshimiwa Jaji naomba Mahakama Itupilie Mbali Maombi ya wakili (Nashon Nkungu)
Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, it's Very Interesting, Leo nimeshuhudia OBJECTION Ya kupinga Identification ya Shahidi, Kama Nilikuwa namuuliza Shahidi ana Elimu gani........
Anakatishwa na Objection..
Wakili wa Serikali Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Samahani, Hakuna suala la Identification ya Shahidi, Kilichopo hapa Ni Kutaja Kumlazimisha Shahidi Kusema Mambo ambayo hawezi Kusema..
Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji, Niendelee Kwenye Submission yangu, Naomba Mahakama Kwa Wivu Mkubwa Mahakama ilinde Mamlaka yake, Hapa shahidi amekula Kiapo Kimoja, la sivyo Mwanzoni Wakati wa Kiapo angesema anakula Kiapo Lakini anakiapo Kingine kinamkataza Kusema Yeye ni nani
Sisi tunaomba Kiapo alichokula hapa Mahakamani Kiwe Juu Ya Viapo Vingine Vyote, Hakuna Sheria ambayo Wametoa Kwamba Inakataza, Bali Tunaona Kwamba Ni Vifungu Vinavyoruhusu Kujua Shahidi Ni nani Na Elimu yake ni Ipi..
Mheshimiwa Jaji Nikienda Kwa Section Moja Moja Kama ambavyo imetajwa hapa, Naona Vyote ni Permissive, Vyote ni Relevant kwa Sababu Lengo lake Ni Kutaka Ku Establish Je ana ujuzi Wa Kile anachokiongea, anatoka Kweli Ngerengere?
Hatuoni kwa namna Gani suala Hilo lina kuwa Relevant, Mheshimiwa Jaji Kiusalama Hakuna Mambo ambayo yanakiuka, Hatuoni Shida Kusema Mtu fulani na Kusema Yeye ni nani, Wamekuja Hapa Watu Wakasema Wao Nia Inspector, Wao ni Ma RCO
Nashon: Mheshimiwa Jaji Hizo Section ambazo wame zitaja Zina refers Kwenye Kifungu cha 151.. Kwamba Hapatakuwa na Excuse Juu ya Kutoa Ushahidi.. Tunahitaji accuracy, Tunahitaji Conformity, Kwa sababu Watakuja Hata Washtakiwa Watasema wao Wana Kiapo..
Nashon Nkungu: Kuna msemo mmoja unasema "Muosha huoshwa", Mahakama hii hii Wakili aliyesimama Abdallah Chavula ndiye aliyesimama kuhoji mashahidi Wakina Adamoo kwamba komandoo mmoja anapiga askari wangapi.. Hatuku' Object, tulimuacha aulize Maswali yake hapa..
Tunaomba Haki iwe pande zote Mbili, Mheshimiwa Jaji Kwenye kutumia Kifungu Sahihi au siyo Sahihi, Ni Kifungu ambacho tunaona ni sahihi...
Nashon: Kuhusiana na Powers Kuhusu Ku' Compel Shahidi, Kwa Kuweka hii Hoja Vizuri Mahakama Kwa Kutumia hivi Vifungu Vya 141, 156, 155, 158 Vyote ni Vifungu Wezeshi ambavyo vinaipa Mahakama Mamlaka Wajibu wa Kutoa Ushahidi
Nashon: Kama Hakuna Kifungu Kinachokataza, Ni Msimamo Wetu Kwamba Shahidi Yupo Compellable Kuweza Kujibu.. Mheshimiwa Jaji Kwenye Hoja Nyingine Kwenye 158 cha Sheria ya Ushahidi Kifungu Kipo Subject kwenye Subsection Two ya 158 ya Sheria ya Ushahidi
Narudia Kumuomba Shahidi ajibu swali langu Kama alivyoulizwa
Wakili Nashon Nkungu: Anakaa Chini Mahakama Ipo Kimya Kidogo
Jaji: Mme' site sheria kadhaa na vifungu kadhaa, Ili niweze kutoa maamuzi ambayo ni sahihi naomba kupitia kidogo hivi, kwa dakika 30 kisha tutarejea..
Jaji anatoka..
======
Jaji ametoa taarifa kuwa kesi itaendelea saa 8 na nusu...
Kuna watu humu wanafikiri Luteni ni mtu mkubwaaa, eti kila kitu SIRI, SIRI - Luteni ana siri gani za jeshi? Kwanza kama hamjui cheo cha Luteni ukifika miaka 45 unaondoka jeshini unless uwe ume-specialize na kupanda kuwa Captain.By the way, Luteni ni mtu mdogo sana jeshine kutaarifiwa kuwa wamefukuzwa kwa utovu wa nidhamu hasa kama washitakiwa waliondolewa jeshini kwa amri ya kuondoka kambini na wala sio barua ya kuwaachisha kazi. Denis alisikia tu habari za kuondolewa kwao, "hakutaarifiwa".
Discredited ushahidi or inadmissible ushahidi as a wholenaona pia wanamkingia shahidi kifua,hawataki aulizwe maswali .kwa nini wamemleta mahakamani?
it was expected so.🤣🤣Mliopo mahakamani huko,Mbowe kavaa miwani kweli?[emoji3][emoji3],Shahidi ameanza kuona Giza mapema mno ndugu zangu.
Uko sahihi Lt ni cheo cha kawaida tu.Kuna watu humu wanafikiri Luteni ni mtu mkubwaaa, eti kila kitu SIRI, SIRI - Luteni ana siri gani za jeshi? Kwanza kama hamjui cheo cha Luteni ukifika miaka 45 unaondoka jeshini unless uwe ume-specialize na kupanda kuwa Captain.
Cheo chenye mamlaka walau kidogo ni kuanzia MEJA kwenda juu - hawa wengine ni mambo ya kuvumilia vumbi na jua kali.