Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake. Shahidi Justine Eliya Kaaya, amtaja Ole Sabaya. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021

Hairuhusiwi mahakama kuomba print out kutoka makampuni ya simu inayoonyesha calls za shahidi na Mbowe?..... naona wakili kauliza tiketi na shahidi hana, mahakama haiwezi kuthibitisha kwa kuangalia movement ya simu ya mhusika hiyo siku..vs mazungumzo yake anayotoa mahakamani... Kama ni uongo mahakama haiwezi kumpiga mvua shahidi kwa kuleta uongo mahakamani.?....

hakuna nilipoona makubaliano ya malipo kati ya huyo shahidi na Mbowe...unawezaje kuombwa tu important information za watu na kutoa kirahisi hivyoo bila makubaliano? ( anyway labda ndio watanzania tulivyo..)
Kwenye hii kesi Hakuna Gaidi aliyekubaliana kiwango na malipo. Magaidi wa Aina hii wanapatikana Tanzania tu.
 
Nashindwa kuelewa mantiki ya kesi hii. Maana Agosti 2020 Mbowe anawaajiri hao komando kuandaa fujo, kuchoma vituo vya mafuta, kukata miti kwenye barabara Moro/Iringa na kumshambulia DC wa Hai?

Halafu mwaka 1 baadaye, wakati hakuna kituo 1 kilichochomwa, hakuna mti ulioanguka kwenye barabara hiyo, na Ole Sabaya alifurahia maisha hadi kupora wafanyabiashara wa Arusha, hao magaida wanakamatwa?

Na katikati hakuna hatua iliyochukuliwa kulinda usalama? Wala hakuna kitendo cha kigaidi kilichotekelezwa?
Abu Nuwasi au mwendesha mashitaka mkuu?

(Hasa kwa sababu mashitaka ya ugaidi yalitumiwa tayari Oktoba 2020, nisipokosei; ni yaleyale ya kuchoma vituo vya mafuta..... sivyo?)
Nafikiri na nadhani Niko sahihi kwamba hao washtakiwa wengine walikamatwa Mwaka Jana
 
Mtobesya: Eleza Mahakama Kwamba huyo Mlinzi alikuwa Diwani wa Kiboriloni

Shahidi: Nilisema

MTOBESYA: elezea Sasa hapo Katika Maandishi yako humo kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Mheshimiwa Jaji MI Leo nilikuwa nafafanua.

Mtobesya: hakuna mahala Kwenye Statement inaonyesha kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Statement Haionyeshi

Mtobesya: kwenye Statement yako kuna sehemu inasema Baada ya Kukutana Mara ya Pili, kwamba Ulimtajia Majina huyo Mbowe watu wanaotembea na Sabaya?

Shahidi: Majina hayajaandikwa hapa kwenye Statement

Mtobesya: Ulipokutana Mara ya Tatu ulisema Ulimtajia pia Majina, hayo Majina yapo kwenye Maelezo Yapo?

Shahidi: Hayapo
Haya sasa ushahidi kwa kufundishwa - shuuli kama ile ya PGO ishaanza !!
 
...
Mtobesya: Soma eneo linalosema Mimi nilikwenda Kwa Kutumia Nauli yangu. Umeona?

Shahidi: anapekua

Shahidi: Mimi nilikwenda Kwa Kutumia Nauli yangu, na Nilipofika alikuja Kunichukua

Mtobesya: Eleza Mahakama Kwamba huyo Mlinzi alikuwa Diwani wa Kiboriloni

Shahidi: Nilisema

MTOBESYA: elezea Sasa hapo Katika Maandishi yako humo kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Mheshimiwa Jaji MI Leo nilikuwa nafafanua.

Mtobesya: hakuna mahala Kwenye Statement inaonyesha kuna Mlinzi anaitwa Bwire

Shahidi: Statement Haionyeshi

Mtobesya: kwenye Statement yako kuna sehemu inasema Baada ya Kukutana Mara ya Pili, kwamba Ulimtajia Majina huyo Mbowe watu wanaotembea na Sabaya?

Shahidi: Majina hayajaandikwa hapa kwenye Statement

Mtobesya: Ulipokutana Mara ya Tatu ulisema Ulimtajia pia Majina, hayo Majina yapo kwenye Maelezo Yapo?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali na huyo uliyemuita Mbowe ulimpigia Sabaya na Baadae Mbunge uliyemjulisha, Je hayo yapo kwenye Statement Yako?

Shahidi: hayapo

Mtobesya: pia wakati wakili wa Serikali anakuongoza nilisikia Majina ya Hotel na Club ulizotaja kwa Majina yake, Hizo Taarifa zipo humo kwenye Statement Yako?

Shahidi: Hazipo

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza Huyo uliyesema ni Bwire alitamka Sabaya ni Mtoto Mdogo atamchezesha, Je yapo kwenye Statement?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza a umesema wewe unajishughulisha na Kilimo na Ukasema unavyofanya Kilimo, Je yapo hapo kwenye Statement..?

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Soma kwa Sauti Kuanzia Sehemu unayosema kuwa Ulikuwa Msaidizi wa Katibu wa CCM Shahidi anasoma Kuwa alikuwa Msaidizi wa Katibu wa CCM na mwanaharakati wa CCM.

Mtobesya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza ulisema kuwa wewe Ulishawahi kuwa Msaidizi wa CCM.

Shahidi: Hapana
... Kaka yangu wakili msomi mwandamizi Mtobesya asimamaye upande wa haki kamlabua kwelikweli huyo mrugaruga na ushahidi wao wa kubumba!

Je, haijapata kuandikwa katika chuo cha manabii, ulimi wa uongo ni wa kitambo tu? Ndicho kinachotokea sasa! Mungu wa Mbinguni asimamaye na wenye haki daima usitufiche uso wako YEHOVA; Ee Mungu bila wewe hatuondoki hapa BWANA!
 
Sisi tu watazamaji tu hakuna kinginej
Jaji naye asije akaachia ngazi
 
Kesi ya kubambikiwa ikitokea kuwa “high profile”, inakuwa aibu tupu. Yani hata kama Samia walimlisha matango pori na yeye akayabugia tu.

Huyo Kaaya ambaye anasema alikuwa mpiga picha, na kwamba ni mkulima, kumbe si kweli. Jamaa alikuwa kada wa ccm na msaidizi wa katibu mkuu wa ccm. Nimeshangaa sana eti aende kuishi nyumbani kwa Sabaya kwasababu ni mpiga picha! Kwani Sabaya alikuwa mwigizaji wa porn?

Kaazi kweli kweli.
 
Hairuhusiwi mahakama kuomba print out kutoka makampuni ya simu inayoonyesha calls za shahidi na Mbowe?..... naona wakili kauliza tiketi na shahidi hana, mahakama haiwezi kuthibitisha kwa kuangalia movement ya simu ya mhusika hiyo siku..vs mazungumzo yake anayotoa mahakamani... Kama ni uongo mahakama haiwezi kumpiga mvua shahidi kwa kuleta uongo mahakamani.?....

hakuna nilipoona makubaliano ya malipo kati ya huyo shahidi na Mbowe...unawezaje kuombwa tu important information za watu na kutoa kirahisi hivyoo bila makubaliano? ( anyway labda ndio watanzania tulivyo..)
Siamini hata hayo makampuni ya simu, yanaweza kulazimishwa kutoa fake print, utetezi walete forensic expert afanye verifications zote kama zipo, serious kesi kama hizi ni long and very expensive lakini kwa wenzetu hawa ni michezo tuu ya mahakama za mbuzi
 
Pia tuhakikishie kupitia hata ikibidi vipimo vya DNA ama finger prints kwamba ile Bunduki alitumiwa na Adamoo na ni yake ambayo alipanga kumlipua Mr. Sabaya.
Tunaambiwa 7Baya angeuwawa kwa kupuliziwa PODA kama UTITIRI!
 
Back
Top Bottom