Simply jaji kaonesha bosi wake ni Kingai, hivyo haikuwa haki kwake kuona bosi wake akitandikwa maswali na yeye subordinate yupo tu anaangalia bila kufanya chochote kwa sababu alibanwa na sheria, ndio maana akaamua kumuomba radhi bosi wake lakini naamini atamtendea wema zaidi bosi wake siku ya hukumu ikifika ili kumuonesha bado anamheshimu.
Naona bado tuna safari ndefu sana ya kutafuta haki ya kweli nchi hii, kama majaji nao wanawafanyia kazi polisi ili kuwaridhisha kwasababu wote ni ndugu moja sijui tutakimbilia wapi, muhimili wa mahakama hasa mahakama kuu unazidi kupoteza thamani yake kila siku tena kwa spidi ya kutisha sana.
Katiba Mpya inavyozidi kuchelewa ndio tunazidi kuoneshwa umuhimu wake kila siku, na ndio maana mpigania haki na wenzake wasio husika wako ndani kama njia ya kumfunga mdomo ili asiwaamshe waliolala.