Nzige Mdudu
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 1,048
- 830
Umefikiria Deep sana mkuu. Yaani inafikirisha sanaMpaka sasa kwenye hii kesi serikali hawana chochote cha kuthibitisha kama Mh.Mbowe na wenzio wamefanya haya makosa.
Ninachokiona hapo,hii kesi wameamua ichukue muda mrefu kwa maslahi yao binafsi kama vile washtakiwa wakae ndani muda mrefu au upande wa utetezi waendelee kupiga pesa ya posho.
Hii kesi yote msingo wake ni Lt.Denis Urio,mtu ambaye ameshindwa kuthibitisha hata kwa asilimia 10 tu kama washtakiwa wanakosa kwenye mashtaka yote waliyofunguliwa. Kama kiini cha kesi siku zote alizoutumia kutoa ushahidi wake,upande wa serikali wanapata wapi hizo nguvu zakuendelea kuleta mashahidi wapya kila siku?? Inawezekana kweli Msingi wa kesi Urio hana ushahidi wa kueleweka then watu waliokuwa wanafanya mapokeo kama Inst.Swila, Kingai na wengine wawe na ushahidi wakuwatia washtakiwa hatiani?