Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Swila aomba ahirisho kuwa hajisikii vizuri; kuendelea na ushahidi 10/02/2022

Mheshimiwa Nyendo ikikupendeza naitwa Farolito nipo na jopo la wana JF wapenda haki tupo tayari kuifuatilia kesi ya Mchongo mpaka mwisho.
Asante
 
Nipo nafasi ya kwanza leo. Wapi Mzee Mgaya johnthebaptist [emoji31]
Mkuu, nimechungulia mpaka chumba namba 36,sijamuona Mzee Mgaya!
Tetesi za chini ya kapeti zinadai, leo kama shahidi Swila akiwahi kumaliza kutoa ushahidi, anapanda yeye kizimbani, na anadai yeye ana ushahidi mzito kuliko hata wa Afande Sirro!
Tunaye mtakia mema Mwenyekiti Mbowe, tujiandae kisaikorojia!
 
Kesi zote huwa Ni pattern mkuu, maana hakim hakuwepo na mawakili hawakuwepo wakati wa matukio, kwa hyo wakiunga dot ndo wanapata majib, mkuu mbona Jambo rahisi tu hili??
Unajua maana ya kuunga unga dots?....kwa kesi kama hi huyu swila alipaswa kua na straight forward evidance ndo ailete mahakamani, evidance inayohitajika ili mtu awe convicted kwa aina ya kesi hi kwa lugha ya kisharia inaitwa watertighen evidance ambao hawana, wali kurupuka kumlaghai Raisi ili wapate vyeo, kwa ushahidi wa dots hi kesi haina hadhi kusikilizwa na kupoteza mali za Ummah
 
Hii kesi angekuwepo;

1) Tundu Lissu
2) Peter Kibatala
3) Nashon Nkungu
4) Fredrick Kihwelo.
5) Mtobesya.
6) John Malya.
7) Fatma Karume.

Jopo la mawakili watetezi lingekua poa sana, mashahidi wangeshikwa matumbo ya kuharisha.
YAANI huwa hata hamtumii akili hivi kweli mashahidi woote hao wanatoa ushahidi kama kesi ingekuwa ya kutengeneza ingeishia njiani tena mapema sana na hivi vitu inaonekana kabisa ni vya muda mrefu ukianza kuhusisha katiba mpya na ugaidi wa mbowe na ushahidiunaotolewani tofauti maana ya kwamba wakati anakamatwa mbowe na mkaanza kusema kakamatwa kwaa jili ya katiba mpya huo ushahidi tayari ulishakusanywa muda mrefu na wakati huo kina komandoo wapo ndani muda mrefu na mbowe aliwatelekeza hakuna mtu alikuwa anawafuatilia HIVI LEO UJE USEME KESI YA MCHONGO ? yaani mbowe hawezi kushindana na serikali kwa ushahidi uiokusanywa na serikali ikishindwa hii kesi watakuwa wameshindwa kizembe mbowe hachomoki wanachootakiwa kuchutama mambo yaishe wakikomaza shingo mtu anaumia hivihivi na wakitegemea rufaa ndiyo hakuna kitu kabisa
 
Wakili Msomi Peter (Kepha- Mwamba), Utembee daima chini ya uvuli wa Mkono wa Mungu. Neema na Baraka Zake Mungu Mwenyezi zikushukie na kukaa nawe na timu nzima ya Makamanda (Mawakili wa upande wa utetezi) wako daima. Amin
 
Jamaa Kibatala kama Simba anamlia timing vibaya sana jana kampeleka kirafiki leo naona anafanya finishing ya kufa mtu.
unajuwa sheria ukiwa unaijuwa sana huwezi kushindana na mtu ambaye hajui sana sheria na ndiyo maana kuna mengine wakati wa upelelexi wake hakuyafanya shahidi kazi yake ndogo sana kusema alichokipelelezasiyo kuanza kuainisha vipengele vya sheria anaema alichokipeleleza na alichogundua kwenye upelelzi wake kibatala analazimisha vit visivyowezekana ni sawa na mtoto mdogo umwambie atoe ushahidi wa tukio akaongea alichokishuhudia halafu uanze kumuuliza masawali ya PGO hataweza kuyasema lakini ukweli kausemautamshindaje hapo?mbowe hachomoki
 
Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa, Ila kuanzia Jana Jioni hali yangu haikuwa Nzuri lakini nitaendelea Kutoa Ushahidi
sasa leo si ndo utakufa kabisa, Maana Wakili Msomi Kibatala leo ana maswali 999 bado mawakili wengine !
Mwonezi anataka huruma ya jaji, utavuna ulichokipanda bwana Inspector, Kazi ni kwako.......
 
Wakili Msomi Peter (Kepha- Mwamba), Utembee daima chini ya uvuli wa Mkono wa Mungu. Neema na Baraka Zake Mungu Mwenyezi zikushukie na kukaa nawe na timu nzima ya Makamanda (Mawakili wa upande wa utetezi) wako daima. Amin
shabiki ni kitu kibaya sana asiye juwa sheria unaweza ukafikili kibatala kuna la maana analolifanya hapo huyo ni mjanja wa maneno tu lakini hakuna anachokifanya kumuokoa mbowe anachokifanya ni kupoteza muda kwa maswali yasiyoisha kumchanganya shahidi hivi muda wote watu wawe walikuwa wanapanga kuchonga kesi ya kumfunga mbowe? siyo kweli makosa kafanya kweli na mwenzenu uko tayari kutoka lakini mmekomaza shingo kuwa hana makosa mwenzenu anateseka maana anajuwa alichokifanya
 
Hivi Kuna ushahidi gani uliouona wewe zaidi ya hearsay? Ushahidi hauwi kitu kimoja ni lazima kuwe na corroboration ya ushahidi ili kesi iwe prima facie.Sijaona ushahidi unaothibisha jinai hapa.Maneno tu yasiyothibitishwa ndo ugaidi! Hakuna kitu hapo. Hata kikao cha pamoja watuhumiwa wote hakionekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…