Yaliyojiri Mikutano ya CCM: Maridhiano ya kitaifa, Mchakato wa Katiba Mpya, Uteuzi, Pongezi kwa Rais Samia na Mwinyi

Makamanda wanashangilia COVID kutemwa Badala ya kushangilia kwamba hatimaye tunaanza mchakato kupata KATIBA mpya.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Acha kuwaza kipumbavu. Kwani ukishangilia wewe haitoshi?
 
Hongera sana Mr. Wassira kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa cc wa chama cha mapinduzi....ILA DUUUU BADO UPO TU....LOO CCM INA WENYEWE
Huyu mzee ni wa kitambo sana asee, yaani nakumbuka nilimsikia kwenye siasa tangu 198 na kenda hadi leo na bado anabonga issue nzito na ninadhani ndiyo sababu ya kumrudisha cc.
 
Yes ni mwanasiasa mkongwe sana,nakumbuka alishawahi kujiunga na NCCR M,good memory imenijia jinsi upepo wa kisurisuri wa Mh.Mrema uliponipitia na kuwa jasiri, na kwa hili lilibadili sana uelekeo wangu wa kimaisha, but I don't blame any one,ulikua ni uchaguzi wangu and still proud na uamuzi ule, Mr. WASSIRA UPO TU...
 
CCM hawaaminiki hasa unafiki wa kikwete na wahafidhina wenzake. Watakubali leo kesho wanageuka
Jambo hili litazamwe kwa mtazamo chanya. Walioharibu mchakato ni wapinzani, walitoka kwenye Bunge Maalum la Katiba na kuwa na madai yasiyo na mashiko. CCM wakati wote ipo kusimamia masilahi ya taifa.
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumatano 22 Juni 2022 Makao Makuu ya CCM katika Ukumbi wa White House Jijini Dodoma kimetoka na maazimio yafuatayo kwa masilahi ya taifa.

1. Maridhiano ya kifaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.

3. Ndg. Steven Wassira ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
...............................................................................
TAARIFA KWA UMMA

YALIYOJIRI KATIKA VIKAO VYA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana leo tarehe 21/06/2022 Ikulu Chamwino, Dodoma kwa kikao cha siku moja cha kawaida na kuongozwa na Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UTEUZI WA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MAMEYA

Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wenyeviti wa halmashauri za wilaya na Mameya kama ifuatavyo:-

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mji
  • Ndg Erasto B. Mpete
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • Ndg Mohamed Festo Bayo
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
1. Ndg Stuart Nathaniel Nkinda
2. Ndg Apaikunda Ayo Naburi
3. Ndg Zuberi Abdallah Kidumo

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kimefanyika leo tarehe 22 Juni, 2022 katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya Chama Jijini Dodoma chini ya Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MARIDHIANO NA PONGEZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ukomavu, ustahimilivu, uhodari na dhamira yake njema ya kufanya maridhiano na vyama vya siasa nchini kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano, mshikamano, amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi wa watanzania wote.

Halmashauri kuu ya Taifa imevipongeza vyama vyote vya siasa kwa kukubali kuunga mkono hatua hiyo. Chama kimeishauri serikali kuharakisha utekelezaji wa masuala yote yatakayojenga kuaminiana, kuimarisha ushirikiano na umoja wa kitaifa kwa ustawi wa wananchi wote. Miongoni mwa mambo ambayo Halmashauri Kuu imeshauri kutazamwa ni pamoja na kesi zenye sura ya kisiasa kwa wafuasi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Chama kimeishauri serikali utekelezaji wa masuala yote ya kuimarisha demokrasia nchini na mazingira ya kisiasa yafanyike bila kuathiri uhuru na usalama wa nchi yetu.

PONGEZI KWA DKT HUSEIN MWINYI

Vilevile Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Husein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuonesha uvumilivu na ukomavu wa kiuongozi katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa hali inayochochea umoja, amani na utulivu kwa wananchi wa Zanzibar na hivyo kuharakisha maendeleo yao.

UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kauli moja imekubaliana kuwa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakubaliana na umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na hivyo kinaishauri serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi mapana ya Taifa na Maendeleo ya watanzania wote.

UCHAGUZI MKUU WA NDANI YA CHAMA

Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kuridhishwa taarifa ya maendeleo ya uchaguzi mkuu wa ndani ya Chama ambao umeshakamilika kwa asilimia 99.5 katika ngazi ya mashina na matawi kote nchini na sasa upo katika ngazi ya Kata/Wadi. Chama kimetakiwa kuzifanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika ngazi hizi ili kuimarisha ushiriki wa haki, usawa na demokrasia katika ngazi zote zinazofuata kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi ya Chama.

UCHAGUZI WA KUJAZA NAFASI ZA WAJUMBE WAWILI WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uchaguzi wa kujaza nafasi mbili za wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa zilizokuwa wazi kwa kuwachagua kwa kura Ndugu Stephen Masatu Wassira na Ndugu Theresia Adriano Mtewele.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi.
22 Juni, 2022.

Maridhiano ya KIFAIFA??????
 
Mlipoambiwa Rais Samia ana dhamira ya kweli ya kuliweka taifa pamoja mlishupaza Shingo.

Wenzenu walipoitika wito wa kwenda kwenye maridhiano mlitukana mitandaoni.

Mlipoona mwelekeo umepatikana mkabadili gia angani mkaanza kushinda Ikulu.

Leo Mama anathibitisha kwa vitendo kwamba anaamini katika haki na maridhiano.

Mama alihitaji zaidi wa tu wa kuzungumza nae na watu wa kumjenga.
Ninyi mkataka kumbomoa.

Nawapongeza CCM kwa kutoa tamko limalohitimisha siasa za visasi.

Taifa letu limakwenda kuwa imara zaidi
 
Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye nia njema na taifa letu; ameonesha mara nyingi kwa vitendo bila kusita. Tumuunge mkono.
 
Jambo hili litazamwe kwa mtazamo chanya. Walioharibu mchakato ni wapinzani, walitoka kwenye Bunge Maalum la Katiba na kuwa na madai yasiyo na mashiko. CCM wakati wote ipo husimamia masilahi ya taifa.
Rubbish
 
Safi sana
Usiwaamini sawa hao. Maana wamesema 'kuanza kwa mchakato..' Wakati kwenye bajeti ya serikali hakuna fungu lililotengwa... Kwa maoni yao wanataka mchakato wa katiba mpya uanze baada ya uchaguzi mkuu 2025
 
Makamanda wanashangilia COVID kutemwa Badala ya kushangilia kwamba hatimaye tunaanza mchakato kupata KATIBA mpya.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Wanashangiloa vyote mbona.
 
Ninyi ni watu wa ajabu sana. Watu ambao msichopenda kufanyiwa ndicho mnachopenda kuwafanyia wenzenu. Mfano hamtaki kutukanwa ila mnatukana wenzenu, Hamtaki udikteta, ninyi wenyewe hamna uvumilivu kabisa na mtu mwenye mawazo tofauti na yenu.

Ndio maana tunasema upinzani wa Tanzania sio wakuaminika kabisa maana waliopo humo hawana moral standards, ni wapiga kelele tu.

Acha maneno bila kujitoa kwa wapinzani Leo CCM ingekubali mchakato wa katiba.
 
Jambo hili litazamwe kwa mtazamo chanya. Walioharibu mchakato ni wapinzani, walitoka kwenye Bunge Maalum la Katiba na kuwa na madai yasiyo na mashiko. CCM wakati wote ipo husimamia masilahi ya taifa.

Nini kiliwashinda CCM kuumaliza.
 
Inapatikana mwaka gani na wahusika utekelezaji ni nani. Vinginevyo ni yaleyale one step forward 2 backward

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumatano 22 Juni 2022 Makao Makuu ya CCM katika Ukumbi wa White House Jijini Dodoma kimetoka na maazimio yafuatayo kwa masilahi ya taifa.

1. Maridhiano ya kitaifa.

Back
Top Bottom