Yaliyojiri Mikutano ya CCM: Maridhiano ya kitaifa, Mchakato wa Katiba Mpya, Uteuzi, Pongezi kwa Rais Samia na Mwinyi

Yaliyojiri Mikutano ya CCM: Maridhiano ya kitaifa, Mchakato wa Katiba Mpya, Uteuzi, Pongezi kwa Rais Samia na Mwinyi

Kwangu ili maridhiano yatimie lazima wale vibaka wote waliokuwa wakitumia madaraka yao vibaya watakapoburuzwa kortini ili iwe fundisho na wanajulikana haina haja ya double standard.

Familia ya Azori Gwanda , Ben Saanane na wengineo lazima wapate haki yao zaidi ya hapo ishukuriwe covid 19 kwa kunyoosha MATAGA.
 
Usiwaamini sawa hao. Maana wamesema 'kuanza kwa mchakato..' Wakati kwenye bajeti ya serikali hakuna fungu lililotengwa... Kwa maoni yao wanataka mchakato wa katiba mpya uanze baada ya uchaguzi mkuu 2025
Uko sawa Kwa upande mmoja ndugu.Tahadhari ni muhimu.

Upande mwingine tuangalie muda uliobaki kufika 2025, Bado miaka 3 na nusu.

Bado muda upo, pressing ikizidi pesa itapatikana, ikiwezekana wananchi TUTACHANGIA Hilo jambo letu, waeke tu maelekezo vzr.

Katiba mpya ni sasa. Amen
 
Huyu mzee ni wa kitambo sana asee, yaani nakumbuka nilimsikia kwenye siasa tangu 198 na kenda hadi leo na bado anabonga issue nzito na ninadhani ndiyo sababu ya kumrudisha cc.
Tujipange Kwa HOJA pia, huyo Mzee upstairs Bado yupo vzr.
 
PCCB na CAG vijana wengi waliofungiliwa kesi za ubadhirifu wa Mali za umma angalieni kesi hizo Zina sura ya siasa chafu za ndani ya CCM,hivi unamkamata Sabaya Halafu Sabaya ana mtaja Jiiwe na Mpango Halafu hao hamuwahoji je hii ni kesi ya kisiasa au ya kiuhujumu uchumi
 
PCCB na CAG vijana wengi waliofungiliwa kesi za ubadhirifu wa Mali za umma angalieni kesi hizo Zina sura ya siasa chafu za ndani ya CCM,hivi unamkamata Sabaya Halafu Sabaya ana mtaja Jiiwe na Mpango Halafu hao hamuwahoji je hii ni kesi ya kisiasa au ya kiuhujumu uchumi
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumatano 22 Juni 2022 Makao Makuu ya CCM katika Ukumbi wa White House Jijini Dodoma kimetoka na maazimio yafuatayo kwa masilahi ya taifa.

1. Maridhiano ya kitaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.

3. Ndg. Steven Wassira ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
...............................................................................
TAARIFA KWA UMMA

YALIYOJIRI KATIKA VIKAO VYA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana leo tarehe 21/06/2022 Ikulu Chamwino, Dodoma kwa kikao cha siku moja cha kawaida na kuongozwa na Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UTEUZI WA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MAMEYA

Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wenyeviti wa halmashauri za wilaya na Mameya kama ifuatavyo:-

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mji
  • Ndg Erasto B. Mpete
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • Ndg Mohamed Festo Bayo
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
1. Ndg Stuart Nathaniel Nkinda
2. Ndg Apaikunda Ayo Naburi
3. Ndg Zuberi Abdallah Kidumo

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kimefanyika leo tarehe 22 Juni, 2022 katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya Chama Jijini Dodoma chini ya Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MARIDHIANO NA PONGEZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ukomavu, ustahimilivu, uhodari na dhamira yake njema ya kufanya maridhiano na vyama vya siasa nchini kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano, mshikamano, amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi wa watanzania wote.

Halmashauri kuu ya Taifa imevipongeza vyama vyote vya siasa kwa kukubali kuunga mkono hatua hiyo. Chama kimeishauri serikali kuharakisha utekelezaji wa masuala yote yatakayojenga kuaminiana, kuimarisha ushirikiano na umoja wa kitaifa kwa ustawi wa wananchi wote. Miongoni mwa mambo ambayo Halmashauri Kuu imeshauri kutazamwa ni pamoja na kesi zenye sura ya kisiasa kwa wafuasi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Chama kimeishauri serikali utekelezaji wa masuala yote ya kuimarisha demokrasia nchini na mazingira ya kisiasa yafanyike bila kuathiri uhuru na usalama wa nchi yetu.

PONGEZI KWA DKT HUSEIN MWINYI

Vilevile Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Husein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuonesha uvumilivu na ukomavu wa kiuongozi katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa hali inayochochea umoja, amani na utulivu kwa wananchi wa Zanzibar na hivyo kuharakisha maendeleo yao.

UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kauli moja imekubaliana kuwa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakubaliana na umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na hivyo kinaishauri serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi mapana ya Taifa na Maendeleo ya watanzania wote.

UCHAGUZI MKUU WA NDANI YA CHAMA

Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kuridhishwa taarifa ya maendeleo ya uchaguzi mkuu wa ndani ya Chama ambao umeshakamilika kwa asilimia 99.5 katika ngazi ya mashina na matawi kote nchini na sasa upo katika ngazi ya Kata/Wadi. Chama kimetakiwa kuzifanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika ngazi hizi ili kuimarisha ushiriki wa haki, usawa na demokrasia katika ngazi zote zinazofuata kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi ya Chama.

UCHAGUZI WA KUJAZA NAFASI ZA WAJUMBE WAWILI WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uchaguzi wa kujaza nafasi mbili za wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa zilizokuwa wazi kwa kuwachagua kwa kura Ndugu Stephen Masatu Wassira na Ndugu Theresia Adriano Mtewele.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi.
22 Juni, 2022.



Wakati wa Nyerere, alikuwepo, wakati wa Mwinyi, alikuwepo, wakati wa Kikwete, alikuwepo, Wakati wa Magufuli hakuwepo, wakati wa mama yupo, du huyu mzee wa Bunda.... sijui ana jipya lipya.
 
Hongera sana Mr. Wassira kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa cc wa chama cha mapinduzi....ILA DUUUU BADO UPO TU....LOO CCM INA WENYEWE
Chawa mzee nae analamba asali bada ya kutoshwa na jiwe, wanrudi mmoja mmoja timu Born town.
 
Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ukomavu, ustahimilivu, uhodari na dhamira yake njema ya kufanya maridhiano na vyama vya siasa nchini kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano, mshikamano, amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi wa watanzania wote.
Samia hoyeeee
 
Makamanda wanashangilia COVID kutemwa Badala ya kushangilia kwamba hatimaye tunaanza mchakato kupata KATIBA mpya.😀😀😀😀😀😀😀😀
Naona umenuna. Mlipinga sisi tukakomaa. Hatimaye mambo yatatiki. Msiotaka katiba Mpya hamieni burundi in Mwogulu's voice
 
Naona Tumia akili anazidi kula katika mkeka wake. Mikeka ya Tumia akili haichanikagi.
Unakumbuka mikeka ya Lissu akiwa Ubeligiji??
1. Mbowe kuachiwa bila masharti
2. Kufuta kesi zoote za kisiasa ba kuwaachia huru wafungwa
3. Lissu kulipwa stahiki zake pamoja na gharama za matibabu
4. Covid 19
5. Kauli ya serikali juu ya wakimbizi wa kisiasa
6. Ombi lake binafsi kupotea passport.
7. Kurejesha mchakato wa Katiba Mpya
 
Sasa najiuliza huyu Zitto na kile kikosi kazi chao waliosema eti mchakato uanze 2026 wanajisikiaje?
Kikao cha jana na Mabalozi yaweza kuwa kulikuwa na shinikizo la aina fulani
Wewe unadhani Lissu kule ulaya anashangaa maghorofa tu? Mungu alimponya ili aje kusaidia Tanzania.

Naishia hapo
 
Back
Top Bottom