Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Leo ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ambao pia utaenda kupitisha mabadiliko ya katiba ya CCM. Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri, anatabiri nini kwenye utawala wa mama Samia baada ya kutabiri ubatizo wa maji kwa Jakaya na ubatizo wa moto kwa Magufuli.
Makamba: Nikasema natabiri ubatizo wa maji na faraja, akaniuliza Gwajima, kwanini faraja? Nikamwambia bwana Yesu alisema bado kitambo kidogo mnaniona na bado kitambo kidogo hamnioni, wanafunzi walipofadhaika akawaambia msifadhaike nakwenda kwa baba yangu kuwaandalia makao lakini baba yango atawaletea mfariji mwingine.
Sasa kama Magufuli ameondoka, anaekuja si Rais tu, ni mfariji, sasa unatufariji maana maji tunapata, umeme tunapata, watoto wanasoma, mikopo ipo. Nikamuuliza Gwajima, basi akasema ungekuwa mchungaji wa kanisa langu, nikamwambia sitaki mimi muislam.
Kwahiyo mama usikasirike tunaposema tumekutabiria ubatizo wa maji na faraja na ilimradi watanzania wote wanafarijika, Rais ni wewe.
Pia Makamba ameongelea mgombea Urais 2025 ambae amesema ni mama Samia na amewaambia upinzani mgombea ni Samia na kama kuna anaejiandaa akae tayari.
Makamba anaendelea kwa kueleza alipotoka na Kinana na anamuelezea kama mtu aliyefanya nae kazi Korogwe ikiwa ni kazi yake ya kwanza akimtaja kama mtu mzuri na anaeweza kujishusha.
Mwisho Makamba anaisifu halmashauri kuu kwa kutambua uhodari wa Kinana na kutimiza ombi la Jakaya kwa kuomba wamtafutie kitu Kinana wampe, wenyewe wakaamua kumpa umakamu badala ya jengo na daraja.
Makamba: Sasa mheshimiwa Kinana tuna ligi 2025, tunataka kushika madaraka nchii hii hakuna kumuachia mtu mwingine, sisi tu.
Wewe sasa kocha msaidizi, sio wa Yanga wala sio wa Simba, ni kocha msaidizi wa CCM, msaidie mwenyekiti tushinde na wala na wewe usiogope.
==========
Mzee Makamba amwambia Kinana awasamehe waliomtupia madongo CCM
“Mimi na Kinana tulipokuwa tunafanya kazi, tulinyeshewa sana na mvua huu ndani ya CCM najua mwenyewe.
“Mimi na Kinana tulifikishwa hadi kwenye Kamati ya Maadili, wapo waliosimama wakatutupia madongo.
“Kinana wewe ndiyo bosi wao, yameisha, watu dhahifu hawawezi kusamehe, usiwe na kinyongo, yameisha,” - Yusuph Makamba
================
Kinachoendelea kwasasa ni zoezi la upigaji kura kwa makamu mwenyekiti aliyependekezwa, AbdulRahman Kinana.
12:46 pm; Spika wa Bunge anasoma taarifa ya uchaguzi
Idadi ya wajumbe waliopiga kura 1875
Kura halali 1875
Kura za hapana 0
Kinana anathibitishwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kwa kura zote 1875 sawa na asilimia 100 ya kura zilizopigwa.
KINANA: LAZIMA TUSIMAMIE DEMOKRASIA
Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana amesema kila mtu awe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa na haki ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye haki miliki ya mawazo.
“Lazima tuimarishe demokrasia, Wanachama wakimchagua mtu, sisi ni nani wa kupinga, inaweza kutokea kwa sababu kadhaa kama za maadili.
“Wanachama wawe huru kutoa mawazo, lazima tuwe tayari kumsikiliza kila mwanachana, ndivyo tutaweza kumsikiliza kila mwananchi, tukiweza kusimamia haki ndani ya CCM basi tutaimarisha haki nje ya CCM,” Kinana akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), leo Aprili 1, 2022.