Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
Leo ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ambao pia utaenda kupitisha mabadiliko ya katiba ya CCM. Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri, anatabiri nini kwenye utawala wa mama Samia baada ya kutabiri ubatizo wa maji kwa Jakaya na ubatizo wa moto kwa Magufuli.

Makamba: Nikasema natabiri ubatizo wa maji na faraja, akaniuliza Gwajima, kwanini faraja? Nikamwambia bwana Yesu alisema bado kitambo kidogo mnaniona na bado kitambo kidogo hamnioni, wanafunzi walipofadhaika akawaambia msifadhaike nakwenda kwa baba yangu kuwaandalia makao lakini baba yango atawaletea mfariji mwingine.

Sasa kama Magufuli ameondoka, anaekuja si Rais tu, ni mfariji, sasa unatufariji maana maji tunapata, umeme tunapata, watoto wanasoma, mikopo ipo. Nikamuuliza Gwajima, basi akasema ungekuwa mchungaji wa kanisa langu, nikamwambia sitaki mimi muislam.

Kwahiyo mama usikasirike tunaposema tumekutabiria ubatizo wa maji na faraja na ilimradi watanzania wote wanafarijika, Rais ni wewe.

Pia Makamba ameongelea mgombea Urais 2025 ambae amesema ni mama Samia na amewaambia upinzani mgombea ni Samia na kama kuna anaejiandaa akae tayari.

Makamba anaendelea kwa kueleza alipotoka na Kinana na anamuelezea kama mtu aliyefanya nae kazi Korogwe ikiwa ni kazi yake ya kwanza akimtaja kama mtu mzuri na anaeweza kujishusha.

Mwisho Makamba anaisifu halmashauri kuu kwa kutambua uhodari wa Kinana na kutimiza ombi la Jakaya kwa kuomba wamtafutie kitu Kinana wampe, wenyewe wakaamua kumpa umakamu badala ya jengo na daraja.

Makamba: Sasa mheshimiwa Kinana tuna ligi 2025, tunataka kushika madaraka nchii hii hakuna kumuachia mtu mwingine, sisi tu.

Wewe sasa kocha msaidizi, sio wa Yanga wala sio wa Simba, ni kocha msaidizi wa CCM, msaidie mwenyekiti tushinde na wala na wewe usiogope.

==========

Mzee Makamba amwambia Kinana awasamehe waliomtupia madongo CCM

“Mimi na Kinana tulipokuwa tunafanya kazi, tulinyeshewa sana na mvua huu ndani ya CCM najua mwenyewe.

“Mimi na Kinana tulifikishwa hadi kwenye Kamati ya Maadili, wapo waliosimama wakatutupia madongo.

“Kinana wewe ndiyo bosi wao, yameisha, watu dhahifu hawawezi kusamehe, usiwe na kinyongo, yameisha,” - Yusuph Makamba

================
Kinachoendelea kwasasa ni zoezi la upigaji kura kwa makamu mwenyekiti aliyependekezwa, AbdulRahman Kinana.

12:46 pm; Spika wa Bunge anasoma taarifa ya uchaguzi

Idadi ya wajumbe waliopiga kura 1875

Kura halali 1875

Kura za hapana 0

Kinana anathibitishwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kwa kura zote 1875 sawa na asilimia 100 ya kura zilizopigwa.


KINANA: LAZIMA TUSIMAMIE DEMOKRASIA

Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana amesema kila mtu awe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa na haki ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye haki miliki ya mawazo.

“Lazima tuimarishe demokrasia, Wanachama wakimchagua mtu, sisi ni nani wa kupinga, inaweza kutokea kwa sababu kadhaa kama za maadili.

“Wanachama wawe huru kutoa mawazo, lazima tuwe tayari kumsikiliza kila mwanachana, ndivyo tutaweza kumsikiliza kila mwananchi, tukiweza kusimamia haki ndani ya CCM basi tutaimarisha haki nje ya CCM,” Kinana akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), leo Aprili 1, 2022.
 
Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri, anatabiri nini kwenye utawala wa mama Samia baada ya kutabiri ubatizo wa maji kwa Jakaya na ubatizo wa moto kwa Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Lyatonga Mrema na mkewa wamehudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika Dodoma Leo Aprili 1, 2022.
 
Mzee Makamba kamtupia Kijembe Dr Bashiru

'…asiekumbuka ilipomnyeshea…hawezi kukumbuka alipokaukia…'

Anasema alipotuhumiwa na kuhojiwa na Chama …aliponea kwa Jakaya

Anamshauri Kinana asiwe na Kinyongo na waliosimama kidete kutaka kumharibia…Camera zikageuzwa kwa Dr Bashiru aliekuwa karibu kabisa na Kinana
 
Aisee
mNLPzh2J9M2Jussf.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wallah hii nchi ngumu kumeza, yaan yajayo yanaliza [emoji24][emoji24][emoji24]
 
(in Y/Makamba voice).Tulikua tunawachora tu haya leteni jeuri zenu tena.

KINANAMAKAMBA.jpg
 
CCM ni kweli itatawala sana ilo halina ubishi haitoki leo wala kesho.

Upinzani wenyewe ni mashabiki wa mambo ya CCM unategemea nini?

Chadema kumejaa uchaga walimchukia sana Magufuli mpaka wamekuwa kama wehu wamekosa direction na sasa hivi wameanzisha mashambulizi kwa wasukuma kila siku wasukuma hivi wasukuma wananyooshwa ila navyowajua wasukuma na ule wingi wao watawafurahisha. Chadema pia imejaa ulutheri maaskofu wa Lutheran ndio wnaharakati wao siku hizi.

ACT ndio sijui hata wanasimamia nini kwa sasa ni kama viongozi wao kina Zitto wamekuwa machawa wa Samia wanamlinda kwa nguvu zote asipate mashambulizi.

Pamoja na mapungufu yote kiukweli CCM bado ni chama imara na afadhali mara 1000000000 kuliko awa wanuka kwapa wa uko upinzani.
 
CCM ni kweli itatawala sana ilo halina ubishi haitoki leo wala kesho.

Upinzani wenyewe ni mashabiki wa mambo ya CCM unategemea nini?

Chadema kumejaa uchaga walimchukia sana Magufuli mpaka wamekuwa kama wehu wamekosa direction na sasa hivi wameanzisha mashambulizi kwa wasukuma kila siku wasukuma hivi wasukuma wananyooshwa ila navyowajua wasukuma na ule wingi wao watawafurahisha. Chadema pia imejaa ulutheri maaskofu wa Lutheran ndio wnaharakati wao siku hizi.

ACT ndio sijui hata wanasimamia nini kwa sasa ni kama viongozi wao kina Zitto wamekuwa machawa wa Samia wanamlinda kwa nguvu zote asipate mashambulizi.

Pamoja na mapungufu yote kiukweli CCM bado ni chama imara na afadhali mara 1000000000 kuliko awa wanuka kwapa wa uko upinzani.
Chadema ni hovyo kabisa, wanapoteza muda kushambulia wasukuma na hayati, huku ccm akichekelea, watakaposhtuka kurudi kwenye siasa tayari CCM na la kuwashambulia, kwamba ni chama kinachohamasisha ukabila na kutoheshimu marehemu, binadamu akishafariki mnamsetiri siyo kumbagaza.
 
CCM ni kweli itatawala sana ilo halina ubishi haitoki leo wala kesho...

Kwanii CCM ikitawala milele Kuna shida gani?. Nini kinchokuumiza?. Unatukana watu wanuka kwapa kisa wapo upinzani?. Acha dharau zako,

Magufuli akichukia chadema mwako ni sawa ? Ila chadema wakimchukia Magufuli sio sawa?

.Kuna watu walikuwa na dharau zaidi yako na walijiona miungu ila walifukiwa Chini huku waliowadharau wakiendelea kupumua.
 
Ukimsikiliza Makamba utatambua Taifa Lina watu wa aina gani; wanasiasa wa aina gani na viongozi wa aina gani. Yeye wakati wa Magufuli alipopata taabu Sana hakusemea Wana CCM alisemea familia yake. Leo ajasemea wananchi anasemea namna Bora yakuweka mfumo wakulinda familia yake.

Ni kweli tunahitaji watu wa aina hii wakibadilika na kukarimu Kila kiongozi hata kama atakosea? Makamba anapodai mafarijiano kwanini asituambie MFARAKANO na kutoelewana kuliletwa na wakina Nani na Sasa wapo wapi?

Siasa hizi haziwezi kuliletea maendeleo Tqifa zitapeleka maendeleo Kwa familia chache. Watu Wanawaza zaidi familia zao kuliko majirani na ndiyo maana kwao hata watu waumizwe vipi as long siyo damu zao hakuna shida.
 
Ukimsikiliza Makamba utatambua Taifa Lina watu wa aina gani; wanasiasa wa aina gani na viongozi wa aina gani. Yeye wakati wa Magufuli alipopata taabu Sana hakusemea Wana CCM alisemea familia yake. Leo ajasemea wananchi anasemea namna Bora yakuweka mfumo wakulinda familia yake...
Hapo wameweka mfumo wao wa kulindana vizuri waibe mali za umma vizuri
 
Ukimsikiliza Makamba utatambua Taifa Lina watu wa aina gani; wanasiasa wa aina gani na viongozi wa aina gani. Yeye wakati wa Magufuli alipopata taabu Sana hakusemea Wana CCM alisemea familia yake. Leo ajasemea wananchi anasemea namna Bora yakuweka mfumo wakulinda familia yake...
Hawa wazee ni wapumbafu sn wanafilisi nchi
 
Back
Top Bottom