Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Kwanii CCM ikitawala milele Kuna shida gani?. Nini kinchokuumiza?. Unatukana watu wanuka kwapa kisa wapo upinzani?. Acha dharau zako,

Magufuli akichukia chadema mwako ni sawa ? Ila chadema wakimchukia Magufuli sio sawa?

.Kuna watu walikuwa na dharau zaidi yako na walijiona miungu ila walifukiwa Chini huku waliowadharau wakiendelea kupumua.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Naona sasa hata uchaguzi wa 2025 utakuwa chadema vs magu

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Tutegemee tembo kuuwawa sn na twiga kupanda ndege kwa wingi
Mtasema ni chuki lakini sio ni ukweli, Kikwete anarudisha mtandao wake kwa kutumia udhaifu wa Bibi mwenye Shamba!! Kikwete ndiye aliyeomba Kinana apewe kitu, hakupewa daraja a kapewa kuwa makamu Mwenyekiti!!

Sasa tunarudi kule kule kwa nchi kuwa tegemezi na kila leo kiguu na njia kwenda kukopa bila kujali kuwa nchi karibu ifilisike(debt stressed)! Nguvu kazi inaharibika kwa madawa ya kulevya kwasababu ya huruma ya kuwatoa jela kimaslahi wauza hayo madawa!!

Wahuni wamekamata nchi!
 
Mtasema ni chuki lakini sio ni ukweli, Kikwete anarudisha mtandao wake kwa kutumia udhaifu wa Bibi mwenye Shamba!! Kikwete ndiye aliyeomba Kinana apewe kitu, hakupewa daraja a kapewa kuwa makamu Mwenyekiti!...
Chadema should bank on this!
 
Chadema ni hovyo kabisa, wanapoteza muda kushambulia wasukuma na hayati, huku ccm akichekelea, watakaposhtuka kurudi kwenye siasa tayari CCM na la kuwashambulia, kwamba ni chama kinachohamasisha ukabila na kutoheshimu marehemu, binadamu akishafariki mnamsetiri siyo kumbagaza.
Chadema wanahusikaje na kukomeshwa kwa wasukuma!

Unajua kabisa neno sukuma gang limetokea humo humo CCM. Waliowanyanyasa kina Kinana na Makamba walikuwa ni Chadema??
Wao ndio waliwapeleka kamati ya maadili?

Nyie watu mnatafuta wa kufa naye!!!
 
Mwisho Makamba anaisifu halmashauri kuu kwa kutambua uhodari wa Kinana na kutimiza ombi la Jakaya kwa kuomba wamtafutie kitu Kinana wampe, wenyewe wakaamua kumpa umakamu badala ya jengo na daraja.

Ndo Mana Wanasema remote
 
Mtasema ni chuki lakini sio ni ukweli, Kikwete anarudisha mtandao wake kwa kutumia udhaifu wa Bibi mwenye Shamba!! Kikwete ndiye aliyeomba Kinana apewe kitu, hakupewa daraja a kapewa kuwa makamu Mwenyekiti...
Hatari sn na aibu
 
Mtasema ni chuki lakini sio ni ukweli, Kikwete anarudisha mtandao wake kwa kutumia udhaifu wa Bibi mwenye Shamba!! Kikwete ndiye aliyeomba Kinana apewe kitu, hakupewa daraja a kapewa kuwa makamu Mwenyekiti!!

Sasa tunarudi kule kule kwa nchi kuwa tegemezi na kila leo kiguu na njia kwenda kukopa bila kujali kuwa nchi karibu ifilisike(debt stressed)! Nguvu kazi inaharibika kwa madawa ya kulevya kwasababu ya huruma ya kuwatoa jela kimaslahi wauza hayo madawa!!

Wahuni wamekamata nchi!
Nchi italiwa haswa
 
Leo ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ambao pia utaenda kupitisha mabadiliko ya katiba ya CCM. Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri...
Yaani hata Ally Hapi kapiga kura ya ndio??? Siamini mimi.
 
CCM ina kila sababu na sifa za kutawala kwa muda mrefu hii nchi, mapungufu yao tutayavumilia...
Ukiongelea udini bakiza maneno ya akiba. Nafikiri hili CCM linaweza kuwepo pia hata kama halisemwi. Angalia kipindi cha jiwe ukimulika vizuri utaona udini (M/kiti, makamu M/kiti, makatibu, mawasiliano Ikulu) na baada ya jiwe angalia ukimulika vizuri kwa mama unaweza kukutana nalo kwa M/kiti, Makamu M/kiti, M/kiti mstaafu, M/kiti Zanzibar, katibu mwenezi.

Tofauti ni kwamba kipindi cha jiwe kazi ilipigwa ki-bara sasa kazi inapigwa ki-zenji.
 
CCM ina kila sababu na sifa za kutawala kwa muda mrefu hii nchi, mapungufu yao tutayavumilia.

Ila awa wabaguzi wa wazi wazi tena kwenye ukabila na udini hawatufai hata kidogo.

Uchaga na ulutheri wa Chadema ni bendera nyekundu kwa wenye akili timamu.

Wewe unawaza chadema pekee. Kuna chauma pia.
 
Leo ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ambao pia utaenda kupitisha mabadiliko ya katiba ya CCM. Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri, anatabiri nini kwenye utawala wa mama Samia baada ya kutabiri ubatizo wa maji kwa Jakaya na ubatizo wa moto kwa Magufuli.

Makamba: Nikasema natabiri ubatizo wa maji na faraja, akaniuliza Gwajima, kwanini faraja? Nikamwambia bwana Yesu alisema bado kitambo kidogo mnaniona na bado kitambo kidogo hamnioni, wanafunzi walipofadhaika akawaambia msifadhaike nakwenda kwa baba yangu kuwaandalia makao lakini baba yango atawaletea mfariji mwingine.

Sasa kama Magufuli ameondoka, anaekuja si Rais tu, ni mfariji, sasa unatufariji maana maji tunapata, umeme tunapata, watoto wanasoma, mikopo ipo. Nikamuuliza Gwajima, basi akasema ungekuwa mchungaji wa kanisa langu, nikamwambia sitaki mimi muislam.

Kwahiyo mama usikasirike tunaposema tumekutabiria ubatizo wa maji na faraja na ilimradi watanzania wote wanafarijika, Rais ni wewe.

Pia Makamba ameongelea mgombea Urais 2025 ambae amesema ni mama Samia na amewaambia upinzani mgombea ni Samia na kama kuna anaejiandaa akae tayari.

Makamba anaendelea kwa kueleza alipotoka na Kinana na anamuelezea kama mtu aliyefanya nae kazi Korogwe ikiwa ni kazi yake ya kwanza akimtaja kama mtu mzuri na anaeweza kujishusha.

Mwisho Makamba anaisifu halmashauri kuu kwa kutambua uhodari wa Kinana na kutimiza ombi la Jakaya kwa kuomba wamtafutie kitu Kinana wampe, wenyewe wakaamua kumpa umakamu badala ya jengo na daraja.

Makamba: Sasa mheshimiwa Kinana tuna ligi 2025, tunataka kushika madaraka nchii hii hakuna kumuachia mtu mwingine, sisi tu.

Wewe sasa kocha msaidizi, sio wa Yanga wala sio wa Simba, ni kocha msaidizi wa CCM, msaidie mwenyekiti tushinde na wala na wewe usiogope.

==========

Mzee Makamba amwambia Kinana awasamehe waliomtupia madongo CCM

“Mimi na Kinana tulipokuwa tunafanya kazi, tulinyeshewa sana na mvua huu ndani ya CCM najua mwenyewe.

“Mimi na Kinana tulifikishwa hadi kwenye Kamati ya Maadili, wapo waliosimama wakatutupia madongo.

“Kinana wewe ndiyo bosi wao, yameisha, watu dhahifu hawawezi kusamehe, usiwe na kinyongo, yameisha,” - Yusuph Makamba

================
Kinachoendelea kwasasa ni zoezi la upigaji kura kwa makamu mwenyekiti aliyependekezwa, AbdulRahman Kinana.

12:46 pm; Spika wa Bunge anasoma taarifa ya uchaguzi

Idadi ya wajumbe waliopiga kura 1875

Kura halali 1875

Kura za hapana 0

Kinana anathibitishwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kwa kura zote 1875 sawa na asilimia 100 ya kura zilizopigwa.


KINANA: LAZIMA TUSIMAMIE DEMOKRASIA

Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana amesema kila mtu awe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa na haki ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye haki miliki ya mawazo.

“Lazima tuimarishe demokrasia, Wanachama wakimchagua mtu, sisi ni nani wa kupinga, inaweza kutokea kwa sababu kadhaa kama za maadili.

“Wanachama wawe huru kutoa mawazo, lazima tuwe tayari kumsikiliza kila mwanachana, ndivyo tutaweza kumsikiliza kila mwananchi, tukiweza kusimamia haki ndani ya CCM basi tutaimarisha haki nje ya CCM,” Kinana akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), leo Aprili 1, 2022.
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa,wacha waendelee kulamba asali!
 
Back
Top Bottom