Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Yaliyojiri Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Najiuliza ale mtu anapostaafu kwenye taasisi na kuagwa na Kisha kurejeshwa yuleyule mstaafu kwenye taasisi Ile tena kwenye nafasi ya juu Ina maana gani kwa taasisi na wafanyakazi wa taasisi Ile?
CCM wameishiwa watu wenye sifa kujaza nafasi hiyo! Angekuwepo Magufuli angeteua mtu kutoka Chadema kuwa Makamu Mwenyekiti!
 
Maana yake CCM wanafuta vumbi silaha zao wakijiandaa kwa mpambano wa 2025, Majenerali wa Siasa wanarudi makambini kupanga strategy za vita tayari kumtwanga adui vilivyo.

Kinana ni msomi wa Harvard, moja ya vyuo Bora kabisa duniani, anakwenda kukipika chama hiki na kukisuka tayari kwa kuzikamata Siasa za nchi hii kwa miaka kumi ijayo. Stratejia za msomi wa havard haziwezi lingana na Mnyika au Mbowe ambao wamesoma open university tena huku wakifeli masomo na kurudia mara kwa mara

Ni tahadhali kwa wanaoimba katiba mpya wanasahau kujipanga kwa uchaguzi.
Kinachosoma ni havard ama chuo hebu acheni kukariri bana. Harvad ni chuo tu kama udsm
 
Ccm inaenda kudharaulika twna and binafsi nitabakia na kadi yao ila nitajua nani nampigia kura but sio yule kibaraka wa wazungu
 
Hawa wazee walishapitwa na wakati and hawana cha kupoteza wanawaza kifo tu. Pia akili zimeshachoka wanahitaji kupumnzzishwa. Yaan unalets mzee wa miaka 70+ kuja kuwa kiongoza chama wakati kuna vijana bado wana uchungu na hii nchi wanaachwa
 
Najiuliza ale mtu anapostaafu kwenye taasisi na kuagwa na Kisha kurejeshwa yuleyule mstaafu kwenye taasisi Ile tena kwenye nafasi ya juu Ina maana gani kwa taasisi na wafanyakazi wa taasisi Ile?
Kwa mfumo wa Magufuli wa alivyoendeasha siasa ndani ya chama na Serikali ni kwamba CCM ilikuwa inategemea Police na NEC kubaki madarakani.

Hakukuwa na demokrasia ya kuhesabu kura wala hamna anayejua CCM inakubalika kiasi gani kwa wananchi. Hivyo Magufuli alikuwa anajidanya tu kuwa eti mwaka 2020 aliishinda uchaguzi kwa 82%.

CCM wamefanya vizuri kuwaleta watu ambao waliwekeza kwenye kujenga chama kwa ushawishi kuanzia kwenye mashina. Nadhani unaikumbuka kazi ya Nape na Kinana mara walipochukua hatamu mwaka 2012. Walikuwa wanapambana na CDM ikiwa chini ya Dr Slaa kwenye operesheni Sangara.

Hata kama kulikuwa wizi wa kura, kwanza ilikuwa kwenye ngazi ya Rais nazo siyo zaidi ya 9%. Lakini Magufuli alikuwa anaiba mpaka uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Naunga mkono ujio wa Kinana ili aweze kuendesha siasa za kistaarabu na siyo zile za kununua wabunge akina Silinde, Mtulya, Gekul na Mollel
 
Maana yake CCM wanafuta vumbi silaha zao wakijiandaa kwa mpambano wa 2025, Majenerali wa Siasa wanarudi makambini kupanga strategy za vita tayari kumtwanga adui vilivyo.

Kinana ni msomi wa Harvard, moja ya vyuo Bora kabisa duniani, anakwenda kukipika chama hiki na kukisuka tayari kwa kuzikamata Siasa za nchi hii kwa miaka kumi ijayo. Stratejia za msomi wa havard haziwezi lingana na Mnyika au Mbowe ambao wamesoma open university tena huku wakifeli masomo na kurudia mara kwa mara

Ni tahadhali kwa wanaoimba katiba mpya wanasahau kujipanga kwa uchaguzi.
Hakukufanyika succession plan kuandaa akina kinana wengine au zaidi Yao? Nae ni binadamu anayo damu.
 
Ni reform ya zama inayoashiria kutokuungwa mkono kwa zama iliyopita swali ni je wale waliokuwa wakikerwa na zama zilizopita walikuwa wakifanya nn wakati wanasubiri zama zilizopita zipite? Walingoja wakiumia kwa machungu au walifanya kitu kuziondoa zama zile
Una maana CCM yenye tabia ya CCM ilipotea awamu ya Tano, Sasa wanakiondoa kile kipande kibovu Cha awamu ya Tano? Wanakata na kuunga mkanda.

Swali ni waumini na wapenzi wa CCM ya awamu ya Tano watakuwa wapi wakifanya nini?
 
Kuna watumishi wanaweza kustaafu, ila muajir akamuhitaji kwa shughuli maalum na hakuna kinacho haribika.
Hii sio shughuli maalumu bali ni nafasi kubwa ya kiuongozi. Kazi maalumu ni kama kuandika katiba, kuwa mshauri, nk
 
Ni reform ya zama inayoashiria kutokuungwa mkono kwa zama iliyopita swali ni je wale waliokuwa wakikerwa na zama zilizopita walikuwa wakifanya nn wakati wanasubiri zama zilizopita zipite? Walingoja wakiumia kwa machungu au walifanya kitu kuziondoa zama zile
Sentesi ya mwisho ndio jibu
 
Nchi inamilikiwa na familia chache.
Ni heri nchi imilikiwe na familia chache kutoka makabila, dini, jinsia na Kanda mbalimbali nchini kuliko kumilikiwa na watu wa Kabila, dini, jinsia au Kanda moja. Hatari yake ni kubwa sana.
 
Hio elim yake ya Havard kaipata juzi?anayo miaka kibao,haiwasidiii wananchi kwani umaskin unazidi kuongezeka,leo Indonesia waliochukua michikichi Kigoma ndio wasambazaji wakubwa wa mafuta duniani,Alizeti inalimwa sehemu kubwa hapa nchini,ila ndo hivyo tena,wasomi wa Havard wako bize kuramba asali
Uko sahihi, elimu kubwa ya Harvard kama haitumiki kusambaza maji, umeme, shule na dhahanati kwa wananchi Haina maana yoyote. Miaka 60 ya Uhuru misitu IPO lakini madawati hakuna.
 
Huko mitaani kuna
1.CCM A.ya kabla ya 2015.wacheza dili,wenye nacho,hawa sio wengi.
2.CCM B. Watu wa hali ya chini ni wengi walioguswa sana kuonjeshwa na awamu ya 5.Na wapo nje ya miji
Ipo kazi kubalance 2025 katika makundi haya mawili
Vyama vya upinzani vina nafasi gani 2025?
 
CCM ndio chama chenye nguvu apa nchini kinacho katisha tamaa majitu ambayo Kwa ushahidi wa wazi au usio wa wazi Kuna watu wamerudishwa kama wanachama au viongozi wanarekodi za wizi na dhulma. Ina maana nchi inarudi nyuma kwenye madawa ya kulevya, dhulma na wizi.
Hivi hakuna namna ya kupata watu safi katika vyama mbadala ili watengeneze umoja na kuishinda CCM? Kweli Kwa wingi wa watanzania inakosekana mbinu ya kuindoa CCM madarakani kupitia Sanduku la kura!!!
 
Akina Mahera na Polisi watakuwa wanfanya kazi gani?
 
Back
Top Bottom